MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MKE WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MKE WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA

May 29, 2014

1 (3) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha mke wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika kumfariji Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana jioni. Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya Kinondoni. Picha na OMR
3 (1) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji katika msiba wa mke wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi,  Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika kumfariji Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana jioni. Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya Kinondoni. Picha na OMR
4 (1) 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Adama Malima, akizungumza machache katika shughuli hiyo ya kuhani msiba huo.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI BABATI

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI BABATI

May 29, 2014

Msafara wa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwa umesimama wakati alipokuwa ukivuka katika mto Magala  katika kata ya Magara akitokea Mbulu, wakati Katibu mkuu huyo alipokuwa akiwasalimiana na wananchi na  kuongea nao kuhusu tatizo  la ujenzi wa daraja katika mto huo. Ambapo kumekuwa kukitokea usumbufu kwa wananchi na wanafunzi wanaopata huduma upande wa pili wa vijiji hivyo vya kata ya Magala, Kinana amewaambia wanakijiji hao kuwa atafuatilia na kuzungumza na Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli ili kujenga hata daraja la muda ili kuwasaidia wananchi hao kwani magari mengi yanayovuka katika mto huo ni madogo yakibeba  watalii na watu lakini pia barabara hiyo ambayo imepitia milimani ni kiungo kati ya Mbulu na Babati, hivyo wananchi wa Mbulu wanapitia barabara hiyo ili kwenda kupata huduma Babati ambako ni makao makuu ya mkoa wa Manyara, Daraja hilo liliahidiwa na Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za mwaka 2010(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE–BABATI)
MAGEREZA NA GEPF WATILIANA MKATABA WA UWEKEZAJI

MAGEREZA NA GEPF WATILIANA MKATABA WA UWEKEZAJI

May 29, 2014

PIX 1  
Kamishna Jenerali wa Magereza Jonn Minja (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (GEPF) Bw. Daud Msangi (kulia) Alhamis 29, 2014
PIX 2 
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam. 
PIX 3 
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya uwekezaji baada ya kutiwa sahini.leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam.