YANGA SC WAMKABIDHI DEUS KASEKE JEZI YA CHUJI

May 25, 2015

Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh (kushoto) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, kiungo mpya Deus Kaseke (kulia) leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu, Jerry Muro.
Kaseke amepewa jezi namba nne iliyoachwa wazi na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athumani Iddi 'Chuji' aliyeachwa misimu miwili iliyopita

JESHI LA POLISI TANZANIA LAKABIDHIWA MASHINE ZA KUWEKA ALAMA SILAHA

May 25, 2015

Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, mashine 2 za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Kituo hicho chenye Makao Makuu yake Jijini Nairobi. Halfa hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akitoa maelezo jinsi mashine za kuweka alama silaha zinavyofanya kazi. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.
Mashine za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania. Uwekaji wa alama katika silaha utasaidia udhibiti wa matumizi ya silaha hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kushukuru msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest Mangu akishukuru kuhusu msaada wa mashine za kuweka alama silaha zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo, Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa nne kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu (wa tatu toka kulia) na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RECSA) Bw. Theoneste Mutsindashyaka (wa nne toka kushoto) baada ya hafla ya kupokea mashine za kuweka alama silaha iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wengine ni Viongozi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu na wageni wengine waalikwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA JUMUIYA YA MADOLA NA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA BARANI AFRIKA, JIJINI DAR

May 25, 2015

Makamau wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo Mei 25 kwenye Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, kufungua rasmi mkutano wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akifurahia jambo na baadhi ya Viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo,uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya kufungua rasmi leo kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika leo Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa

May 25, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015. Wakuu wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama. Wengine ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera. Imetolewa na; Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 25 Mei, 2015
Rais Kikwete afungua Mkutano wa Shirikisho la Vyuo vya elimu ya Juu Dodoma

Rais Kikwete afungua Mkutano wa Shirikisho la Vyuo vya elimu ya Juu Dodoma

May 25, 2015

jk2
Mwenyekiti wa CCM Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu nakala za kanuni za Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu kuzizindua rasmi wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Shirikisho hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kilimani mjiini Dodoma leo. Kulia ni katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,watatu kulia ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula na kushoto ni mlezi wa shirikisho hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknologia Ndugu January Makamba.
jk1
Rais Kikwete akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kwanza wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu mjini Dodoma.
jk3
Rais Kikwete akisalimiana na baadahi ya wanafunzi baada ya kufungua mkutano(picha na Freddy Maro)
UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

May 25, 2015
DSC_0048
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akisalimiana na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe, Geita. Kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha na Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla na wa pili kushoto ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Zainul Mzige wa modewjiblog
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.
Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
“ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
DSC_0062
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.
“ Gari hili litumike kwa matumizi ya wagonjwa tu. Sitegemei kusikia kuwa linapeleka wafanyakazi sokoni kununua nyanya. Na Mkurugenzi atenge bajeti ya mafuta ya gari hili muda wote”, aliagiza Majaliwa.
Hafla ya makabidhiano ya misaada hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Fistula duniani yaliyofanyakia kitaifa katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe katika Wilaya ya Mbogwe , Mkoani Geita.
Akizungumuza katika hafla hiyo Mwakilishi msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dkt. Rutosha Dadi alisema msaada wa vifaa walivyotoa utasadia kumaliza tatizo la Fistula na kuboresha huduma zingine za afya .
“ Tumefanya ukarabati mkubwa sana katika jengo la upasuaji na kutoa vifaa vya kisasa kama vile Ultrasound”, alisema Dkt. Dadi.
DSC_0072
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha (wa nne kulia) akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na umati wa wakazi wa Mbogwe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa miradi ya AMREF, kanda ya ziwa Dkt. Awene Gavyole, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Charles Palanjo, mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Joseph Kisalla, Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon pamoja na Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0204
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Mbogwe mkoa wa Geita.
IMG_1150
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akisisitiza jambo wakati wa kutoa salamu za Umoja wa Mataifa.
DSC_0149
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla akizungumza na wakazi wa Mbogwe ambapo aliwataka kufika katika vituo vya afya vilivyokaribu na makazi yao kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Fistula pindi wanaonapo dalili na moja kwa moja kuwasiliana na Hospitali yake inayotoa huduma za matibabu bure ikiwemo usafiri na malazi mpaka mgonjwa anapopona na kumrejesha anakoishi.
IMG_1089
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akitoa salamu za Vodacom ilivyobega bega katika kupamba na ugonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- kutoka Taasisi ya Vodacom Foundation kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa Fistula nchini wakati wa maadhimisho yanayofanyika kila mwaka Mei 23.
DSC_0248
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon, kwa niaba ya hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Fistula nchini wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mwishoni mwa wiki, Katikati ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla.
DSC_0254
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- kwa Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla (kushoto) na anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.
DSC_0182
Bi. Esther Ernest akitoa ushuhuda wake baada ya kuteseka na ugonjwa wa Fistula kwa takribani miaka 8 na jinsi jamii ilivyomnyanyapaa akiwemo mume wake hadi alipopatiwa matibabu na kupona kabisa hali iliyompelekea kurudisha furaha na nuru katika uso wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0928
Kikundi cha maigizo cha Mrisho Mpoto kikitoa elimu kwa njia ya maigizo jinsi Wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wanavyonyanyapaliwa na waume zao na kudhalilishwa kwa jamii ikiwemo kuitwa majina ya kila aina kutoka na kutokwa na haja ndogo muda wote bila breki.
IMG_0947
Mwigizaji wa kikundi cha sanaa za maigizo cha Mrisho Mpoto akilia kwa uchungu kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula na kunyanyapaliwa na mumewe wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0969
Msanii mahiri wa sanaa ya kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akimliwaza Mwanamke anayenyanyapaliwa na mumewe kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure kabisa bila gharama yoyote na Hospitali ya CCBRT.
IMG_1006
Mume wa mwanamke anayeumwa Fistula wakisoma vipeperushi vya CCBRT vinavyotoa elimu, dalili na nini cha kufanya pindi unapojigundua ni Fistula pamoja na jirani yake wakati wa mchezo wa maigizo kwenye maadhimisho hayo.
IMG_1009
Mrisho Mpoto akiendelea kutumia sanaa ya maigizo kuelemisha umati wa wakazi wa wilaya ya Mbogwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_1030
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kushoto) na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita, Dkt. Joseph Kisalla wakifuatilia igizo la unyanyapaa kwenye jamii kwa wanawake wanaougua Fistula wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0170
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifurahi jambo kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0235
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Fistula CCBRT, Elizabeth Jacob na kumkabidhi pesa taslimu Sh. 20,000/- kama motisha ya kazi anazofanya za kuwasafirisha wagonjwa wa Fistula jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
DSC_0238
Balozi wa Fistula CCRT, Elizabeth Jacob akionyesha pesa alizokabidhiwa kama zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0241
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza na kumkabidhi pesa taslimu sh. 100,000/ kama motisha ya kazi anazofanya za kuelimisha jamii kwa kutumia sanaa na maigizo Mrisho Mpoto aliyekuwa akisheresha sherehe hizo.
DSC_0023
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla ( kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa Sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda (22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula aliahidiwa na Bi. Haika Mawalla (kushoto) mtoto wake atatibiwa bure katika hospitali CCBRT baada ya kusikia matangazo jirani na eneo liliofanyika sherehe hizo ambapo kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.
DSC_0025
Mariam Sanda (22) akiwa amembeba mwanae mwenye mdomo wa Sungura.
DSC_0098
Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbongwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_0958
DSC_0101
IMG_0897
IMG_0891
IMG_1359
Burudani kutoka kwenye kikundi cha Mrisho Mpoto.
IMG_1393
DSC_0272
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Petr Shilogile (kushoto) akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa uliofadhiliwa na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania na ujenzi kusimamiwa na AMREF kabla ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0275
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua cha jiwe la msingi huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi (kulia) akishuhudia tukio hilo.
DSC_0277
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi.
DSC_0281
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
DSC_0282
Sasa limezinduliwa rasmi.
DSC_0287
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0318
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
DSC_0340
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha "Ultra sound" kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0362
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
DSC_0373
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
DSC_0386
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
DSC_0388
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
DSC_0411
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
DSC_0421
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC pamoja na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.