January 31, 2014

WAZIRI WA HABARI,VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE ZA SEKONDARI JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (wa kwanza kushoto)  na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom (wa pili kushoto), Salum Mwalim,Wakikabidhi baadhi ya vifaa vya michezo kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mnazi Mmoja, Shaha Bakari(kulia)Vifaa hivyo vilivyotolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano yatakayoanza hivi karibuni yatahusisha shule za sekondari kumi na mbili(12)za jijini Dar es Salaam.Akishuhudia makabidhiano hayo wapili kutoka kushoto ni Mwalimu michezo wa shule hiyo, Alex Dumien.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (kushoto)Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania (wa pili kushoto), Salum Mwalim wakikabidhi vifaa vya michezo kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mugabe, Juma Shabani (kulia)Vifaa hivyo vimetolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano yatakayo anza hivi karibuni na kuhusisha shule za sekondari kumi na mbili(12) za jijini Dar es Salaam.Akishuhudia wapili kutoka kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo, Farouk Kaburwa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara(wapili toka kushoto)akishuhudia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania(kulia) Salum Mwalim akikabidhi mfano wa hundi ya Milioni moja(1,000,000) kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henry Lihaya (wa pili kushoto) fedha hizo zitatumika katika maandalizi wakati wa mashindano ya michezo shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Prof. Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (wa pili kushoto)akikabidhi moja ya vifaa vya michezo kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila, Simon  Nungu (kulia)Vifaa hivyo vya michezo vilivyotolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya michezo mbalimbali itakayoanza hivi karibuni na kuzihusisha shule za sekondari kumi na mbili(12)za jijini Dar es Salaam.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania(wa tatu kushoto),Salum Mwalim.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA FINLAND BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

January 31, 2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma.
January 31, 2014

*SIMBA KUWAKARIBISHA JKT OLJORO UWANJA WA TAIFA KESHO

Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 wikiendi hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Refa atakuwa Nathan Lazaro kutoka mkoani Kilimanjaro wakati Kamishna ni Hakim Byemba wa Dodoma.
Uwanja wa Azam uliopo Mbagala siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Ashanti United na Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga kwa viingilio vya sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Jumapili (Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni), na Azam vs Kagera Sugar (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 10 kamili jioni).

Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam Complex, Chamazi).
January 31, 2014

BREAKING NEEEEWZ!!! VIONGOZI WA CHADEMA MBOWE, MDEE NA MSIGWA WAKAMATWA NA KUHOJIWA MKOANI IRINGA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wabunge wake wawili, Peter Msigwa na Halima Mdee, waonja joto ya jiwe ya Nondo la lupango za Kituo cha Polisi Kati Mkoani Iringa.

Akizungumza kwa njia ya simu Ripota wa Mtandao huu, alisema kuwa, Viongozi hao wa Chadema, wamekamatwa na Polisi leo asubuhi na kuwashikilia kwa muda kituoni hapo wakihojiwa baada ya jana kupitisha muda katika mkutano wao waliofanya mkoani hapo.

Aidha imeelezwa kuwa viongozi hao walichelewa kufika eneo la mkutano baada ya Rubani wao kupotea angani na kufika eneo hilo zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya muda wa mkutano kumalizika, jambo lililomfanya mwenyekiti huyo kuwaomba Polisi wasimamizi wa usalama kuongea japo kwa dakika chahe ili kuwajulisha wanachama wao kilichotokea.

Baada ya kuruhusiwa kufanya hivyo imedaiwa kuwa mwenyekiti huyo aliyekuwa ameongozana na wabunge wake wawili, alipitisha muda na kuzua maswali miongoni mwa wanausalama wa mkoa huo, jambo lililowapelekea kukamatwa na kuhojiwa kwa muda kituo cha Kati mkoani Iringa leo majira ya saa tatu asubuhi na baadaye kuachiwa wakaendelea na safari zao.