JWTZ YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS KUJENGA UZIO KUZUNGUKA MERERANI

September 21, 2017
Helkopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikitua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Simanjiro na wananchi mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli

 Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikipenya kwenye vichaka wakati wa kukagua eneo litakalojengwa ukuta.
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo la madini ya Tanzanite huko Mererani.

 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo la madini ya Tanzanite huko Mererani.
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee

Tigo yatoa msaada wa mfumo wa kidigitali wa elimu Mkoani Mwanza

September 21, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,akitata utepe wakati wa uzinduzi wa programu ya kompyuta yenye vitabu vya masomo ya shule za sekondari(Tigo eSchool) iliyounganishwa kwenye shule ya sekondari Pamba mkoani Mwanza jana na  Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,akimshukuru  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya(kushoto) baada ya kuzindua programu  ya kompyuta yenye vitabu vya masomo ya shule za sekondari(Tigo eSchool) iliyounganishwa kwenye shule ya sekondari Pamba na  Kampuni ya Tigo, Jumla ya shule tano za mkoa huo zimeunganishwa na huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akijaribu huduma ya Tigo eSchool  kwenye shule ya Sekondari   Pamba mkoani Mwanza. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa, Alli Maswanya (kushoto)na Mbunifu waTovuti toka Shule Direct, Rajabu Mgeni.


Mwanza 21 Septemba,  2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania kupitia mradi wa Tigo E-schools imetoa msaada wa mfumo wa teknologia kwa masomo kumi na moja (11) ya shule kwa sekondari tatu (3) za Mkoani Mwanza.
Ikiwa ni sehemu ya shughuli za jamii zinazoendana na msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa, msaada huu unaonesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa wateja wake na kuwapa huduma zinazoendana na mahitaji yao.   Kupitia mradi wa Tigo e-schools, Tigo imeona na kuelewa hitaji la wanafunzi la maarifa ya Tehama, na inakutana na hitaji hili kupitia  utoaji wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti na mifumo mbali mbali ya elimu. 
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mfumo huo, Meneja Kanda wa Tigo, Ali Maswanya alisema kuwa mfumo huo utawaandaa wanafunzi kuibua fursa na kuwa sehemu ya mabadiliko ya Tehama ulimwenguni. 
‘Dunia ya sasa inaendeshwa kidigitali. Mradi wa Tigo E-shools unawaandaa wanafunzi kuwa sehemu ya ulimwengu huu wa kidigitali. Kupitia mfumo huu, wanafunzi wataongeza busara, kupanua mitazamo na ubunifu wao, na hivyo kuibua fursa pamoja na kukabiliana na changamoto zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa digitali,” Maswanya alisema. 
Alitaja shule za sekondari zilizofaidi kutoka kwa msaada huo Mkoani Mwanza ni Shule ya Sekondari Pamba, Sekondari ya Mwanza na Sekondari ya Mirongo. Tigo E-schools pia itasambaza mfumo huo wa elimu kwa shule 52 za sekondari katika mikoa 12 kati ya mikoa 15 ambayo msimu wa Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa utazuru mwaka huu.  
Mwaka 2016, Tigo ilifanya makubaliano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwezesha kusambazwa kwa mtandao katika shule za sekondari nchini ili kuchangia mpango wa miaka miwili wa serikali kuleta mabadiliko ya elimu kwa njia ya mtandao. 
Kama sehemu ya makubaliano hayo, Wizara ilitoa majina ya shule zisizokuwa na maabara ya kompyuta na pia kutoa mwongozo wa utekelazaji wa mradi huo. Tigo ilishiriki katika ujenzi na kuunganisha maabara mpya za kompyuta na mtandao, na hatua ya tatu ni ya kuunganisha shule husika na teknologia hii ya elimu kwa njia ya mtandao. 
“Kupitia mpango wetu endelevu wa kuwekeza katika hudma za jamii, Tigo inachangia jitahada za serikali za kuigeuza Tanzania kuwa na uchumi wa maarifa ifikapo mwaka 2025.” Maswanya aliongeza. 
Shule ambazo zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama ni Arusha Day, Ilbouru na Arusha Sekondari mkoani Arusha; Mwanza, Pamba na Mirongo Sekondari mkoani Mwanza; Tabora Girls na Milambo Sekondari mkoani Tabora; na Mpwapwa Sekondari mkoani Dodoma. 
Shule nyingine ni Iringa na Kleruu Sekondari mkoani Iringa; Matalawe na Songea Girls Sekondari mkoani Songea; Njombe na Mpechi Sekondari mkoani Njombe; Morogoro Municipal na Mzumbe Sekondari zilizopo Morogoro; pamoja na Handeni na Shemsanga Sekondari huko Tanga. 
Shule nyingine zitakazofaidi mfumo huu wa elimu kutoka Tigo e-schools ni Lyamungo Sekondari na Machame Girls Sekondari huko Moshi; Newala Day na Masasi Day Sekondari zilizopo Mtwara na kwa mkoa wa Dar es  Salaam, sekondari za Mbagala, Kibamba, Benjamin Mkapa na Makumbusho zitaunganishwa na mfumo huo wa elimu kwa njia ya Tehama. 
Kwa mara nyingine, natoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa kuiruhusu Tigo Tanzania kuwa sehemu ya mipango yake ya kuiingiza Tanzania katika mfumo wa uchumi wa maarifa,’ Meneja huyo wa Tigo alimaliza.
Tigo ni mdau muhimu wa elimu na imetoa michango mbali mbali kuinua viwango vya elimu nchini. Mwaka jana Tigo ilichangia madawati zaidi ya 7,100 katika shule za mzingi nchini kote. Vilevile Tigo imetoa kompyuta 77 zilizounganishwa na mtandao wa kasi zaidi wa Tigo kwa vituo vya elimu ya juu nchini. 

ZAIDI YA MILIONI 400 KUTUMIKA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ENEO LA PONGWE HADI MUHEZA

September 21, 2017
Mhandisi wa Mradi wa Maji kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kutoka kampuni ya Koberg Construction Co.Limited Mhandisi Stepheni Kingili kushoto akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu namna watakavyoanza kutekeleza mradi huo kuanzia kesho(leo) wakati wa halfa ya makabidhiano ya vifaa vya mradi huo yaliyofanyika ofisi ndogo za mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) eneo la Pongwe
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ndogo za mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa,Mhandisi Joshua Mgeyekwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akiingia kwenye halfa hiyo

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu

Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa halfa hiyo 
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza katika halfa hiyo
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza katika halfa hiyo
 Sehemu ya wagen kutoka maeneo mbalimbali waliojitokeza kushuhudia makabidhiaano haayo
 Sehemu ya wadau waliohudhuria makabidhiano hayo eneo la Pongwe Jijini Tanga
 Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajaabu wa pili kutoka kulia akiongozana na baadhi ya viongozi kukagua mabomba yatakayotumikaa kwenye mradi huo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Luiza Mlelwa na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo ambao utatoa maji Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani Muheza
Moja kati ya vifaa mbalimbali vitakayotumika kwenye mradi huo.


 Sehemu ya Mabomba ambayo yatatumika kwenye mradi huo mkubwa utakaogharimu zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya kutoa maji eneo la Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani Muheza

WANANCHI wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga wataondokana na adha ya
huduma ya maji baada ya Serikali kutenga fedha zaidi ya milioni 400 kwa ajili mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza.

Hatua hiyo ina lenga kuondoa changamoto ya uhaba wa maji wilayani
  Muheza ambayo ilikuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi kutokana na kutumia muda mwingi kusaka
huduma hiyo badala ya kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

Akizungumza jwakati wa kukabidhi mabomba yatakayotumika kwa mkandarasi wa
  mradi huo katika eneo la Pongwe Jijini Tanga, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi  Rajabu alisema mradi huo utakuwa ndio mkombozi mkubwa kwa wananchi.

Alisema mradi huo ambao ni mkubwa ni moja kati ya ahadi za Rais John
  Magufuli alipofanya ziara mkoani Tanga ambapo alihaidi kuhakikisha wakazi wa mji huo wanaondokana na changamoto ya uhaba wa maji.

"Kwanza nimshukuru mh Rais kwa kutekeleza ahadi yake mapema jambo
  ambalo limetupa faraja kubwa sisi wakazi wa Muheza na vitongoji vyake lakini niwaambie katika mradi huu nitakuwa mkali sana na nitafuatilia kila mwezi kuhakikisha unajengwa kwa viwango kutokana na thamani ya fedha"Alisema.

Aidha alimsisitizia mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kuhakikisha
  ajira zitakazotolewa ziwalenge vijana waliopo katika maeneo hayo ili kuweza kupunguza ukali na ugumu wa maisha kwao na jamii zinawazunguka.

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya
  Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi ya maji inayotarajiwa kutekelezwa wilayani Muheza ili kumaliza tatizo la maji wilayani humo.

Alisema katika mradi huo mamlaka hiyo imetumia zaidi ya milioni 30
  katika bajeti zake kufanya tathimini ya mradi huo huku serikali itokea fedha zote ambazo zitatumika katika mradi huo ambao utakwenda sanjari na ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji eneo la Kilapura litakalokuwa na ujazo wa lita laki saba.

"Lengo la mamlaka ya maji na serikali ya wilaya ya Muheza pamoja na
  Mbunge wa Jimbo hilo kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya huduma ya maji ambayo ndio kilio chao kikubwa kwa wilaya hiyo "Alisema.

Akizungumzia suala la utunzaji wa mradi huo,Mhandisi Mgeyekwa alisema
  mradi huo ni mali ya wananchi hivyo lazima wahakikishe wanakuwa mabalozi wazuri wa kulinda miundombinu ya maji ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.

Naye kwa upande wake,Mkandarasi wa Mradi  huo kutoka Kampuni ya Koberg
  Construction Limited,Mhandisi Stephen Kingili alisema mradi huo utatekelezwa kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Muheza kuweza
kunufuika na huduma hiyo.

Alisema utekelezaji wa mradi huo utaanza kutekelezwa kesho (Septemba 21) ambao
  utakamilika Mei 19 mwakani ukichukua miezi 8 ili kuweza kukamilika na hivyo wananchi kuweza kuutumia.

Aidha alisema mradi huo utakuwa na urefu wa km 16.9 kutoka eneo la
  Pongwe Jijini Tanga mpaka Muheza mjini ambao utakwenda sambamba na maungio ya kuchepusha maji katika vijiji vyote utakaopita ili kuwarahisishia wananchi kuweza kujiunganishia huduma hiyo pindi wanapokuwa wakihitaji.

WAKAZI WA ARUSHA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MKANDARASI

September 21, 2017
 Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo akimueleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4. Kushoto ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale.
 Mafundi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V wakiendelea na ujenzi wa moja kati ya madaraja makubwa saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.
 Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) hatua mbalimbali za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), wakati Waziri huyo alipoikagua, mkoani Arusha.
 Moja kati ya madaraja saba yanayojengwa katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.
 Tingatinga likiendelea na kazi ya ujenzi wa awali ya madaraja katika barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4, jijini Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering Bw. Shin Soo (katikati)alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil-Jiangsu J/V ili kuweza kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara ya mchepuo (Arusha bypass), inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 42.4.

Akikagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo mkoani humo, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na hivyo kuvutia watalii na kukuza uchumi wa mkoa.

"Kukamilika kwa barabara hii ya Arusha bypass kutapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano kwani magari makubwa ya mizigo yatatumia mchepuo huu na kurahisisha huduma za usafirishaji jijini Arusha", amesema Waziri Mbarawa.Ameongeza kuwa Wizara yake itasimamia kwa ukaribu ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyostahili vilivyokubalika.

Aidha, Prof. Mbarawa ameupongeza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani humo kwa usimamizi mzuri wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Ven Ndyamukama, amesema Wizara kwa kushirikiana na TANROADS itaendelea kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanajengwa kwa viwango vilivyopo kwenye usanifu wa kina (Detail design), na thamani ya fedha inapatikana.

Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Mhandisi Johnny Kalupale, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili akamilishe mradi kwa wakati kama walivyokamilisha ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru KM 14.1 na kwa ubora unaostahili.

Mhandisi Kalupale, ameeleza changamoto zinazoikabili barabara hiyo kuwa ni wingi wa  udongo wa tifutifu na  mfinyanzi na hivyo kulazimu Usanifu wa kina wa barabara hiyo kurudiwa upya.

Ujenzi wa Barabara ya Arusha bypass unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 67 ikiwa ni ushirikiano wa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ujenzi wake utahusisha madaraja makubwa 7, maboksi kalvari 55 na madaraja ya bomba 55.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

SALAMU ZA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI

September 21, 2017

Pamoja kwa ajili ya Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa Wote
Hii Siku ya Kimataifa ya Amani huadhimisha nguvu ya ushirikiano wa kimataifa katika kujenga ulimwengu wa amani na endelevu.
Jambo hili linazidi kuwa ni la muhimu sana hasa wakati huu tunapokumbana na changamoto zisizo za kawaida. Nguvu mpya za mgawanyiko zimeibuka, zikieneza chuki na kuondoa kuvumiliana. Ugaidi unachochea vurugu, wakati misimamo mikali inapandikiza sumu ndani ya fikra dhaifu za vijana. Katika maeneo maskini zaidi ya dunia na yasiyo na maendeleo, majanga ya asili yanayohusiana na hali ya hewa yanazidisha hali ya kukosa utulivu, yakiongeza idadi ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao na kuongeza zaidi hatari ya kutokea kwa vurugu.
Vikwazo vya kuifikia amani vina utata mwingi na ni vigumu sana - hakuna nchi moja peke yake inayoweza kuviondoa vikwazo hivyo. Jambo hili linahitaji aina mpya ya mshikamano na hatua za pamoja, na kuanza kuchukua hatua hizo mapema iwezekanavyo.
Hiki ndicho kilichoko katika moyo wa wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kuongeza jitihada zinazolenga kuendeleza amani, kuzishirikisha Serikali na mashirika ya kiraia, pamoja na jumuia za kimataifa na za kikanda.
Mabadiliko yanaenea duniani kote kwa kasi kubwa – ni lazima lengo letu liwe kuyapokea mabadiliko hao katika misingi ya haki za binadamu, kuyapa mwelekeo chanya utakaotupeleka kwenye dunia iliyo ya haki zaidi, jumuishi zaidi na endelevu zaidi.
Utamaduni wa amani ni utamaduni wa mazungumzo na kuzuia uvunjifu wa amani, na katika muktadha huu, jukumu la Umoja wa Mataifa halijawahi kuwa la muhimu sana kama wakati huu. Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu inathibitisha kwamba "hawezi kuwa na maendeleo endelevu bila amani na hakuna amani bila maendeleo endelevu". Moyo huo huo unaungwa mkono na maazimio ya Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Usalama na Mkutano Mkuu ya mwaka 2016 yanayohusu “amani endelevu”.
Tunahitaji namna mpya yenye kina zaidi, itakayoshughulikia sababu za msingi, na kuimarisha utawala wa sheria na kukuza maendeleo endelevu, yote haya katika misingi ya majadiliano na kuheshimiana. Hii ndiyo dira ya hatua zote za UNESCO za kujenga amani kupitia elimu, uhuru wa kujieleza, majadiliano kati ya tamaduni mbalimbali, heshima kwa haki za binadamu na kutambua uwepo wa tamaduni mbalimbali na ushirikiano wa kisayansi.
Katika hii Siku ya Kimataifa ya Amani, imetupasa wote tuweke upya ahadi na nia zetu za kujenga umoja wa kimataifa. Ili kuendeleza amani, ni lazima tuijenge amani kila siku, katika kila jamii, na kila mwanamke na mwanaume, kwa kufanya kazi pamoja ili kufikia wakati ujao ulio bora zaidi kwa wote.

Tamasha la Kimataifa la 36 la Sanaa Bagamoyo kufanyika 23-30 Septemba Bagamoyo

September 21, 2017

Lile tamasha kubwa na la aina yake la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo limewadia kwa msimu huu wa 36, ambapo litafanyika kuanzia 23-30 Septemba mwaka huu katika viwanja vya TaSUBa, Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.
Wakizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar e Salaam, waandaaji hao wamebainisha kuwa maandalizi yote ya tamasha hilo kongwe Barani Afrika yameshakamilika na sasa ni kufanyika huku wakiwaomba wadau wa Sanaa na watu mbalimbali kujitokeza kulishuhudia tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mtendaji Mkuu wa TaSUBa , Dk. Herbert  Makoye amesema Tamasha hilo kwa mwaka huu ni la  kipekee huku likiwa na kauli mbiu ya kupiga vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo dunia inapambana na dawa  hizo hatari kwa maisha ya watu hasa vijana wadogo.
“Sanaa na Utamaduni katika Kupiga Vita Madawa ya Kulevya”  ikiwa ni mahsusi katika kuunga mkono mapambano ya vita dhidi ya usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
Tamasha la Kimataifa Sanaa na Utamaduni Bagamoyo hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ikiwa na malengo ya Kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa Mtanzania, Kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa Tasuba wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka katika fani za sanaa za maonyesho na zile za ufundi”  ameeleza  Dk. Herbert  Makoye.
Dk. Makoye ameweka wazi kuwa, vikundi zaidi ya 60, vitapamba kwenye tamasha hilo la 36 na litapambwa na ngoma za asili, muziki, sarakasi na maigizo pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi huku pia kukiwa na warsha na semina zitakazohusu mambo mbalimbali ya kijamii.
Kati ya vikundi hivyo zaidi ya 60, vilivyothibitisha kushiriki, kati ya hivyo vikundi Saba ni kutoka nje ya nchi  ikiwemo Kenya, Ufaransa, Korea Kusini, Uingereza, Zimbabwe na Mayyote.
“Katika ufunguzi wa tamasha letu mwaka huu, Mgeni rasmi  anatarajiwa kuwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dk Harrison  Mwakyembe (Mb) huku tukio la kufungwa likitarajiwa kufanyika na  Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tamsha hilo, John Mponda  amesema tamasha hilo limekuwa kongwe kutokanana malengo mbalimbali ikiwemo kukuza tamaduni za Watanzania wa maeneo yote.
“Tamasha hili utengeneza jukwaa moja lenye kujenga mahusiano mema  ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho hayo na pia kubadilishana uzoefu na mawazo katika kuendeleza tasnia ya sanaa. Kwa mwaka huu pia tumeweeza kutenga muda muafaka kwa shule mbalimbali kufika kushuhudia kwa muda wa kawaida yaani mchana.” Alieleza Mponda.
Aidha,  Mponda alitaja viingilio kwenye tamsha hilo kuwa kwa Wanafunzi ama wanafunzi wa Vyuo watakaofika kuanzia 100, watalipia punguzo la Tsh 500, kwa kila mmoja huku kwa watoto  wadogo ama wanafunzi kawaida kiigilio ni Tsh. 1000 na Kawaida kwa watu wote ni Tsh.3000 na kwa Raia wa Kigeni ni Tsh. 5,000.
Uongozi huo wa TaSUBa umewakaribisha watu wote huku tayari wakiwa wameshaweka sawa masuala ya Ulinzi na Usalama pamoja na Afya kwa watu wote wanaofika kwenye tamasha hilo.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk. Herbert Makoye akizungumza  na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha hilo la kimataifa la 36, litakalofanyika mjini Bagamoyo, kushoto ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo John Mponda. Kulia ni  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus 
Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa Bagamoyo, John Mponda akizungumza wanahabari wakati wa kutangaza kwa tamsha hilo litakaloanza keshokutwa Septemba 23. Kulia ni  Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk. Herbert Makoye.

AVUNJWA MGUU KWA RISASI

September 21, 2017
Mkazi wa kitongoji cha Endevesi ,kata ya Oljoro wilaya ya Arumeru,Hwanga Ndaskoy(30)amefunjika mkuu wake wa kulia baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni askari polisi mkoani Arusha, wapatao nane kumvamia na kumpigwa risasi ,akiwa shambani kwake .

Akizungumza kwa masikitiko nyumbani kwake, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mount Meru alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja,Ndaskoy ameeleza kwamba tukio hilo limetokea mnamo,Agost 31,mwaka huu majira ya saa saba wakati akivuna mahindi shambani kwake akiwa na familia yake.
Alisema kua alifuatwa na askari hao waliokuwa wamevalia kiraia na mmoja  mwenye silaha akiwa amevaa sare za kipolisi.
Pia askari hao walikuwa wameongozana na mkazi mmoja wa kitongoji hicho aliyemtaja kwa jina la ,Yohane Palay aliyemtambua kuwa ni baba mkwe wake .

‘’Nilimsikia baba mkwe akiwaelekeza askari hao wanikamate huku akiwatahadhalisha kuwa mimi ni mkorofi na wasinisogelee nitawakata na sime jambo ambalo sio kweli,ndipo askari mmoja mwenye silaha aliponifyatulia risasi  ya mguu na kuanguka chini’’alisema Ndaskoy
Aidha alisema askari baada kumpiga risasi walimpakia kwenye gari lao na kumpeleka katika hospital ya Mkoa Mt,Meru ambapo walimweleza daktari kuwa ameanguka na pikipili Jambo ambalo si kweli.

Alieleza kuwa kabla ya tukio hilo ,Agost 26 mwaka huu ,aligombana na mke wa kaka yake aitwaye ,Jehova Baraka ambaye wanaishi jirani baada ya mbuzi kula mahindi yake yaliyokuwa nyumbani .

Alisema ugomvi huo ulienda mbali zaidi kiasi cha kutoleana maneno makali ,ambapo Jehova aliamua kwenda kwa baba yake mzazi aitwaye Yohane Palay na kutoa taarifa kuwa amepigwa na shemeji yake .

Palay aliamua kwenda kituo cha polisi cha Mbauda jijini hapa na kutoa taarifa juu ya tukio hilo,hata hivyo viongozi wa kitongoji hicho wakiwemo wazee wa ukoo waliingilia kati na kumtaka Palay alirejeshe nyumbani ili wazee wa ukoo walipatie ufumbuzi wa kudumu jambo ambalo waliafikiana.

Alisema Kikao cha ukoo kiliketi,agost 30 na kukubaliana kumaliza jambo hilo kwa kuwatoza faini za kimila wahusika wote wawili baada ya kubaini wote wanamakosa,hata hivyo walishangaa kesho yake agost 31 kufuatwa na polisi na kupigwa risasi.

Kwa upande wake,Palay alikiri kupeleka malalamiko yake kituo cha polisi ,Mbauda ,akidai kuwa mtoto wake,ambaye ni mke wa kaka yake na majeruhi alipigwa na kudhalilishwa. Hata hivyo aalikana kuwarubuni Polisi ili wampige risasi mtuhumiwa

Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo alisema kuwa anafuatilia undani wa tukio hilo ikiwemo kubaini ni askari gani walienda kwenye tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi.

"Kwa kweli sina taarifa ya tukio kama hilo ila nitachunguza  kama lipo nitalitolea ufafanuzi" Kauli ya Mkumbo.

Mkumbo alisema analifanyia  uchunguzi jambo hilo kupitia wasaidizi wake na kuahidi kuchukua hatua kali iwapo itabainika hapakuwa na ulazima wa matumizi makubwa ya silaha ya moto kwa askari wake.
Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog 

SHAHIDI AIELEZA MAHAKAMA JINSI DC ALIVYOPEKUWA CHUMBA CHAKE

September 21, 2017


Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
SHAHIDI wa utetezi katika kesi ya kughushi Mukhtasari,wa serikali ya mtaa wa Levolosi ,mfanyabiashara ,Mathew Moleli ameieleza mahakama jinsi mkuu wa wilaya mstaafu  alivyoingia kwa mabavu nyumbani kwake na kuamrisha askari polisi aliokuwa ameambatana nao wapekuwe chumba chake wakitafuta hati inayodaiwa kughushiwa.

Akitoa utetezi  mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha ,anayesikiliza shauri hilo huku akiongozwa na wakili wa utetezi Ephraim Koisenge, aliieleza mahakama hiyo jinsi alivyofedheheshwa wakati askari hao,akiwemo mwendesha bodaboda na mlalamikaji Makanga walivyopekuwa chumba chake wakitafuta hati ambayo ni mali.

Shahidi huyo aliiendelea kueleza kuwa, mnamo oktoba ,2 mwaka 2014 alishtakiwa katika mahakama ya wilaya iliyopo Sekei mkoani Arusha, kwa shauri kama hilo huku mlalamikaji akiwa ni Danny Makanga na baadae oktoba 1,mwaka 2015 kesi hiyo ilifutwa baada ya upande wa jamhuri kuomba kuondoa shauri hilo mahakamani  jambo ambalo anadai linampotezea muda wake.

 Alidai kuwa kufutwa kwa shauri hilo aliandika barua kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa ARUSHA (RCO) kuomba kurejeshewa  hati yake ya nyumba iliyokuwa inashikiliwa ofisi ya RCO, jambo ambalo hakuwahi kujibiwa hadi oktoba ,28 mwaka 2016 alipokamatwa na polisi na kufikishwa  mahakamani akishtakiwa kwa makosa mawili  ya kughushi Mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kuwasilisha nyaraka za kughushi katika ofisi za jiji la Arusha ,

Hata hiyo upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mary Lucas ulimtaka mshtakiwa kueleza uhalali wa eneo anakoishi kwa sasa ,jambo ambalo shahidi huyo alisema ni mali yake na waliuziana kindugu na mlalamikaji Makanga  bila kuandikishana na baadae alifuata taratibu zote za kuomba hati miliki kupitika kikao cha dharura kwa uongozi wa serikali ya mtaa wa Levolosi kilichoketi Septemba,10 mwaka 2006.

Pia shahidi huyo alieleza kuwa tangu kikao hicho cha serikali ya mtaa kiketi kwa dharura na baadae kupeleke maombi ya kupatiwa hati ya umiliki wa nyumba yake kiwanja namba 231 kitalu DD kilichopo Mianziani jijini Arusha ,hakuwahi kupata malalamiko yoyote kuhusu kughushi nyaraka za serikali,jambo ambalo ameiomba mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu malalamiko hayo hayana ukweli wowote.

Kesi hiyo namba 430 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuendelea tena ,Septemba 28 mwaka huu ,ambapo upande wa utetezi unatarajia kufunga utetezi wake kwa shahidi wa pili na wa mwisho baada yashahidi wa kwanza ambaye ni mshtakiwa kukamilisha utetezi,ambaye pia aliwasilisha  nyaraka mbalimbali kama vielelezo mahakamani hapo.

Awali wakili wa serikali Mary Lucasi alipinga kuwasilishwa kwa baadhi ya nyaraka muhimu za mshtakiwa mahakamani hapo kwa madai kuwa nyaraka  hiyo ni kivuli ,jambo ambalo lilipigwa na wakili wa utetezi Koisenge ambaye aliiomba mahakama izipokee kama kilelezo,jambo ambalo hakimu Mwankuga baada ya kuzipitia hoja ya upande wa mashtaka aliona hazina mashiko na kuzipokea ili zitumikea mahakamani hapo kama kielelezo.

SBL yazindua bia mpya ya Pilsner King

September 21, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) Mjumbe  wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma(kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakigonga chupa za kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema usiku wa jana .


Mhudumu akiweka chupa ya Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(katikati)akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(katikati)akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Bw.Christopher Gachuma kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) Mjumbea wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti(SBL) Chacha Gachuma(kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakionja kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema jana usiku.

WAKAGUZI WA NDANI WATAKA TAARIFA ZAO KUFANYIWA KAZI

September 21, 2017

Na Woinde Shizza  wa libeneke la kaskazini blog
WAKAGUZI wa ndani Nchini wamewataka wakurugenzi wa taasisi za umma na sekta binafsi  kuzifanyia kazi taarifa zao za kiukaguzi  na kuacha  kuzikalia pindi wanapokabidhiwa  jambo ambalo linasababisha kupotea kwa ufanisi wa utendaji kazi kwa sekta hizo.


Kauli hiyo imetolewa  jijini Arusha na mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali,Mohamedi Ntonga katika mkutano mkuu wa mwaka wa wakaguzi wa ndani unaowajumuisha wakaguzi kutoka  sekta ya umma na binafsi wakiwemo kutoka nje ya nchi.  


Ntonga alisema kuwa wakaguzi wa ndani wana umuhimu  mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote Duniani hivyo taarifa za kiukaguzi wanapozikabidhi zinapaswa kufanyiwa kazi kwani zinakuwa zimefanyika kitaalamu,hivyo kitendo cha kuzikalia taarifa hizo kinachofanywa na baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi husika kinapelekea kupunguza weledi katika utendaji kazi wao.


Alisema kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa wakaguzi wa ndani katika kubadilishana uzoefu wa taaluma na kukumbushana yale yaliyo muhimu kwa mujibu wa taaluma yao hivyo akiwasihi watanzanzia kuta mbua umuhimu wa kuwatumia wakaguzi wa ndani katika masuala ya uwazi na uwajibikaji.


Aidha akizungumzia faida za wakaguzi wa ndani kuwa wameweza kuibua wafanyakazi hewa,Mishahara hewa ,watumishi wasio kuwa na taaluma,na upotevu wa fedha unaofanyika kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara, na Halmashauri za Serikali .


Kwa upande wake Rais wa Wakaguzi wa Ndani Tanzania Richard Magongo amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakitumika kuchochea mabadiliko ya utendaji kazi ili kukabiliana na wizi wa kimtandao ambao umekuwa ukitumika kutokana na kuongezeka kwa Technolojia Duniani.


Magongo aliongeza kuwa  mkutano huo utajikita kuangalia jinsi gani ya kuzitumia taaluma za wakaguzi ili kuenenda sambamba na mabadiliko ya Technolojia yanayosababisha kuongezeka kwa wizi wa kimtandao .



Akizungumzia changamoto zinazo wakabili wakaguzi wa ndani ni pamoja na kufukuzwa kazi pindi wanapokuwa wamekamilisha taarifa za kiukaguzi zinazoonyesha kugusa maslahi ya baadhi ya watendaji jambo linalowapelekea baadhi yao kuingiwa na uwoga na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.