RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika
Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe
wake,Picha na
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika
Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe
wake,Picha na Ikulu.07/05/2017
……………………………………………………………………….
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Djibouti Ismail Omar Guelleh
ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuanzisha
uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo hasa katika sekta za
maendeleo na uchumi.
Viongozi
walifanya mazungumzo katika ukumbi wa Ikulu ya Djibouti ambapo Rais Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na shukurani kwa Rais Guelleh
kwa mwaliko wake huo nchini mwake.
Katika
mazungumzo hayo viongozi hao kwa kauli moja walieleza haja ya kuanzisha
uhusiano na ushirikiano katika sekta mbali mbali za maendeleo na uchumi
kwa manufaa ya pande mbili hizo.
Rais
wa Djibouti Ismail Omar Guelleh kwa upande wake alimuhakikishia Dk.
Shein kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Zanzibar katika
kuimarisha sekta za mawasiliano, utalii, uwekezaji pamoja na usafiri na
usafirishaji sambamba na utayari wa kujifunza mambo mbali mbali kutoka
Zanzibar ikiwemo sekta ya utalii.
Rais
Guelleh, alieleza kuwa nchi yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano
uliopo kati yake na Tanzania ambao una historia nzuri na kueleza kuwa
Djibout iko tayari kujifunza mbinu zilizotumika na Zanzibar katika
kuimarisha sekta ya utalii.
Ambapo
pia, kiongozi huyo alieleza utayari wa kushirikiana na Zanzibar
kutokana na mafanikio waliyoyapata na njia sambamba na mikakati
waliyoitumia katika kufikia mafanikio waliyoyapata na mikakati
waliyoitumia kufikia mafanikio waliyonayo hasa katika suala zima la
uimarishaji wa bandari, mawasiliano na vitega uchumi.
Kiongozi
huyo wa Djibouti alimkaribisha Dk. Shein pamoja na ujumbe wake nchini
humo huku akisisitiza kuwa Tanzania na Djibouti zina ukaribu mkubwa na
zimekuwa zikishirikiana katika kupambana na uharamia wa baharini kupitia
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Mamlaka ya Serikali ya Kimaendeleo
(IGAD).
Aidha,
Rais Guelleh alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Shein mafanikio
yaliyopatikana nchini mwake hasa kutokana na uimarishaji wa bandari,
mawasiliano na kueleza azma ya nchi yake hivi sasa kujikita katika sekta
ya utalii kutokana na baadhi ya vivutio vilivyopo ikiwemo Ziwa Assal
ambalo chimbuko lake ni Bonde la Ufa pamoja na mambo mengineyo.
Hivyo
kiongozi huyo alimueleza Dk Shein kuwa pande hizo mbili zina mengi ya
kujifunza kwa pamoja kwani kila upande umeweza kupata mafanikio yake.
Kwa
upande wake Rais Dk. Shein, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na
shukurani kwa Rais Guelleh kwa mualiko wake huo aliompa pamoja na
mapokezi makubwa aliyoyapata yeye na ujumbe aliofuatana nao na kueleza
kuwa ziara hiyo itakuwa ndio kichocheo kikubwa cha mashirikiano kati ya
Zanzibar na Djibouti.
Dk.
Shein alimueleza Rais Guelleh kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza
kutoka Djibouti hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo wa kiuchumi inategemea
sekta ambazo Zanzibar nayo imeamua kwa makusudi kuziimarisha ili ziweze
kuimarisha uchumi na kuleta tija.
Alizitaja
miongoni mwa sekta hizo ambazo Djibouti imepata mafanikio ni uendeshaji
wa Bandari,mawasiliano na Maeneo Huru ya Kiuchumi ambayo yamekuwa ndio
kichocheo kikubwa cha uchumi wa nchi hiyo.
Aidha,
Dk. Shein alieleza kuwa ziara hiyo ni kielelezo cha urafiki, heshima na
udugu baina ya Serikali zote mbili pamoja na wananchi wake ambapo
itasaidia sana kuimarisha uhusiano na kuibua maeneo mapya ya
ushirikiano.
Katika
maelezo yake, Dk. Shein alimueleza Rais Guelleh kuwa Zanzibar katika
ziara hiyo ina hamu kubwa ya kufahamu maendeleo makubwa yaliyofikiwa na
Djibouti tokea mwaka 1977 ilipopata uhuru wake kutoka kwa Koloni la
Kifaransa.
Dk.
Shein alieleza kuwa ana hamu kubwa kuona maendeleo yaliofikiwa na nchi
hiyo katika sekta muhimu za kiuchumi na kijamii ikiwemo sekta ya
bandari, kuendeleza maeneo Huru, mawasiliano, uvuvi, viwanda, usafiri na
usafirishaji, afya, elimu na sekta zote muhimu za utoaji wa huduma kwa
wananchi wa nchi hiyo.
Alipongeza
juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya nchi hiyo chini
ya uongozi wa Rais Guelleh ambazo zimepelekea Djibouti kuwa ni mfano
mzuri kwa nchi za Afrika ambazo zinatafuta maendeleo ya haraka,
demokrasia pamoja na kuimarisha hali ya utulivu na usalama wa nchi.
Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kumueleza Rais wa Djibouti mafanikio
yaliopatikana kwa upande wa kisiasa na kimaendeleo na kupelekea
kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni Muungano wa
mfano kwa bara la Afrika na kutoa salamu za Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kiongozi huyo.
Aidha,
Dk. Shein alimuhakikishia Rais huyo utayari wa Zanzibar kushirikiana na
Djibouti na kutoa uweledi wake katika sekta ya utalii kwa nchi hiyo
kutokana na Zanzibar kupata mafanikio makubwa katika sekta ya Utalii.
Pamoja
na hayo, Dk. Sheuin alimuelkeza Rais huyi wa Djibout hatua
zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kuimarisha uchumi wake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari mpya ya
Mpiga Duri, mradi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uingizaji
wa mizigo na makontena na kuipunguzia mzigo Bandari ya Malindi.
Aidha,
alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuifanya Zanzibar
kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020, huku akitumia fursa hiyo
kumualika kiongozi uyo wa Djibouti kutembelea Zanzibar kwa lengo la
kuimarisha uhusiano wa pande mbili hizo.
Dk. Shein yupo nchini Djibouti kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Ismail Omar Guelleh.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar