PICHA ZA MAPOKEZI MAKUBWA : JANUARY MAKAMBA ATUA BUKOBA LEO KUZOA WADHAMINI LUKUKI

June 24, 2015


Mh. January Makamba na mkewe, Ramona Makamba(kulia) baada ya kuwasili mkoani hapa Kagera kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.

Mh. January Makamba na mkewe, Ramona(kulia) mara baada ya kushuka kwenye Ndege leo hii Jumatano asubuhi juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.




Mh. January Makamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera 




Mh. January Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Sekondari waliokuwa Uwanjani hapo ambao bila Shaka walikuwa wanasoma masomo ya Ndege inavyoruka na kutua na mengineyo kiujumla leo jumatano juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba




Mh. January Makamba akisaini kwenye kitabu cha Wageni kwenye Uwanja Ndege Bukoba.




Mh. January Makamba na mkewe, Ramona wakiteta jambo kwa furaha.




Msafara wa Bodaboda kuelekea Mjini kwenye mzunguko na kugeuka kwenye Makao makuu ya CCM Mkoa wa Kagera









Mjini Bukoba, Bodaboda wakimsindikiza Mh. Januari Makamba













Makamba akisalimia Wakazi wa Mji wa Bukoba walijitokeza kwa wingi 




January Makamba ameendelea na Ziara yake ya Kusaka Wadhamini katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania na leo hii jumatano juni 24, 2015 yupo hapa Mkoani Kagera akiomba Uzamini. Mh. January Makamba amepokelewa na wakazi wengi wa Mkoa wa Kagera wakiwemo Vijana walijitokeza kwa wingi kumpokea. Picha na Faustine Ruta, Bukoba




Mh. Januari Makamba baada ya kusalimiana na Wakazi waliojitokeza kwenye Makao makuu ya CCM ameelekea katika Hospitali ya Mkoa kuwaona wagonjwa mbalimbali na Baada ya hapo ameelekea Wilayani Misenyi kwenda kusalimia Wakazi wa huko na Kuwaomba wamdhamini kwa kuweka saini fomu zake za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho cha CCM.




Mh. Januari Makamba Akitia saini Katika kitabu cha wageni Ofisi za CCM 





January Akizungumza na wakazi wa Bukoba waliojitokeza kumsikiliza katika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera leo








Wakazi wa Mji wa Bukoba wakimsikiliza Mh. January Makamba kwa makini leo hii jumatano.




RAIS KIKWETE NA DKT. REGINALD MENGI IKULU, DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE NA DKT. REGINALD MENGI IKULU, DAR ES SALAAM

June 24, 2015

2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) Dkt Reginald Mengi wakiongea na kubadilishanma mawazo Ikulu, Jijini Dar es salaam katika hafla ya kutunuku nishani kwa watumishi wa umma na wananchi waliofanya vyema na kwa uadilifu kwenye sehemu zao za kazi. Dkt Mengi alikuwa mmoja wa watu mashuhuri walioalikwa hapo Ikulu.
PICHA NA IKULU
3

Mawakala wa forodha nchini waaswa kujisajili kwenye mfumo wa himaya moja ya forodha ya afrika mashariki (SINGLE CUSTOM TERRITORY)

Mawakala wa forodha nchini waaswa kujisajili kwenye mfumo wa himaya moja ya forodha ya afrika mashariki (SINGLE CUSTOM TERRITORY)

June 24, 2015

1
Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na kuwataka mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa uondoshaji wa Himaya moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika kwani mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana mpaka sasa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Naibu Kamishna wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya.
2
 Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.
3
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakimsikiliza Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
4
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
5
………………………………………………….
Habari Picha Na Hassan Silayo-MAELEZO
Mawakala wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza kutumika hivi Karibuni.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika.
“Sasa tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza kutokea”. Alisema Bw. Kabisi
Bw. Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala waliojisajili mpaka sasa.
Aidha Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali.
Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha.
Pia Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza katika makusanyo ya mapato ya serikali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete afungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu-juni 24, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete afungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu-juni 24, 2015

June 24, 2015

01
03
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015
02
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoma kwa Profesa Nerey Mvungi wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam juu ya Ubunifu wake wa kutengeneza mfumo wa kidigitali wa kusaidia kupambana na ajali barabarani  kabla hajafungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015
mail.google.com
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoma kwa kijana Godfrey Magila wa Magilatech Company Ltd.  juu ya Ubunifu wake wa kutengeneza mfumo wa teknolojia ya mawasiliano rahisi  kabla hajafungua Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 24, 2015
PICHA NA IKULU
 WAZIRI BERNARD MEMBE AKUTANA NA WASANII WA FILAMU MKOA WA MOROGORO

WAZIRI BERNARD MEMBE AKUTANA NA WASANII WA FILAMU MKOA WA MOROGORO

June 24, 2015


SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.
Picha zote na John Badi
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.