MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YAWASOGEZA HUDUMA YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA NEWLAND WILAYANI MOSHI.

August 09, 2017
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Newland. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa utamburisho wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo alipotembelea Mamlaka hiyo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) .
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa tanki la Maji linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.
Tenki la kuhifadhia Maji kwa ajili ya Mradi wa Maji yanayosambazwa katika kijiji cha Newland.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizindua tenki la Maji katika eneo la Shabaha kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuruenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Prof Faustine Bee na kushoto mwa katbu Mkuu ni Mjumbe wa Bodi hiyo ,Bi Hajira Mmambe.
 
WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA KAMPUNI YA FOTON

WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA KAMPUNI YA FOTON

August 09, 2017
PMO_8782
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Funguo ya Magari matatu  yenye thamani ya Dola za kimarekani 99,700 ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania ,wanaoshuhudia kutoka kushoto  ni Meneja masoko wa kampuni ya Simba Motors Taanzania Bibi Ifigenia Salazar na kutoka kulia ni Afisa masoko wa Foton International , Bwana Fan Liang .makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni Dar es salaam Agosti. 9. 2017
PMO_8835
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia moja ya magari aliyo kabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania. makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni Dar es salaam Agosti. 9. 2017

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.
Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.
“Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali kwa umma.”
Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya vijijini.
Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari 700,000 kwa mwaka, ambayo  yanauzwa katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.
Kuhusu suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa  kuna fursa nzuri za uwekezaji na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.
                                                       
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 9, 2017
RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA WAKURUGENZI YA ZBC,UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII NA MICHEZO

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA WAKURUGENZI YA ZBC,UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII NA MICHEZO

August 09, 2017
1
Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBC Bi.Nasra Mohamed (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo na Uongozi wa ZBC, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Mjumbe wa Bodi Nd,Ali Bakari
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo , Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC pamoja na Uongozi wa ZBC leo   katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,
3
Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Nd,Iman Othman Duwe (kulia) alipokuwa akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo  katika kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC na Uongozi wa ZBC,ambacho kikao hicho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji ya ZBC na Bodi kwa pamoja,(kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini Mhe.Mohamed Fakih,
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,Bodi ya  Wakurugenzi  ya ZBS pamoja na Uongozi wa ZBS     katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,
5
Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof Ali Seif Mshimba (kushoto)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Nd,Said Hassan Said
6
Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof. Ali Seif Mshimba (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),wengine ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya ZBS wakisikiliza kwa makini taarifa hiyo,
Picha na Ikulu.
Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kuwahoji waliokuwa viongozi wa TASO Kanda ya Mashariki

Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kuwahoji waliokuwa viongozi wa TASO Kanda ya Mashariki

August 09, 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwakamata mara moja waliokuwa viongozi wa chama cha wakulima Tanzania TASO kanda ya mashariki kutokana na ubadhirifu wa fedha walioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Dk Kingwangala alitoa agizo hili mara baada ya kupokea taarifa za kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mh. Dk. Steven Kebwe juu ya walioukuwa viongozi wa Taso kanda ya Mashariki kushirikiana kuuza baada ya maeneo kwa wananchi ndani ya uwanja wa maonyesho ya mwalimu Juliaus Nyerere nanenane ulipo mkoani Morogoro. Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho cha Nane nane akimwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Salum, ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka viongozi hao huku akieleza kuwa kutokana na usajili wamashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa ndani ya wizara yake ni, vyema viongozi hao wakatafutwa na kukamatwa ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili. “Kwa mamlaka, tunawaagiza Mkuu wa TAKUKURU kuhakikisha wanawakamata viongozi wa TASO haraka ilikuweza kurudisha mali zote ikiwemo walizowauzia wananchi viwanja ndani ya maeneo haya. Taasisi ama NGO’s zikifilisiwa mali zote ni za Serikali na zinakuwa chini ya uangalizi wa Serikali hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wale waote waliohusika” alieleza Dk. Kigwangalla katika tukio hilo la kufunga kilele cha maadhimisho ya Nane nane, Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar e s Salaam, katika Banda la Mwalimu Julius Nyerere. Dk. Kigwangalla apia ameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Vyeti, hundi za fedha pamoja na vikombe vya ushindi kwa taasisi na mashirika na wadau walioshiriki maonyesho hayo. Hata hivyo Dk. Kigwangalla ameongeza siku mbili zaidi kuendelea kwa maonyesho hayo ambayo yaendelea leo na kesho Alhamisi Agosti 10,2017. Awali amepata Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya viwanja hivyo huku akijionea mazao ya kilimo na ufugaji wa kila aina pamoja na bidhaa zitokanazo na kilimo za wadau wa ndani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa wakati akiwasili viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia namna mashine ya kukoboa mahindi ya kisasa inavyofanya kazi ambayo itakuwa msaada kwa wakulima hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasabahi baadhi ya watoto waliofika kwenye kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017

MGOMBEA URAIS TFF FREDRICK MWAKALEBELA AJA NA MAMBO KUMI YA KUINUA SOKA NCHINI

August 09, 2017
--
Na Mwandishiwetu , Dar es Salaam
Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.

MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI

August 09, 2017


1.      Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.



Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.



1.      Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Na; ELIAFILE SOLLA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA (NANE NANE) KITAIFA MWAKA 2017

August 09, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wakati wa kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.(Picha zote na Mathias Canal)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto) akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Lindi Mhe Salma Kikwete wakati alipotembelea Mabanda ya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.