Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) yaandaa utaratibu wananchi kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) yaandaa utaratibu wananchi kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

June 02, 2015

images 
Na Masanja Mabula -Pemba
………………………………………
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amesema kuwa hakuna mwananchi aliyetimiza sifa na masharti ambaye atakosa fursa ya kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza katika Wilaya ya Micheweni Pemba .
Amesema kuwa Tume imendaa utaratibu ambao utawafanya wananchi wote waliotimiza mashari na wenye vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi ambao hawajawahi kuandikisha kwenye daftari kuandikishwa kwenye daftari hilo .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa zoezi hilo Wilayani hapa , Jecha ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi waliotimiza umri wa miaka kumi na nane na ambao hawakuandikisha kwenye daftari kufika vituoni kwa ajili ya kuandikishwa .
Amefahamisha kwamba kujiandikisha katika daftari ni kutumia haki ya msingi kidemokrasia na kikatiba hivyo ni vyema kila mmoja kuitumia haki hiyo ambayo itamwezesha kupata fursa ya kumchagua kiongozi anayemtaka katika uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu .
“Tume tumejipanga vyema kwamba na kwamba hakuna mwananchi ambaye atakosa haki yake ya kuandikishwa ambaye ametimiza masharti na vigezo , hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwenye vituo vya kuandikisha ” alisema .
Aliongeza kwamba “Hii ni haki ya kila kwa mujibu wa sheria na katiba kwani ndiyo inayompa fursa ya kuweza kuchagua kiongozi anayemtaka na kwamba nawaomba sana waitumie fursa hii ” alisisitiza Jecha .
Nao baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wameipongeza tume ya Uchaguzi kutokana na maandalizi iliyoyafanya kwani hakuna mwananchi ambaye amelalamikia utaratibu huo .
“Utaratibu huu ni lazima Tume tuipongeze kwani ni mzuri hakuna fujo , watendaji wake wako makini cha msingi kila mwananchi mwenye sifa afike kuandikishwa katika daftari ” alisema Raya Ali wa Micheweni .
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Khadija Nassor Abdi amewataka wanasiasa kuacha kutoa vitisho kwa wananchi wenye asili ya Tanzania Bara ambao wanataka kuwazuia ili wasijiandikishe katika daftari licha kwamba wametimiza masharti na vigezo vyote .
“Tumebaini kuwepo na njama zinazofanywa na wapinzani kwa kutaka kuwazuia ndugu zetu wenye asili ya Bara hata kama wametimiza masharti  , wanatishwa lakini sisi tumeibaini na tunatoa wito kwa wanasiasa kuacha kupata uhuru ili watumie haki yake kikatiba ” alieleza Khadija .
Awali Mbunge wa Jimbo la Konde (CUF) Khatib Said aliwataka mawakala wa Chama hicho kuwawekea pingamizi baadhi ya vijana wenye asili ya Bara akidai kwamba hawajatimiza masharti ikiwemo umri wao .
WATANZANIA WAMETAKIWA KUTUNZA NA KUTHAMINI MAZINGIRA

WATANZANIA WAMETAKIWA KUTUNZA NA KUTHAMINI MAZINGIRA

June 02, 2015


003
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani Mheshimiwa Samuel Sitta (aliyemuwakilisha Makamu wa Rais) akitia saini katika kitabu cha wageni maa baadaya kuwasili katika bandala Ofisi ya Makamu wa Rais wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt Binilith Mahenge na Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu waRais-Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Ufunguzi huo ulifanyika katika viwanja vya Tangamano katika jiji la Tanga.
002
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge akimkaribisha mgeni Rasmi ili aweze kuzindua maadhimisho ya wiki ya Mazingira duniani katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
001
Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi Mheshimiwa Samuel Sitta alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira jijini Tanga. Wengine wanaosikiliza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt Binilith Mahenge (kulia) na Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kulia).
………………………………………..
Watanzana wametakiwa kutunza na kuthamini mazingira kwa sababu ni urithi wa thamani kubwa sana kwa kizazi cha sasa na kijacho. Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira Duniani, Mheshimiwa Samuel Sita- Waziri wa Uchukuzi ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Mohammed Gharib Bilal. Akiongea na Wananchi katika viwanja vya Tangamano vilivyopo katika jiji la Tanga Mheshimiwa Sita amesisitiza juhudi zaidi katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kuwaomba Wazazi kuelemisha watoto wao umuhimu wa kuthamini mazingira. Aidha amewapa hongera Wananchi na Viongozi wa jiji la Tanga kwa kutilia mkazo usafi wa mazingira na kufanya jiji hilo kuibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa. Akimkaribisha Mgeni Rasmi ili kufungua sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Binilith Mahenge aliesma ni jukumu la kila mmoja kutunza na kuhifadhi mazingira hivyo basi kila Mwananchi ajitahidi katika hilo. Siku ya mazingira duniani hufanyika kila tarehe tano ya mwezi Juni kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ndoto bilioni saba, dunia Moja , tumia Rasilimali kwa uangalifu. Hii ikimaanisha kutumia vema rasilimali zetu ili kutunza vema mazingira yetu.
NHIF YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA JIJINI TANGA

NHIF YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA JIJINI TANGA

June 02, 2015

1 
Luiza Mtafi wa NHIF akimpima mapigo ya moyo mmoja wa wananchama waliotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako mjini Tanga.
2 
Afisa Matekelezo wa NHIF Bi. Shazy Amasha akitoa elimu kuhusu bima ya Afya  kwa watoto waliotembelea  banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako mjini Tanga.
3 
Nesi Anna Jengo wa hospitali ya Bombo akimpima kiwango cha sukari Bw. Ahmed Ismail aliyetembelea katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupata huduma hiyo.
4 5 
imu ya Maafisa wa NHIF ikifurahia ushindi baada ya kushinda nafasi ya kwanza katika kada ya afya kwenye maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako mjini Tanga.
…………………………………………………………………………………
Na Catherine Kameka
Mamia ya wananchi wa Mkoa wa Tanga, wameendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kupima afya zao.
NHIF Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Makao makuu, inaendesha zoezi la upimaji afya bure kwa wananchi wa Tanga na maeneo ya karibu ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchama wake  na wananchi kwa ujumla.
“Lengo kubwa la NHIF ni kuelimisha wananchama na jamii kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza  ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi”
Meneja wa NHIF Tanga Bw. Ali Mwakababu aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya lililopo katika viwanja vya Mwahako ambapo maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa yanafanyika.
Aliongeza kwa kusema kuwa katika zoezi hili wanachama na wananchi wa mkoa wa Tanga watapimwa shinikizo la damu (BP), sukari na uzito na urefu na kuainisha uwiano kati ya uzito na urefu na watakaokutwa na matatizo watapata ushauri wakitaalamu na madaktari wa Mfuko waliopo kwenye banda hilo.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi  wa Tanga kuutumia muda huo kwa kujitokeza katika viwanja vya Mwahako ili kupima afya zao.
RAIS KIKWETE ZIARANI FINLAND

RAIS KIKWETE ZIARANI FINLAND

June 02, 2015

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa FinladDorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu ya nchi hiyo
3
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
4
Rais Jakaya Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
5
 Akipokea zawadi ya jezi ya timu ya taifa ya Finland ya basketball
6
JK akitoa zawadi ya mchoro wa Tingatinga kwa viongozi wa kampuni ya KONE
7
JK akitembelea  bandari ya Helsinki
9
Rais Kikwete akipata mapokezi Rasmi kwa mwenyeji wake Rais wa Finland Mhe Sauli Niinisto

10
Rais Dk.Shein aondoka Nchini leo

Rais Dk.Shein aondoka Nchini leo

June 02, 2015


sh1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati wakiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani.[Picha na Ikulu.]
sh2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii   katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati akiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani pamoja na Ujumbe wa Viongozi mbali mbali.[Picha na Ikulu.]
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI LEO.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI LEO.

June 02, 2015

lib1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania, wakati walipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Juni 02,2015.
………………………………………………………………….
Na Mwandishi Maalum
Asema :Jitahidini kuepusha migogoro-Dkt. Bilal awaasa wafugaji .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya kuchukua sheria mkononi ili kuhakikisha usalama wao na watu wanaopakana nao unakuwepo wakati wote. Mheshimiwa Makamu wa Rais amezungumza hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka Chama cha Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwernyekiti wao Ally Hamis Lumiye.
 
Makamu wa Rais alisema, si busara kwa wafugaji kujichukulia sheria mkononi na kwamba matatizo yanayowakabili wafugaji ni muhimu yakatatuliwa kwa kufuata sheria za nchi. “Jitahidini kuepusha migogoro hasa ile inayosababisha watu kupoteza maisha. Tusichukue sheria mkononi, sote lazima tuwe watii wa sheria,” Makamu wa Rais alisema.
 
Awali akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Mwenyekiti wa Chama hicho Ally Hamis Lumiye alisema, chama cha wafugaji kwa sasa kinakabiliwa na changamopto kubwa hasa baada ya kuwepo mgawanyiko unaolenga kukimomonyoa chama hicho hasa kufuatia kujitokeza baadhi ya wafugaji kuamua kupora madaraka ya chama hicho na hivyo akaitaka serikali kuungana nao katika kuzima nguvu za waporaji hao.
 
“Mheshimiwa Makamu wa Rais leo hii tumekuja kwako kwa jambo moja nyeti. Wapo baadhi yetu wasiotaka kuona wafugaji tunajikomboa kwa kuwa na umoja kama huu. Wamefikia hatua ya kupora chama hiki na jitihada zetu za kutaka kuwadhibiti zinaonekana kuwa ngumu kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali kuwatambua waporaji hao,” alisema mwenyekiti huyo.
 
Mheshimiwa Makamu wa Rais alisisitiza kuwa jambo la uporaji wa chama kamwe haliwezi kuachwa kimya kwa kuwa wafugaji na chama chao kimesajiliwa hivyo wafuate sheria hizo hizo ili kupata haki yao kama inaonekana kutokuwepo. Pili alisisitiza kuwa atalifanyia kazi suala hilo kupitia nafasi ziliozpo chini yake na kulipatia ufuimbuzi wa haraka.
 
“Mimi nami ni mfugaji, chama hiki ni muhimu kwa maslahi ya wafugaji. Kwa kuwa tuna katiba inayokiongoza na kwamba tunazo sheria ambazo zilifuatwa hadi kukipatia chama hiki usajili, basi hakuna haja ya kusikitika sana. Tutumie taratibu hizi hizi ili kuondokana na hao wanaotaka kupora mamlaka ya chama hiki,” alisema na kuongeza:
 
“Ni muhimu kiwepo chama imara kwa maslahi ya wafugaji wote. Chama hiki kinaweza kuwasaidia sana katika kukabiliana na changamoto mlizonazo maana kwa kuwa wamoja ni nguvu.”