NENO MAALUM KUTOKA KWA RIDHIWANI KIKWETE

April 16, 2014


Baada ya safari ya miaka 34 ya kutembea duniani na mafanikio ambayo mungu amenipa , naomba kutumia kurasa huu kuwashukuru tena ninyi wazazi wangu,marafiki zangu, wananchi wenzangu wa Chalinze kwa heshima kubwa mliyonipa.
Ninapoingia mwaka wa 35 wa maisha yangu hakika ni kumshukuru mungu kwa yote aliyonitendea na familia yangu kwa kuwa pamoja nami.Lililo mbele yangu ni utumishi uliotukuka na kuendeleza urafiki na kujenga mahusiano mema.
THANK U ALL.
Ridhiwani Kikwete

UFUNGUZI WA MAONYESHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO

April 16, 2014

 Kikundi cha ngoma toka Jeshi la Kujenga Taifa kikitumbuiza kwenye uzinduzi wa maonyesho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi mmoja 
 Mgeni Rasmi wa maonyesho ya miaka 50 ya Muungano ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamad akitoa hutuba ya ufunguzi wa maonyesho hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Chungu na kibuyu vilivyotumika na waasisi wa Muungano kuchanganya udongo mwaka 1964, vinapatikana katika banda la Ofisi ya Makamu wa Rais. 
 Mgeni Rasmi wa maonyesho ya miaka 50 ya Muungano ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamad akiwa ndani ya Banda la Ofisi ya Makamu wa Rais akipata maelekezo juu ya  chungu na vibuyu vilivyotumika kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanziabr mwaka 1964
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutemebelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakiangalia majarida mbalimbali bandani hapo na kusaini kitabu cha wageni.

UVCCM SAME YAMSIMIKA KAIRUKI KUWA KAMANDA WAO

April 16, 2014
Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM  Sixtus Mapunda, akimsimika Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki, kuwa Kamanda wa  Vijana wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Katibu mkuu wa umoja wa Vijana UVCCM, Sixtus Mapunda  akimsomea , Naibu waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki kiapo cha ukamanda.
Naibu waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki, akila kiapo cha kusimikwa kuwa kamanda wa umoja wa vijana UVCCM wilaya  ya Same.
Naibu waziri wa Sheria na Katiba  Angellah Kairuki  akizindua Shina la wakereketwa wa umoja wa Vijana Uvccm, baada ya  kusimikwa kuwa kamanda wa umoja huo wilayani Same.
Naibu waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki akiwa  kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  viongozi wa timu za mpira, baada  ya kuwakabidhi vifaa vya michezo, kama njia ya kuwaunganisha vijana
pamoja. Picha zote na Fadhili Athumani