MACHAVA FC KUTUMIA UZI MPYA TOKA MEGATRADE KATIKA MECHI YAO DHIDI YA PANONE FC ITAKAYOSHUHUDIWA NA MAGWIJI WA REAL MADRID UWANJA WA USHIRIKA MOSHI.

August 23, 2014

Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa nahodha wa timu ya soka ya Machava fc.
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka(kushoto) akikabidhi msaada wa jezi kwa mlinda Mlango wa  timu ya soka ya Machava fc
Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka (kushoto)akikabidhi msaada wa jezi kwa Makamu mwenyekiti wa timu ya soka ya Machava fc,Abuu Masudi.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha timu ya Machava fc ya mkoani Kilimanjaro wakionesha uzi mpya waliopewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Panone fc uliondaliwa mahususi kwa ajili ya Magwiji wa soka wa klabu ya Real Madrid utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.

MAGWIJI wa klabu ya Real Madrid ya Hispania leo (kesho) wanaendelea na ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa watatembelea lango la kupandia mlima Kilimanjaro la
Marangu.
Katika ziara hiyo ya kitalii chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kimeiteua klabu ya soka inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Panone FC kuwa wenyeji wa magwiji hao ambao pia watashuhudia mchezo wa
kirafiki kati ya timu za Panone fc na Machava fc utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema ofisi yake imeandaa utaratibu wa namna ya kuwapokea magwiji hao pamoja na kuandaa ratiba maalumu ya kutembelea vivutio ukiwemo mlima Kilimanjaro pamoja na
kushuhudia mchezo mmoja wa Kirafiki.
“Katika  tasnia ya michezo nchi yetu  imepata bahati kubwa ya kutembelewa na wachezaji  wa zamani  Real Madrid ambao pamoja na ziara yao wamepanga kutembelea mkoa kwetu ,kikosi hicho kitaingia kati ya saa tano au saa tano na nusu watashuka uwanja wa ndege wa KIA,”alisema
Gama.
Alisema baada ya kupokelewa moja kwa moja magwiji hao watapelekwa Mlima Kilimanjaro katika ofisi za hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA ambako watapata fursa ya kupanda mlima huo kwa hatua chache baada ya kupokea taarifa ya shughuli za utalii kwa ujumla.
“Tumewaandalia sehemu ya kupata chakula cha mchana na wenyeji wao klabu ya Panone fc , baada ya chakula tukasema ni vizuri waone hatupo mbali katika michezo, kwa hiyo tumepanga kuwa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Panone fc na Machava ikitanguliwa na ikitanguliwa na mechi ya vijana chini ya miaka 15 .”alisema Gama.
Gama aliwataka  wadau na wapenzi wa michezo mkoani humo kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika mapokezi makubwa ya wachezaji hao wa zamani na kwamba licha ya kuwa dhamira yao ni kuimarisha utalii lakini pia wangependa kuona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro.
“Ni vizuri wakaona hali ya michezo katika mkoa wa Kilimanjaro na pengine wakapata nafasi ya kuona vipaji vyetu ,mimi ninauhakika hapa kuna wachezaji wanaweza kuchukuliwa na Real Madrid kwa sababu tunaweza
kufanya vizuri sana,,,kwa hiyo niwaombe wanamichezo wetu wajitokeze kwa wingi tukawaone nyota hawa wa Madrid na pengine tuwape ukarimu wetu wa kitanzania tuliouzoea.”alisema Gama.
Kwa upande wao klabu ya soka ya Panone fc kupitia msemaji wake Kassim Mwinyi alisema wamefurahishwa na ujio huo na kwamba klabu imejipanga kujenga mahusiano na magiwji hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu
katika maswala ya michezo.
“Tumepata fursa kama Panone fc  ya kukutana na Magwiji hawa wa Madrid ,sisi tumejipanga kutumia ujio huu katika kujenga mahusiano ya kitimu kati yetu na wao ,na hakika utakuwa ni mwanzo mwema kwa klabu yetu
ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza”alisema Mwinyi.
Magwiji hao watakao ongozwa na wanasoka waliowahi kutamba katika ulimwengu wa soka kwenye ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga,ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Bacrays,michuano ya Mabingwa na ile ya kombe la dunia wakiwa na nchi zao wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya ziara maalumu.
Baadhi ya Wanandinga hao wa zamani waliotamba na Real Madrid kwenye michuano ya La Liga, UEFA pamoja na kombe la dunia wakiwa na nchi zao watakaofanya ziara ya siku nne nchini ni pamoja na Zinedine zidane, Luis Figo, Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima, Christian karembeu na
Michael Owen.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya kaskazini,
MHE.SITTA AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA PAMBA

MHE.SITTA AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA PAMBA

August 23, 2014

0D6A6917Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza na baadhi  viongozi na wajumbe kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma  kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.
0D6A6935 
Kaimu Mwenyekiti wa kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA), Godfrey  Mokiri(katikati) akizungumza  na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta(kulia)  katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati  baadhi  viongozi na wajumbe wa chama hicho  walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma  kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.Kushoto ni Katibu wa chama hicho, George Mpanduji.
0D6A6980 
Baadhi  viongozi na wajumbe wa  Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) wakiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Khamis Hamad (wa tatu kulia )walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la  kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba  kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima  Tanzania.
PINDA AFANYA ZIARA FUPI JIJINI MWANZA

PINDA AFANYA ZIARA FUPI JIJINI MWANZA

August 23, 2014

PG4A2820 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa mbele ya kaburi la Vedasto Kitwanga,mtoto wa Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Wanne kulia)  wakati alipokwenda nyumbani kwa Naibu Waziri huyo  eneo la Usagara Mwanza August 23, 2014 kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae . Wengine pichani ni mke wa Naibu Waziri huyo, Matrida   (wanne kushoto) na  kushoto kwa Waziri Mkuu ni binti yao, Agness Misoji Kitwanga  . Kulia ni  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga  na Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Erasto Ndikilo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 PG4A2872 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kulia) baada ya kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambako alikwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 PG4A2888 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipigiwa magoti na Matrida Kitwanga (kulia) mke wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kulia) baada ya kuwasili nyumbani kwa Naibu Waziri huyo, eneo la Usagara, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambako alikwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mwanae Vedastus Kitwanga kilichotokea hivi karibuni. Katikati ni binti wa familia hiyo,Agnes Misoji Kitwanga.(Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A2947 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  wadau wa ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege katika  uwanja wa ndege wa Mwanza unaoboreshwa wakati alipofanya ziara ya kukagua maboresho ya uwanja huo August 23, 3024 Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dr. Charles Tizeba.(Picha na Ofisi ya Waziri MKuu) PG4A2951
PG4A2964 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua eneo  panapojengwa mnara wa kuongozea ndege kwenye uwanja wa Mwanza August 23, 3014. Kushoto kwake ni Waziri wa Uchukuzi, Dr. Charles Tizeba,(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A2972 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na baadhi  ya vibarua wanaofanyakazi ya ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa  Mwanza baada ya kukagua ujenzi huo August 23, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A3009 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na   baadhi   ya vibarua wanaofanyakazi ya ujenzi wa jengo lenye Mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege wa  Mwanza baada ya kukagua ujenzi huo August 23, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A3034 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na vibarua wanaofanya kazi ya kupanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza wakati alipokagua upanuzi wa uwanja huo August 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A3111 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Eliud Sanga  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Soko la Kimataifa linalojengwa kwa ubia kati ya jiji la Mwanza na LAPF jijini humo August 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MJINI MOROGORO, AWATAKA VIONGOZI WAACHE WOGA KUSIMAMIA SHERIA

August 23, 2014
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi 
mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wataalamu walioshughulikia ufungwaji wa mtambo huowakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Morogoro mjini Mhe Aziz Aboud wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wadau wa mji wa Morogoro wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Jengo la  mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Baadhi ya wafanyakazi wa MORUWASA  wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Burudani wakati wa sherehe hizo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akifungua pazia la sherehe hizo
Sehemu ya jengo la mradi huo
Kwa ubavuni
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu akitoa muhtasari wa mradi huo
Bango linajieleza
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Rais Kikwete akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu kwa kufanuikisha mradi
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiongea machache 
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher akisoma hotuba yake kwa Kiswahili wakati wa sherehe hizo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akiongea wakati wa sherehe hizo na kumkaribisha Rais Kikwete aongee na wananchi
Rais Kikwete akizungumza na kuzindua rasmi mradi huo mkubwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king’ora kuzindua rasmi mradi huo
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikata utepe kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akipata maelezo ya mradi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASA 
Sehemu ya mitambo ya mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikagua mitambo ya  mradi huo
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiendelea kutoa maelezo ya mradi
Ukaguzi ukiendelea
Ukaguzi wa sehemu ya kusafishia maji

SITTI MTEMVU AWA MALKIA WA TEMEKE 2014

August 23, 2014


 Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu akipunga mkono huku akiwa na mshindi wa Pili, Salma Saleh (kushoto) na watatu, Neema Mollel, baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo.
 Warembo walioingia Tano bora wakipozi kusubiri hatua ya kupambana katika kujibu maswali.

 Miss Ilala, wakifuatilia shindano la Redd's Miss Temeke, Viwanja vya TCC Club, Chang'ombe, Dar es Salaam
 Washiriki wa Redd's Miss Temeke, wakionesha shoo, wakati wa shindano hilo.

Mshindi wa Pili wa Redd's Miss Temeke 2013, Narietha Boniface, akimvisha taji Redd's Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo, TCC Chang'ombe