DC WA HAI,ANTHONY MTAKA AMALIZA MGOGORO WA MAJI KATI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) NA WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA SHIRI NJORO.

February 16, 2016
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na baadhi ya wanakijiji cha Shiri Njoro wakitembelea chanzo cha maji cha Shiri.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony akiwa na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA pamoja na viongozi wa kijiji cha Shiri Njoro wakifanya maombi kabla ya kufanyika kwa kikao cha usuluhishi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akimsikiliza mmoja wa viongozi wa kijiji cha Shiri .
DC Mtaka akizungumza jambo mara baada ya kumsikia malalamiko ya wanakijiji hao.
Mkuu wa wilaya akipitia rekodi ya kiwango cha maji ambacho kimekuwa kikirekodiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).
Afisa kutoka bondde la Pangani,Brown Mwangoka akizungumza namna ambavyo mgawanyo wa maji katika chanzo cha Shiri unafanyika.
DC Mtaka akizungumza.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro ,Clemence Nkya akimueleza jambo mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Shirimatunda Beda Massawe akizungumza jambo katika kikao hicho.
DC Mtaka akitoa ushauri katika kikao hicho ambacho wakulima walilalamika kupata maji pungufu kwa ajili ya kumwagilia mazao yao.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi,MUWSA Joyce Msiru akimuelekeza afisa uhusiano wa mamlaka hiyo,Flora Nguma kuchukua mambo mbalimbali yaliyotolewa katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo katika eneo ambalo hugawanya maji kwenda katika mifereji mitatu inayotumiwa na wakulima katika kijiji cha Shiri.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro,Clemence Nkya akishauri jambo kwa Mkurugenzi wa MUWSA,Joyce Msiru.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MILIONI 100 KWA WAFUGAJI WA KUKU, KIJIJI CHA MSOGA, CHALINZE

MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MILIONI 100 KWA WAFUGAJI WA KUKU, KIJIJI CHA MSOGA, CHALINZE

February 16, 2016
Mo Dewji Foundation
Afisa Mahusiano wa Mo Dewji Foundation, Zainul Mzige (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 100 kwa Mwenyekiti wa mradi ufugaji kuku wa kienyeji katika kijiji cha Msoga, Michael Mkindo (wa tatu kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya ya Bagamoyo, Mh. Majid Mwanga (kushoto) na Diwani wa kata ya Msoga, Hassan Mwinyikondo (kulia).
IMG_2999Afisa Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige akisoma hotuba wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji chotara kutoka kijiji cha Msoga, Chalince mkoa wa Pwani. Wa kwanza kushoto ni mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chalinze, Majid Mwanga, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Msoga, Hassan Mwinyikondo.
Mfuko wa MO Dewji umeupatia mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara wa kijiji cha Msoga mkoani Pwani shilingi milioni 100 kufanikisha uendeshaji wa mradi huo awamu ya kwanza.
Mradi huo unaokisiwa kuwa na makisio ya uzalishaji ya sh 2,777,901,500 ulibuniwa mwaka 2013 kwa lengo la kukabiliana na umaskini kijijini hapo.
Kwa mujibu wa taarifa za mradi makisio ya mapato kutokana na mauzo ya mayai, vifaranga na kuku baada ya kukoma kutaga zinakadiriwa kuwa sh 4,913,708,000
Aidha mradi huu unasimamiwa na kufadhiliwa na rais Mstaafu Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Akikabidhi hundi hiyo ya sh milioni 100, Afisa Mahusiano wa Mo Dewji Foundation, Zainul Mzige alisema kwamba fedha hizo zitaumika kujenga mabanda 200, ununuzi wa vifaranga, ununuzi wa chakula cha kuku, chanjo na dawa na malipo kwa wataalamu.
IMG_3008
Afisa Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige akisoma hotuba wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji chotara kutoka kijiji cha Msoga.
Mambo mengine ni utawala, mawasiliano, ununuzi wa chachu za mpunga na vifaa vya chakula na maji.
Mzige alisema pamoja na kutoa fedha hizo kuunga mkono juhudi za Msoga Poultry Farming Project (MPFP) kuendesha na kuuendeleza mradi kibiashara, aliwataka wahisaniwa kutambua kwamba maendeleo ya mradi wao yatategemea sana namna wanavyokuwa makini kutumia fursa mbalimbali kujiimarisha.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Mo Dewji Foundation imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya kijamii nchini.
Aidha hivi karibuni Mfuko wa MO Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited walizindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasirimali miongoni mwa vijana.
Shindano ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali Tanzania.
Ili kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Ofisa Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL Group na mwenyekiti wa Mo DewjiFoundation) ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na kuikuza.
Kwa niaba ya wananchi wa Msoga, mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alimshukuru Mwenyekiti wa Taasisi ya Mo Dewji, Mohammed Dewji kw ufadhili ambao ameufanya kwa wananchi wa kijiji cha Msogo na kumtaka kuwa na moyo wa kutoa zaidi ili azidi kusaidia wananchi walio na mahitaji.
Mo Dewji Foundation
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani kwa MO Dewji Foundation mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 100 kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa kienyeji Chotara.
Alisema kuwa kupitia mradi huo wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara, wananchi wa kijiji cha Msoga wataweza kujikwamua na janga la umasikini na wataendelea kuwa wakiandika maombi ya miradi mbalimbali ambayo wanataka kuifanya ili kuzidi kutengeza ajira zaidi kwa wananchi wa Mzoga.
“Tunamshukuru Mohammed Dewji kwa msaada huu tunaimani utasaidia wananchi wa Mzoga na namuomba asisite kutupokea muda mwingine tunapokuwa na miradi mingine,” alisema Kikwete.
Nae Mratibu wa Mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara (Msoga Poultry Farming Project), Novatus Kailembo alisema wazo la kuanzisha mradi huo lilitolewa na Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2013 ili kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa Msoga kama kiuchumi, kielimu na kiafya.
Alisema wanataraji kuanza na wanakijiji 300 ukiwa ni mradi wa mfano, awamu ya kwanza ambao wanataraji kuanza kufanyika katika vitongoji tisa ambavyo ni Hospital, Takalagame, Kota, Mnazi Mmoja, Tumbi Juu, Tumbi Chini, Kingugi, Mkundi na Mokela.
Mo Dewji Foundation
Mkuu wa Wilaya ya Chalinze, Majid Mwanga akimshukuru Mwenyekiti wa MO Dewji Foundation, Mohammed Dewji kwa ufadhili ambao ameutoa kwa wilaya yake kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara ambapo ufugaji huo unataraji kufanyika katika kijiji cha Msoga.

OFA YA UPENDO KUTOKA HUAWEI MSIMU HUU WA VALENTINE

February 16, 2016
Mabalozi wa Huawei wakipozi siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakipata picha ya ukumbusho na balozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa wateja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wateja walioshiriki katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania.
Bw. Sylvester Manyara, Meneja Mwandamizi  Huawei Tanzania(Kushoto) akimkabidhi Mteja mfuko wa zawadi pamoja na kadi katika uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3   inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki hii, Mlimani City Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa mabalozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam. 

Na Mwandishi wetu, 
Kampuni ya simu ya Huawei, inayoshika nafasi ya tatu kwa utengenezaji na uuzaji wa simu za mkononi ulimwenguni imezindua promosheni ya Valentine ya muda wa wiki 3 inayohusisha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji zawadi kwa wanunuzi wa simu za Huawei kutoka kwenye maduka yao mbalimbali ya rejareja yaliyosajiliwa.
Promotion hiyo itahusisha simu kuu mbili ambazo ni Huawei P8 na Huawei G8. Zawadi zinazotolewa kwa wateja ni pamoja na “selfie sticks, spika za Bluetooth na T-shirts. Pamoja na zawadi zote hizo ,wateja hao pia wanapewa fursa ya kupata picha nzuri za kumbukumbu ili waweze kuzitumia kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na mingine.
Kampeni hii Iliyozinduliwa wikiendi hii mjini Dar es Salaam eneo la  Mlimani City, inawaahidi wateja wa Huawei kuona thamani ya pesa yao kutokana na zawadi watakazopatiwa .
Kwa mujibu wa report ya simu za mkononi ya hivi karibuni nchini Tanzania ilivyochapishwa mwaka jana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya watanzania wanaotumia simu za mkononi, waliojisajili imeongezeka kwa asilimia 16 kwa mwaka 2014 kufikia milioni 31.86 hiyo ni sawa na asilimia 67 kwa watanzania wote wanaotumia simu.
Huawei Tanzania wanaahidi kuendelea kutatua uhitaji wa wateja wao kwa kuwapatia   simu zenye ubora wa hali ya juu na orijino.
Tunatarajia kutoa huduma bora ya mawasiliano na intanet kwa bei nafuu kwa wananchi na pia kuwazawadia wateja wetu wale wazamani na wapya,  vifaa bora na vya kisasa vitakavyoweza kuongeza wigo katika matumizi ya simu zao za smatiphone  na intaneti pia” alisema Bw. Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania katika uzinduzi wa Promotion hiyo.
Akielezea promosheni hiyo, Bw. Peter Zhangjunliang alisema; promosheni hii ya wiki 3 ni ya nchi nzima na ipo wazi kwa watanzania wote watakao nunua simu za G8 na P8 kutoka Huawei.”

Huawei, rafiki yako kwa simu origino.

Kuhusu Huawei
Kampuni ya Huawei imejizatiti katika kutengeneza bidhaa bora kwa matoleo tofauti ulimwenguni, kutoa huduma rafiki za simu, kwenye intaneti kwa wateja wake. Kampuni ya Huawei inajulikana duniani katika utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti na vifaa vya majumbani.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, bidhaa vya Kampuni ya Huawei zinapatikana  zaidi ya nchi 150 ulimwenguni kote. Huawei ni kampuni ya 3 katika usambazaji wa simu (2015) ikiwa imesambaza zaidi ya milioni 100 ulimwenguni. Kampuni ya Huawei imeanzisha ushirikiano  na makampuni makubwa duniani kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom. 
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea www.huaweidevice.com
DK. KIGWANGALLA ADHURU KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA IRINGA, ATOA MAAGIZO YA KISERIKALI KUWASAIDIA WANANCHI

DK. KIGWANGALLA ADHURU KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA IRINGA, ATOA MAAGIZO YA KISERIKALI KUWASAIDIA WANANCHI

February 16, 2016
kigwa5Eneo la vijiji vya Pawaga linavyoonekana kwa picha za angani wakati wa Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangallla amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kufika katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Tarafa ya Pawaga iliyopo Iringa vijijini Mkoani hapa ambapo mbali na kutoa pole pia ameweza kutoa huduma za kitabibu kwa baadhi ya watu waliozidiwa waliokuwa bado hawajaokolewa.
Awali Dk. Kigwangalla alipodhuru kwa wananchi waliopo kwenye kambi ya muda baada ya kunusurika na mafuriko hayo, aliwaeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega kwani Serikali ya "Hapa Kazi Tu" haina ngoja ngoja ndio maana yeye ameweza kufika haraka kuakikisha wananchi wapo salama na wanapatiwa huduma zote za msingi na za kijamii ikiwemo matibabu na elimu ya kijikinga na milipuko ya magonjwa ikiwemo magonjwa ya kipindupindu ambacho kimewakumba wananchi hao.
Dk. Kigwangalla ameweza kufanya hilo baada ya Chopa iliyokuwa ikimtembeza angani kufika katika maeneo yaliyozingirwa, alimuru rubani wake kushusha chini na kisha kutoa msaada wa haraka kwa akina mama na watoto waliokuwa wamezingirwa kwenye moja ya maeneo hayo zaidi ya siku tatu bila kuokolewa ambapo alitoa huduma na kisha Chopa hiyo iliwabeba hadi katika eneo maalum waliopo wahanga wengine waliookolewa.
Pia Dk. Kigwangalla aliweza kutoa elimu na maelekezo mbalimbali kwa wahanga hao kujiepusha na masuala ya kutumia mahitaji salama ilikuepukak kipindupindu kisienee zaidi kwani hadi sasa eneo hilo limeweza kupatikana wagonjwa wa ugonjwa huo zaidi ya 220 huku hadi wanatembelea katika kambi ya Mtakatifu Lucas iliyopo Pawaga, ilikuwa na wagonjwa zaidi ya 40.
Imeandaliwa na Magreth Kinabo–MAELEZO, Andrew Chale, modewjiblog-Iringa
kigwazzNaibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa katika eneo lililokumbwa na mafuriko hayo kijiji cha Mbolimboli
IMG_2036 - CopyBaadhi ya wananchi waliookolewa baada ya Naibu Waziri, Dk.Kigwangalla kuamuru wawaishwe katika kambi waliopo wahanga wengine.
kigwa 11Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipewa maelezo namna wanawake hao pamoja na watoto wao wadogo walivyoweza kuzingirwa na maji kwa muda wa siku tatu bila kuwa na huduma muhimu ambapo hata hivyo, Naibu Waziri aliweza kuwasaidia ikiwemoo kuamuru Chopa hiyo iwapeleke kwenye kambi maalum na kisha wao kubaki hapo kabla ya kurudiwa tena na kuendelea na safari ya Kambi ya watu wa Kipihdupindu.
kigwa21Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipata maelezo ya mmoja wa waokoaji wanaotumia boti maalum namna walivyoweza kupata taabu jinsi ya uokoaji katika eneo hilo.
kigwa2Baadhi ya wahanga wa mafuriko wa vijiji vya Mbolimboli katika Tarafa ya Pawaga wakipata maji maalum yenye dawa ilikujikinga na ugonjwa wa kipindupindu ambao hata hivyo umeenea katika eneo hilo kutokana na maji yake kuchafuliwa na vinyesi vya vyoo vilivyokumbwa na mafuriko.
kigwa3Naibu Waziri, Dk.Kigwangalla akisisitiza wahanga hao wa mafuriko kuakikisha wanatumia vyakula na vitu vingine kwa hali ya usafi ilikueupuka ugonjwa huo wa kipindupindu.
kigwa9Baadhi ya akina mama wakipanda Chopa baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla kuamuru wapelekwe kwenye kambi haraka kutokana na watoto waliokuwa nao kuzidiwa (wanawake hao wanaoonekana pichani ndani ya chopa).
kigwangalla 111Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa wakiwa katika Chopa juu wakiangalia namna mafuriko hayo yalivyosababisha athari kubwa na kufanya kuwa kisiwa katika vijiji hivyo vya Mbolimboli.
kigwa6eneo la chini linavyookena kutokana na mafuriko hayo.
mafuriko33Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akioneshwa moja ya maeneo namna maji yake yalivyochafuliwa na kinyesi baada ya vyoo kuharibiwa na mafuriko hayo.
mafuriikoBaadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati alipofika katika eneo lililokuwa akina mama hao na watoto ambao wamekaa siku tatu bila kupata huduma muhimu.
kigwa 16Pichani ni baadhi ya akina mama na watoto ambao walikwama kwa zaidi ya si tatu kwenye mafuriko hayo huku wakishindwa kupata mahitaji muhimu ambapo pia vifaa vya uokoaji na waokoaji kushindwa kuwafikia ambapo hata hivyo Naibu Waziri wa Afya. Dk. Kigwangalla alipoamuru Chopa iliyokuwa ikipita kuangalia athari hizo kushuka kisha kuwachunguza na kupelekwa kwenye kambi maalum.
kigwa11uokoaji ukiendelea..
mafuriko
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, wakielekea katika kambi ya wahanga hao wa mafurikoeneo la Itunundu..
mafurikooBaadhi ya watoto wakiwa katika eneo la kambi ya wahanga ambao wengi wao wamekimbia kwenye maeneo hayo yaliyokumbwa na mafuriko.
kigwaNaibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akisaidiana na mmoja wa watoa huduma baada ya mtoto huyo kuzidiwa katika kambi hiyo maalum.
mafuriko 2Kambi maalum inayohudumiwa wagonjwa wa kipindupindu lililo eneo la Mtakatifu Lucas