TSN Group Tanzania na MIMOSA CONCIERGE wasaini Mkataba leo Dar es salam

July 17, 2017

TSN Group Tanzania, katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, imeingia mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo.
Meneja Masoko wa TSN, Jahu M. Kessy Pamoja na  Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi wakati wa kusaini mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, leo Meneja Masoko wa TSN alisema, Jahu M. Kessy amesema TSN imelenga kuongeza tija katika kutoa huduma zake.

“Tunarahisisha na kuboresha huduma zetu kuwa bora na za kisasa. Pengine huduma hii itapanua wigo wa wateja wetu watumiao Black Cards kwa Dar es salaam lakini kwa Mwanza TSN Hypermarket inakuwa kampuni ya kwanza kupokea na kukubali malipo kupitia Black card ya Mimosa. Hatua ambayo ni kubwa kuchukuliwa na TSN katika kuwajali wateja wake.”

“Sasa ukifanya malipo kupitia kadi ya Mimosa kwenye supermarket zetu na Petrol station unajiweka katika nafasi ya kushinda punguzo la zaidi ya asilimia 5 pamoja na kuponi ya zawadi wa kwateja watakao tumia kiasi cha shillingi laki moja kwa manunuzi ya mara moja,” alisema Jahu.
Akieleza zaidi juu ya huduma na faida wazipatazo wateja watumiayo kadi hizo, Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi alisema kupitia kadi hii Mteja wa TSN hatapata tu punguzo la bei kutoka TSN pekee lakini pia atapata offer mbalimbali zitokanazo na kadi hiyo kupitia discount partners wengine ambao ni zaidi ya watoa huduma 71 Nchi Nzima. 

Jahu alisema TSN inajiimarisha katika kutoa huduma zake kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia, hivyo basi kuona umuhimu wa kuwapatia wateja wake wenye MIMISA black card nafasi ya kufanya malipo yao kwa uhuru na furaha.

Alisema,”hatua hii inafuatia hatua nyinginezo nyingi tulizochukua kuhakikisha wateja wa TSN wanafurahia huduma zetu, ikiwemo malipo kutupitia miamala ya simu, bank cheques, malipo ya dola na sasa pia kupitia Mimosa Black Card.
Leonce alisema kupitia kadi hii TSN itakuwa ikipokea malipo na kuongezaa tija kwa mteja, lengo ni kuhakikisha mteja mwenye kadi ya Mimosa hashindwi kufanya malipo yake akiwepo katika vionga vyao, na pia kufurahia ofa na punguzo mbalimbali zipatikanazo na mtangamano huu.

 “Teknolojia imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta matokeo chanya siku hadi siku. Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji kazi lakini pia upokeaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa kawaida kumerahisishwa.” Alisema Jahu.
Katika kutambua fursa hiyo, TSN itaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi zinaenda sambamba na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Leonce aliipongeza TSN kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaweka urahisi kwa wateja wake na hiyo imekuwa ni chachu kubwa katika kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.
Makamba Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu na Wajumbe NEMC.

Makamba Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu na Wajumbe NEMC.

July 17, 2017
PIX1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola.
PIX2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akifafanua jambo mbele yanwaandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola na kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
PIX3
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) alipokuwa akitangaza uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na wajumbe saba wa Bodi ya baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
………………………………………………………………………….
Frank Mvungi –Maelezo
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (Mb) ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ili kuongeza tija na kutekeleza kwa vitendo dhana ya Ujenzi wa uchumi wa viwanda.
 Kwa kuzingatia mamlaka  aliyonayo Waziri chini ya Sheria ya Mazingira kifungu cha 19 (2) anaweza kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Baraza hilo na wajumbe wake.
Akizungumza na vyombo vya Habari leo Jijini Dar es Salaam Waziri Makamba amesema kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira  na uharakishaji wa miradi ya maendeleo na uwekezaji hasa ujenzi wa viwanda kama azma ya Mheshimiwa Rais John Magufuli inavyoelekeza.
Kufuatia mabadiliko hayo Waziri Makamba amemteua Dkt. Elikana Kalumanga ambaye ni Mhadhiri katika Taasisi ya Usimamizi na Tathmini ya Rasilimali Asili,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC hadi Rais atakapoteua Mkurugenzi Mkuu.
“Utendaji wa NEMC umekuwa ukilegalega sana na umekuwa hauridhishi na kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wawekezaji  wa ndani na nje ya nchi kuhusu ucheleweshaji na urasimu usiokuwa wa lazima katika mchakato wa tathmini ya athari kwa mazingira (EIA)” Alisisitiza Mhe. Makamba
Aliongeza kuwa ametengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa Bodi ya NEMC ili baadaye ateue wajumbe wapya ambao wataendana na kasi na ari ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuelekea uchumi wa Viwanda, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni Mheshimiwa Rais,ataendelea kuwepo hadi Mheshimiwa Rais atakapoteua mwingine.
Akifafanua Makamba amesema kuwa changamoto nyingine zilizobainika ni kuwaelekeza wawekezaji kwa makampuni ya kufanya Tathmini ya athari za mazingira ambayo yanamilikiwa au yenye ubia na watumishi wa NEMC, bila kujali mgongano wa kimaslahi jambo ambalo haliruhusiwi katika utumishi wa umma.
Jambo jingine ni kuwarundikia maandiko ya miradi ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) watumishi wachache wakati wengine hawana kazi ili waelekeze miradi hiyo katika makampuni ambayo baadaye huwapatia malipo yasiyo halali.
Hatua nyingine zilizochukuliwa na Waziri Makamba ni pamoja na kuiagiza NEMC kufuta watu binfsi na Makampuni yote ya ushauri wa EIA (Consultants) ambayo hayana sifa au yameshindwa kutekeleza kazi zao vizuri na watangaze kwenye magazeti  orodha ya watu na makampuni yanayoruhusiwa kufanya kazi kama washauri elekezi.
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ni muhimu katika kuhakikisha ustawi wa mazingira na mustakabili wa maendeleo endelevu ya nchi tunapoelekea kuwa Taifa la uchumi wa viwanda lazima usimamizi wa mazingira uwe thabiti.

WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA MGAWANYO SAHIHI WA RASILIMALIWATU

July 17, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza katika kikao kazi na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama cha TALGWU, Bw. Ibrahim Zambi akiwasilisha hoja mbalimbali zinazowahusu watumishi wa umma wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Askari Msaidizi wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Germini Massawe akiwasilisha malalamiko kuhusu kada yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Loyce Lugoye akifafanua jambo kuhusiana na masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia mgawanyo sahihi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili kuwa na utendaji bora na wenye matokeo katika utumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoomba kibali cha kuajiri watumishi ni vema akazingatia mahitaji kulingana na majukumu yaliyopo ili kuondoa ziada ya watumishi wa umma wasio na kazi kuendana na fani walizosomea kwa lengo la kuwa na utendaji mzuri.

“Ni vizuri sana wakati tunaomba vibali vya kuajiri watumishi wa umma tukazingatia mgawanyo sahihi wa rasilimaliwatu katika maeneo yetu kulingana na majukumu ya watumishi tunaowahitaji badala ya kuomba watumishi wengi ambao wanasababisha kuwa na ziada ambayo haitumika ipasavyo” Mhe. Kairuki amesema.

Waziri Kairuki amesema katika vibali 10,184 vilivyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, Halmashauri ya Manisapaa ya Ubungo imetengewa jumla ya nafasi 140.

Aidha, ameongeza kuwa, Halmashauri hiyo imetengewa jumla ya nafasi za ajira mpya 397 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hivyo zitendewe haki kwa kuhakikisha watumishi watakaoajiriwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mpango uliopo.

Mhe. Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama kwa lengo la kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

BALOZI ADADI :AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANS

July 17, 2017
Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi
Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo  Julitha Akko
Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari
Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini
MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini.
Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini.

Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya Muheza.

“Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma kwa bidii “Alisema.

Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na sera ya viwanda.

“ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma kwa bidii “Alisema

Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu ili kuona namna ya kulimaliza.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Afisa elimu sekondari wilaya Muheza Julitha Akko amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopatiwa vifaa hivyo kuacha tabia ya kufungia ndani ya makabati na badala yake vitumike kama ilivyokusudiwa.

Aidha alisema kuwa lazima kuwekwe utaratibu wa namna ya kuvitunza vifaa hivyo na kuagiza visitumike kinyume na makusudio yake na kuwataka wanafunzi waelekeze nguvu zao kwenye masomo ili kuongeza wataalamu wengi.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Muheza(Muheza high school) Alex Birumo alisema yapo mategemeo makubwa ya kuongeza ufaulu hasa kwa masomo ya sayansi kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo wanafunzi walikosa fursa kwa miaka mingi kujifunza kwa vitendo.

“Shule yetu hii ni ya masomo ya sayansi ya michepuo ya PCB NA CBG na ni ya kidato cha tano na sita unapokuwa na wanafunzi zaidi ya 150 unawafundisha bila ya vifaa vya maabara kiukweli mafunzo yetu kwa wanafunzi hao yahakuwa na tija”Alisem

UCHIMBAJI NA UCHOTAJI MCHANGA KIHOLELA WASITISHWA

July 17, 2017

Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.

 Katika picha eneo la mto Nyakasangwe lililopo kaika kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.
Eneo la mto Nyakasangwe lililogeuzwa kuwa Dampo na wakazi wa eneo hilo lililopo katika kata ya Bunju. (Picha na Evelyn Mkokoi)

NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga  Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi. 

Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.
Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa  kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.
“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina
Alisema watafanya Operasheni ya  usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba  mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa  hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao. 

USIKOSE UZINDUZI WA ALBAMU YA JERUSALEM CITY SINGERS MWANZA

USIKOSE UZINDUZI WA ALBAMU YA JERUSALEM CITY SINGERS MWANZA

July 17, 2017
Uzinduzi wa albamu ya tatu kutoka kwaya ya JERUSALEM CITY SINGERS ya Bugarika Jijini Mwanza, unatarajiwa kufanyika jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza. Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Samwel Maneno amesema hakuna kiingilio katika uzinduzi huo na kwamba shughuli nzima itaanza majira ya saa saba kamili mchana ambapo waimbaji mbalimbali wakiwemo Born To Praise, Voice Of Calvary na Lake Zone watahudumu siku hiyo. "Hii ni albamu yetu ya tatu ya video iitwayo MUNGU WA AJABU ambapo imetanguliwa na albamu mbili ambazo ni DUNIA MAHUTUTI na HAJAKUSAHAU hivyo nawakaribisha watu wote kushiriki nasi kwenye uzinduzi huo". Amesema Maneno. Usikose uzinduzi huu, ni Jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza, kuanzia saa saba kamili mchana, ambapo hakuna kiingilio. Wasiliana na Jerusalem City Singers 0758 06 10 44[/caption]
Bonyeza HAPA taarifa zaidi

JUMIA NI CHACHU KWA UKUAJI WA BIASHARA ZA MTANDAONI BARANI AFRIKA

July 17, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Mwaka 2017 kampuni ya Jumia ambayo inajishughulisha na huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao barani Afrika inatimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2012.

Kampuni hiyo ambapo awali ilikuwa ikijulikana kama Africa Internet Group (AIG) pindi inaanzishwa imejikita zaidi na shughuli zake mtandaoni katika maeneo kama ya huduma za chakula (Jumia Food), manunuzi ya bidhaa mbalimbali (Jumia Market), hoteli na usafiri wa ndege (Jumia Travel), makazi (Jumia House), magari (Jumia Cars), matangazo (Jumia Deals) na kazi (Jumia Jobs).
Katika kuzikabili changamoto zinazolikabili bara la Afrika kama vile miundombinu hafifu kama vile usafiri wa barabara na anga, umbali wa maeneo na foleni ndefu za barabarani ambazo husababisha watu kupoteza muda mwingi kufika maeneo mbalimbali zote hizi zinatoa fursa kwa kutumika njia ya mtandao wa intaneti ili kuokoa muda na gharama.