DC MGAZA AWATAKA WAKINA MAMA WAJASARIAMALI KUBADILIKA ILI KUENDANA NA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

February 22, 2015
MKUU WA WILAYA YA MKINGA NA KAIMU MKUU WA WILAYA YA TANGA,MBONI MGAZA AKIZUNGUMZA NA WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI WA KIKUNDI CHA IMANI VICOBA WAKATI ALIPOKWENDA KUZINDUA MIRADI YA WAKINA MAMA HAO

MKUU WA WILAYA YA MKINGA NA KAIMU MKUU WA WILAYA YA TANGA,MBONI MGAZA AKIWA KWENYE MAANDAMANO NA WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI WA KIKUNDI CHA VICOBA CHA IMANI



MKUU WA WILAYA YA MKINGA NA KAIMU MKUU WA WILAYA YA TANGA,MBONI MGAZA AKIANGALIA BIDHAA MBALIMBALI VINAZOTENGENEZWA NA WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI WA KIKUNDI CHA IMANI JIJINI TANGA






WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI WANAOUNDA KIKUNDI CHA IMANI VICOBA WAKIMSIKILIZA MKUUWA WILAYA YA MKINGA NA KAIMU MKUU WA WILAYA YA TANGA,MBONI MGAZA

MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA KATIKA MKOA WA TANGA.

February 22, 2015

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete ameteua  Wakuu wa Wilaya wapya 12, waliobadilishwa vituo vya kazi 64 na waliobaki kwenye vituo vya zamani 42. Katika Mkoa wa Tanga yafuatayo ni mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya.

Wakuu wa Wilaya Wapya.
1      Wilaya ya Tanga
Mhe. Abdula Suleiman Lutavi anayetokea Wilaya Namtumbo

2    Wilaya ya Muheza
 Mhe. Esterina Julio Kilas akitokea  Wilaya ya Wanging’ombe

3    Wilaya ya Pangani
Mhe. Regina Regnald Chonjo akitokea Wilaya ya  Nachingwea

4   Wilaya ya Lushoto
     Mhe. Mariam M. Juma ambaye ni uteuzi mpya 

5    Wilaya ya Handeni
Mhe. Husna Rajab Msangi ambaye ni uteuzi mpya

Wakuu wa Wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ndani ya Mkoa
1   Mhe.Hafsa Mahinya Mtasiwa ambaye amehamishiwa Wilaya ya Korogwe akitokea Wilaya ya Pangani.

Wakuu wa Wilaya waliobaki kwenye vituo vyao vya zamani ndani ya Mkoa
1     Mhe.Mboni Mwanahamis Mgaza, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga
2     Mhe. Suleman Salum Liwowa, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi

Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na kupangiwa kazi nyingine
1.      Mhe. Mrisho Gambo, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe

Waliokuwa Wakuu wa Wilaya za Tanga na kuhamishiwa Wilaya zingine Nchini
1. Mhe. Subira Hamis Mgalu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza amehamishiwa Wilaya ya             Kisarawe
2. Mhe. Magid Hemed Mwanga alieykuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto amehamishiwa Wilaya ya         Bagamoyo
3. Mhe.  Muhingo Rweyemamu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni amehamishiwa Wilaya ya         Makete
CHANZO:MKOA WA TANGA BLOG

WAZIRI MKUU: ANZISHENI HALMASHAURI NYINGINE KILOLO

February 22, 2015

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa uangalie uwezekano wa kuanzisha Halmashauri mpya katika wilaya ya Kilolo kata ya Mahenge na tarafa ya Mahenge kwa sababu ya hali ya kijiografia ya eneo hilo.

“Makao makuu ya wilaya hii yako Kilolo kule milimani. Ukitaka kuja huku ni lazima upite kwanza mjini ndipo ufike huku. Hapana! Hatuwezi kuwasaidia wananchi hawa kujiletea maendeleo kwa staili hii,” alisema Waziri Mkuu.
Alikuwa akihutubia wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda wilayani Kilolo, jana jioni (Jumamosi, Februari 21, 2015) mara baada ya kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa ambao ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu. Vijiji hivyo viko umbali wa km. 120 kutoka Ipogoro ilipo njia panda ya kwenda Iringa mjini na km. 155 kutoka Kilolo mjini yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Waziri Mkuu alisema kata za tarafa hiyo ni kubwa mno kwa mtendaji kuweza kusukuma maendeleo ya wananchi. “Kata hii imeanzia Kitonga hadi huku Nyanzwa. Hivi ni mtendaji gani anayeweza kuja kuhimiza shughuli za maendeleo akitokea huko?” alihoji Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Alisema mbali na idadi ya watu, suala la kijiografia huwa linaangaliwa wakati wa kuanzisha maeneo ya utawala. “Hili eneo ni zuri, fursa zipo lakini linakosa usimamizi ndiyo maana hata wilaya hii inaongoza kwa umaskini kuliko wilaya nyingine za mkoa huu. Acheni wilaya ibaki moja, mbunge abaki mmoja lakini Halmashauri ziwe mbili ili muweze kusukuma maendeleo ya eneo hili kwa sababu mtakuwa na madiwani wenu na bajeti yenu,” alisema.
Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kijiji cha Nyanzwa, Bw. Hekima Masanula Katemo alisema skimu ya umwagiliaji ya Nyanzwa ilijengwa mwaka 1960 wakati huo kwa kutumia banio la miti na magunia ya mchanga. Ilikuja kuboreshwa miaka ya 90 kwa ufadhili kutoka Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Sweden.
“Hata hivyo, skimu hii ambayo inahudumia wakulima 3,469 wakiwemo wanaume 1,662 na wanawake 1,807; inakabiliwa na uhaba wa maji kwani ni hekta 256 tu ambazo zinamwagiliwa kwa sasa wakati eneo lote la mradi ni hekta 940,” alisema Bw. Masanula.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Iringa kwa kutembelea Manispaa ya Iringa ambako atakagua ujenzi wa maabara kwenye shule ya sekondari Kihesa, kuzindua kituo cha polisi cha Semtema, na kukagua huduma za afya kwenye hospitali ya manispaa ya iringa. Pia atakagua mradi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewela kabla ya kutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja wa shule ya msingi Ipogolo.

MASHUJAA BAND KUBURUDISHA KILIMANJARO MARATHON

February 22, 2015

Na Mwandishi Wetu

BENDI mpya inayotamba kwa sasa hapa nchini na ambayo imechukua tuzo mbalimbali za muziki hapa nchini Mashujaa Band Jumapili tarehe 1 Machi inatarajia kushuka mjini Moshi katika ukumbi wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika kuwapa burudani washiriki pamoja na wananchi wote watakaofika kwenye uwanja huo kwa ajili ya mbio za Kilimanjaro Marathon 2015.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema kuwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeandaa burudani hiyo ikiwa ni mojawapo ya burudani zilizoandaliwa kwa ajili ya kuongeza msisimko katika mbio hizo.
Alisema kuwa siku ya Kilimanjaro Marathon bendi ya Mashujaa watatoa burudani hiyo kwa kushirikiana na kundi la Jambo Squad kutoka Arusha.

Kikuli aliongeza kuwa Jambo Squad pamoja na Warriors From The East la Arusha kwa pamoja wataanza kuchangamsha mji wa Moshi kuanzia usiku wa Ijumaa tarehe 27 ambapo watatoa burudani kabambe kwa wakazi wa Moshi kwenye ukumbi wa Voda House ikiwa ni burudani mahususi kuelekea Kilimanjaro Marathon.

Mbali na burudani ya muziki siku ya Kilimanjaro Marathon kutakuwa na burudani mbalimbali katika viwanja hivyo pamoja na nyama choma kutoka bar mbalimbali maarufu za Moshi ambao watachoma nyama na kuuza vinywaji uwanjani hapo.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema kuwa wanariadha wanaotaka kushiriki mbio hizo wataweza kujiandikisha tarehe 26 jijini Arusha kwenye Hoteli ya Kibo Palace na kwa Moshi watajiandikisha Keys Hotel tarehe 27 na tarehe 28 Februari 2015 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Aliongeza kuwa mbio ndefu la Kilimanjaro Premium Lager Marathon za kilomita 42 zitaanza saa 12.30 asubuhi kutokea uwanja wa Ushirika wakati mbio za Tigo Kili Half Marathon zitaanzia nje ya geti la Chuo cha Ushirika saa moja kamili asubuhi na kukimbia wakielekea Mweka na mbio yao itaishia hapo hapo uwanjani. Wakati huo huo mbio za walemavu za Gapco zitaanza saa 12.45 (saa moja kasorobo) kutokea uwanja wa Ushirika na huku mbio za kujifurahisha za 5 km Fun Run zikianza saa 1.45 asubuhi kwenye mzunguko wa YMCA na kumalizikia uwanjani.

Addison alisema kuwa maandalizi ya kutosha yamefanyika kuhakikisha washiriki wanafurahia mbio hizo kwani kila mdhamini atakuwa na vituo maalum vya maji ya kunywa na viburudisho na burudani nyingine katika vituo hivyo ambavyo vitakuwepo kila baada ya kilometa chache katika njia zitakapopita njia hizo”.

Mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zinaratibiwa na Executive Solutions kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Tigo, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA na Kilimanjaro Water.

MKUTANO WA 16 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI,KENYA, KATIKA PICHA

February 22, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa
Burundi jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwindikiza na Rais Pierre Nkurunzinza wa
Burundi walipokutana jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipigiwa wimbo wa taifa wa
Tanzania baada ya kuwasili  kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Kulia ni Naibu
Rais wa kenya Mhe. William Samoei
Ruto
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakisimama kwa wimbo wa mataifa
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki   kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 16
wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakiwa meza kuu  kwenye
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiongoza  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akipeana mikono na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada
ya kupokea kijiti cha kuongoza jumuiya hiyo wakati wa   mkutano
wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia
ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison
Mwakyembe akiwasilisha ripoti ya mwaka ya baraza hilo   mkutano
wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Bango la wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Waziri wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri
wa Jumuiya baada ya kukabidhiwa  ripoti ya mwaka ya baraza hilo
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akimuaga Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyekwemnda
kumuomba udhuru ili kuondoka mapema kabla ya kumalizika kwa
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Jaji
Geoffrey W. M. Kiryabwire akiongozwa kuelekea jukwaani kula kiapo kuwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete  akimpongeza Jaji Audace Ngiye kutoka Burundi
baada ya kula  kiapo  kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete  akimpongeza Mhe Liberag Mpfumukeko kutoka Burundi
baada ya kuteuliwa kuwa Nibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki February 20, 2015
Waziri wa Ushirikiano wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki wa
Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya
hiyo Dkt Harrison Mwakyembe akishauriana jambo na  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika MasharikiJoyce
Mapunjo 
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Wanafunzi washindi wa Insha wakisubiri kupokea tuzo zao katika
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Rais
Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akipungia mkono wajumbe walioko
Kampala baada ya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais
Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya moja
kwa moja kwa njia ya video uitwao Telepresence katika  mkutano wa
16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Ujumbe wa Tanzania katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015, Kutoka kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe Bernard Membe, WAZIRI wa nchi
ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora
Mhe. 
George Huruma Mkuchika,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe 
 George
Mcheche 
Masaju, Waziri wa Fedha, Mhe, Saada
Mkuya
 Salum na Waziri wa Maliasili
na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akihutubia katika kilele cha   mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya na
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini
baada ya  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya, Rais Pierre
Nkurunzinza wa Burundi na Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto  baada ya
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015. Picha zote na IKULU
 SIRI IMEFICHUKA KUMBE DIMPOZ MA WEMA SEPETU SI LOLOTE WALA CHOCHOTE...DIMPOZ MSHIKA PEMBE TU

SIRI IMEFICHUKA KUMBE DIMPOZ MA WEMA SEPETU SI LOLOTE WALA CHOCHOTE...DIMPOZ MSHIKA PEMBE TU

February 22, 2015

HABARI ya mjini ni kwamba, lile penzi linalonadiwa la Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limejaa magumashi, ikidaiwa kuwa jamaa huyo kawekwa kama boya tu, nyuma yake kuna kigogo mzito serikalini ndiye anayekula vinono, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akiwa na mwigizaji Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Dimpoz ameagizwa na kigogo huyo awe mpenzi kivuli wa Wema ili kuzuga watu wasishtukie mchezo kama yeye ndiye anayesukuma gududumu la malovee kwa Madam.

“Kutokana na unyeti wa kazi yake, jamaa hataki kujitokeza ‘front’ ndiyo maana ameamua kumtumia Dimpoz kama kanyaboya huku yeye akiendelea kula vyake,” kilisema chanzo hicho.Kikizidi kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilidai kigogo huyo ndiye anayedhamini safari zote za Wema na Dimpoz nje ya nchi ikiwemo ile ya juzikati nchini Marekani ambayo ilibuma. “Jamaa ana pesa chafu, amemnunulia Wema viwanja viwili kimoja kipo Tabata na kingine Kigamboni, Dar, ndiye anayemwezesha Wema katika shughuli zake za kila siku.“Kigogo huyo ndiye chanzo cha Wema kummwaga Diamond, alimpotezea kwa sababu ya maslahi zaidi, hata kwenye bethidei ya Wema mwaka jana, kigogo huyo ndiye aliyegharamia vitu kibao hadi kusababisha Diamond ahoji,” kilisema chanzo chetu. Jitihada za kumsaka kigogo huyo ili azungumzie ishu hiyo hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Dimpoz na kusomewa tuhuma hizo, alijibu:“Watu watambue kuwa uhusiano wangu na Wema upo kwa ajili ya ‘project’ zangu, niacheni please niinjoi maisha yangu kuhusu huyo kigogo muulizeni vizuri Wema mwenyewe,” alisema Dimpoz. Mwanahabari wetu alipomvutia waya Wema, alijibu kwa kifupi na kukata simu: “Ujue sasa hivi mimi sitaki malumbano na mtu, najua kila mtu siku hizi anaongea kila anachojisikia, naomba niachwe na maisha yangu, unayoyasema hayana maana, wanasema kwa sababu hakuna anayemjua mpenzi wangu wa sasa sina muda wa kubishana.” Hivi karibuni, wakiwa Sauz, Wema na Dimpoz, picha zao wakiwa kimahaba zilivuja mitandaoni hivyo kuibuka gumzo kuwa huenda kwa sasa nao wanatoka