MHE BITEKO AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUKOMESHA UTORO MASHULENI, ACHANGIA MATOFALI 10,000 UJENZI WA MAABARA

April 02, 2018


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua majengo ya maabara za shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala, Leo 2 Aprili 2018.


Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakifatilia mkutano wa hadhara ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua ujenzi wa nyumba za madaktari wa kituo cha afya cha Uyovu akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018

Na Mathias Canal, Geita

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 2 Aprili 2018 amechangia matofali 10,000 kwa ajili ya ukamilishaji Wa vyumba vya maabara ili kurahisisha uanzisha Wa shule ya sekondari Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe.

Shule ya sekondari Busonzo inahitaji kukamilisha maabara tatu ili iweze kufunguliwa ambapo serikali imetoa milioni 40 kwa ajili ya kazi hiyo.

Mhe Biteko amechangia matofali hayo Mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa wakati Wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita kwa kuwataka viongozi wa mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni.

"Mkoa wetu tumepata aibu kubwa kwa kuwa namba mbili kwa utoro kati ya mikoa yote nchini, utoro huu hapa wilayani kwetu unachangiwa na umbali wa kwenda shuleni, hapa Busonzo watoto wetu wanasoma Runzewe ambapo ni mbali sana. Umbali huo unachangia utoro" alisisitiza Mhe. Biteko

Katika sherehe hizo zilizonakshiwa na Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ambayo ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’ Waziri Mkuu alisema kuwa utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni mkubwa zaidi kwa Mikoa husika kuliko shule za msingi.

Mara baada ya uzinduzi Wa Mwenge huo wa Uhuru kabla ya kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za Bunge zinazotarajiwa kuanza kesho 3 Aprili 2018 Mhe Doto Biteko amezuru Kijiji cha Nampalahala kilichopo Kata ya Busonzo na kujionea jinsi ujenzi Wa maabara unavyoendelea.

Mara baada ya kubaini kuwa kuna upungufu wa matofali 10,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, Naibu Waziri huyo amechagiza ujenzi huo kwa kuchangia gharama za ununuzi wa matofali hayo ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu ameshatoa maelekezo ya kukomesha utoro naomba tukimbie kulitekeleza hilo na ninaomba wazazi tuhakikishe watoto wote wanakuwa shuleni ni aibu mno sisi kuwa vinara wa utoro". Aliongeza Mhe. Mbunge Na Naibu Waziri huyo.

Alisema kukithiri jambo ambalo limepelekea Mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa utoro Kitaifa kwa asilimia 8.1, ambapo Mtwara imekuwa nafasi ya tatu kwa asilimia 6.4, Shinyanga asilimia 6.3 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Mkoa Wa Tabora kwa asilimia 9.7

Aidha, Mhe Biteko ameonyesha kusikitishwa na takwimu za Mkoa Wa Geita kushika nafasi ya pili pia katika kwa utoro kwa shule za msingi kwa kwa asilimia 3.1 nyuma ya Mkoa Wa Rukwa unaoongoza kwa asilimia 3.2

Aliongeza kuwa anatamani kuona Wilaya ya Bukombe inahakikisha inafikia viwango bora vya elimSerikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imedhamiria kuboresha elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu hivyo wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kwa maendeleo ya wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla aliwaomba pia wananchi wa kata ya Busonzo kumuombea Rais Magufuli na kuunga mkono juhudi za serikali
WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI GEITA

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI GEITA

April 02, 2018



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo,Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kiongozi wa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita Aprili 2, 2018



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.



Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Karume akizungumza katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel wakati alipotoa salamu za mkoa huo katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita Aprili 2, 2018.



Watoto wakionyesha halaiki katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru zilizoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

………………

*Ataja mikoa saba inayoongoza kwa utoro wa wanafunzi shuleni


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za sekondari wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni.

“Kwa ujumla utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni mkubwa zaidi kwa Mikoa husika kuliko shule za msingi. Nitumie nafasi hii kuikumbusha Mikoa niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi wenyewe kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio shuleni.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Aprili 02, 2018) wakati akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita. Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’

Waziri Mkuu amesema dhamira ya Serikali kupitia kaulimbiu hiyo ni kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwekeza katika elimu na kuzalisha rasilimali watu yenye ujuzi na stadi zitakazowezesha kuchochea mapinduzi ya viwanda ili nchi iwe ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

Akizungumzia kuhusu utoro kwa shule za sekondari nchini, Waziri Mkuu amesema mkoa wa Tabora ndio unaongoza kwa utoro kwa kuwa na silimia 9.7,

Geita asilimia 8.1, Mtwara asilimia 6.4 na Shinyanga asilimia 6.3.

Kuhusu utoro wa wanafunzi wa shule za Msingi nchini, Waziri Mkuu amesema mkoa unaoongoza ni wa Rukwa kwa asilimia 3.2, Geita asilimia 3.1, Tabora asilimia 2.9, Simiyu asilimia 2.0 na Singida asilimia1.9.

Amesema mikoa yenye kiwango kikubwa cha utoro wa wanafunzi na kuacha shule ihakikishe mahudhurio yanadhibitiwa shuleni ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaoandikishwa wanahudhuria, wanasoma na kuhitimu ngazi husika.

“Ukitaka kuleta maendeleo ya uchumi ulio imara, ukitaka kujenga jamii inayo heshimu na kufuata misingi ya uwajibikaji na ubunifu, ukitaka kujenga Taifa lenye amani na utulivu, lazima uwekeze zaidi katika elimu”.

“Kwa hiyo, uwekezaji katika elimu haumaanishi tu kuhakikisha watoto wetu na Watanzania kwa jumla wanapata haki yao ya msingi bali ni kuweka misingi imara itakayo liwezesha Taifa na mtu binafsi kufikia hatua bora ya maisha”.

Waziri Mkuu amesema ili kuhakikisha Taifa linafikia viwango bora vya elimu, Serikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imedhamilia kuboresha elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zitaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa kwa sababu bado ipo na inaendelea kuwa ni adui wa haki na kudhoofisha jitihada za Serikali za kuimarisha uchumi, kuimarisha huduma za jamii na Utawala bora.

Amesema athari zinazotokana na vitendo vya rushwa huwaathiri watu wa kawaida zaidi na kuendelea kubaki wanyonge katika jamii, hivyo Serikali itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa bila kuchoka mpaka jamii itakapoachana na vitendo hivyo vya kidhalimu.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bibi Jenista Mhagama alisema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa takribani kilomita 103,440.7 kwa siku 195 katika mikoa yote 31 nchini na halmashauri za wilaya 195.

Alisema kazi hiyo itafanywa na vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao wameandaliwa kikamilifu ili kuhakikisha wanaendelea kuwakumbusha Watanzania historia ya falsafa ya Mwenge wa Uhuru, kufikisha kwa ufasaha ujumbe wa mwaka huu na kukagua na kuzindua miradi yamaendeleo kwa umakini.

Bibi Jenista alisema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zinaongozwa na Bw. Charles Kabeho kutoka mkoa wa Dar es Salaam akishirikiana na Bw. Issa Abasi Mohamed (Kusini Pemba), Bi. gusta Safari (Geita), Bw. Ipyana Mlilo (Tanga), Bw. Dominick Njunwa (Kigoma) na Bi. Riziki Hassan Ali (Kusini Unguja).

Naye, Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume alisema atahakikisha ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unawafikia wananchi wote pamoja na kupita katika miradi yote ya maendeleo iliyopangwa.

Balozi Karume ametumia fursa hiyo kuwapongeza Rais Dkt. Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein kwa jitihada zao za kudumisha amani, utulivu, kuwaletea wananchi maendeleo bila ya ubaguzi pamoja na kupambana na maadui wanaotaka kudhoofisha maendeleo nchini.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA USIMIKAJI WA MFUMO WA RADA 4 KATIKA VIWANJA VYA NDEGE VINNE NCHINI PIA APOKEA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER Q400 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA USIMIKAJI WA MFUMO WA RADA 4 KATIKA VIWANJA VYA NDEGE VINNE NCHINI PIA APOKEA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER Q400 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE

April 02, 2018

Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku ikipewa heshma ya kumwagiwa maji(water salute) mara baada ya kutua.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, pamoja na viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa Serikali wakipiga makofi wakati wakiipokea Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwa imeegeshwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono na kushukuru wakati akiingia katika ndege hiyo mpya ya Bombardier Q400 iliyowasili kutoka nchini Canada.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono marubani wawili waliokuja na ndege hiyo mpya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi mfumo wa usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege (Mwalimu Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwanamuziki wa Bongo flavor Naseeb Abdul-Diamond platinum mara baada ya kuweka jiwe la msingi mfumo wa usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege (Mwalimu Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

TANZANIA YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI KUBORESHA BARABARA YA UVINZA-MALAGARASI KWA KIWANGO CHA LAMI

April 02, 2018



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akisalimiana na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, alipowasili Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi, kwa ajili ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (wa tatu kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, kabla ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami. kulia kwake ni Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk na Mkuu wa Dawati la Abu Dhabi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Kuchaka.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), akisindikizwa na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, baada ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami




Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51 kwa kiwango cha lami.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakibadilishana mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakionesha mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa shilingi bilioni 34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)



Benny Mwaipaja, Abu Dhabi


Tanzania imeendelea kuaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ambapo Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Falme za Kiarabu-Abu Dhabi, umeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 15, sawa na shilingi bilioni 34 za Tanzania, kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi yenye urefu wa kilometa 51, kwa kiwango cha lami

Hafla fupi ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya Mfuko huo yaliyopo Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, amesaini kwa niaba ya Serikali, na Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa niaba ya Mfuko huo.

Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, Katibu Mkuu-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa ni kiungo kikuu cha usafiri wa abiria na mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Kigoma na nchi jirani za Burundi na Kongo DRC.

Amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuboresha barabara hiyo kwa kiwango cha lami umelenga kuchochea uchumi wa nchi kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao ya wakulima pamoja na kupunguza gharama na kuongeza uwezo wa kufanya biashara na nchi hizo jirani.

"Tutabakiwa na kipande cha barabara yenye urefu wa kilometa 28 kutoka Urambo hadi Kaliua na kilometa 42 kutoka Chagu hadi Kazilambwa, barabara ambazo Serikali inaendelea kuzitafutia fedha ili kukamilisha barabara yote inayoelekea ukanda huo wa kati kutokea Dar es Salaam, Manyoni (Singida), Tabora hadi Kigoma" Alisema Mhandisi Iyombe.

Ameushukuru Mfuko huo kwa kuendelea kuiamini Serikali na kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu baada ya kufanya hivyo hivi karibuni kwa kutoa mkopo mwingine wa dola milioni 57, uliofanikisha kuboreshwa kwa barabara ya Kidahwe hadi Uvinza yenye urefu wa kilometa 77 kwa kiwango cha lami.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi, kwa upande wake, amesema kuwa Mfuko huo uko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Amefafanua kuwa mradi huo ambao mkataba umesainiwa mjini Abu Dhabi, utakuwa ni wa nne kufadhiliwa na Mfuko wake Tangu uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Tanzania uanzishwe mwaka 1977, ukiwemo mradi wa kuendeleza kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mradi wa Maji Vijijini huko Viwani Zanzibar na Mradi wa kuboresha barabara ya Kidahwe hadi Uvinza kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk amesema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni kiashiria cha kukubalika kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ya haraka na kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

"Hatua hii ni uthibitisho wa mahuasiano mazuri ya kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1977" Alisisitiza Mhe.Mbarouk

Mhe. Mbarouk amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ya Uvinza hadi Malagarasi kutachochea maendeleo ya kiuchumi na mapinduzi ya viwanda kwa kuunganisha shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na maliasili pamoja na kukuza utalii.

JUMIA FOOD YAFANYA MABORESHO KWENYE PROGRAMU YAKE YA SIMU

April 02, 2018

JUMIA Food, mtandao unaoongoza kwa huduma ya chakula barani Afrika, umezindua toleo jipya la programu yake ya simu ikiwa na maboresho zaidi yanayotarajiwa kuleta mapinduzi nchini Tanzania. Maboresho hayo yatampatia mteja uwezo wa kipekee wa kuweza kuitumia kwa urahisi zaidi na namna aitakavyo.




“tumejizatiti kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi za kidigitali, huku tukiwahakikishia uharaka wa kufikiwa na huduma ya chakula katika maeneo walipo. Maboresho ya programu yetu ya simu ni mojawapo ya mikakati ya mwaka 2018, pamoja na kuongeza unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma ya chakula,” alisema Joe Falter, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Food.



Programu mpya yenye maboresho zaidi, ambayo asilimia 35 ya wateja huitembelea, itaboresha mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao pamoja na mawasiliano; ikiwaruhusu wateja kuuliza kuhusu migahawa inayopatikana kwenye Jumia Food kwa mawakala wa huduma kwa wateja. Huduma za chakula zinazofanywa kupitia kompyuta bado zinaongoza kwa asilimia 40, wakati programu ya iOS inayotumiwa na wateja wenye simu za iPhone ikiwa na watumiaji kwa kiwango cha asilimia 25 katika nchi nyinginezo barani Afrika.



Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Jumia Food Tanzania, Xavier Gerniers ameongezea kuwa, “maboresho yaliyofanywa kwenye programu mpya ya simu ya Jumia Food hayatoleta muonekano mpya pekee bali pia kuwapatia uwezo wateja kuitumia namna watakavyo hususani kupata taarifa juu ya migahawa waipendayo. Kwa mfano, wateja wanaweza kutafuta aina vyakula wanavyovipenda na kisha programu ikawaletea orodha ya migahawa inayotoa huduma hiyo papo hapo. Tofauti na awali, toleo hili jipya limezingatia urahisi wa wateja kujiunga, kutafuta huduma na kuagiza chakula papo hapo. Cha kuvutia zaidi, wateja wanaweza pia kufuatilia mwenendo wa chakula walichokiagiza kitawafikia ndani ya muda gani!”








Kwa hivi sasa, programu hii inapatikana kwa watumiaji wa Android wakati kwa watumiaji wa iOS toleo litatoka mnamo katikati ya mwezi wa Aprili.

“siku zote Jumia Food ipo kuhakikisha inawahudumia watumiaji wa huduma za chakula Tanzania kwa weledi zaidi wakati huo huo ikiendana na mabadiliko ya soko. Tukiwa na zaidi ya migahawa 79 kwenye mtandao wetu, tunaamini kwamba hatimaye tutaweza kuwafikia wateja wote kwa njia ya mtandao,” alihitimisha Bw. Gerniers.



Kuhusu Jumia Food
Jumia Food Tanzania ni mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma ya chakula kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. Jumia Food ipo kwenye nchi 11 barani Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Morocco na Uganda. Huduma hii huwawezesha wateja kwa kupata huduma ndani ya wakati, huongeza wateja, kusaidia uendeshaji na njia za masoko.

WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME

April 02, 2018
"Shemeji zangu walikuwa sita walinipiga sana kwa kweli kwa sababu ya kutaka kumiliki Mali za Mume wangu ambaye ni Marehemu" , ni mmoja ya wanawake wa Tarime akisimlia  kwa masikitiko kutokana na ukatili alioupata baada ya kufiwa na mumewe, ambapo ndugu wa mume alilazimisha kumrithi yeye na mali za mumewe. Mila kama hizi zinazomkandamiza mwanamke zinapaswa kusitishwa 
"Tumekubali kabisa watoto wetu wa kike wasiendelee kukeketwa ,lakini bado jamii zetu hazituelewi tunaendelea kuwaelimisha ili nao wabadilike."- Mzee wa Kimila (Aliyesimama). Bado kuna kazi kubwa ya kumaliza swala la ukeketaji lakini kupitia elimu mbalimbali na mafunzo yanayotelewa kuhusu maswala ya ukeketaji juu ya hasara na madhara yake inaendelea kupunguza idadi ya wanaokeketwa.
"Kwa Tarime mwanamke kupigwa na kuvuliwa nguo hadhalani ilikuwa ni kitendo cha kawaida tu" - Sara Boniface (aliyesimama) , alielezea kwa kina kuhusu ukatili wa kupigwa ambapo aliongeza kwamba kwa sasa ukatili huo umepungua kutokana na elimu wanayoipata wanajamii juu ya ukatili wa kijinsia.
Mmoja wa wazee wa Kimira kutoka Tarime(aliyesimama) akieleza juu ya ukeketaji na kudai kuwa mwanamke aliyekeketwa anakuwa na thamani kubwa kama ilivyo kwa mwanamke mweupe kwa wasukuma, hii ni moja ya sababu zinazosababisha ukeketaji uendelee. Ikiwa elimu itaendelea kutolewa ukeketaji huu utapungua kwa kiasi kikubwa.
 "Ukatili wa ukeketaji ulikuwa unafanyika hadharani  kweupe, wazazi walikuwa wanalazimisha mabinti zao kukeketwa ili wapate mahali nyingi zaidi, ambapo fedha hizo ziwasaidie katika kupata kipato zaidi" - Nyakerandi Mariba. Swala hili limepungua sana kutokana na juhudi za wanamabadiliko kuendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
"Maswala ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika jamii zetu,hasa kwa mabinti na akina  mama"-Lucy Matemba Afisa maendeleo ya jamii Tarime
Meneja wa kampeni ya Tunaweza Bi. Eunice Mayengela akiendelea kutoa Muongozo wa majadiliano
Wanamabadiliko wakiendelea kufuatilia mjadala
"Kila wiki tunapokea kesi zaidi ya kumi (10) zanazoripotiwa Tarime zikihusu kipigo,ubakaji, ulawiti na wanawake kutishiwa kuuwa,kupigwa sana kisha kubakwa kwa lazima ama kulawitiwa"- Dawati la Jinsia . Licha ya kesi hizo kuwa nyingi lakini elimu inayoendelea kutolewa na kampeni ya tunaweza imesaidia sana kupunguza ukatili wa kijinsia.
Wazee wa Kimila kutoka Tarime wakiteta jambo wakati wa mjadala
 Wanamabadiliko wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Fredy Njeje
Blogs za Mikoa Tanzania Network Email: blogzamikoa@live.com Facebook/instagram/twitter @blogszamikoa Website: www.blogszamikoa.co.tz