RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

April 28, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.


Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

April 28, 2016

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA

April 28, 2016
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Butusyo Mwambelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya  (Hawapo pichani)katika kuzngumzia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu katika duka la kuuzia  vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .

Baadhi ya askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .

Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu.


Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya)
JESHI  la Polisi mkoani Mbeya  limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watu watano  wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine , walifika kijijini hapo  kwa lengo la kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji  mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la Matundasi Chunya..
Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha mochwari katika  hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na makazi yao bado hayajajulikana.
Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio  watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo  kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS   aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo .
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza  kurusha  risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka .
Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha msako usiku huo   na kufanikiwa kuwaua majambazi  wengine wawili  ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu hao.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana
bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27  kwenye magazine.  Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja na panga .

Mwambelo  alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao bado hayajatambulika.
Mwisho

WAZIRI MKUU KATIKA MATUKIO YA BUNGENI LEO.

April 28, 2016

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
  Mbunge wa Welezo, Saada  Salum Mkuya akichangia Bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Kushoto ni Mbenge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi  (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Bariadi na Mwenyekiti wa Bunge Mtemi Andrew Chenge kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Aprili 28, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MNADA WA MADINI WAINGIZIA SERIKALI BILIONI 1.6

April 28, 2016

Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Elias Kayandabila akisisitiza jambo kabla ya ufunguzi wa masanduku yenye bahasha za ahadi ya bei za madini yaliyopigwa mnada katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili, 2016. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Zena Kongoi na kushoto ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Sky Associates Faisal Juma Shahbhai inayomiliki mgodi wa Tanzanite One kwa ubia na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo akiangalia maombi ya ahadi za bei ya madini yaliyopigwa mnada katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili, 2016. Wanaoshuhudia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Uchumi na Biashara, Salim Salim (Wa Pili kushoto), Wa Pili kulia ni Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini na Huduma za Kimaabara katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Gilay Shamika na wa kwanza kulia ni Mthamini Almas wa Serikali, Edward Rweyemamu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo akionesha masanduku yenye bahasha za ahadi ya bei za madini yaliyopigwa mnada katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili, 2016. Wanaoshuhudia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Uchumi na Biashara, Salim Salim (katikati) na kulia ni Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini na Huduma za Kimaabara katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Gilay Shamika.
Wadau mbalimbali walioshiriki Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21 wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo (hayupo pichani) wakati akitangaza matokeo ya mnada wa madini uliofanyika katika Maonesho hayo.
Wadau mbalimbali wakishuhudia, Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo akifungua masanduku yenye bahasha za ahadi ya bei za madini yaliyopigwa mnada katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili, 2016.

Na Teresia Mhagama na Asteria Muhozya, Arusha

Serikali imepata jumla ya shilingi bilioni 1.6 ikiwa ni mapato yaliyopatikana katika mnada wa madini uliofanyika wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya Mt.Meru kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili mwaka huu.

Hayo yameelezwa hivi karibuni jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo, wakati akitangaza matokeo ya mnada huo.

Katika maonesho hayo, kulikuwa na Tenda Tatu; Tenda ya Kwanza ilikuwa ya Serikali ikihusisha madini mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na Kamishna wa Madini ambapo jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 1.3 zilipatikana kutokana na mauzo ya madini hayo.

Tenda ya pili ilikuwa ni madini ya Tanzanite ghafi yaliyozalishwa na mgodi wa TanzaniteOne unaomilikiwa kwa ubia kati ya kampuni ya Sky Associates na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

“Napenda kushukuru mgodi wa TanzaniteOne kwani wametuletea madini ya Tanzanite ambayo ni ghafi yenye thamani kubwa ambapo madini yote kutoka mgodi huu yamenunuliwa kwa thamani ya shilingi za Kitanzania Bilioni Tano (5),” alisema Kalugendo.

Kalugendo alisema kuwa tenda ya tatu ya mnada huo ilikuwa ya kampuni ya El-Hilal inayochimba madini ya Almas nchini. Alifafanua kuwa, kampuni mbili zilizojitokeza katika tenda hiyo hazikufikia kiwango cha chini cha bei iliyowekwa na Serikali hivyo kupelekea madini hayo kutokuuzwa katika mnada huo.

“ Hii ni kusema kwamba madini yote ya Tanzanite yaliyoletwa na mgodi wa TanzaniteOne na Tanzanite iliyoletwa na Serikali katika kifurushi cha kwanza pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika kifurushi hicho yameuzwa,” alisema Kalugendo.

Aliongeza kuwa, fedha yote iliyopatikana kutokana na mauzo ya madini yaliyokuwa yakishikiliwa na Kamishna wa Madini, inaingizwa katika mfuko wa Serikali na kwamba madini ghafi yaliyouzwa kutoka TanzaniteOne yatalipiwa mrabaha serikalini wa shilingi milioni 245,686,000 ili madini hayo yaweze kusafirishwa popote.

Aidha, Kalugendo alisisitiza kuwa mapato hayo ni ya mnada tu hivyo mauzo ya jumla ya maonesho hayo yatatangazwa baada ya kujumuisha matokeo ya mauzo yote yaliyofanyika katika Maonesho husika.

Pia, Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini na Huduma za Kimaabara kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Gilay Shamika, akiwa katika Mnada wa Madini yaliyo chini ya Kamishna wa Madini, alitoa wito kwa wafanyabiashara kufuata sheria, taratibu na kanuni za biashara ya Madini ili kutotaifishiwa Madini yao mara wanapokamatwa bila kuwa na vibali husika.

‘Madini haya unayoyaona yakipigwa mnada, yalikamatwa na kutaifishwa pindi yakitoroshwa nje ya nchi bila wahusika kuwa na vibali vya usafirishaji. Ni vema wafanyabiashara kufuata taratibu kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010,’’ Alisema Shamika.

Naye kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim aliwashukuru wadau wote walioshiriki na kudhamini maonesho hayo ambayo ni muhimu katika uendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.

Nape Apania Kuiboresha Tasnia ya Habari

April 28, 2016

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.

Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.

Kwa jinsi hii tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Nchi kwa kutujalia kupata kiongozi wa nchi ambaye ni mchapakazi na aliyejaliwa kipawa cha kuona mbali kwa kuwaweka viongozi wa chini yake katika nafasi za uongozi wanazostahili.

Sekta ya habari ni sekta nyeti na muhimu sana katika dunia hii kwa kua bila kupashana habari na kujua kinachoendelea daima hakutakua na maendeleo kwa hiyo, ni sekta inayohitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuhakikisha kwamba inachukuliwa uzito na inapewa kipaumbele kwa kupewa vifaa na elimu ya kutosha ili kuepusha upotoshaji na kukosekana kwa habari muhimu hasa za Serikali zinazotakiwa kuwafikia wananchi kwa muda husika.

Tukiangalia katika sekta ya habari, Mhe.Rais hakukosea kabisa kumuweka Waziri Mhe. Nape kwa kuwa ameanza kuitumikia Wizara kwa kasi nzuri na ameonyesha nia ya kuiboresha Wizara hasa kwa tasnia ya habari kwa kuanzia kwenye wizara yake hadi katika ofisi za umma zilizoko mikoani ili kuhakikisha wanahabari wote nchini wanatambua thamani ya kazi yao. 

Kwa maneno yake aliyoyatoa Jijini Mbeya alipokua akigawa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya mawasiliano yaani ipad kwa maafisa mawasiliano wa mkoa huo alikaririwa akisema,"Nataka Wizara ihamie mikoani" hii haimaanishi kuwa Wizara ihamie mikoani kama alivyosema bali alimaanisha kiutendaji zaidi kuwa yale yote anayoyafanya katika Wizara yake atahakikisha na maafisa wa mikoani pia wanafanyiwa hivyo ikiwemo kugawiwa vitendea kazi pamoja na mambo mengine. 

Katika kuhakikisha hilo, kwa upande wa sekta ya habari, Waziri Nape ameanza kwa kugawa ipad  kwa maafisa mawasiliano walioko mikoa ya pembezoni ambao wana upungufu mkubwa wa vitendea kazi na kwa muda mrefu wameshindwa kuifanya kazi yao kwa ufanisi kwa sababu ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi hiyo.

Ipad hizo zilizotolewa kama msaada kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kampuni ya Startimes ambayo imeahidi kuwa bega kwa bega na Wizara hii  katika kuisaidia ili kuongeza ufanisi hasa katika sekta hii nyeti ya habari maana kwa maneno mengine tunaweza kusema sekta ya habari ndio daraja linalounganisha serikali na wananchi.

Siku aliyokabidhiwa ipad hizo Mhe. Nape alikaririwa akisema "Nawashukuru sana Startimes kwa kutujali,ipad hizi tutaanza kuzigawa kwa maafisa habari wa mikoa ya pembezoni kwa kuwa ndiko kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa kwa maafisa hao"alisema Mhe Nape.

Maneno haya ya Mhe.Nape yanaungana na usemi wake wa kuifanya Wizara kuhamia mikoani kwa maana ya kuwapa kipaumbele katika kuwapatia vitendea kazi ili nao wasijione kuwa wametengwa au kutokuthaminiwa kama maafisa mawasiliano wengine hasa walioko Dar es salaam na mikoa mingine iiliyoendelea. Maana anaamini kuwa mikoani ndiko kuna wadau na ndiko ziliko shughuli nyingi kwa kuwa watu wengi wenye uwezo wa kuzikuza tasnia anazozifuatilia wapo mikoani.

Ni mengi sana Mhe.Nape ameyaongea hasa kwenye ziara zake alizozifanya kwenye baadhi ya mikoa kama Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita, Simiyu,Dodoma, Kagera pamoja na Mwanza ambako alipita kugawa ipad na kuangalia jinsi maafisa habari wanavyofanya kazi katika vituo vyao vya  kazi. Ziara hiyo pia inalenga katika kujua changamoto wanazokumbana nazo ili kuweza kufanya kila kinachowezekana kuzitatua ili kufanya sekta hii kufanya kazi ya kupeleka taarifa kwa wananchi kama inavyopaswa kufanyika ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari Mkuu Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Kiongozi huyu ameongelea kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishirikisha wadau mbali mbali hasa wahariri pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari kutoa maoni yao ambayo kwa asilimia 99 maoni hayo yamewekwa katika muswada huo.

"Muswada huo umeshakamilika, uko tayari kufikishwa bungeni, pia nataka niwathibitishie kuwa muswada huo utalinda maslahi ya waandishi wa habari kuanzia mishahara yao, mikataba ya kazi zao pamoja na bima ya matatizo wanayoyapata kwenye kazi zao lakini muswada huo utakua na sheria zitakazobana ufundishwaji wa masomo ya habari ili tupate waandishi ambao wamebobea katika fani hiyo" alisema Mhe. Nape.

Ndoto ya changamoto zinazoikabili tasnia ya habari mikoani zinakaribia kuwa historia kwa kuwa Waziri Nape amepanga kuleta teknolojia mpya na kuzitoa zile zilizopitwa na wakati ili kuharakisha ufanisi wa utoaji wa taarifa, kuweka busta kwa baadhi ya maeneo ili televisheni ya taifa (TBC) iwe bora zaidi na kuongeza urefu wa minara ili matangazo yafike mbali zaidi.

Waziri Nape ameamua kuboresha urefu wa minara ili matangazo yafike mbali kwani mikoa mingi ya pembezoni imepakana na nchi ambazo teknolojia zao za mawasiliano ni kubwa kiasi kwamba wananchi wengi wa mipakani wanasikiliza redio za nchi jirani na kuacha kusikiliza redio za hapa nyumbani Tanzania.

Katika harakati za kuboresha tasnia ya habari, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla ameelezea changamoto na jinsi alivyopanga mikakati ya kusaidia na kuiboresha tasnia hii mkoani kwake ambapo alikaririwa akisema "Mkoa wangu unaomba kibali cha kuajiri maafisa habari ili kila Halmashauri iwe na afisa habari wake pia naahidi kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya maafisa hao".

Wakati huo huo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wananchi kuanzisha vituo vya utangazaji 19 katika Wilaya na Halmashauri mbalimbali na wamewaomba wadau kutuma maombi kabla ya Aprili 29 mwaka huu.

Akiongea katika mkutano wa Mhe.Nape na wadau wake, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Lilian Mwangoka alisema, "Mamlaka ya Mawasiliano ipo tayari kushirikiana na wananchi kuongeza vituo vya utangazaji ili kuongeza idadi ya vituo na kuongeza fursa katika ukusanyaji wa kodi".

Aidha, Waziri Nape amesisitiza suala la maafisa habari kupewa ruhusa ya kushiriki katika vikao vya maamuzi ili wajue mambo yanayoendelea katika ofisi zao kwani kufanya hivi kutasaidia maafisa habari kuacha kuwakimbia waandishi wa habari na badala yake kuwapa taarifa kamili ili wakawajulishe wananchi taarifa sahihi kuhusu Serikali yao.

Akiongea kwa kujiamini Waziri Nape amehakikisha kuwa yote yatawezekana maana fedha za kutatua kero hizo zitapatikana kwa kuwa Mhe.Rais tayari alifanya maamuzi ya kuziamuru taasisi zote za Serikali zilizopewa huduma ya kutoa matangazo yao kupitia Televisheni ya Taifa bila kulipa waanze kulipa madeni yao mara moja kwa hiyo fedha hizo ndizo hasa zitatumika katika kuboresha tasnia hii.

Sasa ni wakati wa maafisa habari pamoja na waandishi wa habari wote nchini kuunga mkono jitihada za waziri wetu kwa kufanya kazi za kukusanya na kutawanya taarifa kwa ufanisi na usahihi wa hali ya juu  ili kuifanya jamii ielewe umuhimu wetu pamoja na kukuza uchumi wa nchi kupitia taarifa tunazozitoa kwenye vyombo vya habari.

Wahenga wanasema Taifa lisilo na taarifa haliwezi kukua kiuchumi, litadumaa. Hivyo tumuunge mkono Mzalendo huyu ili kukuza na kuinua Tasnia ya Habari na ionekane kweli kuwa muhimili wanne wa dola ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo.
April 28, 2016

Meneja wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.



Meneja wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam.



 Dar es Salaam, Aprili 28, 2016   Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imeingia   ubia na mgahawa ya Samaki Samaki  ambao ilianzishwa tangu  mwaka 2007  ukiwa na matawi matatu  yaliyopo Mlimani City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam,  ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja  kwa kuleta  bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.

Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo  ni moja ya alama ambazo zinajenga imani  kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha  kupitia migahawa ya Samaki Samaki
Tigo imeweka  mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja  wake kufurahia  intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila  na kunywa  kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula  vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu  utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita  kwenye kuboresha  mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza kwenye kutoa  teknolojia ya kisasa  na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.

 Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema  Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania  na wameungana na Tigo  ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu  nchini kuwapatia wateja wake   kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo  zilivyo  hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa  intaneti. Kwa ushirikiano huu  tutawapatia wateja wetu  miradi mingi mipya, maboresho  pamoja na ofa.

Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu  sisi kupata fedha tu, bali inahusu  ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika  ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza  kufanya kazi pamoja  na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.
Tunaweza kuwa ni  mgahawa unaoongoza kwa vyakula  vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini  tunapenda kufanya  jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu.
Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo  kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja  huduma ya bure ya intaneti  bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.

ATLETICO YAI'BEEP' BAYERN 1-0

April 28, 2016
ATLETICO Madrid jana wamepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwenye uwanja wa Vicente Calderon, jijini Madrid.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa katika dakika 11 na kiungo kinda wa timu ya taifa ya Hispania chini ya miaka 21 (U21), Saul Niguel baada ya kutumia uwezo binafsi na kuwapoteza walinzi wa Bayern.

Katika mchezo huo ambao Bayern walitawala kwa kiasi kikubwa huku wakifanikiwa kulifikia lango la wenyeji mara kwa mara, zilishuhudiwa kadi za njano tano ambapo Atletico walipata moja (Niguez) na Bayern wakizawadiwa nne ambazo zilienda kwa Douglas Costa, Mehdi Benatia, Manuel Neuer na Arturo Vidal.

Kocha wa Bayern, Josep Guardiola alilazimika kufanya mabadiliko matatu akijaribu kupata ushindi au sare kwa kuwatoa Kingsley Coman, Thiago Alcantara na Juan Bernat huku nafasi zao zikichukuliwa na Franck Ribery, Thomas Mueller na Benatia. Kwa upande wa Atletico alitoka Niguez na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas.

Kwa ushindi huo, vijana wa Diego Simeone watakwenda Allianz Arena wiki ijayo wakihitaji ushindi wowote au hata sare ili wafaulu kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya.

MONGELLA AZINDUA MRADI WA UZINDUZI WA MRADI WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA KATIKA MKOA WA MWANZA

April 28, 2016



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.

Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza).




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.

Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza)




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.

Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza)


HOTUBA YA MGENI RASMI, KWENYE UZINDUZI WA MRADI WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA KATIKA MKOA WA MWANZA
APRILI 27, 2016


Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa,
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya,
Ndugu Kiongozi wa Timu ya Mradi,
Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mwanza,
Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri,
Ndugu Wataalam kutoka Sekretarieti ya Mkoa,
Ndugu Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Ndugu Wataalam kutoka TAMISEMI na Taasisi zingine za Serikali,
Ndugu Watendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma na Binafsi,
Ndugu Wakuu wa Idara kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Ndugu wana Habari,
Ndugu Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.


Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sisi sote afya njema na kutuwezesha kufika mahali hapa salama.  Aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Sekretarieti ya Mkoa na Timu ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa maandalizi mazuri ya Mkutano huu wa uzinduzi wa Mradi. Nawashukuru Wageni waalikwa wote kwa kukubali mwaliko wa kushiriki katika Mkutano huu muhimu.

Binafsi nimefarijika sana kwa kunipa heshima kubwa ya kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi huu wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma “Public Sector Systems Strengthening (PS3)” kwa mkoa wa Mwanza.

Ndugu Washiriki,
Mkoa wa Mwanza umekuwa na bahati kubwa ya kuwa mmoja kati ya Mikoa 13 hapa nchini ambayo itafaidika na mradi huu.  Ninafahamu kwamba mradi huu umezinduliwa katika Mikoa ya Iringa, Shinyanga, Dodoma, na Morogoro. Nimeambiwa hivi sasa Mkoa wa Mwanza unafanya uzinduzi sambamba na Mikoa ya Mbeya na Mtwara. Natoa shukrani zangu za dhati kwa Watu wa Marekani ambao ndiyo wafadhili wa Mradi huu, kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Ndugu Washiriki,
Mradi huu wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma umeanza kwa wakati muafaka. Kama mnavyofahamu, tayari kuna juhudi kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali yetu chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Juhudi hizi zinadhihirisha kwamba serikali ina dhamira njema ya kuhakikisha inawahudumia wananchi ipasavyo, na kwamba mifumo iliyopo Serikalini inakuwa na Tija kwa ajili ya kumsaidia mwananchi katika Taifa letu.

Serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani kwa ari kubwa ya kuchapa kazi na juhudi kubwa zimekuwa zikifanyika katika kurekebisha mifumo tuliyo nayo hivi sasa.  Ni imani yangu kuwa Mradi huu utakuwa tija kwa utoaji wa huduma bora za Serikali kwa wananchi.

Leo tumejumuika pamoja na  Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya na Watendaji mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, hii ni  ishara kubwa  kuonesha kuwa kazi ambayo Mradi huu unalenga kufanya ni kubwa na muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Mkoa wetu wa Mwanza na Taifa kwa ujumla. Ni vizuri tukatambua umuhimu huo na kushirikiana kikamilifu na Wataalam wa mradi ili kuhakikisha kwamba lengo lililokusudiwa linafikiwa.

Ndugu Washiriki,
Kuanzia miaka ya 1990, Serikali ilikuwa ikitekeleza Maboresho katika Sekta ya Utumishi wa Umma kwa awamu mbalimbali, na katika awamu hizo, moja ya maboresho ambayo Serikali ilitekeleza ilikuwa ni Mpango wa Kurekebisha Utumishi Serikalini (Civil Service Reform Programme).  Baadhi ya mambo muhimu yaliyokuwepo kwenye mpango huo ni kuweka utaratibu ambao ungeondoa wizi wa fedha za Umma uliokuwa ukifanywa kwa njia mbalimbali kama vile kuwepo kwa Watumishi hewa.

Chini ya Programu hiyo ya kuboresha Utumishi wa Sekta za Umma, Serikali imeweka Mifumo ya Kimenejimenti kwa kusaidia kuongeza uwajibikaji katika shughuli za Serikali. Maeneo ambayo yamekuwa yakishughulikiwa, ni pamoja na uwekaji Muundo mpya wa Utumishi wa Umma, Uboreshaji utendaji kazi, Uboreshaji maslahi ya Watumishi, na Uboreshaji mifumo ya kumbukumbu, Nyaraka na taarifa za watumishi. Pia eneo lingine muhimu lililoangaliwa ni la kujengea watumishi uwezo zaidi katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Ndugu washiriki,
Serikali imeanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao unalenga kutoa msukumo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali tuliyojiwekea kwa ufanisi mkubwa zaidi. Moja ya mambo yanayozungumzwa kwenye Mpango huu ni kuimarisha mifumo kwa sababu bila mifumo imara utekelezwaji wa kazi tulizojipangia hauwezi kufanikiwa.

Kwa wale wafuatiliaji wa mambo yanayoendela hapa nchini, mtakumbuka kwamba wakati Waheshimiwa Wakuu wapya wa Mikoa tulipokuwa tunaapishwa, Mhe. Rais alitupa agizo la kuhakikisha Watumishi hewa wote wanaondolewa kwenye Ankara za Mishahara ndani ya siku kumi na Tano  (15). Hii inaonyesha namna tatizo lilivyo kubwa, na namna serikali ilivyokusudia kuliondoa kabisa. Jambo hili lazima litekelezwe,  na huu ndiyo Uimarishaji wa mifumo yenyewe.

Ndugu Washiriki,
Ni muhimu tukumbuke kwamba upatikanaji wa Huduma Bora za Serikali ni haki ya kila raia wa nchi hii. Hata hivyo, ili tuweze kutekeleza kazi za Serikali za kuhudumia Wananchi kwa ufanisi, ni lazima tuwe na mifumo imara. Nimeambiwa kuwa Mradi huu unaouzinduliwa leo katika Mkoa wa Mwanza utashirikiana na Serikali na Sekta nyingine katika maeneo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia, Rasilimali watu, Fedha, Mifumo ya Mawasiliano, na Tafiti Tendaji.  Haya ni maeneo muhimu ambayo bila shaka yatazipa Halmashauri zetu uwezo wa kumhudumia mwananchi kwa ufanisi zaidi.

Uwepo wenu Watendaji wa ngazi ya Mkoa na Halmashaurini muhimu sana katika uzinduzi huu, kwa sababu ninyi ndio mnaotegemewa kutekeleza shughuli za Serikali katika maeneo yenu, na ndio wenye mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi wa kawaida. 

Napenda kutoa  Rai kwa Watendaji wote wa ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa mnatoa ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi bega kwa bega na wataalam wanaoendesha Mradi huu wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma. Kwa kutambua na kufahamu kwamba mradi huu ni wa kwetu kwa manufaa ya nchi yetu, hivyo uwajibikaji ni muhimu ili kuhakikisha kwamba mradi huu unakuwa na mafanikio makubwa.

Ndugu Washiriki,
Sisi sote tuliopo mahali hapa tunao wajibu wa kuitekeleza Falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba mifumo tuliyo nayo inaboreshwa na mradi huu unafanikiwa kikamilifu. Ni matumaini yangu kuwa katika siku mtakazo kuwa hapa kujadiliana namna ya kutekeleza Mradi huu katika Halmashauri zenu, mtaandaa Mpango Kazi wa utekelezaji wa shughulina kuainisha maeneo ya vipaumbele ambayo mna uhakika kwamba ndiyo yenye tija katika kutekeleza Mradi huu kwa ushirikiano.

Mwisho,  napenda tena kutoa shukrani zangu za dhati kwa timu ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa utayari wao wa kuusaidia Mkoa wetu katika Mradi huu na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Karibuni sana katika Mkoa wa Mwanza.

Baada ya maelezo haya, sasa napenda kutamka kwamba Mradi huu wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma umezinduliwa Rasmi Mkoani Mwanza.

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA