FOS YATOA RIPOTI YA UTAFITI WA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015 JIJINI DAR

February 03, 2016
Meneja wa Mradi wa kitengo cha haki Jinsia kutoka Oxfam Bi. Rishida shariff akielezea kwa kina namna walivyofanya mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa
 Mtafiti mkuu wa kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Profesa Ruth Meena akifafanua kwa kina namna ya utafiti ulivyofanyika.
 Dkt. Alexander Makulilo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akifanya uchambuzi wa namna utafiti ulivyofanyika.
 Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 Mama Anna Mgwila akichangia jambo wakati wa uzinduzi huo
 Baadhi ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Idara ya Uratibu Shuguli za SMZ Dar es salaam wa kwanza na wa pili (Kushoto) na Bi. Msangu Said (wa tatu kushoto) kutoka shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC
 Baadhi ya wadau waliohudhulia katika uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu 2015
 Baadhi ya vijarida na Ripoti
(Picha na Fredy Njeje Blogs za Mikoa)


Kitengo cha Haki za jinsia cha Oxfam nchini Tanzania Fahamu Ongea Sikilizwa(FOS) imezindua kitabu chake cha utafiti kughusu taarifa za kushiriki kwa wanawake kati masuala ya uchaguzi mkuu maka 2015 na 2016 nchini Tanzania.

Uzinduzi wa taarifa hiyo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Double view na Meneja wa kitengo cha haki za binadamu na jinsia kutoka Oxfam Bi. Rashida Shariff huku akieleza baadhi ya mikoa iliyofanyiwa utafiti huo kuwaTanzania bara kwa mikoa nane ikiwemo Shinyanga, Dodoma, Tanga, Arusha,  Dar es salaam, Morogoro,Lindi na Mwanza na Tanzania visiwani Zanzibar ni Kusini Unguja
Bi. Rashida amebainisha lengo kuu la utafiti huo likiwa ni kuwapauwezo wa kujiamini wanawake kushiriki kikamilifu katika kujitokez kikamilifu kupiga kura pamoja na kujikita kwenye masuala ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini bila woga.

Aidha ameongeza kuwa utafiti umelenga kupata changamoto za wanawake walizokuwa wanapata hususani kwa wagombea ambapo wagombea sita wanawake kutoka katika vyamba mbalimbali vya siasa Mh. Angelina Mabula, Anna Mghwira, Nancy Mrikaria, Khadija Msawira, Magreth Mshenene na Mh. Safia Mkamama wametumiwa kuelezea changamoto zilizowakabili na mafanikio waliyoyapata ikiwemo ni pamoja na kuongeza kujiamini
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea urais kwa kupitia Chama cha ACT -Wazalendo Anna Ngwila amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika uchaguzi bado umeelekezwa kwenye ushabiki ambapo wanawake hutumiwa katika vyama kwa lengo la kutoa kura zao kuliko wao wenyewe kugombea.
  
Bi Anna akitolea mfano yeye mwenyewe alisema kuwa changamoto aliyokumbana nayo ni ndani ya vyama ilikuwa ni kutiliwa mashaka kama ataweza mikikimikiki ya uchaguzi lakini wanasahau kuwa wanawake nao wanaweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili kijamii.


Naye mtafiti mkuu wa utafiti huo Profesa Luth Meena ameongezea kuwa taarifa hii itasaidia vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo vyama vya siasa, msajili wa vyama vya siasa, tume za uchaguzi, vyombo vya habari, TAKUKURU, pamioja na Asasi za kiraia na jamii kwa ujumla kuzumgumzia kwa usahihi ikiwemo kuchukua hatua za kisera, kisheria katika kuleta usawa wa kijinsia katika michakato ya uchaguzi huku ikiwapa uwezo wa kujiamini kwa wanawake katika kushiriki katika masuala ya uchaguzi.




Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com Call Send SMS Add to Skype You'll need Skype CreditFree via Skype

AZAM HABARI ZA NYUMBANI AZAM FC WATWAA UBINGWA ZAMBIA BILA KUPOTEZA MCHEZO AZAM FC WATWAA UBINGWA ZAMBIA BILA KUPOTEZA MCHEZO

February 03, 2016
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, jioni ya leo imetwaa ubingwa wa michuano maalumu iliyomalizika jijini Ndola Zambia baada ya kutoa suluhu dhidi ya Zanaco FC ndani ya Uwanja wa Levy Mwanawasa.
Sare hiyo imeifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi tano sawa na washindi wa pili Zanaco, lakini imewazidi washindi wa pili hao wa Ligi Kuu Zambia, kwa wastani wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam FC kama ingekuwa makini kwenye mchezo huo huenda ingejiandikia bao la uongozi dakika ya 8 baada ya kufanya shambulizi kali langoni mwa Zanaco, lakini shuti alililopiga Kipre Tchetche nje kidogo ya eneo la 18, lilipanguliwa na kipa na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Licha ya juhudi za Zanaco FC nao kutaka kupata bao kwa kufanya mashambulizi kadhaa, safu ya ulinzi ya Azam FC na eneo la kiungo lilikuwa makini kuondoa hatari zote.
Azam FC ilipoteza nafasi nyingine dakika ya 41 baada ya beki Shomari Kapombe kuingia vizuri kwenye eneo la 18 la Zanaco akipokea pande safi la Tchetche, lakini shuti alilopiga lilitoka sm chache ya lango.
Hivyo hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote ziliweza kutoshana nguvu kwa kutofungana, ambapo kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kufanya mabadiliko matatu, akitoka beki Pascal Wawa na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Jean Mugiraneza, mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi uwanjani kasoro golini.
Wengine waliotoka kwa upande wa Azam FC ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’ na kuingia Allan Wanga, pia alitoka Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kuingia Mudathir Yahya, mabadiliko ambayo yalisaidia kuimarisha zaidi eneo la kiungo na Azam FC kumiliki sehemu kubwa ya mchezo.
Dakika ya 72 Allan Wanga alishindwa kutumia vema pasi ya Domayo baada ya kuchelewa kufunga bao akiwa anatazaman na kipa wa Zanaco kufuatia mabeki kumuwahi na kuokoa hatari hiyo, dakika mbili baadaye Azam FF alitoka Thetche na kuingia Ame Ally ‘Zungu’.
Kutokana na Azam FC kuhitaji sare tu au ushindi katika mchezo huo ili kuibuka mabingwa, ilibadilisha mchezo kuelekea dakika 20 za mwisho na kucheza soka la kujilinda zaidi na hadi dakika 90 zinamalizika iliweza kutimiza lengo lake hilo.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika timu zote mbili zilipata fursa ya kupongezana pamoja na kusalimiana na waamuzi, kuashiria kutimiza sheria ya kiungwana mchezoni ya ‘Fair Play’.
Wakati Azam FC ikiwa inashiriki kwa mara ya pili michuano hiyo, kihistoria timu ya Power Dynamos ya Zambia ndio timu ya kwanza kutwaa ubingwa huo mwaka juzi kabla ya mwaka jana kuchukuliwa na TP Mazembe, ambayo ilienda kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Azam FC kutwaa ubingwa huo kunaifanya izidi kujiongezea mataji waliyotwaa msimu huu tokea kurejea kwa Kocha Stewart Hall, kufuatia Agosti mwaka jana kutwaa taji la michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup).
Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania kesho usiku na kitawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere (JNIA) Ijumaa Alfajiri.
Kikosi Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Ramadhan Singano ‘Messi’, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Abdallah Kheri, Pascal Wawa/Mugiraneza dk45, Michael Bolou, Frank Domayo, Salum Abubakar/Mudathir dk45, Kipre Tchetche/Ame Ally dk74 na John Bocco/Allan Wanga dk45
NHIF YATUMIA MTANDAO WA SIMU KUWASILISHA TAARIFA ZA MAMA MJAMZITO NA WATOTO WACHANGA

NHIF YATUMIA MTANDAO WA SIMU KUWASILISHA TAARIFA ZA MAMA MJAMZITO NA WATOTO WACHANGA

February 03, 2016

6
Afisa Mradi wa KFW kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Francis Mbwana akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo
kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya Afya mkoani Tanga iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa.
7
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga, Dinna Mlwilo akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa
mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.
3
4 
Watoa huduma za afya ya mama na mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Tanga wakati wa ufunguzi wa
mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.
………………………………………………………………………………
MFUKO wa bima ya afya kupitia mradi wake wa KFW umeanza kutoa elimu kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto namna ya kutumia mitandao ya simu kuwasilisha taarifa za afya mama mjamzito na mtoto mchanga.
Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha wanapunguza ikiwemo na kuzuia kwa kiasi kikubwa changamoto ya vifo vya wajawazito pamoja na watoto wa changa nchini kote. Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi wa KFW mkoa wa Tanga Francis Mbwana wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani hapa. Alisema kuwa utaratibu huo wa kutumia teknolojia ya simu katika kusajili na kufuatilia hali za afya za mama wajawazito na watoto zitasaidi kupata taarifa za maendeleo ya afya zao mapema tofauti na sasa. “Kupitia mradi huu wa KFW muda mwingi fomu za wanachama wapya zilikuwa zinachelewa kutufikia ,huku wakati mwingine mjamzito anakuwa katika hali ya hatari tunashindwa kumfuatilia kwa wakati lakini kupiti njia ya simu tutaweza kufanya malipo na ufuatiliaji kwa haraka”alibainisha Mbwana. Aliongeza kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha wajawazito wote nchini wanapata fursa ya kujiunga na huduma hiyo hususani maeneo ya vijijini ili kuhakikisha wanapata fursa ya kufaidika na mradi huo. Nae mmoja wa Wauguzi wa afya Ester Kimweri alisema kuwa toka KFW ianze miaka miatau iliyopita mahudhurio ya wajawazito yamekuwa yakiongezeka kila siku tofauti na hapo awali. “Mpango wa KFW umesaidia wajawazito wengi kuona umuhimu wa kujifunguali katika vituo vya afya,zahanati na hospitali tofauti na hapo awali mahudhurio yalikuwa ni madogo”alisema Kimweri.

WAAJIRI WALALAMIKIA RUSHWA KUKWAMISHA BIASHARA.

February 03, 2016

 Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka  akiwa anafafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha  waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha leo






 wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa  wakiwa wanajadili  kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua .
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa  Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka  akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za  ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi 


Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.

Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.

TASWIRA MBALIMBALI MTANANGE WA YANGA NA PRISON ULIOCHEZWA KATIKA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA

February 03, 2016

Mtanange wa Yanga na Tanzania Prison watoka Sale ya gori Mbili  kwa Mbili ambapo Mchezaji wa Timu ya Yanga Hamis Tabwe alifunguwa Lango la Timu ya Tanzania Prison kwa Gori la kwanza Dakika ya 36 kisha Jeremia Juma Mchezaji wa Tanzania Prison kusawazisha Bao la kwanza Dakika ya 41 kwa Timu yao ya Tanzania Prison, kisha Mhammed Mpoki Mchezaji wa Prison kuongeza tena Gori la pili Dakika ya 63 kwa Timu ya Prison na Saimoni Msuva kutoka Yanga kusawazisha Gori la pili kwa Timu ya Yanga ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kikosi Kazi cha Timu ya Yanga.
Kikosi Kazi cha Timu ya Tanzania Prison..
Baadhi ya mashabiki walio zuwa Gumzo Uwanjani mara baada ya Kumwaga Razi kwa kuvuwa Nguo zao kuishangilia Timu yao ya Prison iliyokuwa ikichuwana na Yanga katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mashabiki kinazi wa Timu ya Dar es salam Young Africa wakishangilia Timu yao ya Yanga.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO GLOBU YA JAMII MBEYA.
MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA KAMBI YA WAZEE WASIOJIWEZA NA WALEMAVU YA NUNGE, KIGAMBONI, DAR ES SALAAM LEO

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA KAMBI YA WAZEE WASIOJIWEZA NA WALEMAVU YA NUNGE, KIGAMBONI, DAR ES SALAAM LEO

February 03, 2016

1
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
2 3
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
4
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
5
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akioneshwa maeneo mbalimbali  na Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
6
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
8
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
9
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
10
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
11
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
13
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
14
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani kutoka kwa Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti  wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
15
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru  Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti  wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
PICHA NA IKULU