COASTAL UNION KUKIPIGA NA COMBINE POLISI TANZANIA.

COASTAL UNION KUKIPIGA NA COMBINE POLISI TANZANIA.

August 08, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
TIMU ya Coastal Union "Wagosi wa Kaya"wanatarajia kucheza mechi ya Kirafiki na timu ya Combine Polisi Tanzania Iddi Pili katika uwanja wa Mkwakwani mjini hapa ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara ambao utaanza Agosti 24 mwaka huu.

Akizungumza na Blog hii,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa ni siku ya mchezo huo.

Aurora alisema timu hiyo itaingia mkoani hapa leo jioni tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao Coastal Union  unautumia kwa umuhimu mkubwa wa kujiimarisha kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu hapa nchini.

Aidha alisema kwenye mchezo huo pia utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wao wageni akiwemo kiboko wa Yanga na Simba kutoka klabu ya URA ya Uganda Yayo Lutimba ambaye alisajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili .

Aidha aliongeza kuwa mechi nyengine itachezwa leo kati ya timu ya Coastal Union B ambao watawakabili Kilimani ya Zanzibar mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote.

WAISLAMU WAMETAKIWA KUTUNZA FADHILI WALIZOCHUMA MWEZI WA RAMADHANI.

August 08, 2013


Na Mbaruku Yusuph.
Waislamu Mkoani Tanga wametakiwa kutunza fadhila zote walizozichuma  katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kuonyesha siha nzuri kwa jamii kitu kinachopolekea kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kujenga umoja uliyo imara katika uislamu hapa nchini

Akizungumza mapema leo Ofisini kwake Sheikh wa Mkoa wa Tanga Ally Juma Luwuchu alisema kuwa kunamiezi mingi sana yenye fadhila lakini miezi hiyo haiwezi kuufikia mwezi Mtukufu wa   Ramadhani,ambao fadhila zake unaweza kuchukua miaka nenda rudi kuzihesabu na hakika ni mwezi wenye fadhila nyingi mno mpaka ALLAH (s.w) akauita mwezi huu kuwa ni mwezi wa Rahma,mwezi wa Baraka,Imani,Msamaha,na ni mwezi wa kumtii Mweyezi Mungu.

Alisema kwa hakika  wale walioutumia muda wao ndani ya mwezi huu kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu(s.w) kwa kutenda matendo mazuri,wakawa si wenye kula na kufanya mambo maovu bali wakauona mwezi huu ni mwezi wa kuzidisha sana ibada,kuomba maghfira, kusameheana, kuhurumiana,kusoma Quran,kumswalia zaidi Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w)  basi kwa hakika watafaulu sana kwa kupata fadhila za Mwenyeezi Mungu (s.w) na msamaha wake.

“Wafahamu kwamba Mungu ambae ndugu wote wa kiislam wamerudi kwake kwa kufanya meme ndani ya mwezi wa Ramadhani basi ni Mungu huyohuyo anayetuamrisha kuacha kufanya maovu katika miezi ya kawaida na anatutaka kufanya mema katika maisha yetu yote” Alisma Sheikh Luwichu.

Sheikh Luwuchu aliwaomba  waslam kuondoa tofauti zao za kiimani na wawe wamoja , wasikivu kwa viongozi wao  wakuu wa kidini hasa inapofikia wakati wa kupata tamko kutoka kwa viongozi hao kitu kitakachowapelekea kuonyesha umoja wetu na mshikamano katika maswala yote yanayohusu uislam.

Aidha alisema kuwa swala la kufunga na ufungua kwa mwezi linatokana na kuonekana kwa mwezi au kukamilisha siku thelathini kama mwenyezi Mungu alivyotuamrisha  au kufuata taarifa kutoka kwa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania au kadhi Mkuu ambao wanamamlaka kutokana na sheria za dini wao wakautangaza mwezi.

Alisema sikukuu ya  Eid -il-fitry kitaifa itafanyika katika Mkoa wa Tabora itakayoongozwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Issa bin Shaaban Simba na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Dk.Kharib Billal ambae ni makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katika Mkoa waTanga  Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wata watafanya Dhifa maalum itakayoambatana na Baraza la Eidy litakalofanyika katika ukumbi uliopo ndani ya shule ya sekondari ya Jumuiya saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mh;Omari Nundu mbunge wa Tanga Mjini.

Hata hivyo aliwaomba waislam wote katika Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi katika Dhifa hiyo na Baraza la Eid  katika sikukuu ya Eid - il fitry ili kujenga umoja na mshikamano kwa waislam  katika dini ya mwenyezi Mungu.

Mwisho.