Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sosipiter Muhongo akijibu hoja za wabunge kabla ya kupitishwa bajeti ya
wizara yake mjini Dodoma juzi.Bunge lilipitisha Sh. tirioni moja kwa
wizara hiyo.
Waziri Muhongo (kulia) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi wakipongeza baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara yao.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete (kulia), akimpongeza Waziri Muhongo baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo.
Mdau wa sekta ya Nishati na Madini (kushoto), akimpongeza Waziri Muhongo kwa bajeti ya wizara yake kupitishwa na Bunge.
Mdau mwingine wa sekta ya Nishati na Madini akimpongeza Waziri Muhongo (kulia) baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo.
Wabunge wamfagilia Muhongo
Dotto Mwaibale, Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wamempongeza Waziri wa Nishati na madini Profesa
Sosipiter Muhongo, kwa jitihada zake za kuisimamia kikamilifu wizara
hiyo ambapo wamemtaka aendelee kuchapa kazi na aache kusikia majungu na
maneno ya watu.
Hayo yalisemwa na Wabunge walipokuwa
wakichangia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 ya Wizara ya Nishati na
Madini mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Akichangia hotuba hiyo Mbunge wa Same
Mashariki (CCM)Anne Kilango Malesela, alisema kazi inayofanywa na
Wizara ya Nishati na Madini chini ya uongozi wa waziri Muhongo na timu
yake haipaswi kubezwa kwani wanafanya vizuri kuhakikisha wananchi kila
kona wanapata umeme.
"Waziri Muhongo na timu yake
wanafanya kazi nzuri ni lazima tuwapongeze na kama kutakuwa na watu
wanaopinga jitihada wanazo zifanya watakuwa na sababu zake kwani hivi
sasa umeme upo hadi maeneo ya milimani" alisema Kilango.
kwa upande wake Mbunge wa Mtera,
Livingstone Lusinde alisema kazi inayofanywa na wizara hiyo ni kubwa
hivyo Muhongo na watendaji wake wasiogope vitisho na majungu wachape
kazi kwani wanachokifanya kinaonekana kwa wananchi.
Mbunge wa Karagwe,Gosbert Blandes
alisema wananchi wa jimbo lake wanapongeza kazi inayofanywa na wizara
hiyo na kuwa iwapo ikitokea siku moja waziri Muhogo akifika jimboni humo
atajionea mwenyewe jinsi anavyowa kubalika.
Hata hivyo walimpongeza kwa kitendo chake cha kufanya jiji la Dar es salaam kutokuwa na umeme wa mgao toka aingie wizarani.