TAASISI YA AGRI-BUSNESS MEDIA INNITIATIVE YA JIJINI MWANZA YAWAHIMIZA VIJANA KUJIKITA KWENYE KILIMO
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Na Binagi Media Group
Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia, nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.
Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani, maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.
"Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa Taasisi ya AMI-TZ.
Mallaba anawasisitiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.
"Napenda kuwaambia akina dada waamuke maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa vijana wengine". Anasisitiza Aneth Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/ Afisa Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akimwagilia maji kwenye shamba la bamia
Wachapa kazi wakichakarika
Kilimo cha nyanya
Mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia mashine kutoka Ziwa Victoria ndio hutumika kwenye shamba hili.
Kwa msaada na ushauri, piga simu nambari 0754 99 66 13
RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Rais wa Uturuki, Mheshimiwa ,
Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini
Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 21, 2017.Mheshimiwa Majaliwa
alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan aliyefuatana na
mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja
wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo
kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 21, 2017. Mheshimiwa Majaliwa
alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo
jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na
kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na
kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais.
Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na
Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt
Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat Zeybekekci na Waziri wa
Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
.
Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
SIMBA YATINGA 16 BORA YA FA CUP,YAILAZA POLISI DAR
Klabu ya Simba imewafuata
wapinzani wao Yanga katika hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Azam
Sport Federation baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 kwenye mechi
yake dhidi ya Police Dar mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
Athanas Pastory aliifungia Simba
bao la kwanza kipindi cha kwanza lakini Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’
akaifungia Simba bao la pili kipindi cha pili.
Simba inasonga mbele katika hatua
inayofata baada ya kuifunga Polisi Dar es Salaam na kuiondosha kwenye
mashindano hayo ambayo mshindi wake atapata fursa ya kuiwakilisha
Tanzania kwenye kombe la shirikisho Afrika.
Matokeo ya mechi nyingine za kombe la FA
Mbeya Kwanza 1-2 Tanzania Prisons
Toto Africans 2-0Mwadui FC
Ruvu Shooting 1-2 Kiluvya United
MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AFUNGUA RASMI LIGI YA MBUNGE (ULEGA CUP)
Na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii
LIGI
ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga (Ulega Cup) imefunguliwa rasmi leo kwa
kuzikutanisha timu za Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Mashindano
hayo yamefunguliwa na mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Firbato Sanga
ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed pamoja na baadhi ya madiwani
wanaounda halmashauri hiyo.
Michuano
hiyo ambayo ilianzia ngazi ya Vijiji ilishirikisha timu 125 na baadae
kuchujwa na kubakia timu 25 ambazo zimeingia ngazi ya wilaya na mshindi
wa ligi hiyo ndio atakuwa bingwa wa wilaya.
Akizungumza
na wachezaji wa timu hizo katika ufunguzi wa michuano hiyo Mkuu wa
Wilaya hiyo Firbato Sanga alisema michezo ni udugu na ujirani mwema
hivyo aliwatakia michezo mwema.
Akizungumzia
michuano hiyo Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega amesema kuwa ni
matarajio yake michuano hiyo itakwenda vyema na lengo lake kubwa
nikuona wanapata vijana wenye vipaji na watakaoweza kuipaisha Mkuranga.
"Nimatarajio
yangu mambo yatakwenda kama nilivyopanga na kama mnavyoona wenyewe
waandishi wa habari vijana wa kutoka Mkuranga ndio wanaocheza "alisema
Ulega
Amesema
tangu awali alisha kataa timu hizo kukodi watu Kutoka nje ya Mkuranga
na anashukuru Mungu hayo yamezingatiwa na katika michuano hiyo mshindi
ndio atakuwa bingwa wa Wilaya.
Amesema
kuwa ana matumaini makubwa kwamba kupitia ligi hiyo watapatikanika
vijana wenye uwezo ambao wataweza kuchukuliwa na timu kubwa.
Aidha
amesema kuwa michezo ni Afya ,ajira,na upendo kwani kupitia mashindano
hayo watakuwa wametengeneza ujirani mwema hivyo watumie fursa hiyo
kudumisha Umoja na mshikamono miongoni mwao.
Mchezo
huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya
Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika ya kumi kipindi cha
kwanza.
Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
(Ulega Cup) uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akizungumza na wachezaji wa timu
za Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini katika ufunguzi wa
Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga (Ulega Cup) uliofanyika katika
uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
ALHAJ ALI HASSAN MWINYI AWATAKA WATANZANIA KUWA NA TABIA YA KUENDELEZA YALIYO MEMA.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan
Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema
wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu
ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).
Akizungumza katika hafla hiyo ya Maulid
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Alhaji Mwinyi amesema kuwa Mtume
Muhammad (S.A.W) alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya
kusherekea siku aliyozaliwa.
Hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa
kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku
akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza
mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo
Sheikh Ally Basaleh.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne
Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo,
Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi
Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa
Mkuranga Abdallah Ulega. Viongozi wa dini waliokuwepo ni pamoja na Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah
Mnyaa.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na
viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali juu ya watanzania
kuyafanyia muendelezo wa yale mema kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES
kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali katika kusherekea kumbukumbu ya
mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam,Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza machache katika hafla hiyo ya
Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk. Hamisi Kigwangalla leo
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri
Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Sehemu ya viongozi mbalimbali
wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akutana na mamlaka za udhibiti na utoaji leseni.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka
taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya marekebisho ya wepesi wa
kufanya shughuli nchini, kushoto kwa waziri ni Katibu Mkuu biashara na
uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Mwenyekiti wa kamati ya kuboresha
mazingira ya biashara Dkt. John Mduma, kulia kwa waziri ni Katibu tawala
Kibaha Ndg. Anatory Mhango.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka
taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya
kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na
muhogo mjini Kibaha.
Katibu Mkuu Biashara na Uwekezaji,
Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kikao cha wadau kutoka
taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya
kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na
muhogo mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali za
serikali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya
biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo
mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali
waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini
katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali
waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini
katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
………………
Waziri wa viwanda, Biashara na
uwekezaji akutana na kamati ya kuboresha ya mazingira ya biashara ambayo
inahusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika wizara zote, TBS,
EWURA, SUMATRA, TRA, OSHA, WMA, NCC, n.k na kujadili changamoto
mbalimbali ambazo ni vikwazo katika wepesi wa kufanya shughuli.
Waziri amehimiza wataalamu hawa
kujadili changamoto na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa kero hizo
ili kuboresha urahisi wa kufanya shughuli nchini Tanzania na kuvutia
wawekezaji.
Waziri amehimiza ulipaji wa kodi
ili kuleta maendeleo ya watu, kwani kwa takwimu Tanzania ni ya 154 kati
ya nchi 190 hivyo kuhimiza wafanyabiashara wote kuwa na Tin namba na pia
kulipa kodi.
Mkutano huu umefanyika jumamosi tarehe 21/1/2017 ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA GEREZA LA RUANDA JIJINI MBEYA
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi
Paul Kajida (kulia) wakati alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji
thamani za ndani na sabuni katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo
jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu
wa Kiwanda cha Gereza la Ruanda ASP Michael Kuga, akisoma taarifa ya
hali ya uzalishaji wa sabuni na thamani za ndani mbele ya Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa
ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo zinazofanyika katika
magereza yaliyopo jijini Mbeya.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(wapili kushoto) akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa kiti
kinachotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na
wataalamu wa Jeshi la Magereza.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara
ya kikazi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(wakwanza kulia waliokaa), akiangalia picha za thamani za ndani
zinazotengenezwa na wafungwa wa Gereza la Ruanda wakishirikiana na
wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wengine waliokaa baada ya Naibu Waziri ni
Mkuu wa Kiwanda hicho,ASP Michael Kuga ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto
Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko na Kaimu Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya
kwa ziara ya kikazi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza alipotembelea Kiwanda cha sabuni zinazotengenezwa na
wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la
Magereza.Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Kiwanda() na Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(katikati) akiangalia moja ya sabuni zinazozalishwa na wafungwa wa
Gereza la Luanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Kulia
ni Mkuu wa Kiwanda hicho.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya
kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MWANJALE MCHEZAJI BORA WA DESEMBA 2016
Sentahafu wa Simba, Method Mwanjale amechaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Beki huyo wa kati, aliwashinda kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna
Niyonzima na beki Yakubu Mohamed wa Azam FC. Mwezi Desemba ulichezwa
raundi tatu za Ligi hiyo, huku Simba ikicheza mechi mbili ugenini na
moja nyumbani. Raundi hizo ni ya 16, 17 na 18.
Mwanjali aliiongoza Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake
kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa, na kubaki
katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi, nafasi ambayo
walikuwa nayo wakati wanaingia raundi ya 16.
Pia katika raundi hizo tatu ambapo Simba haikufungwa bao hata moja,
Mwanjali alicheza dakika zote 270, na bila kuonyeshwa kadi yoyote.
Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya timu yake huku
akiongoza safu ya ulinzi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora, Mwanjali atazawadiwa kitita
cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wakuu wa Ligi hiyo Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa
2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza
Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Happygod Msuva wa Yanga
(Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LAFURAHISHWA NA HUDUMA YA KWAYA YA EAGT KAANGAYE
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye kutoka Nyakato Jijini Mwanza, leo wamefanyika Baraka kubwa baada ya kuhudumu vyema katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.
Waumini wengi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wamefurahishwa na huduma ya kwaya hiyo. Pongezi kubwa ziwaendee Mwenyekiti wa kwanya hiyo, Abednego Magesa na Mchungaji Samson Mniko kwa malezi mema yaliyofanikisha wanakwaya hao kumtumikia Mungu kwa bidii kubwa.
Na Binagi Media Group
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye lililopo Nyakato Jijini Mwanza, wakihudumu kwa bashasha kubwa kwenye ibada za hii leo jumapili katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo kwenye ibada za hii leo jumapili. Ibada ya kwanza kila jumapili huanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30 asubuhi.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia ibada za leo jumapli
Mahubiri na Mafundisho ya neno la Mungu kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya pia yanarushwa kupitia runinga ya Star Religion inayopatikana kwenye kisimbuzi cha Continental ambapo visimbuzi hivyo vinapatikana kanisani hapo kwa punguzo kubwa.
Picha na Craty Cleophace @EAGT Lumala Mya
Subscribe to:
Posts (Atom)