Edward Lowassa aungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka

April 04, 2015

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa ameungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front la Dar es Salaam leo.
Ibada ikiendelea.
Sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika leo.
 
Igizo la Yesu likiongozwa na Bw. Moses Kombe alivyokuwa na wanafunzi wake kabla ya kuteswa hadi kutungikwa msalabani, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam leo.
Mh. Edward Lowassa akifatilia igizo la mateso ya Yesu, lililoigizwa na Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Igizo likiendelea.
Mmoja wa watoto waliokuwepo Kanisani hapo akiangalia Igizo hilo.
Mmoja wa Waigizaji hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipitia vifungu vya Biblia wakati Igizo la Yesu likiendelea.
Yesu akipelekwa kwa Pilato.
Vijana hao wakiigiza pale Yesu alipofikiswa kwa Pilato kuhukumiwa, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Azania Front Dar es Salaam
Huzuni ilitawala wakati wa Igizo hilo.
Yesu akiwa amebebeshwa Msalaba katika Igizo hilo.
Muumini wa Kikristo, Moses Kombe akitungikwa msalabani kama Yesu katika igizo lililofanywa na Vijana wa Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Kuna waliomlilia na Wengine kufurahia.
PRESIDENT KIKWETE ADRESSES WORLD AFFAIRS COUNCIL, MEETS WITH TANZANIANS LIVING IN SEATTLE

PRESIDENT KIKWETE ADRESSES WORLD AFFAIRS COUNCIL, MEETS WITH TANZANIANS LIVING IN SEATTLE

April 04, 2015

jk 1
President Jakaya Mrisho Kikwete addresses a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk 2
President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Carmen Hummel who had asked him a question on how his childhood was during a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk3
President Jakaya Mrisho Kikwete is mobbed by excited stidents after addressing a meeting of the World  Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
jk4 jk5 jk6
President Jakaya Mrisho Kikwete greets members of the Tanzanian Community based in Seattle  during his one-day visit of the city on Thursday April 2, 2015
STATE HOUSE PHOTOS
AFYA YA GWAJIMA UTATA

AFYA YA GWAJIMA UTATA

April 04, 2015

gwajima2
KUDHOOFU kwa afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye wiki moja iliyopita alizimia wakati akihojiwa na Polisi, kumezua utata.
Wakati baadhi wakijenga hisia kwamba hatua hiyo huenda ikawa ina mkono wa Mungu, au imetokana na kuvurugika kwa mfumo wa kawaida wa ufahamu, hata hivyo maofisa wa Jeshi la Polisi wa Kituo Kikuu Kanda Maalumu ya Dar es Salaam waliofika kumuhoji Gwajima ambaye aliwasili kituoni hapo akiwa mzima wa afya, wamenyooshewa kidole.

MSIWARUHUSU WATOTO KWENDA KWENYE FUKWE ZA BAHARI BILA WAANGALIZI”

April 04, 2015
TANGA.
 JESHI la Polisi Mkoani Tanga limetoa tahadhari kwa wazazi na walezi mkoani hapa kutowaruhusu watoto wao bila kuwepo uangalizi kwenda kwenya fukwe za bahari nyakati za sikukuu ya Pasaka kwani wanaweza kuogelea na kupoteza maisha.

Tahadhari hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea sikuuu hiyo ambapo alisema kuwa katika jambo hilo wazazi wanapaswa kuwa makini sana kwani furaha inaweza kugeuka kilio.

Alisema kuwa licha ya hivyo wamiliki wa kumbi mbalimbali za stahere mkoani hapa kuacha kujaza watoto wengi mahali ambapo hakuna hewa kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea matatizo kwao.

Aidha alisema kuelekea siku hiyo Jeshi hilo limejipanga vilivyo kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa pamoja na kuwataka wananchi kutoa taarifa watakapobaini kuwepo viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

  “Jeshi letu limejipanga na kujithatiti vilivyo kuhakikisha wananchi katika maeneo mbalimbali wanasheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu kwa kuimarisha ulinzi “Alisema Kaimu Kamanda Ndaki.

Hata hivyo aliwataka wananchi kutoa taarifa za uhalifu endapo zitakuwa zikijitokeza kwenye maeneo yao ili kuweza kuyapatia ufumbuzi haraka pamoja na kuwa waangalifu wanapotoka kwenye nyumba zao kwenda kwenye ibada za usiku.

Alisema wananchi watakaokwenda kwenye ibada za usiku wahakikishe wanakuwepo waangalizi kwenye nyumba zao ili kuendelea kuangalia hali ya usalama mpaka watakaporudi.

PICHA ZA TUKIO LA MPASUAJI MAWE KATIKA MIAMBA ILIYOPO KITALU ZED B MINING KUFARIKI DUNIA JANA. KWENYE KITALU HICHO

April 04, 2015
 Wananchi kutoka maeneo mbalimbali
kwenye jijini Tanga wakiupokea mwili wa mpasuaji mawe katika miamba iliyopo kitalu Zed B Mining yaliyopo mtaa kongwa kata ya Mzizima Tarafa ya Chumbageni Jijini Tanga,Justin Masaka baada ya kuangukiwa na mawe ya miamba hiyo wakati akiendelea na shughuli zake jana,



Wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali jijini Tanga wakifuatilia tukio hilo la kutolewa kwa mwili wa mpasuaji mawe katika miamba iliyopo kitalu Zed B Mining yaliyopo mtaa kongwa kata ya Mzizima Tarafa ya Chumbageni Jijini Tanga Justin
Masaka baada ya kuangukiwa na mawe ya miamba hiyo wakati akiendelea nashughuli zake jana,