RAIS MAGUFULI AZINDUA JENGO JIPYA LA TAWI LA CRDB WILAYANI CHATO

March 09, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe ishara ya uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018

Na Mathias Canal, Chato-Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Maguguli Leo 9 Machi 2018 amezindua jengo jipya la Benki ya CRDB Tawi la Chato Mkoani Geita.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe Dkt. Magufuli amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo utarahisisha huduma za uhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wa samaki Wilayani Chato sambamba na wananchi ambao kwa kiasi kikubwa katika msimu wa Kilimo wamenilima Pamba kwa wingi.

Ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuzifungia baadhi ya Benki nchini na kuzipa onyo zingine ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwa mazoea na kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za uendeshaji.

Alisema ni bora kuwa na Benki chache nchini ambazo zinaweza kuwahudumia wananchi wengi hususani masikini kama ilivyo CRDB ambayo imewafikia kwa kiasi kikubwa wananchi vijijini hivyo kuendelea kuzifungia Benki zote ambazo zimeshindwa kuendesha vyema shughuli zake na kusalia kufanya huduma Jijini Dar es salaam pekee.

Rais Magufuli ameiomba benki ya CRDB kupunguza riba ya mikopo kwani ni asilimia 16 pekee ya watanzania ndio wanaohudumiwa kwenye Benki nchini hivyo ili wananchi wote waweze kukopa na kuweka mitaji yao midogo kwa ajili ya faida yao ya Sasa na badae ni lazima kuwa na riba rafiki kwa wananchi.

JPM ameipongeza Benki hiyo kwa kuajiri wafanyakazi wapatao 3200 tangu ilipoanza rasmi nchini mwaka 1972 wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeielewa dhana halisi ya kuwasaidia wananchi vijijini kutokana na usumbufu mkubwa wanaoupata katika huduma za kifedha.

Alisema kuwa anayo imani kubwa na Benki ya CRDB kwani naye ni mteja wa benki hiyo hivyo ili kuendeleza mahusiano mema tayari seikali imelipa Deni lote la shilingi Bilioni 16 ambalo ilikuwa inadaiwa na benki hiyo kutokana na mikopo katika miaka ya nyuma.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewahamasisha wananchi kutunza fedha zao benki na kuachana na dhana ya kuhifadhi fedha majumbani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa fedha hizo na maisha yao wenyewe.

Mhe Magufuli amesisitiza watanzania kuwa wazalendo huku akisema kuwa anatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamesalia na jukumu la kuandika katika mitandao na vyombo vya habari mambo ambayo ni kinyume na utendaji wa serikali jambo ambalo ni uchonganishi dhidi ya wananchi na serikali yao.

Aidha, Mhe Rais Magufuli alikataa ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei aliyetaka Benki hiyo kuitwa CRDB JOHN POMBE MAGUFULI-CHATO huku akisema kuwa isalie kuitwa CRDB tawi ka CHATO.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania, Dkt Charles Kimei ametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Benki hiyo huku akielezea namna ambavyo amekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua watanzania kupitia rasilimali zao jambo ambalo litawanufaisha na kuwainua kiuchumi.

Alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kubuni njia nzuri za mikopo huku akisisitiza kuwa Benki hiyo kuendelea kuwasaidia wananchi kupitia SACCOS zao kupata mikopo nafuu ili kujinufaisha kwa kuwa na uchumi imara utakaowawezesha kukuza biashara zao.

Sambamba na hayo pia amekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati la kujenga uwanja wa kisasa wa Mpira wa miguu ambapo kwa niaba ya Benki hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Benki ya CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari amekabidhi Hundi la Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya hatua za mwanzo za kuanza ujenzi wa uwanja huo huku akiahidi Benki hiyo kuwa wadhamini wa timu ya mpira wa miguu ya wilaya ya Chato.

Dhifa ya uzinduzi wa Benki hiyo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Wa Nishati Mhe Medard M.Kalemani (Mb), Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Mkuu Wa Mkoa Wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Naibu Waziri Wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijazi (Mb), Naibu Gavana Wa Benki Kuu Tanzania Dkt Bernard Yohana Kibese, Balozi Wa Denmark nchini Tanzania Mhe Einar Hebogard Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari, Mkurugenzi Mtendaji CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, na Wabunge wa majimbo mbalimbali ikiwemo jimbo la Busanda na Mbogwe.
ACT WAPATA PIGO ,VIONGOZI WA NNE NA WAFUASI 45 WATIMKIA CCM

ACT WAPATA PIGO ,VIONGOZI WA NNE NA WAFUASI 45 WATIMKIA CCM

March 09, 2018

Chama cha ACT Wazalendo wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma , kimepata pigo baada ya viongozi wake wa nne na wafuasi 14 ambao ni wananchama kuhamia Chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM). Viongozi hao wamesema wamechukua maamuzi ya kuhamia CCM baada ya kuona utendaji kazi wa Mhe , Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Maguful kuwa ni mzuri,pamoja na kusema chama hicho cha ACT hakina uwezo wala mwelekeo wa kuchukua dola, hivyo wamesema wapo sahihi kuhamia CCM ili kuendana na kasi ya Rais kuweza kuleta maendeleo katika wilaya hiyo ya Tunduru na Taifa kwa ujumla.

Tigo Yawakabidhi simu washindi 84 wa Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

March 09, 2018

Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Michael Peter Ngwashi, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.

Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbagala, Grace Gastory Mandai, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.

Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Mohammed Omar Sabuni, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali. 



Balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali (kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara wa Vingunguti, Jasper Michael Kimei, zawadi ya simu ya 4G aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni hiyo. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#

  • Wateja 84 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure baada ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#

  • Zaidi ya simu 840 pamoja na bonasi za uhakika za intaneti bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Machi 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 84 wapya  wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.

Akikabidhi zawadi hizo kwa baadhi ya washindi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Mtaalam wa usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kufikia sasa promosheni hiyo imeibua washindi wa simu 240 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

‘Kila anayenunua bando la intaneti kuanzia  TZS 1,000 kupita *147*00# anapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pia anaingizwa kwenye droo ya kushinda mojawapo ya simu zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zinazoshindaniwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus.’


‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa kasi ya juu ya 4G,’ Jasper Dethuel Kimei, mfanyabiashara na mkaazi wa Vingunguti Dar es Salaam alisema baada ya kupokea zawadi yake ya simu.


“Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwani baio tuna simu 840 zinazozubiri kunyakuliwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus,’ alisema balozi wa promosheni hiyo, Meena Ali.


Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

UNIDO TAYARI KUSAIDIA TANZANIA YA VIWANDA

UNIDO TAYARI KUSAIDIA TANZANIA YA VIWANDA

March 09, 2018

UNIDO tayari kusaidia Tanzania ya viwanda
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Viwanda (UNIDO) limesema litasaidia Watanzania kutimiza ndoto za kuwa taifa lenye uchumi wa kati linalotegemea viwanda kwa kuunga mkono utendaji wa pamoja wa sekta ya umma na binafsi.
Kauli hiyo imetolewa katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania na pia ya kwanza nje ya makao makuu ya Shirika hilo baada ya kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili mwaka jana.
Alisema katika hotuba yake kwamba moja ya majukumu makubwa ya shirika hilo ni kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) hasa lengo namba tisa la maendeleo na teknolojia kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo.
Aidha alisema ili kufanikisha hilo kumesisitizwa ushirikiano ambao ni lengo namba 17 la SDGs.
Alisema sekta binafsi ikishirikiana vyema na serikali ndiyo inayoendesha uchumi hasa katika kutoa fursa za kazi kwani asilimia 80 ya kazi kila mwaka hutolewa na sekta binafsi.
Alisema katika hotuba yake hiyo kwamba amefurahishwa na malengo ya Tanzania na nia ya Shirika hilo kuona kwamba malengo hayo kuelekea uchumi wa kati wa viwanda yanatekelezwa kwa kuangalia vionjo muhimu.
Aidha alisema kwamba wataendelea kushirikiana na sekta binafsi kupitia TSPF kuhakikisha kwamba wananchi wanashirikishwa katika malengo ya maendeleo ili kuwa na malengo endelevu na yanayozingatia mazingira.
Naye Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akizungumza katika hafla hiyo aliitaka UNIDO kusaidia kutengeneza utajiri nchini Tanzania.
Dr. Mengi alisema kwamba ziara ya kiongozi huyo imekuja wakati muafaka, wakati ambapo Tanzania inaelekeza macho yake katika uchumi wa kati na hivyo kuwa na nafasi ya kusaidia ndoto hiyo kufanikiwa.
Alisema wakati nchi nyingi zimekuwa zikipiga maendeleo, zimekuwa na msingi dhaifu wa uchumi wa viwanda kutokana na kusafirisha zaidi bidhaa ambazo hazijasindikwa au zinazotokana na uziduaji.
Alisema hali hiyo pamoja na kuipa utajiri nchi imekuwa haitawanyi utajiri uliopo.
Alisema kutokana na hali hiyo, UNIDO ina kazi kubwa ya kusaidia Tanzania kufikia lengo lake la viwanda hata kusaidia kuanzishwa kwa maeneo ya viwanda (Industrial Park).
Aidha aliishukuru UNIDO kwa kuwezesha sekta binafsi na serikali kukaa pamoja kupitia Baraza la Taifa la Biashara ambako kunakuwa na mazungumzo yenye tija kuhusiana na maendeleo ya biashara na uchumi nchini Tanzania.
Alifafanua kwamba UNIDO ina nafasi kubwa ya kuisaidia Tanzania hasa katika mipango mikakati yake kwa kuunganisha sekta binafsi na umma ili kuiharakisha Tanzania kuelekea uchumi wa kati wenye kutegemea viwanda.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda pamoja na Kimataifa Dr Augustine Mahiga, ambaye wizara yake ndiye ilimwalika Mkurugenzi mkuu huyo, pamoja na kumshukuru kwa kuitikia wito huo aliitakabkusaidia kuchagiza maendeleo ya viwanda.
Alisema kwamba viwanda vya Tanzania bado vichanga na vinahitaji kusaidiwa na kupewa nguvu ya kuendelea mbele kwani pamoja na uchanga wake mchango wake katika kuelekea uchumi wa kati ni mkubwa.
Awali kabla ya hafla ya chakula cha mchana UNIDO ilitiliana saini na serikali ya Tanzania waraka wa kusaidia kuitoa Tanzania katika mipango ya kitaifa kwenda kwenye mipango ya nchi na washirika ili kufikia uchumi wa kati.
Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO, Li Yong huku yakishuhudiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa tatu kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (wa pili kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dr Augustine Mahiga (kulia) katika chumba maalum mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na sekta binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNIDO iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akitoa utambulisho wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akisalimia wadau wa sekta binafsi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (wa pili kulia) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda nchini (UNIDO), Stephen Kargbo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodegar Tenga (kushoto) wakiwa meza kuu.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) na wadau walioshiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa UNIDO ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza ambapo alisema Tanzania inategemea kunufaika na ujio wa mgeni huyo, katika uendelezaji wa viwanda nchini wakati wa hafla hiyo ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dr Augustine Mahiga akizungumza katika hafla hiyo ambapo alisema ujio huo unatokana na mwaliko wa wizara yake uliofanywa kimkakati wakati huu ambapo serikali imedhamiria kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong akitoa salamu za UNIDO wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kulia) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda nchini (UNIDO), Stephen Kargbo wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa meza kuu wakifanya ‘Cheers’ ishara ya kutakiana afya njema na ushirikiano mwema katika maendeleo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa sekta binafsi na serikali walioshiriki kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Li Yong (hayupo pichani) ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong katika picha ya pamoja na wadau wa sekta binafsi na viongozi wa serikali mara baada ya hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda – UNIDO Bw. Li Yong wakiagana kwa furaha mara baada ya zoezi la picha ya pamoja wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Sekta Binafsi kwa Mkurugenzi Mkuu huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MAJI ZATANGAZWA TENA

March 09, 2018



Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini na ne ya Tanzania kupitia programu yake ya Uhakika wa Maji, imetangaza kuongezwa muda wa uwasilishwaji wa machapisho na programu za redio na runinga kutoka kwa waandishi na vyombo vya habari ili kuwania tuzo za uandishi wa habari za maji.

Tuzo hizi, zilizinduliwa  na Shahidi wa Maji pamoja na washirika wake kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka 2017, na kupewa jina la ‘Tuzo za Habari za Maji. Ili kushiriki katika tuzo hizi, waandishi watapaswa kuwasilisha kazi zao walizochapisha au walizorusha katika vyombo mbalimbali vya habari zinazohusu masuala mtambuka ya maji kama vile; usimamizi na utawala wa rasilimali maji, ukame, mafuriko, usambazaji maji, uchafuzi wa mito na vyanzo vya maji na kadhalika.

Vyombo vya habari pamoja na waandishi watakaoshinda tuzo hizi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, vifaa vya kuboresha ufanisi wa kazi kama vile kamera na kompyuta mpakato, kombe la tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki, hii ikiwa na lengo la kuboresha uwajibikaji miongoni wa wadau wa sekta ya habari katika kuchapa na kusambaza habari zihusuzo maji ili kuleta mabadiliko chanya, endelevu na ya kudumu katika sekta ya maji na kuleta hali ya usalama na uhakika wa maji kwa watanzania wote.

Pia, makala/kazi a za washindi   zitapata fursa ya kurushwa kwenye tovuti zetu na kusambazwa katika vyomba mbalimbali vya habari na mitandao ya kimataifa kama vile: BBC, UK Guardian, Circle of Blue and Ooska News ambayo ni nafasi na fursa ya kipekee kwa waandishi na vyombo vya habari kusomwa zaidi na kutambuliwa kwa mchango wao katika kusaidia kuboresha sekta ya maji nchini.
Tuzo hizi zimeandaliwa mahsusi kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinatoa taarifa za masuala ya maji, kuchochea mabadiliko chanya katika uwajibikaji wa wadau wa sekta ya maji.  Shahidi wa Maji na washirika wake imejikita katika kufanya kazi kubadilisha namna ambavyo rasilimali maji inasimamiwa kwa manufaa ya wananchi wote, mazingira na uchumi wa nchi. Aidha, ili kufanikisha hayo shirika hilo na washirika wake wanafanya kazi kwa namna mbalimbali kama vile; Kusaidia jamii zenye uhitaji kuweza kutambua haki na wajibu walionao katika kuwezesha utekelezaji wa sheria zilizopo na kuwezesha jamii kufuatilia utatuzi wa matatizo ya usalama wa maji katika maeneo yao kwa watoa huduma ikiwemo serikali na sekta binafsi.

Mwisho wa uwasilishaji wa kazi za waandishi na vyombo vya habari umetajwa kuwa tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2018. Kufahamu zaidi kuhusu namna ya ushiriki na kupakua chapisho la maelekezo, vigezo na masharti tafadhali tembelea http://www.shahidiwamaji.org au tuma baruapepe kwenda kennedymmari@shahidiwamaji.org

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI MKOANI GEITA WAKUMBUSHWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA WANAWAKE

March 09, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel akisisitiza umuhimu wa kuheshimu wanawake wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe Mkoani humo, Jana 8 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wanawake Wilayani Bukombe wakifatilia maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya hiyo Mkoani humo, Jana 8 Machi 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel akiongoza zoezi la ukataji keki kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe Mkoni humo, Jana 8 Machi 2018.
Mbnge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akichangia shilingi 500,000 kuunga mkono harambee iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel ambaye naye alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya jukwaa la wanawake Jimbo la Bukombe

Na Mathias Canal, Geita

Wakurugenzi wa Halamshauri za Wilaya katika Mkoa wa Geita wamekumbushwa kutekeleza wajibu wao kwa kutenga fedha asilimia 4 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake, asilimia 4 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya vijana na asilimia 2 kwa ajili ya watu kwenye ulemavu.

Wakurugenzi hao wametakiwa kuongeza kasi katika kuendelea kuchambua na kutambua vikundi vya wanawake na vijana vyenye mwelekeo wa kuzalisha Mali ghafi kwa ajili ya kulisha viwanda vidogo na vya kati ili kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoadhimishwa kimkoa katika Wilaya ya Bukombe.

Alisisitiza kuwa vikundi hivyo vinapaswa kujengewa uwezo wa kifedha, mafunzo pamoja na vifaa na hatimaye viweze kuchangia katika azma ya Serikali ya Tanzania ya uchumi wa viwanda kwani kupitia fursa hizo wanawake wengi watajiajiri na kuajiri watu wengine katika sekta isiyo rasmi.

Alisema kuwa sambamba na kuwajengea uwezo wanawake lipo jukumu la kuwalinda wanawake hao pamoja na wasichana dhidi ya vitendo vya ukatili kimwili kama vipigo, ubakwaji, ndoa za utotoni na kuwarubuni kimapanzi wabinti wadogo.

Aidha, amezitaka mamlaka zote ndani ya Mkoa wa Geita kuhakikisha zinatoa ushirikiano kwa wajumbe wa kamati zinazoundwa katika ngazi zote ili kwa pamoja kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinatokomezwa.

Katika hatua nyingine Mhe Gabriel amezitaka Halmashauri za Wilaya kushirikiana na wadau mbalimbali kutenga bajeti na kuendelea kuweka mipango shirikishi ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu na usalama wa mtoto wa kike na kulinda mustakabali wake kwa kumuwezesha kiuchumi, kielimu, kiafya na kumlinda dhidi ya vitendo vya ukatili kimwili.

Alisema kuwa kauli mbiu ya Kitaifa kwa mwaka huu ni "KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI" imeakisi dira ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa muktadha wa kuhakikisha Tanzania inakuwa ni nchi ya uchumi wa viwanda.

Alisema Serikali inatambua nguvu na ufanisi wa wanawake kwani kupitia vikundi vya kiuchumi, VICOBA, SACCOS na vikundi vya kijamii wamekuwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi; Uchakataji wa malighafi ili kuongeza thamani, biashara ndogondogo, ufugaji ushonaji nguo, kilimo cha mazao, bustani za mbogamboga na matunda na nyinginezo.

Katika maadhimisho hayo Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko amewapongeza wanawake Duniani kote kwa maadhimisho hayo ya siku muhimu kwao huku akiahidi kuongeza ushirikiano kupitia vikundi vya mbalimbali ambavyo ni msingi wa ustawi na uimara wa Jumbo hilo na Taifa kwa ujumla wake.

Sambamba na hayo pia Mhe Biteko amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa kuunga mkono harambee iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel ambaye naye alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya jukwaa la wanawake Jimbo la Bukombe.