TAZARA WACHANGIA DAMU WAKIADHIMISHA MIAKA 40 YA UWEPO WAO

August 03, 2016
Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu 
 Wakati Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu salama Tanzania.

Akizungumza na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 40  ya kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu 

Amesema kuwa zoezi hilo linaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa TAZARA wamekuwa wakiguswa na maswala mbalimbali ya kijamii hususani swala la ukosefu wa Damu mahospitalini huku akiyataka mashirika mengine na watu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachangia damu mara kwa mara wawezavyo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wamaopoteza maisha yao kwa kukosa Damu.


Aidha mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.

Mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa watanzania

Mwandishi wa mtandao huu wa HABARI24 BLOG alishughudia wafanyakazi wa TAZARA wakijitokeza kwa wingi kuchangia Damu ambapo walimueleza mwandishi wetu kuwa ni swala la kizalendo na utu kwa mtanzania kujali na kusaidia watanzania wengine ambao wana uhitaji mkubwa wa damu nchini.PICHA ZAIDI ZIPO CHINI HAPA

KITUO CHA TELEVISHENI CHA TV 1 KURUSHA MATANGAZO YA LIGI KUU SOKA YA UINGEREZA EPL

August 03, 2016
 Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino 
 Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.  
 Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
 Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakiwa kazini.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
 Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
 Wapiga picha za habari wakiwa kazini.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Mkutano ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

KITUO cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu.

Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.

TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.

Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania  Joseph Sayi alisema  hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.

Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo  hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.

Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo  kilianza kurusha matangazo yake rasmi  Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.

Waziri Mahiga atembelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.

August 03, 2016

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia  maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa  hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016.
Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza.
Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na AmerikaBi. Mona Mahecha nawakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga na mgeni wake Waziri Ayrault wakiwa katika picha ya pamoja.
Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Ayrault mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

NAIBU WAZIRI SULEIMANI JAFFO AHIMIZA USAFI KWENYE MAJIJI,AKAGUA MAGARI MAALUMU JIJINI ARUSHA

August 03, 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kusimamia na kutumia mitambo na magari ya kisasa ya kukusanya Taka ngumu kwenye majiji na halmashauri zilizopo kwenye mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia,kushoto ni Mratibu wa Mradi huo,Mhandisi Davis Shemangale na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu Waziri,Suleimani Jaffo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo(aliyevaa tai nyekundu) akiwa ujumbe ofisi yake na watumishi  wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakati akikagua eneo lililotengwa kwaajili ya kuchomea taka ngumu lilipo Dampo Kuu jijini humo katika mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akikagua Dampo la Jiji la Arusha liliboreshwa miundombinu yake  kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Sehemu ya magari maalumu yatakayohusika kukusanya Taka ngumu kutoka mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha. Naibu Waziri Jaffo alitaka mitambo hiyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kufanyiwa matengenezo kila mara ili iwe endelevu na kuongeza kuwa serikali imeshaweka mikakati ya miji yote kuwa misafi.

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANIBARI BOSTON, SEHEMU YA PILI

August 03, 2016
Na Mwandishi wetu Boston
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza awamu ya pili ya ziara zake za Kimataafa hapa nchini Marekani iliyoanza wiki mbili zilizopita.
Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibar 
Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.
Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo, Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.
Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.
Madhumuni ya Ziara zake.
Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, alielezea lengo la mizunguko yake hiyo kuwa ni kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa nchi na taasisi alizozitembelea ili kuwapa picha halisi ya hali ya mambo ilivyo huko Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika nyanja za demokrasia na haki za binadamu kufuatia uchaguzi huo.
"Tumekuwa tukiwasiliana ili kuwapa 'brief' (maelezo) ya hali halisi ilivyo" aligogoteza Maalim.
Alisema kuwa nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zikitetea demokrasia, na wala siyo chama au kiongozi fulani.
"Nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zinatetea demokrasia, na wala siyo CUF wala Maalim Seif", alisema gwiji huyo wa siasa, na kuongeza kuwa, "Msimamo huo ndio uliotusukuma kutembelea nchi hizi ili kuwapa 'utandu na ukoko', kwani kwa kufanya hivi tunapata nafasi ya kukutana na watunga sera wenyewe"

WASANII, WATANGAZAJI NA WATU MAARUFU KUVUNA MAPESA KUTOKANA NA MITANDAO YAO YA JAMII

August 03, 2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
 Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
---
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
Uzinduzi wa kitengo hiki cha matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na wanamichezo.
Kampuni ya Binary kwa kuanza tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa urahisi.
Huduma hii mpya ya matangazo katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia nyingine za matangazo.
Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana na huduma hii mpya ya matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza kuwa ushirikiano wa Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea akaunti zao.
“Viwango vya matangazo viko wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''