KANDA YA ZIWA WAENDELEA KUJISHINDIA ZAWADI ZA 'MCHONGO CHINI YA KIZIBO' YA COCA-COLA

October 29, 2017
Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Washindi wa Mchongo chini ya kizibo ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi na zawadi zao, wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Cocacola mkoani Mwanza Samwel Makenge,(kushoto) akimkabidhi pikipiki Marysiana Kijita, baada ya kushinda promosheni ya ‘ Mchongo chini ya kizibo’ wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika jijini Mwanza. 

Wakazi wa kanda ya ziwa na mikoa jirani mambo yanazidi kuwanyokea kutokana na kuendelea kujishindia zawadi za pikipiki,Televisheni bapa za kisasa ,fedha taslimu na zawadi nyinginezo kupitia promosheni ya Coca-Cola inayoendelea ijulikanayo kama ‘Mchongo chini ya kizibo’ Wiki iliyopita washindi wa pikipiki 6 walikabidhiwa zawadi zao sambamba na washindi 2 wa televisheni wakiwemo wengine wengi waliojishindia fedha taslimu na t-shirt kutoka kampuni ya Coca-Cola. 

Waliokabidhiwa pikipiki ni Derick Magnus (Nyakato), Ismail Hamis (Magu), Joseph Mafuru (Mahina Mwanza) Pendo (Bariadi Mkoani Simiyu), Daniel Keheta (Mkolani),na Marysiana Kijita (Hungumalwa).Waliokabidhiwa televisheni ni Rhoda Joel, Marco Kitula. 

Wakiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi hao waliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kubuni promosheni zenye lengo la kuinua maisha ya wateja wake “Nimefurahi kujishindia pikipiki kutoka Coca-Cola nitaitumia katika shughuli za biashara ili kuongeza kipato cha familia yangu”.

Alisema Marysiana Kijita,kwa furaha. Derick Magnus alisema kuwa amefurahi kujishindia zawadi ya pikipiki kupitia promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’na kudai kuwa itamrahisishia usafiri wake binafsi na familia yake “Chombo hiki kitarahisisha usafari katika shughuli zangu za ujasiriamali sambamba na usafiri kwa familia yangu”

.Alisema. Mmoja wa washindi wa televisheni,Marco Kitula ,alisema kuwa zawadi aliyojishindia imekuja kwa wakati mwafaka ambapo ataweza kuona matukio mengi na michezo mbalimbali kupitia televisheni yake ya kisasa aliyojishindia “Napenda sana kuangalia matukio kupitia luninga na michezo mbalimbali nitaburudika vizuri na familia na marafiki”.

Alisema kwa furaha. Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika kiwanda cha Nyanza mwishoni mwa wiki ,Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Japhet Kisusi,amesema kuwa promosheni hii ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya wateja wanaotumia bidhaa za kampuni inaendelea vizuri na washindi wanaendelea kukabidhiwa zawadi zao. 

Aliwataka wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa kuendelea kuchangamkia promosheni kupitia kunywa soda za kampuni ya Coca-Cola na kuongeza kuwa zawadi bado ziko nyingi.

”Mchongo Chini ya Kizibo inawezesha kujishindia zawadi nono za fedha taslimu,bodaboda,televisheni aina ya SONY LED,kofia na soda za bure. Alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda.

 Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’. 

 -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability'' Quick Reply To: Cathbert Kajuna

CCM YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UDIWANI KIJICHI LEO, KUSILAWE ASEMA CCM ITASHINDA UDIWANI KATA ZOTE TATU DAR

October 29, 2017
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo. Akizungumza amesema CCM itashinda Udiwani kata zote tatu ambako uchaguzi unarudiwa mkoani Dar es Salaam. Kata zingine ni Saranga na Mbweni.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano kuzindua kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kijichi, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal
 Wananchi na wana CCM wakishangilia wakati Kusilawe na viongozi wenzake wakiingia Uwanjani
 Vijana wa hamasa wakichangamsha mkutano huo
 Madansa wakicheza muziki kuchangamsha mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM za Udiwani kata ya Kijichi.
 Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje akisalimia baada ya kutambulishwa kutambulishwa kwenye mkutano huo
 Mtalawanje akitroti baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Temeke
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani kusalimia.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akipongezwa na Mgombea Udiwani kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje baada ya kutoka jukwaani kusalimia.
 Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu, akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal akisalimia wananchi na kumkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuhutubia mkutano huo na kumtambulisha mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Kijichi
 Vijana wa hamasa na wananchi wakiwa wametulia kumsikiliza 
 Baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo

SERIKALI YATAIFISHA KUNDI LINGINE LA NG’OMBEKUTOKA RWANDA

October 29, 2017

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kulia) akiongea na team ya Wilaya ya Kasulu iliyoshiriki katika zoezi la kukamata ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda,  waliovamia katika kijiji cha Kakere, kushoto kwake ni kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mwanahawa Mrindoko.


Katika Picha Ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda, waliotaifishwa na serikali katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za mahakama kwa ajili ya kupigwa mnada.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, akiangalia Ng’ombe aina ya nyankole waliopo katika kijiji cha Kakere baada ya kutaifishwa na serikali.

Waziri Mpina akiongea na wanahabari hawapo katika picha baada ya zoezi la kutaifisha kundi la ng’ombe waliovamia katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu.
NA MWANDISHI MAALUM – KASULU
Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kiasi cha ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Akiongea katika zoezi hilo Waziri Mpina amesema Wilaya za mipakani mwa Nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo na kuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada. “Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” alisema Mpina.
Mpina aliongeza kusema kuwa, ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika, na kuitaka  kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu  kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na kuhakikisha mifugo yote inapatikana.
Sambamba na hilo, Waziri Mpina aliwataka wananchi kujiadhari  na kuondoka katika kununua kesi zisizokuwa za kwao kwa kuikubali mifugo kutoka nje ya nchi kuwa ni ya kwao, kwani ni kujitaftia matatizo na kuisadia serikali katika jitahada hizi za kukamata mifugo inayoingia ndani ya nchi kinyume na taratibu.
 “Kwa hiyo wananchi wawe namba moja kuwafichua watu hao, na wale tunaowabaini  kuwa wanaitikia mifugo toka nje ya nchi kuwa ni mali yao lazima wachukuliwe hatua.” alisisitiza Mpina.
Awali akitoa taarifa ya ng’ombe hao waliokamatwa katika Wilaya hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mwanahawa Mrindoko alisema ng’ombe hao ni mali ya  raia wa Rwanda kwani Serikali ya wilaya ilikuwa inawatafuta Raia  wahamiaji haramu  na kuwapata, hivyo sheria itachukua mkondo wake, na aliongeza kwa kusema kuwa kamati ya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi la kuwatafuta wafugaji ambao ni wahamiaji haramu.
Akiwa katika wilaya ya Kakonko Waziri Mpina aliagiza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo  kupitia Mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagalla kuanza mara moja zoezi la oparesheni ya kukamata mifugo toka nje ya nchi kwani tarifa za awali zinasema kuwa Wilaya hiyo ilikuwa haijaanza kabisa kutekeleza agizo hilo na ni moja ya Wilaya ya mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.