BARCA TAYARI KUSAINI BEKI LA KUSHAMBULIA LA KIBRAZIL

August 27, 2014

KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana.

Uhamisho unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika klabu yake mpya.
Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.

Beki la kushambulia: Beki huyo amefunga mabao sita katika mechi 124 alizoichezea Sao Paulo miaka mitatu iliyopita

AZAM FC WAANZA KUIPASHIA YANGA SC KESHO CHAMAZI, KIMBEMBE KITAKUWA TAIFA SEPTEMBA 13

August 27, 2014
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Bara, Azam FC wanatarajiwa kuanza tena mazoezi kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya kurejea kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ ameiambia Tanga Raha leo kwamba wachezaji wote wataanza mazoezi kesho, kasoro wale ambao wameitwa timu ya taifa.
Father amesema kwamba wachezaji wawili, Aishi Manula na Kevin Friday japokuwa hawapo kwenye kikosi cha Taifa Stars, wao wamepewa mapumziko zaidi- hivyo si lazima waanze kesho.
Azam FC wanatarajiwa kuanza mazoezi kesho kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC Septemba 13, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Aidha, Father alisema kwamba Simba SC waliomba mchezo wa kirafiki na wao wikiendi hii, lakini imeshindikana kwa sababu kocha Joseph Marius Omog amesema hawezi kuwa na mechi baada ya mazoezi ya siku mbili.
ANGEL Di MARIA AWEKA HISTORIA ENGLAND, ASAINI MKATABA MKATABA WA MIAKA 5 NA KLABU YA MAN UNITED

ANGEL Di MARIA AWEKA HISTORIA ENGLAND, ASAINI MKATABA MKATABA WA MIAKA 5 NA KLABU YA MAN UNITED

August 27, 2014


Photo: 'United are the only club I could have left Madrid for': Di Maria signs five-year deal at Old Trafford to smash British transfer recordAngel di Maria Akiwa amebeba jezi yake leo hii wakati anasaini mkataba na Klabu yake mpya ya Man United leo. Angel di Maria ametokea katika Ligi ya Spain kwenye timu ya Real Madrid.
Got him! Angel di Maria poses with Manchester United boss Louis van Gaal upon signing
Angel di Maria akiwa kwenye picha ya pamoja na Bosi wake Mpya wa  Manchester United Louis van Gaal
New motor: Di Maria poses in front of a Chevrolet car outside Aon Training Complex
Di Maria akiwa na Gari aina ya Chevrolet nje ya Uwanja wa mazoezi Aon Complex

Angalia Mamba alivyoshambuliwa na Simba watatu Kenya, wamchangia lakini awatoa nishai

August 27, 2014


Tazama video ya mapigano kati ya simba watatu na mamba mmoja ambapo pamoja na kuchangiwa na simba hao watatu,mamba aliweza kukabiliana nao na baadae kukimbilia majini.
Hoja ya Maalim Seif kupokezana urais yawa ‘ngumu kumeza’

Hoja ya Maalim Seif kupokezana urais yawa ‘ngumu kumeza’

August 27, 2014


Dar/Dodoma. Kauli ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuhusu haja ya kupokezana nafasi ya urais kati ya Bara na Visiwani imekuwa ‘ngumu kumeza’ kwa wanasiasa walio wengi.
Baadhi ya wanasiasa wakiwamo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wasomi wengine waliozungumza na waandishi wetu wamepinga kauli hiyo wakieleza kuwa suala hilo halitawezekana kwa sababu linaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa katika jamii.
Mwanasiasa pekee aliyeonyesha kuiunga mkono kauli hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyesema jambo hilo linazungumzika kwa sababu huwezi kuwa na nchi mbili zilizoungana lakini nchi moja pekee ndiyo inayotoa rais mara zote.
“Miaka ya nyuma utaratibu huu ulikuwapo lakini baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka, CCM wakauondoa. Kitendo cha rais kutoka Tanzania Bara kila baada ya miaka 10, ndicho chanzo cha Zanzibar kubadili Katiba yao na kuifanya nchi hiyo kuwa na mamlaka kamili yasiyoweza kuingiliwa na rais wa Muungano,” alisema Mbowe.
Hata hivyo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, alisema mfumo wa kubadilishana urais, utaleta mgawanyiko kwa makundi na maeneo mengine ya nchi kudai kuwa na zamu ya urais.
“Hatuwezi kwenda katika mfumo huo. Utasababisha kugawanyika kwa sababu ukishasema hivyo watatokea Waunguja nao watadai, Wakaskazini, Waislamu na Wakristo nao watadai,” alisema.
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, alisema utaratibu huo unaweza kuleta matatizo kwa vyama katika kumpata mgombea mwenye sifa.

JUX HAKUWEZA KUSUBIRI???

August 27, 2014


Jux na V Money
Jux na Jackie
aliemuimbia nitasubiri ambapo
uvumilivu umemshinda kabisaaa
Habari ya mujini ni Jux na V Money watu pipooo, mahaba ni nyonge ni kill kabisa, Jux aliimba nitasubiri inaonekana uvumilivu umemshinda mwayego na kaamua kukama mtoto mulito anayekuja kwa kasi katika anga  la music V Money uwiii chezeya wapareee wewe full mipagawisho, so all pares can call Jux Vuitton shemeji , ila kumvumilia mtu ambaye hujui lini atatoka nayo yataka moyo jamaniii tusimlaumu sana Jux hata kama ingekuwa wewe

we do the seeking n you do the judging

YAENDESHA WARSHA JUU YA UTOAJI TAARIFA SPS

August 27, 2014
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, kutoka Wizara ya Viawanda na Biashara, Ismail Mfinanga akifungua warsha ya siku tatu ya viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka wizara za Viwanda, Kilimo na Afya wakishiriki warsha hiyo juu ya utoaji taarifa na uulizwaji taarifa (SPS). Mkutano huo ulianza Dar es Salaam Agosti 26-28 mwaka huu.
 Oswald Chinyamakobvu kutoka Secretariet ya SADC akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo.
  Chiluba Mwape kutoka Secretariet ya SADC akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo.
 Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi.
 meza kuu ikifuatilia utambulishi wa wajumbe.
 Washiriki wakiendelea na ufutailiaji wa ufunguzi.
 Chiluba Mwape kutoka Secretariet ya SADC akielezea kwa ufupi mpango huo wa SPS ambao unalengo la kuweka uwazi katika upatikanaji wa taarifa za bidhaa  zizalishwazo katika ukanda huo.
Picha ya pamoja ya washiriki wote.
MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

August 27, 2014

ga10 
Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
ga14 
Rais Kikwete akiagana na baadhi ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga11 
Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga12 
Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na wazee wa mji wa gairo waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
ga13  
Rais Kikwete akiagana na baadhi ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014ga7 
Sehemu ya maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga6 
Mmoja wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro akichukua kumbukumbu wakati wa  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara  ga5 
Sehemu ya maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga4 
Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Mabhut Shabiby akimkaribisha Rais Kikwete kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, ga3 ga1 
Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) wawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na Rasimu ya Katiba Mpya.

Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) wawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na Rasimu ya Katiba Mpya.

August 27, 2014
PIX 1 
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya Katiba Mpya jana 26 Agosti, 2014.
PIX 2 
Chifu John Nyanza (aliyekaa katikati) wa kutoka Magu akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 3. 
Chifu Agnes Ndaturu (kushoto) wa kutoka Ntuzu, Bariadi akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye jana 26 Agosti, 2014. kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 4. 
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) akipokea mapendekezo ya maoni toka kwa Chifu John Nyanza alieuwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26 Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
PIX 5. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari walikifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo toka kwa Machifu waliouwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) jana 26 Agosti, 2014.kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
26/08/2014.
UMOJA wa Machifu wa Tanzania (UMT) kupitia wawakilishi wake, jana 26 Agosti, 2014 umewasilisha nyongeza ya mapendekezo yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akiuwakilisha Umoja wa Machifu Tanzani (UMT), Chifu kutoka Magu John Nyanza amemueleza Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuwa wanaishauri Serikali kutayarisha mkakati wa Kitaifa wa Utamaduni kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa masuala ya Utamaduni ili mpango mkakati huo uwe na Dira ya Utamaduni itakayobainisha cha kufanya ili kujenga, kuhamasisha na kuendeleza Utamduni katika maeneo yote nchini.
“Chifu kutoka Magu, John Nyanza amesema kuwa lengo la kuwasilisha mapendekezo hayo kwaajili ya kusisitiza masuala mazuri ya Utamduni kuendelea ili kuweza kudumisha madili kwa nia nzuri ya kudumisha amni na ushirikiano”. Alisema Chifu Nyanza.
Naye Chifu kutoka Ntuzu, Bariadi Chifu Agnes Ndaturu ameeleza kuwa mapendekezo yao yatasaidia kuweza kuwatambua waganga wa Jadi ambapo hapo zamani , mganga wa Jadi alikuwa anatambulika na kufanya kazi katika eneo husika analotoka, lakini hivi sasa waganga wengi wa jadi wamekuwa na tabia ya kufanya kazi zao bila mipaka.
”Mapendekezo haya yatasaidia viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga wanaokiuka maadili ya shughuli zao mfano mauaji ya Albino, kwakuwa kila kiongozi atakuwa anawatambua waganga wa eneo lake husika”. Alisema Chifu Ndaturu.
Aidha, Machifu hao wameongeza kuwa, Wajumbe wenzao waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya umuhimu wa Utamaduni kupewa nafasi rasmi katika Katiba mpya na Serikali ili pawepo na kipaumbele katika utekelezaji wake nchini.
Wakizungumza kwa kauli moja Umoja wa Machifu wa Tanzania wamesema kuwa suala la Utamaduni katika Rasimu ya Pili ya Katiba lifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo yaliyoibainishwa huku msisitizo wao ukiwa katika Katiba kueleza wazi kuwa sera na Sheria mpya zitakazotungwa zihakikishe kuwa Tume ya Taifa ya Utamaduni inaanzishwa kisheria ili kusimamia masuala ya Utamaduni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatotoa wasiwasi wawakilishi wa Umoja wa Machifu hao wa Tanzania aliokutana nao kwa kuwaeleza kuwa atayawasilisha katika Uongozi wa Kamati ya Bunge ambapo Kamati Ndogo ya Uongozi inatarajiwa kukutana leo jioni ili kuweza kuyajadili.
“Nimeyapokea mapendekezo yenu, kwakuwa Kamati zinaendelea na kazi ambapo wiki hii kamati zitakuwa zimemaliza kazi zake na hakutakuwa na nafasi tena ya kuyapokea mapendekezo na maoni mengine”. Alisema Samia.
Hivi karibuni, makundi mbalimbali yaliwasilisha mapendekezo yao ambapo baadhi ya makundi hayo yakiwemo Wafugaji, Wasanii na Wanahabari yaliwasilisha.