MTOTO AKAA SIKU 60 ICU HOSPITALI IKITUMIA MILIONI 10,100,000 KUMTIBU

January 25, 2024

 


 



Januari 26, 2024, Dodoma

Na Raymond Mtani-BMH

Novemba 11, 2023, Bi. Janeth (35), mkazi wa Manyoni Singida, alifika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) baada ya kukaa siku saba katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni akiimuuguza mwanaye aliyepatwa “degedege”.

Siku hiyo, ikawa safari ya siku 60 za mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 4 kwenye Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda ya Kati.

“watu walikuwa wanakuja, wanaruhusiwa wanamuacha mwanangu, wakati mwingine anabaki peke yake”. alisema Bi. Janeth.

Dkt. Venance Misago ni Bingwa wa Ganzi na Wagonjwa Mahututi, na Mkuu wa Idara ya Huduma za Uangalizi Maalumu BMH amesema, Moyo wa mtoto huyo ulisimama ghafla (cardiac arrest) mara nne (4) ndani ya siku 60 mtoto huyo alipokuwa ICU.

“aligundulika kuwa na maambukizi kwenye Ubongo (meningitis), hali iliyokuwa inasababisha apoteze fahamu mara kwa mara” alieleza Dkt. Misago.

Aidha, Dkt. Misago amesema kuwa kwa kawaida mgonjwa hukaa katika Chumba cha uangalizi maalumu siku 3 hadi 14 lakini maambukizi aliyokuwa nayo mtoto huyo yalisambaa kiasi cha kusababisha presha kushuka na kupelekea Moyo kusimama (septic shock) mara kwa mara.

Ingawa hali hiyo haikuwa rahisi kwa Bi. Janeth, hakusita kumshukuru Mungu, Madaktari na Wauguzi waliyomhudumia mwanaye.

“...nilipitia wakati mgumu kiasi cha kukata tamaa, namshukuru Mungu kwa kumponya mwanangu, nawashukuru Madaktari na wauguzi kwa kumpambania mwanangu” alieleza Bi. Janeth kwa furaha.

Kwa mujibu wa Awadhi Mohamed, Mkurugenzi Msaidizi huduma za Usitawi wa Jamii Hospitali ya Benjamin Mkapa imetumia Shilingi 10, 100,000 kugharamia dawa, vifaa tiba na chakula kwa kipindi chote cha siku 60 Mtoto wa Bi. Janeth alipokuwa ICU.

Kupona kwa mtoto huyo ni kielelezo cha faida za uwekezaji katika sekta ya Afya nchini, hasa mapinduzi yanayofanywa katika kuboresha huduma za Wagonjwa Mahututi.

Ingawa, wakosoaji wa serikali hasa Wizara ya Afya wamekuwa na jicho la kutoridhishwa na hatua za maboresho hususani kasi ya utekelezaji na ubora wa huduma, historia ni mwalimu mzuri.

Historia inakili kwamba, maboresho ya huduma ni mchakato, huduma za Afya nchini haziwezi kutokea ghafla mithili ya kimbunga, zinapitia mkondo huo huo wa mchakato wa maboresho ikiwa ni pamoja na huduma za ICU.

Mathalani, taarifa za Maktaba ya Historia ya Tiba ya Nchini Marekani zinadokeza mchakato wa maboresho ya huduma za ICU katika nchi za Ulaya ulianza kwa kanuni za kutenga majeruhi wa vita vya Crimean kwa kuwaweka mahututi jirani na vituo vya wauguzi (nursing stations) ili wapewe uangalizi maalumu.

Hiyo ilikuwa 1854, maboresho hayo yaliyohamasishwa na Bi. Florance Nightingale kusaidia kuokoa Maisha ya Majeruhi wengi wa vita, Ulaya ilisubiri karibu miaka 100 na mlipuko wa Polio kuwa na ICU ya kwanza, iliyojengwa 1953 huko Copenhagen, Denmark.

Hali hii ni tofauti na Tanzania, kwa mujibu wa Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, alipowasilisha Makadiliyo ya bajeti, mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa Fedha 2023/2024, aliliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu hatua kubwa zilizopigwa katika huduma za Wagonjwa Mahututi.

Waziri huyo wa Sekta ya Afya, alinukuliwa Mei 12, 2023 akisema kuwa baada ya shambulio la Uviko 19, serikali imeweza kuongeza wodi za Wagonjwa Mahututi kutoka 45 had 258 ndani ya kipindi cha miaka 2, yaani 2020 hadi 2023.

“Tunaweza kulaza wagonjwa mahututi 1000 kila siku nchini” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Hapana shaka, kama ilivyo kwa Mtoto wa Bi. Janeth, maboresho ya huduma za ICU yaliyofanyika katika kipindi hicho cha miaka 2 yamesaidia kuokoa maelfu ya Maisha ya Watoto na watu wazima waliyokumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya zilizowalazimu kuhitaji ICU.

Mwaka 2020, Hospitali ya Benjamin Mkapa ilikuwa na Wodi ya Wagonjwa Mahututi yenye vitanda 6 pekee, lakini kupitia maboresho hayo, hadi Makala haya yanaandi.kwa, Hospitali hiyo ina Wodi mbili za wagonjwa Mahututi zenye vitanda 22.

Kwa mujibu wa Dkt. Misago, vitanda hivyo vina mashine za kusafisha mfumo wa hewa (Suction Machine), mashine za kusaidia kupumua (Ventilator), mashine za kusaidia Moyo, Figo na Kuzuia damu Kuganda (Syringe pump and Infusion Pump) pamoja na mashine za uangalizi wa mwenendo wa matibabu ya Mgonjwa (Monitors).

Hali hiyo, inasaidi kuokoa Maisha ya wanchi wengi wenye kuhitaji huduma hizo kwa uhakika, kumbuka iliichukua Ulaya miaka 99 kupata ICU ya kwanza, huku Tanzania ikijenga ICU zaidi ya 200 ndani ya siku 730.

RAIS SAMIA AHUTUBIA KATIKA JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI, JAKARTA NCHINI INDONESIA

January 25, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na Wawekezaji wa Tanzania na Indonesia katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji. Mkutano huo ulifanyika Jijini Jakarta katika muendelezo wa ziara yake ya Kitaifa nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji uliofanyika Jijini Jakarta katika muendelezo wa ziara yake ya Kitaifa nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2025.

Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji uliofanyika Jijini Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2025.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji uliofanyika Jijini Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2025.
Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji uliofanyika Jijini Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2025.

AMEND ,UBALOZI WA USWIS WATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA BODABODA DODOMA

January 25, 2024

 Na Mwandishi Wetu,Dodoma



SHIRIKA la Amend kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania wametoa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda zaidi ya 250 katika Jiji la Dodoma , lengo ni kuliepusha kundi hilo pamoja na watumiaji wengine wa barabara dhidi ya ajali za barabarani.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyohusisha pia wadau mbalimbali, Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo amesema wametoa mafunzo hayo kwa kutambua kuwa ajali za barabarani zimekuwa chanzo kikubwa cha ajali na ajali nyingi zinatokana na uendeshaji usizingatia usalama barabarani.


“Ajali za barabarani ni sababu kuu ya vifo vya watoto na vijana kati ya miaka 5 na 29 ulimwenguni. Bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara lina viwango vya juu zaidi vya vifo vya barabarani duniani.


“Takwimu zilizochapishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha zaidi ya waendesha pikipiki 3,700 walikufa kwenye barabara za Tanzania mnamo 2016(mwaka wa hivi karibuni ambao data kamili zinapatikana).


“Hii ni sawa na kiwango cha vifo vya waendesha pikipiki cha 6.7 kwa kila watu 100,000 -mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya vifo vya pikipiki barani Afrika,”amesema Kalolo.


Ameongeza pamoja na kusababisha ajali kwa madereva na abiria wake, pikipiki pia husababisha hatari kwa watumiaji wengine wa barabara, haswa watembea kwa miguu.


Amesema kwa bahati nzuri hatua madhubuti za kuzuia ajali za barabarani zinafahamika, zikijumuisha elimu ya kina kwa watembea kwa miguu na mafunzo ya usalamabarabarani kwa waendesha pikipiki, ambayo yametolewa chini ya mradi huu.


“Jijini Dodoma, Ubalozi wa Uswisi umefadhili utoaji mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki (boda-boda) 250. Mradi huu wa mafunzo ya pikipiki umeandaliwa mahususi kwa waendesha pikipiki na mazingira ya Tanzania.


“Muundo wa mafunzo hayo unatokana na mafunzo ya msingi ya lazima ya Uingereza kwa waendesha pikipiki, lakini umetoa nafasi kwa wakufunzi wa Kitanzania kuyarekebisha ili kukidhi mahitaji halisi ya hapa nchini.


“Mafunzo hayo yalitoa elimu ya vitendo iliyolenga kujenga uwezo ambao madereva wengi wa pikipiki wanajulikana kuukosa. Mazoezi ya vitendo yalijumuisha matumizi sahihi ya makutano na mizunguko, kuvuka vyombo vingine vya moto kwa usalama, na jinsi ya kusimama haraka katika dharura,”amesema.


Ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Amend katika kufanikisha utolewaji wa mafunzo ya usalama barabarani katika mikoa mbalimbali ukiwemo wa Dodoma.


Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya katika Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania Viviane Hasselmann amesema kwa kuwa asilimia 62 ya Watanzania wana umri chini ya miaka 25, ni muhimu kuelekeza afua za maendeleo kwa vijana, na kushughulikia changamoto na mahitaji yao mahususi.


“Kupitia mradi huu, na mafunzo haya ya pikipiki, Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Amend, wanalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki, abiria na watumiaji wengine wa barabara, na hivyo kuzuia vifo na majeruhi wengi vijana kadri inavyowezekana,”amesema.


Akizungumza mbele ya wadau wa usalama barabarani Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweli ametoa shukrani kwa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania kwa kufadhili mafunzo hayo kwa waendesha bodaboda kwani yanachangia kupunguza ajali za barabarani nchini.


Amesema kuwa katika mwaka 2023 watu zaidi ya milioni 61 wamefariki duniani na kati hayo waliofariki kwa ajali za barabarani ni watu zaidi ya milioni moja na hiyo ni picha ya dunia.


“Tukiangalia kwa Tanzania Jeshi la Polisi liliripoti makosa ya barabarani 2534 kwa mwaka mzima na ajali za barabarani zilizokuwa zimetolewa taarifa 1760 lakini vifo vilivyotokana na hizo ajali ni vifo zaidi ya 1000 kwa maana katika kila ajali tatu kuna mtu mmoja alikufa.


“Kwa Dodoma hali inasura inayofanana na hiyo , imeripotiwa ajali zaidi ya 1000 na kati ya hao 59 wamefariki dunia.Na hizo ni taarifa ambazo zimeripotiwa na jeshi la polisi.Kwa hiyo mafunzo haya yana umuhimu wa kipekee,”amesema Shekimweri.


Amesisitiza ajenda ya mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yanaumuhimu wa kipekee kwani mbali ya vifo ajali hizo zinasababisha ulemavu wa kudumu huku akieleza takwimu za sensa zinaonesha asilimia kubwa ya watanzania ni vijana na kutokana na changamoto za ajira watu wengi wameamua kujikita katika ujasiriamali na bodaboda.


Amesisitiza kuwa ili kuendelea kukomesha ajali za barabarani iko haja kwa Amend, Ubalozi wa Uswisi na wadau wengine kuendelea kutoa mafunzo kwa kundi hilo la waendesha bodaboda huku akitoa rai kwa kuwataka kuzingatia sheria za usalama barabarani.


Awali Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi Michael Deleli amesema watumiaji wengi wa bodaboda walihama kutoka katika kuendesha baiskeli, hivyo mafunzo hayo ni muhimu kwao.


“Wengi wetu tunaendesha pikipiki kwa uzoefu wa baiskeli hivyo wengi hawakupitia mafunzo rasmi ya udereva.Sisi kama Jeshi la Polisi tunaendelea kupongeza wadau ambao wanajitolea kutoa mafunzo kama haya, kwetu inakuwa furaha kubwa.


Amesema mafunzo ambayo wamefundishwa ni vema wakayapeleka na kwa watumiaji wengine ambao hawajahudhuria mafunzo hayo ili wote wawe salama huku akielezea umuhimu wa kuvaa kofia ngumu kwani ndio usalama wa mhusika.


“Usipovaa kofia ngumu ukianguka sehemu kubwa ya mwili ambao unaumia na hasa ukiwa spidi ni kichwani.vifo vingi vya pikipiki ni kuangukia sehemu ya kichwa, kwa hiyo tusipovaa kofia ngumu maisha yanakuwa hatarini,hivyo nisisisitize wote tunapokuwa katika bodaboda tuvae kofia ngumu.”
Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri (wa nne kulia) ,  Mkurugenzi wa Amend Tanzania Simon Kalolo( wa pili kulia) Mkuu wa Idara ya Afya Ubalozi wa Uswisi Tanzania Viviane Hasselmann( wa tatu kulia) Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma Mjini Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mbwiga Mwakatobe( wa kwanza kushoto) Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Michael Deleli( wa pili kushoto) na Naibu Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma Asma Karama( wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha bodaboda waliopata mafunzo ya usalama barabarani waliosimama nyuma wakiwa na vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo hayo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma Asma Karama( kushoto) akimkabidhi cheti cha mafunzo ya usalama barabarani yaliyotolewa na Shirika la Amend Tanzania kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi Omari Guzu (wa pili kulia) .Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na Mkurugenzi wa Amend Tanzania Simon Kalolo( kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri( kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo( kulia) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda zaidi ya 250 wanaotoa huduma ya kusafirisha abiria katika Jiji la Dodoma.Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Ubalozi wa Uswiz nchini Tanzania
Wadau wa usalama barabarani wakiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma wakiwa makini kufuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa kufunga mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda wa Jiji la Dodoma.Mafunzo hayo yametolewa na Shirika la Amend kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi nchini

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri ( kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya Afya kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Vivian Hasselmann wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda katika Jiji la Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akizungumza na wadau wa usalama barabarani wakati wa kufunga mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda katika Jiji la Dodoma
Mkuu wa Idara ya Afya kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania Viviane Hasselman akieleza sababu za ubalozi huo kufadhili utolewaji wa mafunzo hayo kwa waendesha bodaboda Jiji la Dodoma ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mafunzo hayo yanafikia kwa madereva wengi zaidi

DKT. NCHIMBI AWAHAKIKISHIA USHINDI WA CCM MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA

January 25, 2024


Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi amewahakikishia Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kwamba Chama Cha Mapinduzi kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika changuzi za mwaka huu na mwaka kesho, kwa maana ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kilichofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwapongeza Chama Cha ZANU - PF cha Zimbabwe Kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wao walioufanya huku akivitakia pia heri ya ushindi NAMIBIA NA AFRIKA KUSINI kwenye uchaguzi wao mkuu ambao wao wanaufanya baadae mwaka huu na ANC cha Afrika kusini ambacho kimesheherekea kumbukumbu ya miaka 112 tangu kuanzishwa kwake.







NEMC YASHIRIKIANA NA KITUO CHA SAYANSI NA MAZINGIRA INDIA KUTOA MAFUNZO YA UKAGUZI MAZINGIRA

January 25, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya warsha Maalumu kwa Kushirikiana na kituo Cha Sayansi na Mazingira kutoka India (CSE India) yenye lengo la kutambua namna ya  mfumo wa ukaguzi wa mazingira unavyofanya kazi pamoja na kupeana uzoefu katika Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wahabari leo Januari 25,2024, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka NEMC Bw. Novatus Mushi amesema kuwa mchakato wa usimamizi na Uhifadhi wa mazingira unahitaji uelewa mpana zaidi na taaluma mbalimbali ili kufanya ubobevu mkubwa katika ukaguzi huo.

"Ukaguzi wa mazingira lazima uhusishe wataalamu mbalimbali ili uweze kuzipata taarifa zote kwa ujumla wake ambazo utazihitaji kukuongoza katika ukaguzi wa mazingira ". Amesema Bw.Novatus.

Amesema kuwa NEMC wataendelea kujifunza kwa wageni wa mataifa mengine kwa kubeba mazuri ambayo wanayo na kuboresha katika huduma zao wanazotoa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Program ya Kupambana na Uchafuzi kutoka Viwandani Bw.Nivit Kumar wa Kituo Cha Sayansi na Mazingira India (CSE india) amesema kuwa anafikiri ni wakati sahihi kwa Mamlaka za Udhibiti wa Mazingira katika nchi za kiafrika kutumia ubunifu kuhifadhi mazingira ya nchi zao.

Aidha ameeleza kuwa walipofanya utafiti waligundua ripoti  za ukaguzi zilikuwa zikifanyika hazikuwa vizuri, hivyo wamejitahidi kuweka maelekezo vizuri jinsi ya kuchukua taarifa hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya (ECI) kutoka Kenya Bw. Gerphas Opondo amesema kuwa changamoto ya uchafuzi zilizopo Kenya na Tanzania ni zilezile, ijapokuwa Sheria za Uhifadhi zipo lakini watu bado wanakiuka taratibu hizo.

Warsha hiyo itafanyika kwa siku tatu na imejumuisha wadau mbalimbali kutoka mamlaka zinazosimamia mazingira kwenye mataifa mengine ya Afrika.





RC CHALAMILA AGAWA VITENDEA KAZI KWA JESHI LA POLISI

January 25, 2024












MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Arbert Chalamila leo Januari 25,2024 amewakabidhi Jeshi la Polisi, Jeshi la Uokoaji na Zimamoto na Jeshi la Uhamiaji Vifaa vya kazi kwaajili ya kuendelea kuimarisha Ulinzi na usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kati ya wadau mbalimbali na jeshi la polisi, amesema kuwa Ulinzi na Usalama katika jiji umeimarika kutokana na kutokuwepo na vikwazo vinavyosababisha mwananchi asiendelee kufanya kazi kwa amani.


RC Chalamila ametoa sababu ya kwanini anagawa vifaa hivyo vya kazi kuwa ni ameangalia usalama wa kanda, Wilaya na mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla.


"Hali ya Usalama imeimarika kwa kiasi kikubwa sana, ila kumekuwa na matukio kadhaa ambayo yamehatarisha hata maisha ya Askari wetu, tusiruhusu hata kidogo raia kukipeleka kidole chake kwenye jicho la Askari yeyote."


Pia ametoa rai kwa wananchi wote kudumiasha amani katika taifa letu wani ndio walinzi wa amani hiyo na wasije wakaingia kwenye katika mtego wowote wa kuona Askari wa aina yeyote ni adui kwenye maendeleo yao.


Mkuu wa Mkoa amesema kuwa aliona kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kukosekana kwa usalama kwenye eneo la Tanganyika Pekers pale Kawe na akampigia simu RPC wa Kinondoni.


" Figisu figisu huwa zinakuwepo hata kwenye taasisi za dini na nikamshirikisha Apostle Boniface Mwamposa kwamba na yeye awe sehemu ya kuimarisha amani ya mkoa wetu." Ameeleza


RC Chalamila amesema kuwa amani huwa hailindwi na neno la Mungu tuu, inalindwa kwa nguvu zote ambazo Mungu alizotoa kwa wanadamu.


Vifaa hivyo vya kazi vilivyotolewa ni Pikipiki 10 zilizotolewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Bakharesa, Kanisa la kuhani Musa Richard Mwasha lililoko Kimara Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam pamoja na Askofu wa Kanisa la Rise and Shine, Boniface Mwamposa 'Bulldozer'.

KATIBU MWENEZI CCM PAUL MAKONDA AHIMIZA WATANZANIA KUIPENDA NCHI YAO KWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

KATIBU MWENEZI CCM PAUL MAKONDA AHIMIZA WATANZANIA KUIPENDA NCHI YAO KWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

January 25, 2024






*Atoa rai kwa Watanzania kutotoa maneno ya kulaani Nchi kwani kufanya hivyo ni kujinyima mafanikio katika Nchi uishiyo._

“Tuna kila sababu ya kuipenda Tanzania, ndio nchi yetu, hazina yetu, urithi wetu na ndio mpango wa Mungu wetu kuwepo hapa lazima tuendelee kuimarisha Amani na Utulivu wetu”

“Watu wengi wanapenda kulaani nchi yao lakini mimi niwasihi isije ikatokea jambo ukaanza kutamka maneno ya laana kwasababu hautafanikiwa kwenye nchi uliyoilaani”

“Ukikasilishwa na mtu usitoe neno la kulaani Taifa lako kwakuwa Taifa hili ndio litabeba watoto wa watoto wako kama sio wewe basi watakula neema watoto zako na kama sio watoto zako basi wajukuu zako”

“Kwahiyo tuendelee kuliombea Taifa letu na Rais Samia na tunaposema tumuombee Rais wetu na Viongozi wetu watu wengi wanahitaji tunataka kuwaombea nini, we fikiria kama sio Utulivu, Msaada, Upendo wa Rais Dkt. Samia leo hii kungekuwa na maridhiano? na haya yote anaendelea kuyafanya kwa kuzingatia kanuni yake ya 4R ? Ndio maana tunasema tumuombee”

Makonda ameyasema hayo wakati akiwahutubia wana CCM na wanamchi wa Babati mkoani Manyara akiwa katika Diary yake ya kuhamasisha uhai wa Chama cha Mapinduzi na utlfuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayoendelea katika mikoa 20 ya Tanzania.

    

RAIS DKT SAMIA AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAKABURI YA MASHUJAA YA KALIBATA,JAKARTA NCHINI INDONESIA

January 25, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mashuhuri mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mashuhuri mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kabla ya kutoa heshima mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata, wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kabla ya kutoa heshima mbele ya mnara wa Kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata, wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024


WAZIRI AWESO AWASHA MOTO HUDUMA KUBORESHWA MAMLAKA YA MAJI ARUSHA,ATOA SIKU 30

January 25, 2024



 Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso(MB) amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama ikiwa ni siku moja tu baada ya maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa Katibu wa NEC Itikati, Uenezi na Mafunzo CCM Ndg.Paul Makonda.

Akiwa jijini Arusha ameianza kazi kwa kufanya vikao vya ndani na Serikali  ya Mkoa na Wilaya ya Arusha pamoja na kuketi na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Arusha.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amefanya ziara ya aina yake kwa kushtukiza katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Arusha kujionea hali halisi ya  utoaji huduma na upatikanaji wa maji na kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi.

Aidha, Akizungumza baada ya kuzungukia mitaa mbalimbali Aweso amekemea vikali changamoto zilizobainika na kutoa siku 30 kwa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Arusha (AUWSA) kuhakikisha wanaboresha matatizo yote.
Changamoyo zilizoonekana kwa haraka ni pamoja na maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wateja eneo lenye malalamiko kwa muda mrefu, Huduma kwa wateja isioridhisha, upotevu wa maji na mambo mengine.

Waziri Aweso kwa hisia akizungumza kwa hisia kali, amesisitiza suala la ushirikishwaji wa wananchi katika kupata taarifa na kutowabambikia bili za maji na kutanabaisha kuwa ni muda muafaka sasa wa Serikali kuanza matumizi ya Mita za Lipa kabla (Pre-paid meter).

Akihitimisha amemtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Arusha AUWSA Mhandisi Rujomba kufanya mabadiliko ya vitengo mbalimbali na kuondoa watu wazembe ikiwa ni pamoja na kutengeneza mpango kazi mpya.

LSF NA NMB FOUNDATION YAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA WASICHANA KIJAMII NA KIUCHUMI

January 25, 2024

 Shirika lisilo la Kiserikali la LSF na NMB Foundation yamesaini makubalinao ya mashirikiano kwa lengo la kutekeleza kwa pamoja miradi ya kijamii yenye lenye lengo la kuwainua wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi .Mashirikiano haya yamesainiwa leo katika ukumbi wa mikutano wa benki ya NMB, na yanategemewa kuwa makubaliano ya muda wa miaka mitatu.


Makubaliano hayo yamelenga kutekeleza miradi iliyo katika sekta za Elimu, Ujasiriamali, Afya na Mazingira maeneo ambayo mashirika haya yamekuwa yakitekeleza miradi yake Kupitia makubaliano haya LSF na NMB Foundation zimelenga kuweka nguvu ya pamoja katika kutafuta rasilimali fedha za pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021 NMB foundation imekuwa ikitekeleza miradi yake katika sekta hizi muhimu za Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira na Ujasiriamali. Kwa lengo la kukuza ujumuishaji endelevu na wa kiuchumi. Aidha LSF imejikita katika kuhakikisha haki ya wanawake kijamii na kiuchumi zinafikiwa nchi nzima kwa kutoa elimu na kuwajengea uwezo jamii, kuhakikisha usawa na fulsa mbalimbali zinapatikana kwa wote ikiwemo elimu, afya bora, mazingira safi, na rasilimali kwa kutekeleza miradi ya jamii katika kata na wilaya Tanzania bara na Zanzibar

Makubalino haya kati ya LSF na NMB foundation yanakuja katika kipindi ambacho nchi yetu inatekeleza agenda ya kuinua wanawake kiuchumi na kupiga hatua katika kufikaia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Kitiafa ya mwaka 2025 na malengo ya SDG ifikapo 2030. Hivyo mashirikiano haya yamelenga kuchangia katika kufikia malengo haya. Akiongea wakati wa utiaji Saini wa makubaliano haya, Bw. Nelson Karumuna, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, alielezea shauku yake kuhusu ushirikiano huo, akisema, "Kama taasisi

inayotekeleza miradi ya kijamii, NMB Foundation inategemea makubwa sana kutokana na mashirikiano haya. Huu ni ushirikiano kati ya taasisi mbili zenye ushawishi katika maeneo yake ya kiutendaji. Sisi tupo zaidi katika sekta ambayo tunaweza kushirikiana na Taasisi ya LSF katika kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchimi. Hivyo ni mategemeo yetu kuwa kuunganishwa kwa nguvu zetu kwa Pamoja kutawezesha miradi mingi kuanzishwa na kuwafikia watanzania wengi zaidi Tanzania Bara na Zanzibar. Tumejiwekea lengo la kuwekeza nguvu katika kutafuta rasilimali fedha kwa pamoja kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani na nje kwa muda wa miaka mitatu Alisema Bw. Karumuna.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LSF , Bi Lulu Ng’wanakilala alisema” Tunajisikia fahari kuingia makubaliano na sekta binafsi na tunafurahi kuona Sekta binafsi kama NMB Foundation inakuwa mstari wa mbele katika kuibua mbinu mbadala za mashirikiano yenye tija katika kutatua changamoto za kijamii na NMB Foundation ni mfano Dhahiri leo. Sisi LSF kwa takribani miaka 12 tumekuwa tukitekeleza miradi yetu katika ngazi za jamii na bado tumeona kuna changamoto kubwa katika kuwawezesha wanawake na watoto wakike kielimu, kiafya, kiuchumi hivyo ushirikiano tunaoanzisha leo na NMB foundation yataleta tija katika kuchangia kutatua changamoto hizi.

LSF tunaamini kwa wadau kuungana na kuweka nguvu ya pamoja na hivyo tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na Serikali na taasisi zake, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi hivyo kusaini makubaliano haya na NMB foundation leo ni hatua kubwa katika kufanya program zetu kuwa endelevu.Ni dhahiri kwamba mashirikiano haya yalioingiawa leo kati ya Taasisi hizi mbili yatakua na tija katika kuongeza nguvu za pamoja na kuweka rasilimali za pamoja katika kuchangia kutokomeza umasikini, kutokomeza tofauti za kijinsia, na kukuza ukuaji wa kiuchumi unaowajumuisha watu wote nchini Tanzania hususani wanawake na wasichana ambao wamekuwa wakiachwa nyuma. aliongeza Ng’wanakilala

LSF na NMB Foundation zinaamini katika mashirikiano kama chachu ya kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Makubaliano haya ni mwanzo wa utekelezaji wa miradi yenye lengo la kuendelea kuzikifikia jamii na vikundi mbalimbali vyenye uhitaji Tanzania Bara na Zanzibar.

LSF na NMB Foundation wamesaini makubaliano ya ushirikiano kwa lengo la kutekeleza kwa pamoja miradi ya kijamii yenye lengo la kuwainua wanawake na watoto wa kike kijamii na kiuchumi. Makubaliano hayo yamelenga kutekeleza miradi iliyo katika sekta za Elimu, Ujasiriamali, Afya na Mazingira, maeneo ambayo mashirika haya yamekuwa yakitekeleza miradi yake. Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna

Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya ushirikiano ya miaka mitatu yatawawezesha kushirikiana katika kutafuta rasilimali na kutekeleza miradi ya pamoja katika sekta za elimu, afya, ujasiriamali, na mazingira.

Tumejipanga kuwawezesha wanawake kijamii na kiuchumi , Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna katika picha mara baada ya kusaini makubaliano