MRADI WA USANIFU WA BWAWA LA FARKWA WASAINIWA ,LITAJAZA MAJI LITA MILIONI 440

October 23, 2023

 Wizara ya Maji imesaini Mkataba wa mwaka mmoja na  Kampuni ya SU-YAPI Engineering Consulting Inc. kwa ajili ya kufanya kazi ya usanifu wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa litakalojengwa katika Wilaya ya Chemba, ambalo litanufanisha wakazi wa Wilaya za Chemba, Chamwino,Bahi na Jiji la Dodoma.

Mkataba umesainiwa leo tarehe 23 Oktoba,  ikiwa ni awamu ya kwanza, mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 312 kwa ujenzi wa Bwawa lenye ujazo wa lita za maji milioni  440.

Waziri wa Maji  Mhe. Jumaa  Aweso (Mb) ameshuhudia Hafla hiyo na amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 312 ili kuondosha tatizo la maji katika  Wilaya nne za Mkoa wa Dodoma ili wakazi wake wapate majisafi, salama na yenye kutosheleza.

Mhe. Aweso amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Chemba kuwa, Wizara ya Maji itatekeleza mradi huo kwa kuwashirikisha wananchi ili wawe sehemu ya mradi na ujenzi ukamilike kwa wakati kama ilivyopangwa na Serikali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira,  Mhe. Jackson Kiswaga,  Mbunge wa Jimbo la Kalenga, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kujitoa na kupeleka fedha  kiasi cha shilingi Bilioni 312 kwa ajili ya ujenzi wa  Awamu ya kwanza ya Bwawa la Farkwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule akiongea katika Hafla hiyo amewaomba wananchi wa Wilaya ya Chemba kuwa na imani na serikali yao kwa kuwa tatizo la upatikanaji wa maji linaisha, kwani Serikali imedhamiria kumaliza kabisa changamoto ya uhaba wa maji kwa wakazi wa Wilaya ya Chemba.

Imbeju ya Benki ya CRDB yatoa mtaji wezeshi shilingi bilioni moja mpaka sasa

October 23, 2023

Newala. Tarehe 22 Oktoba 2023: Katika kuwafikia na kuwanufaisha zaidi wanawake wajasiriamali, CRDB Bank Foundation imeshiriki Mkutano Mkuu wa nne wa Mwaka wa BUT Vicoba uliowakutanisha zaidi wanachama 3,500 kutoka vikundi 318 vilivyoshiriki na kutoa mtaji wezeshi wa fedha taslimu na pikipiki. 

Akizungumza na wanachama hao, Mkurugenzi Mtandaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa kwa hamasa aliyoiona ameamini kuwa kweli BUTA Vicoba ni taasisi kubwa yenye uwakilishi nchi nzima jambo linaloleta matumaini ya kulikomboa kiuchumi kundi hilo.

Tully amesema ni jambo la kujivunia kuona wanawake wanakusanyika kwa pamoja kupanga maendeleo ya uchumi wao binafsi na wa familia zao jambo litakalowaongezea ushiriki wao kwenye uchumi wa taifa letu.
“Leo tunakabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 pamoja na pikipiki 5 zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa wana BUTA Vicoba. Huu ni mtaji wezeshi kwa baadhi yenu waliokidhi vigezo. Lengo la kuanzishwa kwa CDRB Bank Foundation ni kuwahudumia Watanzania hasa makundi yasiyopewa kipaumbele na taasisi nyingi za fedha nchini ambayo ni wanawake na vijana. Mliopata mtaji huu wezeshi leo mnaungana na wenzenu ambao tayari tumeshatoa shilingi bilioni 1 kwao,” amesema Tully.

CRDB Bank Foudation ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2022 kwa lengo mahsusi la kuwawezesha vijana na wanawake. Kwa sasa taasisi hii inatekeleza Programu ya Imbeju iliyotengewa bajeti ya kuanzia kiasi cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya makundi hayo.

Ili kuyafikia makundi hayo kirahisi, inashirikiana na wadau muhimu wenye mtandao mpana. Kwa vijana wenye bunifu za kiteknolojia (startups), taasisi inashirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Tume ya TEHAMA (ICTC) na kwa wanawake wajasiriamali kuna BUTA Vicoba, Shirika la Care International, Citizen Foundation na wengine.
Tangu Programu ya Imbeju ilipozinduliwa Machi 12 mwaka huu, vijana 709 walijitokeza kutuma maombi ambayo yalipochujwa, miradi 196 ilikubaliwa na kuingia hatua ya mafunzo ya kujengewa uwezo wa kuendesha biashara kwa viwango vinavyofaa ndani ya nchi na kimataifa. 

Bunifu 51 kati ya 196 zilikidhi vigezo vya kuendelea na tayari baadhi ya vijana wakundi hili wameanza kupewa mtaji wezeshi ili kukuza miradi yao.

Kuhusu mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya fedha, Tully amesema makundi yote mawili yanapata na mpaka sasa tayari zaidi ya wajasiriamali 100,000 wamefunzwa; wanawake kwa wanaume.

“Tunapowawezesha wanawake na vijana, naomba nieleweke kuwa tunaangazia wanawake na vijana waliopo kwenye vikundi, vile vilivyosajiliwa na ambavyo vimefanya kazi walau kwa miaka mitatu mpaka sasa na lazima viingie mkataba wa makubaliano (Memorandum of Understanding) na  CRDB Bank Foundation na kikundi kiwe na akaunti Benki ya CRDB. 
 
Vikundi ambavyo havijakidhi vigezo hivi pia vinakaribishwa kujiunga kwani watapewa mafunzo ambayo yatawakuza na kuwawezesha kunufaika na Programu ya Imbeju huko mbeleni,” amesema Tully. 

Tully pia aliitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa BUTA Vicoba, Semeni Gama kwa jinsi anavyojiyoa kuhakikisha wananchi wanachakarika nchini ili kujikwamua kiuchumi.

“Katika safari hii ya mafanikio tunao watu vinara waliotushika mkono sisi CRDB Bank Foundation na Programu ya Imbeju. Vinara hawa wanaongozwa na Mama Semeni. Sisi tunamwita mwamba kwani amekuwa na mchango mkubwa kwenye idadi ya wanawake tuliowapa mafunzo na wale waliofungua Akaunti ya Imbeju. 
 
CRDB Bank Foundation tunampongeza Mama Semeni kwa jinsi anavyojitoa kwa ajili ya maendeleo na mafanikio ya wanawake wenzake. Tukiwa na watu wengi kama hawa wasiotulia mpaka waone wenzao nao wanachakarika, nina uhakika tutafanikiwa kukabiliana na umasikini unaozisumbua kaya zetu nyingi hapa nchini,” amesema Tully.

Kwa upande wake, Semeni ameishukuru Benki ya CRDB kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation kwa jinsi ilivyojitoa kuwawezesha wanawake ambao wengi hawapewi nafasi kwenye taasisi nyingi za fedha kutokana na kutokidhi vigezo vilivyowekwa.

“Ili kupata mkopo kwenye taasisi nyingi za fedha nchini, mteja anahitaji kuwa na dhamana lakini wanawake wengi hawamiliki ardhi kutokana na mila zilizopo maeneo mengi. Programu ya Imbeju ambayo imeondoa kigezo hicho inawafaa wanawake wengi watakaoweza kuanzisha biashara zao hivyo kujiingizia kipato cha uhakika,” amesema Semeni.

TUONGEZE KASI YA UTOAJI ELIMU NA UPIMAJI WA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

October 23, 2023

 Na. WAF - Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanlaus Nyongo ameishauri Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu (TB) na Ukoma kuongeza juhudi za utolewaji wa elimu kwa jamii na upimaji wa TB.

Mhe. Nyongo amesema hayo leo Oktoba 23, 2023 baada ya kupokea taarifa ya mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu pamoja na taarifa ya huduma za mama na mtoto kutoka Wizara ya Afya iliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma.

“Kwanza niwapongeze sana Wizara ya Afya mnafanya kazi nzuri ya kuwatumikia Watanzania lakini pia niwaombe kupitia mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma izidi kutoa elimu kwa jamii na upimaji hasa katika kampeni kubwa kubwa ili kuwagundua wagonjwa mapema na kuwaanzishia matibabu kwa lengo la kupunguza zaidi maambukizi”. Amesema Mhe. Nyongo

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema elimu ikiendelea kutolewa na jamii ikaelewa vizuri itasaidia kupunguza maambukizi pamoja na vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu nchini.

Amesema, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2022 Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuwaibua wagonjwa wa TB na kuwapatia matibabu kutoka asilimia 37 hadi asilimia 65.

Aidha, Waziri Ummy amesema lengo la Shirika la Afya Duniani ni kuibua wagonjwa wa Kifua Kikuu ambapo Tanzania imefanikiwa kwa 65% lakini pia kupunguza vifo vitikanavyo na ugonjwa huo, Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Ili kuzidi kufanikiwa hilo kwa Tanzania Waziri Ummy ameitaka jamii iache tabia ya kuwaficha wagonjwa wa TB bali ichukue hatua za kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma za Afya mapema ikiwa watagundua dalili za ugonjwa huo.

“Familia ikiwa na mgonjwa wa Kifua Kikuu inatakiwa kutoa taarifa mapema ili isaidiwe haraka na Serikali itimize matakwa ya WHO ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo pamoja na vifo”. Amesema Waziri Ummy

Pia, Waziri Ummy amesema watu 70 hufariki kila siku kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini Tanzania hali ambayo imekuwa ikishusha nguvu kazi katika jamii pamoja na uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Ikitokea ajali ikaua watu 70, Watanzania watashtuka sana na kila sehemu tutaona pole zikitolewa lakini tufahamu kuwa watu 70 hufariki kila siku kutokana na ugonjwa wa TB lakini kwa sababu hatuwaoni kutokana wanakufa sehemu mbalimbali nchini nzima ndio maana hatuchukulii maanani”. Amesema Waziri Ummy

SPIKA DKT. TULIA AKIFANYA KAMPENI ZA URAIS WA IPU NCHINI ANGOLA

October 23, 2023

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifurahia jambo na Spika wa Seychelles Mhe. Roger Mancienne (katikati) pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mussa Zungu walipokutana katika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Bunge la Angola uliopo Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 23 Oktoba, 2023. Dkt. Tulia anagombea nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 nchini humo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati), akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Namibia Mhe. Peter Katjavivi (kushoto) pamoja na Spika wa Bunge la Zambia Mhe. Nelly Mutti (kulia) wakati walipokutana katika Ofisi ndogo za Bunge la Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ukiendelea nchini humo leo tarehe 23 Oktoba, 2023

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Oktoba, 2023 akizungumza na Wajumbe wa kundi la Latini na Amerika kusini katika ukumbi mdogo wa Bunge la Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa IPU akiwaomba wampigie kura katika Uchaguzi wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 nchini humo.

UWEKAJI WA JIME LA UZINDUZI HOSPITALI YA WILAYA KIVUNGE MKOA KASKAZINI UNGUJA.

October 23, 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ( wa tatu kulia) pamoja na Waziri wa Afya (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakifungua pazia kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la Uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja.[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Jengo jipya la Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja limefunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mfulizo wa ziara zake katika Mikoa ya Unguja.[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ( wa pili kulia) akiwasalimia Viongozi mbali mbali alipowasili katika uwekaji wa Jiwe la Uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud.[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ( katikati) akikata utepe kuzindua Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,Viongozi mbali mbali wakishuhudia uzinduzi huo leo akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja(kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanzania wa Saifee Hospitali Bw.Murtaza Ali Bhai.[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ( katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanzania wa Saifee Hospitali Bw.Murtaza Ali Bhai (kushoto) wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,mara baada ya uzinduzi rasmi leo ambapo viongozi Viongozi mbali mbali walishuhudia uzinduzi huo, akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja .[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Dr.Navil Aggarwal wa Saifee Hospitali Bw.Murtaza Ali Bhai (kushoto) wakati alipotembelea Chumba cha huduma za X Ray Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,mara baada ya uzinduzi rasmi leo ambapo viongozi Viongozi mbali mbali walishuhudia uzinduzi huo, akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja .[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Baadhi ya Vifaa vipya vya Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,ambayo leo imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi. [Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dr. Husein Hassanali Mtaalam wa Upasuaji wa Mishipa ya Moyo katika Saifee Hospital Zanzibar inayoendesha kutoa huduma za Afya kwa Hospitali za Wilaya Zanzibar (katikati) wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,mara baada ya uzinduzi rasmi leo akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja (kushoto) Mkurugenzi na Daktari wa masuala ya Familia Dr.Murtaza Haidarbhai, .[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiwasalimia wananchi waliofika kupata matibabu kwa maradhi mbali mbali wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati alipotembelea vyumba mbali mbali katika Hospitali hiyo akiwa katika ziara kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja .[Picha na Ikulu] 23/10/2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo akiwa katika ziara zake kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mikoa ya Unguja(kushoto) Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.[Picha na Ikulu] 23/10/2023.

BARAZA LA MANISPAA CHAKECHAKE LAAGIZWA KUSIMAMIA VYEMA VYANZO VYA UKUSANYAJI WA MAPATO

October 23, 2023

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Baraza la Mji la Chake Chake Pemba ambalo limepandishwa hadhi na kuwa Baraza la Manispaa Chake Chake kuhakikisha wanasimamia vyema vyanzo na ukusanyaji mzuri wa mapato ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba katika Viwanja vya Tibirinzi Pemba Mhe. Hemed ameipongeza Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi kubwa ya kuimarisha utendaji kazi katika Serikali za Mitaa na kuridhia mapendekezo ya kulipandisha hadhi Baraza la Mji Chake Chake na kuwa Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba kwa kuzingatia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Amesema kuwa matarajio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Baraza hilo jipya litahakikisha huduma za kijamii zinakuwa bora na za ufanisi zaidi ambazo zitawaondolea usumbufu wananchi kwa kupata huduma hizo pamoja na kuandaa mipango bora ya kimkakati itakayotoa tija kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.

Aidha Mhe. Hemed amewasisitiza Watendaji wa Baraza la Manispaa Chake Chake kusimamia vyema makusanyo kwa kutumia mifumo ya risiti za kielektroniki, kuwa na matumizi sahihi ya rasilimali watu na rasilimali fedha, kuibua Miradi mbali mbali ya maendeleo, kuimrisha usafi wa mazingira na kusimamia Amani na mshikamano katika jamii.

Amelitaka Baraza la Manispaa Chake Chake Pemba na watendaji wake kukemea vitendo vya rushwa na utumiaji mzuri wa rasilimali za Serikali, kuacha ,uhali na kutanguliza maslahi ya Taifa ili kuwa Baraza la mfano litakalotoa hamasa wa ushindani wa kimaendeleo kwa kuongeza mapato Serikalini na kuzitumia fursa mbali mbali zinazopatikana katika Wilaya hiyo.

Ameutaka Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba kuwa na mipango shirikishi jamii kwa kuzishirikisha Kamati za mashauriano za Shehia na Mabaraza ya wadi, Kamati za Wilaya na Mikoa ili kupata mazingatio na ushauri katika maendeleo.

Sambamba hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa endapo Mabaraza ya Manispaa na Miji Zanzibar yatatekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa yataleta matokeo mazuri yenye tija na kuepusha Migogoro katika jamii.

Pamoja na hayo amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuridhia Baraza la Mji la Chake Chake Chake kupandishwa hadhi na kuwa Baraza la Manispaa kumetokana na miongozo na maelekezo yake kwa watendaji wa Baraza hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed ameishukuru Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuridhia kulipandisha hadhi Baraza la Manispaa Chake Chake ni kurahisisha kasi ya upatikanaji wa maendeleo na ukuwaji wa uchumi ndani ya Mkoa huo.

Aidha amewataka watendaji wa Baraza la Manispaa Chake Chake kwa kushirikiana na wananchi kuongeza kasi katika utendaji wao wa kazi, kuwa wabunifu wa miradi mbali mbali itakayowaongezea kipato kitakachosaidia kukuza uchumi hasa katika Mkoa huo.

Amesema mashirikiano ndio silaha katika kutimiza majukumu yetu ya kazi na kuwataka kuachana na kufanya kazi kwa utashi binafsi na kuelekeza nguvu zao katika kulitumikia Taifa.

Sambamba na hayo Mhe. Masoud amemuhakikisha makamu wa pili wa rais wa Zanzibar wizara itahakikisha inafata maelekezo na maagizo yote yanayotolewa na viongozi wakuu wa nchi katika kuwaleetea maendeleo wananchi wote pamoja na kuifata ilani ya chama cha mapinduzi ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mattar Zahor Massoud amesema endapo viongozi watafanya kazi kwa pamoja hasa katika shuhuli za maendeleo na kuwataka kuachana na tabia ya kukwamisha na kuzorotesha Miradi mbali mbali ya maendeleo kwani kufanya hivyo ni kuikwamisha Serikali kwa ujumla.

Mhe. Mattar ameahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi na wananchi kwa kufuata miongozo ya Nchi na kamwe hatokatishwa tamaa na wachache wasioitakia mema nchi yetu na amesema jitihada pekee ndio zitakazolipandisha zaidi Baraza hilo la Manispaa kuwa Jiji muda mfupi ujao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa chake chake Ndugu Maulid Mwalim Ali amesema kupandisha hadhi kwa baraza la manispaa la chake chake kutawajengea ari na morali wafanyakazi katika kufanya kazi kwa umakini na weledi wa hali ya juuu katika kufanikisha malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Amesema Baraza la Manispaa Chake Chake litahakikisha linaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kuimarisha usafi wa mazingira na kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo pamoja na kuwapatia elimu zaidi wafanyakazi ili kuleta ufanisi nzuri wa kazi.

Aidha amesema Baraza la Manispaa Chake chake litafanyakazi kwa kasi na ufanisi zaidi ili kuhakikisha linapanda hadhi Zaidi kwa maslahi ya wanachi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

WAFANYABIASHARA WALIOWEZESHWA NA BENKI YA NBC KWENDA CHINI WAREJEA NCHINI, WAELEZA MATUMAINI NA FURSA MPYA

October 23, 2023

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini waliopata fursa ya kwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Trade Fair kwa uratibu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia klabu yake ya Biashara ijulikanayo kama NBC B-Club wamerejea nchini huku wakielezea mafanikio, matumaini na fursa mbalimbali walizozipa kupitia safari hiyo.

Sambamba na Maonesho hayo ya Canton Trade Fair yaliyofanyika hivi karibuni Guangzhou, China, wafanyabiashara hao pia walipata fursa ya kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza teknolojia mpya sambamba na kutafuta muunganiko mpya wa kibishara na masoko baina yao na wafanyabiashara kutoka China.

Aidha, wakiwa njiani kuelekea na kurudi katika safari hiyo wafanyabiashara hao pia walipata wasaa wa kutembelea nchi ya Misri na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii na historia ya taifa hilo.

Akizungumza mara tu baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam mapema hii leo, Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje alisema kupitia safari hiyo ya siku 10 wafanyabiashara hao walipata fursa ya kujifunza mambo mengi ikiwemo fursa za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kibiashara huku pia wakipata fursa ya kutembelea viwanda na masoko mbalimbali nchini.

“Zaidi, tukiwa China, tulipata fursa ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa, wamiliki wa viwanda vikubwa na vidogo. Pia wafanyabiashara waliweza kujifunza teknolojia mpya sambamba na kupata muunganiko mpya wa kibiashara na wenzao kutoka China. Kuna ambao walihitaji mashine na zana mbalimbali kwa ajili ya kazi zao wamepata na pia wapo waliopata washirika wapya kibiashara. Ni matumaini yetu kwamba hivi karibuni tutashuhudia uwekezaji wao mpya kupitia viwanda,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Bitababaje wakiwa Guangzhou, China walipata fursa ya kukutana na Balozi mdogo wa Tanzania nchini China ambae pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo muhimu aliwasisitiza Watanzania kutumia vema ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili kwa kuwa na maono ya kuanzisha viwanda nchini Tanzania badala ya kutegemea tu kuagiza bidhaa kutoka China.

“Kwa mujibu wa Mheshimiwa Balozi Mdogo ni kwamba China kuna teknolojia za ukubwa tofauti hivyo Watanzania wana fursa ya kuangalia teknolojia wanazozimudu ikiwemo teknolojia rahisi itakayowawezesha kuzalisha baadhi ya bidhaa ndogo ndogo hapa hapa nchini ili kupunguza idadi ya bidhaa zinazoingizwa kutoka China.’’ Alinukuu Bitababaje huku akibainisha kuwa benki hiyo ipo tayari kuwasaidia wafanyabiashara hao kwa kuwapatia mitaji itakayowasaidia kuyatimiza kwa vitendo yale yote waliyojifunza nchini China.

‘’Niwaombe sana wafanyabiashara waendelee kuchangamkia fursa ya safari hizi ambazo zinaendelea kuja kupitia uratibu wa NBC B-Club ambapo tunatarajia kuwa na safari nyingine za China mwezi Aprili na Oktoba hapo mwakani. Tofauti na China pia tutakuwa na safari za Ulaya, Asia na baadhi ya nchi za Afrika ambazo tunaushirikiano mkubwa wa kibiashara,’’ aliongeza.

Wakizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wengine waliopata fursa hiyo Mhandisi Renatusi Porini na Bi Sarah Munuo pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa uratibu wa safari hiyo, walisema wamejifunza mambo mengi ikiwemo pia fursa mpya nyingi za kimasoko na mahusiano ya biashara hatua ambayo imewajenga zaidi kibiashara.

“Kimsigi tulivyorudi leo sio kama tulivyoenda! Tukiwa China na Misri tumetembelea vmaeneo mbalimbali vikiwemo viwanda na pia tumeongeza mawasiliano zaidi na wenzetu wa huko China. Binafsi nikiwa kama mhandisi nimepata ‘materials’ mpya na teknolojia mpya ya ujenzi hatua ambayo ni muhimu sana kwa biashara yangu.

Tunawashukuru sana NBC kwa hili hasa tukizingatia kwamba pamoja na hatua hii wametuthibitishia dhamira yao ya dhati kabisa ya kutupatia mikopo ili kukamilisha kwa vitendo haya tuliyojifunza huku,’’ alishukuru Mhandisi Porini.

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje (wa tatu kulia) akiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam alioporejea nchini sambamba na baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini waliopata fursa ya kwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Trade Fair kwa uratibu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia klabu yake ya Biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Wafanyabiashara hao waliwasili jijini Dar es Salaam leo alfajiri baada ya kukamilisha safari hiyo ya siku 10.

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje (wa pili kulia) akiwatakia heri mara baada ya kurejea nchini baadhi ya wafanyabiashara waliopata fursa ya kwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Trade Fair kwa uratibu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia klabu yake ya Biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Wafanyabiashara hao waliwasili jijini Dar es Salaam leo alfajiri baada ya kukamilisha safari hiyo ya siku 10.

Sambamba na Maonesho hayo ya Canton Trade Fair yaliyofanyika hivi karibuni Guangzhou, China, wafanyabiashara hao pia walipata fursa ya kukutana na wasafirishaji wa mizigo kutoka China, wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza teknolojia mpya sambamba na kutafuta muunganiko mpya wa kibishara na masoko baina yao na wafanyabiashara kutoka China

Aidha, wakiwa njiani kuelekea na kurudi katika safari hiyo wafanyabiashara hao pia walipata wasaa wa kutembelea nchi ya Misri na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii na historia ya taifa hilo.

Imbeju Ya Benki Ya CRDB Yatoa Mtaji Wezeshi Shilingi Bilioni Moja Mpaka Sasa