TAIFA STARS YAPOROMOKA TENA FIFA, SASA IPO KAPU LA AKINA SOMALIA HUKO!

August 06, 2015

TANZANIA imeporomoka kwa nafasi 13 ndani ya miezi miwili hadi ya 140 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Tanzania iliporomoja hadi nafasi ya 139 mwezi uliopita na mwezi huu imeporomoka kwa nafasi moja zaidi katika viwango vya FIFA, maana yake kidogo mambo yameanza kunyooka.
Juni mwaka huu baada ya matokeo mabaya mfululizo kuanzia kwenye Kombe la COSAFA ambako ilifungwa mechi zote tatu za Kundi B, mechi ya kwanza kufuzu AFCON ilipochapwa 3-0 na Misri kabla ya kutolewa kwa mabao 4-1 na Uganda kufuzu CHAN 2016, Tanzania iliporomoka kwa nafasi 12.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kushoto) na Msaidizi wake, Hemed Morocco kulia

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likamfukuza kocha Mholanzi, Mart Nooij baada ya matokeo hayo na nafasi yake sasa anakaimu, Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ambaye amepewa miezi mitatu ya majaribio.
Mkwasa alianza vizuri kwa sare ya ugenini ya 1-1 dhidi ya Uganda kufuzu CHAN na wakati wowote atataja kikosi cha kuingia kwenye kambi ya maandalizi ya mchezo wa pili kufuzu AFCON dhidi ya Nigeria mwezi ujao.
Kwa Afrika Mashariki na Kati, Uganda inaoongoza ikiwa nafasi ya 74 duniani, ikifuatiwa na Sudan 87, Rwanda 91, Ethiopia 99, Kenya 116, Burundi 132, Tanzania 140, Sudan Kusini 195, Eritrea 203, Somalia 204 na Djibouti 206.  
Kwa Afrika, Algeria bado inaongoza ikiwa nafasi ya 19 kwenye viwango vya dunia ikifuatiwa na Ivory Coast iliyo nafasi ya 20, Ghana 27, Tunisia 34 na Senegal 39.
Argentina inashika namba moja kwa ubora wa soka duniani ikifuatiwa na Ubelgiji, Ujerumani, Colombia na Brazil katika tano bora.

RAIS KIKWETE AAGA RASMI IDARA YA MAHAKAMA, YAMPA TUZO KWA MAKUBWA ALIYOFANYA KATIKA MIAKA 10

August 06, 2015

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutokana na mambo makubwa liyoifanyia idara hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi. PICHA ZOTE NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha  tuzo maalumu aliyoipokea kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Sehemu ya wastaafu na viongozi wa taasisi wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
MC wa shughuli  katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Meza Kuu katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete akisalimiana na Majaji wa  Mahakama Kuu  jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Kikwete katika picha ya pamoja Majaji wa  Mahakama Kuu  ya Rufani jijini  Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
 Rais Kikwete katika picha ya Mwanasheria Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Mahahama, Rais wa Tanganyika Law Society jijini  Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AJIUZULU NYAZIFA ZOTE CUF NA UKAWA, ABAKI MWANACHAMA WA KAWAIDA

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA AJIUZULU NYAZIFA ZOTE CUF NA UKAWA, ABAKI MWANACHAMA WA KAWAIDA

August 06, 2015

????????????????????????????????????
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock leo jijini Dar es salaam wakati akitangaza kujuuzulu nyazifa zake zote katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kutokana kile alichokiita dhamira inamsuta.(NA KIKOSKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akionyesha rasimu ya katiba iliyoandaliwa na tume ya katiba mpya iliyokuwa ikipendekezwa  iliyoandaliwa na Jaji Joseph Warioba ambayo anadai imefinyangwa.
……………………………………………………………………………..
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama hicho akisema  dhamira inamsuta. 
Profesa Ibrahim Lipumba Amezungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo, Profesa Lipumba amesema  amejitahidi kujenga chama hicho hasa Tanzania bara, amejenga umoja wa Wazanzibari hivyo anajiuzulu kulinda heshima yake.
Amesema ameikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu, barua yake ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yake imelipiwa mpaka mwaka 2020.
Ameeleza sababu  za kujiuzulu ni Umoja wa huo wa UKAWA kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la katiba.
Profesa Lipumba amekiri kushiriki katika vikao mbalimbali vya Ukawa mpaka hapa walipofikia . lakini akasema . Nafsi yangu inanisuta kuwa katika maamuzi yetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa za utu, uadilifu, uzalendo, uwajibikaji,, umoja,na uwazi .

MASHIRIKA MATANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA(FOS) YAUNGANA KWA PAMOJA KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

August 06, 2015


 
Wasemaji kutoka Mashirika Matano Kutoka kushoto ni Msemaji kutoka LHRC,OXFAM, Restless Development, BBC na VSO
  Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Oxfam Jane Foster ambao pia ndio waandaaji wa Mkutano huu na waandashi wa Habari akieleza kwa kina nia ya Mkutano huo ambao lengo kuu ni kuzungumzia maswala ya Uchaguzi kuwa kila mtu anahaki ya kupiga kura.
 
Hellen Kijo Bisimba ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa
kituo cha sheria na haki  za binadamu
(LHRC) (Kushoto) akiongea jinsi walivyo endesha zoezi zima la kusimamia uandikishaji wa Daftari la uandikishaji wa wapigakura la kudumu BVR na ushiriki wao kwa ujumla.

DIRISHA LA USAJILI SASA KUFUNGWA AGOSTI 20

August 06, 2015


MKWASA ATANGAZA 29 STARS
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini siku ya Jumapili tarehe 9, Agosti katika hoteli ya Tansoma iliyopoe eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.

Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 nchini Uturuki.

Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.

Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).

Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).

Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).

Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza)


DIRISHA LA USAJILI SASA KUFUNGWA AGOSTI 20
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) mpaka Agosti 20 mwaka huu.

Awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo Agosti 6, na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20, 2015.

Tarehe 21- 28 Agosti, 2015 ni kipindi cha pingamizi, tarehe 29-30 Agosti 2015, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.

Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kiamataifa (FIFA –TMS) litafungwa tarehe 06 Septemba, 2015 na Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.

TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKAMILISHA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU MKOA WA DAR ES SALAAM KWA MAFANIKIO MAKUBWA

August 06, 2015
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kukamilika kwa zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu kwa kutumia mfumo wa BVR Mkoani Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani zoezi hilio limefanikiwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizojitokeza.