BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI TANESCO LAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI

October 07, 2017

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
 KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito E. Mwinuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo kulia akiwa na  Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale wakisikiliza kwa umakini hoja za wafanyakazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi akizungumza katika mkutano huo 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi kushoto akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa Tuico Tanzania,Paul Sangeze akizungumza  katika mkutano huo
Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wajumbe wa baraza hilo
Mmmoja wa wafanyakazi na mjumbe wa baraza hilo akichangia kwenye mkutano huo
mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Janet Vesso akichangia mada
Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi wa pili kutoka kushoto,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kulia na Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze wa kwanza kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale

BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais  Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na ufanisi.
 
Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika linafikia malengo yake muhimu.
Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.
Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ile.
Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA WILAYANI CHATO

October 07, 2017

Na Binagi Media Group
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu 2017, benki ya CRDB jana simetoa semina kwa wateja wake katika wilaya ya Chato mkoani Geita na pia kupokea maoni yao ili kuboresha zaidi huduma zake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini aliwahakikishia wateja wa benki hiyo huduma ya mikopo kwa muda wa siku saba na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kuitumia benki fursa hiyo kukuza mitaji yao ya biashara.

Aidha alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwa ni benki inayoongoza kwa kutoa mikopo hapa nchini huku pia jamii ikiendelea kunufaika na benki hiyo kupitia gawio la faida ambalo hutolewa kila mwaka ili kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

“Tunaomba tuendelee kushirikiana pamoja ambapo CRDB ni benki ya muda mrefu iliyo salama na imara kufanya nayo kazi ikiongoza kwa zaidi ya miaka 10 sasa kwa kutoa huduma bora na zenye riba nafuu nchini”. Alisisitiza Nkini kwenye semina hiyo iliyojumuisha pia wateja wa CRDB kutoka Geita, Muleba, Ngara na Bihalamulo.

Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga alisema benki hiyo imeendelea kuwafikia wateja wake kote nchini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo Fahari Huduma, Simu Banking pamoja na Internet Banking na hivyo kuwa benki yenye mtandao mkubwa unaowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.

“Huduma zetu ni bora kuliko benki nyingine yoyote nchini hivyo natoa rai wateja wetu kutumia huduma zetu ikiwemo mikopo kwa ajili ya mitaji ya biashara zao kwani tunao uwezo mkubwa wa kuwahudumia”. Alidokeza Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus.

Baadhi ya wateja wa CRDB, Mellia Alloyce pamoja na Ristides Ramadhan walikiri kunufaika na benki hiyo kupitia huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mikopo na hivyo kukuza biashara zao huku hivi sasa wakifurahia uharaka wa huduma hiyo tofauti na hapo awali.

Katika hatua nyingine benki ya CRDB ilisaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A katika halmashauri ya wilaya ya Chato ambapo msaada huo ulijumuisha mifuko 150 ya saruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo. Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji CRDB. Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye semina hiyo. Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga akizungumza kwenye semina hiyo. 
        Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas , akichangia mada kwenye semina hiyo.        

NHIF YATOA HUDUMA ZA UPIMAJI KWENYE BONANZA LA MICHEZO JIJINI TANGA LEO

October 07, 2017
 Afisa Mdhibiti wa Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dkt Lawi Kupaza akiangalia taarifa za moja ya wakazi wa Jiji la Tanga ambao walijitokeza kupima uzito,sukari na presha wakati wa bonanza la michezo ambalo limefanyika leo kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 Daktari wa NHIF kushoto akimpima presha Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa bonanza la michezo
Afisa Mdhibiti Viwango na Ubora Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dkt Lawi Kupaza akichukua maelezo ya Ofisa wa Polisi kutoka Ofisi ya RCO,Saidi Mwagara wakati wa bonanza hilo
Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel katikati aliyevaa tisheti ya njano akifuatilia taarifa wakati wa wananchi walipojitokeza kwenye banda lao kwenye bonanza la michezo ambalo lilifanyika viwanja wa shule ya Sekondari Popatlaly kupima afya 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akiwa kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kuangalia zoezi la upimaji wa afya kwa wanamichezo 150 waliweza kupima afya ambapo kati yao
waliokuwa na uzito mkubwa 65,waliokutwa na sukari juu wanne,waliokuwa na Presse sita na wasiokuwa na matatizo 75
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba akiwaongoza askari wa Jeshi hilo kuwavuta kamba Bandari Tanga wakati wa Bonanza hilo leo
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC) Benedict Wakulyamba kulia akifurahia jambo wakati wa bonanza hilo
 Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga,Crispin ngonyani akiwaongoza idara hiyo kuvuta kamba kwenye bonanza hilo

 wa Pili kutoka kushoto ni Afisa wa NHIF Mkoa wa Tanga akiteta jambo na wanamichezo walioshiriki bonanza hilo leo

 Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel kulia kushoto ni Afisa Madai wa Mfuko huo pia Petro Aloyce wakigawa vipeperushi vinavyohamasisha huduma wanazozitoa kwa wanamichezo
 Afisa Madai wa NHIF mkoani Tanga,Marry Daniel kulia akiendelea kuwahamaisha wanamichezo namna ya kuweza kujiunga na mfuko huo
 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga,Sadick Nombo kushoto akibalishana mawazo na Afisa Utumishi Mkoa wa Tanga,Jakobo Kingazi wakati wa bonanza hilo

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akisalimiana na moja kati ya timu zilizokuwa zinashiriki bonanza hilo ambapo alisema michezo ina imarisha mahusiano mazuri kazini na ni muhimu kuimarisha miili yao na kuongeza ufanisi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja

Wateja wa Tigo mkoani Njombe wafurahia huduma zitolewazo na Tigo msimu huu wa Fiesta

October 07, 2017
Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Vaileth Burton akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.
Mtoa huduma wa duka la Tigo mkoani Njombe, Israel Joseph akitoa huduma kwa wateja waliofika dukani leo hapo kupata huduma mbalimbali msimu huu wa Tigo fiesta 2017 ambapo bidhaa za Tigo zinapatikana kwa bei nafuu.

Baadhi ya wateja wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kujipatia tiketi za Tigo Fiesta mkoani Njombe.

RC NCHIMBI AAGIZA KUVUNJWA KWA BODI YA USHIRIKA MSAI WILAYANI IRAMBA, NDANI YA WIKI MBILI

October 07, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Katibu Tawala Wilaya ya Iramba Pius Songoma akishiriki kuwaelekea wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Konyo Mjika ambaye ni mkulima hodari wa pamba wilaya ya Iramba kutoka kijiji cha Msai akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa zawadi ya kilo tano za mbegu ya pamba aliyopewa.

  Zakaria Marko Mwakilishi wa Kampuni ya Biosustain itakayosambaza mbegu za pamba tani 300 mkoani Singida akizungumza na wakulima wa zao hilo Katika kijiji cha Msai Wilayani Iramba.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Wamesema wana ushirika walijitahidi kutuma mwenyekiti wa Kijiji hicho kufuatilia upotevu huo bila mafanikio jambo lililowakatisha tamaa ya kuendelea na ushirika.

Dkt Nchimbi amesema “moja ya Muhimili wa mafanikio ya kilimo cha pamba ni ushirika ulio imara, tunakoelekea kwenye kilimo cha pamba chenye tija hawa wasiowaaminifu kwenye bodi watatukwaza na kutukwamishwa, kama bodi haifanyi kazi vizuri kwanini iendelee?, Mkuu wa Wilaya naimani kwa utendaji wako mzuri hili halitachukua zaidi ya wiki mbili”.

Aidha amemtaka Afisa Ushirika Mkoa wa Singida kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu wakati wa kuvunjwa kwa bodi hiyo kwakuwa kazi ya mkoa ni kusuluhisha sio kutafuta maelezo marefu huku wananchi wanapotezewa muda.

“Afisa Ushirika hakikisha tarehe ishirini mwezi huu bodi hiyo iwe imeivunjwe na kuundwa bodi mpya ambayo itasimamia ushirika kwa umakini ili kuinua kilimo cha pamba Iramba”, amesisitiza Dkt Nchimbi.

Aidha Dkt Nchimbi amewatoa hofu wakulima kwakuwa mbegu aina ya UKM 08 za manyoya pamoja na viuatilifu zitafika na kusambazwa kwa wakati huku akiwataka kupanda kitaalamu ili kwa ekari moja iwe na miche elfu 22 na mkulima avune zaidi ya kilo elfu moja za pamba.

BENKI YA AZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA BEGA KWA BEGA NA WATEJA WAO

October 07, 2017
Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akikata keki kwa niaba ya wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe na kulia ni Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Azania Tawi la Kariakoo alipotembelea benki hiyo ili kuwa bega kwa bega na wateja katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzungumzia baadhi ya bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimlisha keki Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni kwa niaba ya wafanyakazi wa tawi hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwalisha keki baadhi wateja wa benki ya Azania tawi la Kariakoo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo benki ya Azania iko bega kwa bega na wateja wao.
Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akitoa maoni yake kuhusu benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja