POULSEN AMTEMA IVO MAPUNDA TAIFA STARS

November 11, 2013


Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemtema kipa Ivo Mapunda katika kikosi chake.

Baada ya zaidi ya miaka mitatu, Ivo anayekipiga Gor Mahia ya Kenya aliitwa katika kikosi hicho.

Lakini baadaye Poulsen amemuondoa katika kikosi hicho kwa madai kulikuwa na ukimya.
 
"Sikusikia lolote kuhusiana na Mapunda, sifanya mkutano wa waandishi lakini ni uamuzi umepita kwa ajili huenda atakuwa na majukumu mengine," alisema.

Hata hivyo kuna taarifa zinaeleza TFF hawakupeleka barua ya kumtambulisha Ivo kuitwa katika kikosi hicho.

Ivo ni kati ya makipa wlaiong'ara katika Ligi Kuu Kenya na amesaidia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa Kenya ambao mara ya mwisho waliubeba miaka 13 iliyopita.
 
chanzo:salehjembe.blogspot.com

BALOZI IDDI AWAASA WATANZANIA WAISHIO SEATTLE KUWEKEZA NYUMBANI

November 11, 2013

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwaasa Wanajumiya ya Watanzania wanaoishi Seattle kukumbuka hatma ya maisha yao ya baadaye kwa kuwekeza nyumbani.
*************************************
 Watanzania waishio na kuendesha maisha yao Nchini Marekani wameawa kuwa makini katika kuutumia  vyema muda wao wa maisha Nchini humo kwa kufikiria  mbinu za kujiwekea mitaji itakaowajengea hatma njema hapo baadaye endapo watafikia maamuzi ya kurejea  kuishi nyumbani siku zijazo.
Nasaha hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Mji wa Seattle ndani ya Jimbo la Washington kwenye tafrija maalum iliyoandaliwa na wana jumuiya hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Ramada Tukwila Mjini Seattle.
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya Watanzania  waliobahatika kupata fursa na nafasi nzuri za kuendesha maisha katika Mataifa mbali mbali ya nje hasa  ya ulaya lakini wengi kati yao wameishia kuwa na maisha mabovu kwa kukosa kujiwekea misingi mizuri.
Alisema tabia ya kuendelea na kuendekeza starehe sambamba na matumizi ya kifahari kwa msingi wa kutaka sifa hutoa sura mbaya kwao lakini kinachoumiza zaidi ni kile kizazi chao kinachowategemea.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wana Jumuiya hiyo ya Watanzania wanaoshi Mjini Seattle kuzingatia na kuheshimu sheria na taratibu za nchi wanayoishi  ili kulinda desturi na ukarimu walionao.
Amewapongeza wana jumuiya hiyo ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle kwa umoja na ushirikiano waliokuwa nao bila ya mgongano na ubaguzi wa uzawa ambao ndio utanaowasaidia katika kuimarisha mila na silka zao.
“ Ukweli sifa tulizokuwa nazo sisi Watanzania hatufanani na wenzetu wa mataifa mengine . Hivyo Utanzania wetu ni vyema tukauendeleza kwa kusaidiana na ofisi za balozi zetu zilizo  karibu “. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Akijibu baadhi ya maswali alioulizwa na Wanajumuiya hiyo ya Watanzania waishio Mjini Seattle Balozi Seif aliwatoa hofu wanajumiya hao kwa kuwaeleza kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hivi sasa inaendelea kuwa shwari licha ya vituko vinavyotokea katika baadhi ya wakati hasa vile vilivyokuwa vikiwatia hofu wananchi  vya kumwagiwa watu tindikali.
Alieleza kwamba Serikali iko makini katika kuhakikisha vitendo vya uvunjaji wa amani havipewi nafasi na tayari vyombo vya ulinzi vinaendelea na operesheni za kuwasaka watu wenye tabia kama hizo zinayotishia maisha ya Jamii.
Akijibu swala la operesheni kimbunga iliyowakumba watu waliokuwa wakiishi kinyume na taratibu za uhamiaji Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali iliamua kufanya operesheni hiyo baada ya kugundua  wahamiaji haramu ndio wanaohusika na masuala ya ujambazi Nchini.
Alifahamisha kwamba watu wote walioondoshwa Nchini Tanzania kupitia operesheni Kimbunga hiyo wamebainika kutokuwa na kibali jambo ambalo ni kosa kwa  mujibu wa mfumo na taratibu za uhamiaji Kimataifa.
Hata hivyo Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuheshimu haki za Binaadamu haijamkataza mtu wa nchi yoyote Duniani kuishi Tanzania endapo atazingatia sheria za Nchi zilizopo.
“ Serikali imelazimika kuwa makini katika kulinda usalama wa wananchi baada ya kugundua kwamba wengi wa wahamiaji haramu ndio waliokuwa wakihusika katika masuala ya ujambazi na matukio ya hatari hapa Nchini “. Alisema Balozi Seif.
Wakitoa salamu zao kwa wanajumiya hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui  wamewashauri wanajumuiya hao kuzitumia fursa za mitaji zilizopo nchini humo kwa kuanzisha miradi Nchini Tanzania.
Mawaziri hao walisema mitaji hiyo ambayo fedha zake hazina masharti makubwa zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ajira hasa kwa vijana pamoja na kuongeza vipato vyao vitakavyopunguza umaskini.
Walieleza kwamba wanajumiya hayo  ni vyema wakaitumia Diasfora wakielewa kwamba Tanzania ni yao na kwame bila ya wao hakutakuwa na mgeni atakayeweza kuweka misingi ya kuimarisha uchumi wa taifa.
Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle  Jimboni Washington Nchini Marekani Nd. Yona Isimika alisema jumuiya yao iliyoanzishwa mwaka 2008 hivi sasa ina karibu wanachama Mia Nne.
Nd. Yona alisema Jumuiya yao iliyolenga kuuendeleza Utamaduni, Mila na Silka zao za Kitanzania iko katika mchakato wa kubadilisha katiba ili ikidhi matihaji yao hasa wakati wanapopatwa na matatizo.
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Watanzania waoishi Seattle Washington alipongeza Ujumbe huo wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa hatua yake ya kukutana nao ikiwa ni ugeni wa mwanzo tokea kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 2008.

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA VIONGOZI WA KABILA LA JAMII YA WAFUGAJI KUHUSU AFYA YA UZAZI NA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

November 11, 2013

 Mke wa RaiS Mama Salma Kikwete akivishwa mavazi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakati wa warsha ya viongozi wa kimila iliyofanyika Dar jana. Baadaye Mama Salma alipokea zawadi kwa ajili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi warsha ya siku moja ya viongozi wa kibila la jamii ya wafugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya ufugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi wanaonekana wakisikiliza kwa makini mambo yaliyokuwa yakiongelewa kwenye warsha hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya ufugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi wanaonekana wakisikiliza kwa makini mambo yaliyokuwa yakiongelewa kwenye warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji wqakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
 Baadhi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakicheza ngoma za asili wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar.
Katibu Mtendaji wa WAMA Bwana Daud Nassib akizungumza na wajumbe wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji hapa nchini iliyofanyika. PICHA NA JOHN LUKUWI

MALAIKA MUSIC BAND KUWASHA MOTO TANGA NOVEMBA 23.

November 11, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
BENDI Mpya ya Malaika Music Bendi inatarajiwa kufanya uzinduzi wa aina yake mkoani Tanga Novemba 23 mwaka huu katika ukumbi wa Tanga Hotel jijini Tanga ikiwa na waimbaji wake wote.
Akizungumza na blog hii,Meneja Masoko wa Bendi hiyo,Juma Abajalo alisema maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri ambapo kabla ya kuja mkoani hapa itafanya uzinduzi wake Novemba 15 mwaka huu Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam na baada ya hapo wataelekea mkoani Morogoro na hatiamye kutua mkoani Tanga.
Abajalo alisema lengo la kuanzishwa bendi hiyo ni kuhakikisha wanakata kiu za wapenda mziki wa dansi hapa nchini kutokana na kusheheni wasanii nguli ambao wanajua kulitawala jukwaaa.
Meneja huyo alisema katika onyesho hilo,Rais wao Christiani Bella “Obama akisaidiwa na marapa pembeni Totoo Ze Bingwa,Fadii na mpiga kibodi maarufu nchini Andrew Sekedia.
Aidha aliwataka wakazi wa mkoa wa Tanga kukaa mkao wa kula ili kuweza kusikiliza masauti makali ya Christiani Bela “Obama”na wasanii wengine ambao wanaunda bendi hiyo watakaowasha moto siku hiyo.
   “Ninachoweza kusema burudani itakayopatikana hapo itakuwa sio ya mchezo hivyo nawaomba wakazi wa mkoa wa Tanga kuhakikisha wanapata nafasi ya kushuhudia uzunduzi huo ambao utakuwa wa aina yake “Alisema Abajalo.
 WATU TISA WAKAMATWA KWA KUHUSISHWA KWENYE UVAMIZI WA DR.MVUNGI

WATU TISA WAKAMATWA KWA KUHUSISHWA KWENYE UVAMIZI WA DR.MVUNGI

November 11, 2013

PIX 1



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. 
Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. PIX 3Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. 
Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. 
Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. 
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 4Sehemu ya waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba.
 Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo:Handenikwetublogspot.com

ZDFA:HATUNA MPANGO NA HALL

November 11, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba .11/11/2013.

Siku chache baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Azma Stewart John Hall kufungasha virago kutoka  klabu hiyo , Chama cha Soka cha Zanzibar ZFA kimesema hakina mpango wa kumuita kocha huyo kwa ajili ya kuifundisha timu ya taifa ya Zanzibar .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  , katibu Mkuu wa ZFA Kassim Haji amesema kuwa mpango wa kumrejesha kocha huyo kukionoa kikosi cha Heroes hakupo na badala yake wataendelea kumwamini Salum Bausi .

Kassim amezidi kufahamisha kwamba pamoja na  ZFA kuwa ndiyo iliyomleta Stowart kwa mara ya kwanza hapa nchini , lakini fursa ya kuifundisha timu ya Taifa ya Zanzibar kwa sasa itakuwa ni ndoto .

"Tunaelewa uwezo wa Stowart , kwani ndiyo sisi tuliomfungulia milango hapa nchini , lakini mipango ya kumrejesha kwa sasa haipo kwani tunawapa nafasi makocha wazawa " alifahamisha Kassim .

Aidha akizungumzia maandalizi ya timu hiyo ambayo inajiandaa na michuano ya Tusker Challenge Cup , Kassim amesema kuwa yanaendelea vyema na kupongeza uwamuzi wa kocha wa  kuwapima afya wachezaji .

Hata hivyo alikiri kuwa  ZFA inakabiliwa na ukata wa fedha wa kuweza kuindalia michezo ya kimataifa ya kujipima nguvu kabla ya kuelekea Mjini Nairobu Kenya kushiriki michuano hiyo .

"Kunahitajika zaidi ya shilingi milioni 15 , kuandaa  mechi ya kimataifa , kwani tunatakiwa kuigharamia timu ili iweze kufika Zanzibar au timu yetu kuweza kusafiri , lakini tuna mpango wa kucheza mechi za kirafiki na vilabu vya Tanzania Bara ikiwemo Kilimanjaro Stars " alieleza .

Awali uteuzi wa timu ya Taifa ya Zanzibar ulipingwa na wajumbe wa kamati Tendaji wa ZFA Pemba ambayo nayo ilitangaza kikosi cha wachezaji 30 kuunda  timu ya kombaini  ya Pemba kwa lengo la kukutana na iliyochaguliwa na Bausi ili kupata kikosi cha Heroes