PRESS CLUB ZANZIBAR YAFANYA UCHAGUZI NA KUSISITIZA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

PRESS CLUB ZANZIBAR YAFANYA UCHAGUZI NA KUSISITIZA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

August 10, 2015
unnamed (73)
Katibu Mkuu msaafu wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Suzan Peter Kundambi katikati akitoa taarifa ya mwaka kwa Wanachama wa Jumuiya hiyo katika mkutano wa Mwaka wa ZPC ulioambatana na uchaguzi. Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (74)
Wajumbe walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (75)
Wajumbe walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (76)
Katibu Mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akiomba kura kwa Wanachama (hawapo pichani)kabla ya kufanyika Uchaguzi huo. Katibu huyo anashika nafasi ya Suzan Peter mara baada ya kushika nafasi hiyo katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo uliambatana na uchaguzi huko ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (77)
Mweyekiti mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kulia akipongezana na aliyekuwa mpinzani wake katika nafasi ya Uenyekiti Suleiman Abdallah mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
………………………………………………………………………………..
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 
WAANDISHI wa habari nchini wamesisitizwa kulinda maadili ya kazi zao ikiwemo kutumia kalamu zao vizuri hasa kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa ikiwa waandishi watatumia vibaya kalamu zao basi wanaweza kuvuruga hali ya amani na utulivu na kuweka nchi katika hali ya machafuko.
Hayo yalielezwa na Meneja Bima ya Maisha Tawi la Zanzibar Aisha Rubenic Makorogo, wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari uliombatana na Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya uliofanyika katika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Alisema, kazi muhimu ya wanahabari ni kuona wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na kutokubali kutumiwa vibaya na watu wenye maslahi binafsina badala yake wafanye majukumu yao kwa kutenda haki kwa pande zote ili nchi iweze kuvuka salama.
Aidha alisema, tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika jamii ambayo inategemewa na kila mtu kwani inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanachi wanaoishi mijini na vijijini kupata habari zinazotokea nchini kupitia vyombo wanavyofanyia kazi.
Meneja huyo, aliwaomba waandishi kufanya kazi kwa ueledi wa juu ili kuona nchi yao inaendelea kuwa na hali ya utulivu na usalama.
Hata hivyo, aliwaomba wanachama wa ZPC kuchagua viongozi ambao wataweza kuiimarisha na kufanya Jumuiya yao iondokane na utegegemezi wa misaada huku wakiwa wabunifu ambao watachagua njia mbadala itakayowaletea kipato katika jumuiya yao.
“Ili kuweza kufanikiwa na jumuiya yenu kuimarika zaidi basi ni vyema kujenga mshikamano na wanachama wenu na kuwa wabunifu wa kutegemea vyanzo vingi vya kujiingizia mapato ili kuikuza jumuiya yenu,” Aliwaasa Meneja Aisha.
Sambamba na hayo aliwaomba wanajumuiya hao kujiunga na Bima ya maisha ambayo inatoa fursa nyingi kwa malengo ya maisha ya baadae kwa mwanachama.
Nae Mjumbe mstaafu wa Kamati Tendaji wa Jumuiya hiyo Suleiman Seif Omar, akitoa shukrani kwa niaba ya wanajumuiya wenzake waliahidi kuendelea kudumisha maadili ya kazi zao na wajibu wao katika kuitumikia jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Viongozi wapya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Abdalla Abdul-rahman Mfaume aliwaomba wajumbe kuzidisha mashirikiano na kuwaahidi kufanya kazi kwa moyo mmoja ili kuiletea ZPC maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Mkutano huo mkuu ulimchagua Abdalla Abdul-rahman Mfaume kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo baada ya kupata kura 40 na kumshinda mpinzani mwenzake Suleiman Abdalla ambae amepata kura tisa,
Katibu Mtendaji wa ZPC Faki Mjaka ambaye hakuwa na Mpinzani alipata kura 46 na Naibu Katibu Mwinyimvua Nzukwi alipata kura 37 baada ya kumshinda Takdir Ali aliyeata kura 13.
Makamo Mwenyekiti wa Jumiya hiyo ni Abdalla Pandu aliyepata kura 28 na kumshinda Rahma Suleiman aliyepata kura 23. Mshika fedha Halima Tamim Thuwein aliyekuwa Mgombea pekee alipata kura 49 .Wajumbe sita wa kamati tendaji ni Aziza Hassan, Ghania Mohammed, Mwashamba Haji Juma,  Ishaka Omar, Maulid Hassan Kipevu na Saleh Hassan.

SEMINA YA MPANGO WA KUPUNGUZA VIFO VYA AJALI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

August 10, 2015

 Ofisa Mradi wa mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani unaosimamiwa kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO)  na Serikali ya Tanzania, Mary Kessi (katikati), akitoa mada kwenye semina hiyo iliyowajumuisha wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri inayohusu  mpango huo wa utekelezaji wa mkakati huo.
 Mtaalamu Mwelekezi, Callie Long kutoka Canada akitoa mada kwenye semina hiyo. 
 Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Asah Mwambene akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi Sokoni Deus (katikati), akitoa mada kwenye semina ya siku mbili ya wanahabari na wadau wa sekta ya usafiri Dar es Salaam leo asubuhi, inayohusu  mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mmoja wa wadau wa semina hiyo akichangia jambo.
……………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
Mradi wa usalama barabarani kwa kushirikiana na  Bloomberg (BIGRS), Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa  umeanza kutoa mafunzo kdau wa sekta wa usafiri wakiwemo wanahari, wanasheria kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ajali.
 
Akizungumza Dar es salaam leo kwenye semina ya siku mbili  inayohusu mpango wa kutekeleza  mkakati wa kupunguza  vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kwa kusisitiza usalama  Barabarani, Ofisa Mradi huo,  Mary Kessi alisema waandishi wamekuwa wakisubiri matukio ya ajali ndipo waripoti habari hizo jambo ambalo si lazima lisubiriwe na inachotakiwa ni kujenga mazoea ya kuandika habari za kufundisha jamii na watumiaji wa vyombo vya moto namna ya kuweza kuepuka kusababisha ajali.
 
“Dhumuni la semina hii ni kujua jinsi ya kuripoti habari hizi za usalama barabarani ili kufikia walengwa kwa kuongea kupitia vyombo vyenu vya habari ili kuwapa ulewa watu wote’ alisema  Kessi.
 
Alisema kuwa mpango huo wa miaka mitano utaelekeza katika kupunguza ajali za barabarani  huku takwimu zinaonyesha ajali hizo zimekuwa zikiua watu milioni1.24 kila mwaka Duniani, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya taifa huku kati ya hao 20 upata ulemavu kutokana na ajali.
 
Alifafanua kuwa uzembe wa madereva usababisha ajali zinazoweza kuzuilika na kuzitaja sababu hizo kuu ni kutofunga mikanda ,kuendesha gari kwa kasi ,matumizi ya pombe kupita kiwango na kutoweka vizuwizi vya watoto.
 
“Uendeshaji wa gari ukiwa umelewa ni kitu kibaya sana wengine wanaendesha gari huu wanachati na simu bila kujali kilichokua mbele wala nyuma yake”alisema
 
Daktari wa Kitengo cha Maafa na Dharura wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Mery Kitambi,alisema Hospitali za mikoa zilizopo nchini hapa zimejaa majeruhu wa ajali pamoja na vifo vinavyo sababishwa na ajali hizo.
 
Alisema waandishi wanatakiwa kuleta fikra mpya kwa  watumia wa vyombo hivyo vya moto ili wajue ni kiasi gani wanajiweka katika hatari na jinsi ya kuepuka hatari hizo.
 
“Ukienda hospitali utawakuta majeruhi wa ajali ni wengi kuliko unavyo fikiria hivyo ni vyema wakajua kwa undani jinsi gani ya kuepuka ajali za kizembe”alisema Kitambi.
 
 
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Mkaguzi wa Polisi, Sokoni Deus, alisema wazazi wanatakiwa kuacha tabia ya kuwapa watoto walio chini ya miaka 18 kuendesha vyombo vya moto kwani usababisha ajali.

TAMASHA LA MUZIKI MNENE BAR KWA BAR KUENDELEA KIVINGINE

August 10, 2015

Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habri Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni Mtangazaji, Dina Marios.
 
 ……………………………………………………………………………………….
 
Na Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Redio cha EFM kimeamua kuendelea kufanya tamasha la muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza.
 
Hayo yalibainishwa na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo hicho, Denis Ssebo wakati akizungumza na waandishi wa habri Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu tamasha hilo.
 
“Baada  ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena Kituo chetu cha  Redio cha Efm kimekubali  ombi hilo na sasa tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa  limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi” alisema Ssebo.
 
Alisema Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.
 
Ssebo alitaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Alisema Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 5 mwaka huu lakini katika kuelekea huko efm imeanza na muziki mnene bango katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.
 
Aliongeza kuwa mwishoni kutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.
 
“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”. alisema Ssebo.
 
Ssebo alipenda kutumia fursa hiyo kuwajulisha umma kwamba katika kuhakikisha wanaendelea kutoa burudani iliyobora zaidi kupitia vipindi vyao mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo mkubwa wame mtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake  wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com simu namba 0712-727062)
Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred yatoa mafunzo kwa albino 20 Kigoma

Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred yatoa mafunzo kwa albino 20 Kigoma

August 10, 2015

unnamed (69)
.Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizindua ujenzi wa bweni la Albino Buhangija mkoani Shinyanga.
unnamed (70)
Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi yake ya BAF ambayo kwa kushirikiana na Junior Achievement (JA) huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa albino Tanzania nzima. Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
unnamed (71)
Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Albino mara baada ya kuzindua mafunzo ya Ujasiriamali Makumbusho ya Taifa.
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Junior Achievement (JA)  imeendeleza zoezi la kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wajamii ya watu wenye albino nchini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya albino 20 walifaidika na mafunzo hayo yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, kanali mstaafu Issa Machibya. Mbali ya watu wenye albino, washiriki wengine katika mafunzo hayo walikuwa wanawake na vijana.
Machibya alitoa wito kwa taaisis nyingine kuiga mfano taasisi ya Brigitte na Junior Achievements ambayo mpaka sasa imetoa mafunzo kama hayo kwa vijana na akina mama 25,000.
Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mafunzo ya ujasiliamari ni muhimu kwa kila mtu na kupongeza juhudi za mrembo huyo ambaye mpaka sasa ametoa mafunzo kwa watu wenye albino 70. Kati ya hao 70, albino 50 walipata mafunzo jijini Dar es Salaam.
 “Haya ndiyo mambo muhimu ya kuigwa kwa jamii, taasisi ya Brigite imetoa elimu ambayo itawawezesha wahitimu kufanyakazi ya ujasiriamali na kujipatia kipato kwa jasho lako, nawapongeza sana na taasisi nyingine zifuate nyayo,” alisema Mashibya.
Mratibu wa mafunzo hayo, Stanley Mosha alisema kuwa kwa kupitia BAF kwa sasa unaende vizuri na lengo lao ni kutoa mafunzo kwa watu wenye albino kila mkoa na wamepanga kutoa mafunzo kwa albino 300 nchi nzima kwa mwaka 2015.
Mosha alisema kuwa lengo lao mafunzo hayo ni kuwawezesha kiuchumi vikundimbalimbali hususani vijana na wakinamama. Alisema kuwa hatua hiyo imetokana na mafanikio ya Brigitte katika mashindano ya urembo ya Dunia ya mwaka 2013  nchini Indonesia na kushika nafasi ya tatu kupitia taji la mrembo mwenye malengo baada ya kuonyesha dunia jitihada zake za kusaidia watu wenye ualbino nchini Tanzania.
Alisema kuwa kuanzia hapo, Brigitte amekuwa Balozi wa watu kwa watu wenye ualbino Tanzania na kufanya shughuli mbalimbali za kuwasaidia mfano ujenzi wa bweni la kisasa lenye uwezo wa kuchukua idadi ya watoto 60, na uboreshaji  mazingira kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga.
“Nimefuraishwa na Mwitikio na ushirikiano walioonyesha kwa kutambua na kukubali kuliingiza kundi hili na kuweza kuungana na makundi mengine ya vijana katika program za ujasiriamali. Kulitambua na kulijumuisha kundi hili katika kuwajengea uwezo ni hatua kubwa inayowezesha kupanua wigo na juhudi za kuwezesha makundi ya vijana na wakinamama kiuchumi na tunaomba wadau wengine waungane nasi katika hili,” alisema Mosha.
Kwa upande wake, Brigitte alisema kuwa ataendeleza mpango huo hapa nchini na anaamini atafikia lengo lake. “Nashukuru Junior Achievement kwa kuniunga mkono katika mpango huu ambao kwa sasa unapata mafanikio makubwa, naomba kuungwa mkono kwani jukumu hili ni la watanzania wote,” alisema Brigitte.
Kimbisa Amkaribisha Rais Kikwete Dodoma

Kimbisa Amkaribisha Rais Kikwete Dodoma

August 10, 2015

unnamed (66)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.Ndugu kimbisa alikanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana   (Picha na Freddy Maro)
unnamed (67)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Katikati ni Ndugu kimbisa alikanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni   (Picha na Freddy Maro)
unnamed (68)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma leo
Wateja wamiminika banda la NHC Nane Nane, Lindi

Wateja wamiminika banda la NHC Nane Nane, Lindi

August 10, 2015

image (3)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitia saini kwenye kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la NHC lilikuwapo katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi kulikokuwa kukifanyika maonesho hayo ya Nane Nane kitaifa.
image (5)
Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi. 
image (7)
Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.  
image (9)
Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
image (11)
image (13) image
0I7A0544
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
0I7A0550
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

CCM MTWARA WAUNGANA KUMHAKIKISHIA USHINDI MAGUFULI

August 10, 2015

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimia wanachama wa CCM mkoa wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mtwara.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wana CCM wa mkoa wa Mtwara nje ya ofisi za CCM mkoa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wana CCM wa mkoa wa Mtwara nje ya Ofisi ya CCM mkoa na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuimarisha Chama.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mtwara ambapo alifika kusalimia na kusaini vitabu vya wageni.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwigulu Nchemba.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana an Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego akizungumza wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimu Mgombea Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli aliyefika ofisini hapo kutoa shukrani kwa wadhamini 231 waliomdhamini kwenye nafasi ya Urais mkoa wa Mtwara ikiwa sehemu ya kutimiza taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Mtwara na kuwaambia Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli atashinda mapema mno.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara  ambapo alihakikisha kuwa Mtwara itaongoza katika kumpigia kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Husnain Murji akiwahutubia wana CCM nje ya ofisi ya CCM Mtwara na kuwaambia kuwa ushindi kwa CCM utakuwa wa kishindo .
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

August 10, 2015

download (8)

Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani na uwanja wa Mafunzo vilivyopo kisiwani Zanzibar.
Twiga Stars iko kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo- Brazzavile kuanzia Septemba 04 – 19 mwaka huu.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ameendelea kukinoa kikosi chake cha wachezaji 25 waliopo kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika.
Twiga Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.
KIHANGA MWENYEKITI FA MOROGORO
Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Morogoro (MRFA) jana kilifanya uchaguzi wa viongozi wake katika nafasi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mjumbe wa mkutano mkuu pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Katika uchaguzi huo Paschal Kihanga aliibuka na ushindi katika nafasi ya mwenyekiti, huku Gracian Max Makota  akishinda nafasi ya makamu mwneyekiti, nafasi ya katibu mkuu imechukuliwa na Charles Mwakambaya na katibu msaidizi Jimmy Lengme.
Nafasi ya Mweka Hazina imechukuliwa na Peter Mshigati, Mjumbe wa mkutano mkuu ni Hassan Mamba na mwakilishi wa vilabu ni Ramadhani Wagala, Kamati ya utendaji wamechaguliwa Mrisho Javu, Rajabu Kiwanga na Boniface Kiwale.
TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuongoza chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kazi za kila siku za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI MALAWI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za rambi rambi kwa Rais wa Chama cha Soka nchini Malawi (FAM), Walter Nyamilandu kufutia kifo cha aliyekua Rais wa chama hicho John Zingale.
John Zangale alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi wiki iliyopita katika hospitali ya  Mlambe iliyopo Blantyre nchini Malawi na kuzikwa mwishoni mwa wiki alikuwa Rais wa FAM mwaka 1998- 2002.
Katika salam zake kwenda kwa Rais wa FAM, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu pamoja na chama cha soka nchini Malawi kwa msiba huo, na kusema TFF kwa niaba ya Watanzania iko pamoja nao katika kipindi hicho cha maombelzo.
WATANZANIA SABA WAULA KAMATI ZA CAF
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF ) kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Cairo nchini Misri, kimewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.
Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:
  1. Leodeger Tenga- (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama).
  1. Jamal Malinzi – (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
  1. Mwesigwa Selestine – (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
  1. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)
5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)
  1. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)
  1. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania – TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.

ZITTO ; FILIKUNJOMBE NI MCHAPAKAZI MZURI, CHIKU AMTAKA MBUNGE MSIGWA AONYESHE ALICHOFANYA JIMBONI

August 10, 2015

Ziito Kabwe  akiwa na mume  wa Chiku Abwao na Chiku Abwao  na kada wa ACT wazalendo.
Zitto kabwe  akiwa na wapambanaji
Zitto kabwe  akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Chiku  Abwao  akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Mgombe  udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea  ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwao.
KIONGOZI  wa  chama  cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe (CCM)  kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana na utendaji kazi  wake mkubwa badala ya maneno bila  vitendo.

Huku aliyekuwa mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa  Chiku Abwao akimtaka  mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji  Peter  Msigwa (chadema) kuwaeleza  wakazi  wa jimbo  hilo ndani ya  miaka  mitano ya  ubunge  wake  amefanya  nini zaidi ya maandamano  na kutukana  watu .

Kauli   hiyo  waliotoa wakati  wa mkutano wa hadhara wa  kuwatambulisha   wagombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya  mkoa  wa Iringa na  kuwa siasa si maneno  matupu  siasa ni  kazi  zaidi ya  kuwakomboa wananchi   waliokuamini katika maendeleo .

Alisema  Bw  Kabwe  kuwa mbali ya  kuwa  yeye  ni  ACT  wazalendo  ila hata acha  kuwazungumzia  baadhi ya  wabunge   waliofanya kazi nzuri ya  kuwatumikia  wananchi  wao na  miongoni mwa  wabunge hao ni pamoja na mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya  jimboni inaonekana na kazi aliyoifanya  ndani ya  bunge katika  kupigania maendeleo ya  wana Ludewa na  Taifa  kila mtazania anatambua mchango  wake .

Kwani  alisema  kuwa kati ya manho makubwa ambayo  Filikunjombe kama  makamu  wake  mwenyekiti  waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati liyoifanya  ni pamoja na  kuhakikisha ripoti ya Escrow inalindwa  pasipo  kuibiwa wakiwa wabunge  watatu ambao  walikesha  wakilinda  ripoti hiyo  isiibwe  na mawaziri  waliokuwa  wakizingira  jengo  walilokuwepo  ili  kuiba ripoti hiyo .

'' Siku   ile  tulikesha na mashuka  yetu ya  kimasai  kuhakikisha  ripoti yetu  haiibwi ili  tuiingize  bungeni  na tukaiingiza  bunge  lakini  ile  ripoti hadi  leo kuna  mambo hayajamalizwa  kwani kampuni ya IPTL ambao  imenunuliwa na kampuni ya PAP ya  Singa  singa na kampuni   hiyo ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh  bilioni 4 kila mwezi kutoka  Tanesco  hapo  wazalishe ama  wasizalishe'' alisema  Kabwe


Alisema  kuwa kampuni  hiyo  asilimia 50  inamilikiwa na Seth Singa  singa na  asilimia 50  nyingine  zinamilikiwa na kampuni  inaitwa simba  Trust  iliyosajiliwa nje  ya  Tanzania  na  wamiliki  wake  hawafahamiki na  kuwa hizo ndizo  hoja ambazo  ACT wazalendo  wamejiandaa kutembea  nazo katika kampeni  ya uchaguzi mkuu .

Kabwe  alisema  kuwa sakata  ya ECROW  bado  halijaisha kwani  bunge liliagiza mtambo wa IPTL  utaifishwe  ila hadi  leo bado kuna  kigugumizi katika  kuchukua hatua  juu ya suala   hilo la kampuni ya kitapeli  kuendelea  kulipwa mabilioni ya shilingi  hivyo  alisema kuwa haja ya chama cha  kati  kuingia Ikulu ili  kuweza kupambana na mafisadi  wa Richimond ambao leo  wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .

Hivyo  alisema kuwa kila  sababu  wabunge kufanya kazi wanayotumwa na  wananchi  wao kwa uadilifu  badala ya  kuwa  wabunge wa maneno  bila  vitendo na kuwa wakati tukielekea katika  uchaguzi mkuu ni vema  wananchi  kuwapima  wabunge  wanaowachagua kwa  kueleza  wamefanya  nini majimboni  badala ya kuwa na mbunge  mpiga  kelele zisizo  za kimaendeleo kwa wananchi  wake .

Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa ACT wazalendo   jimbo la  Iringa mjini Bi Abwao  ambae  amejiunga na  chama  hicho kutoka Chadema  alisema mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Msigwa ajiandae  kukabidhi  jimbo   hilo kwa  ACT wazalendo kwani ameshindwa  kuwatumikia  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini kazi  waliyomtuma bungeni .

Alisema  kuwa kipindi  cha  miaka mitano ya  mbunge mchungaji Msigwa  jimboni hapo  hakuna  jipya ambalo amelifanya  zaidi ya  maandamano na  vurugu ambazo  wakazi  wa Iringa mjini hawajapata  kuziona na  kuwa atazunguka kila moja hadi nyingine  kuwaeleza  wananchi jinsi  ambavyo mbunge  huyo  alivyojaribu kuua nguvu  ya  vyama  vya  upinzani na  kushindwa  kuwajibika kwa wananchi  waliomchagua.