KAMPUNI YA BIMA YA BUMACO YAILIPA KAMPUNI YA BATCO MAMILIONI

September 08, 2017


Na Binagi Media Group
Kampuni ya Bima ya BUMACO imeilipa kampuni ya mabasi ya BATCO inayofanya safari zake katika ya mikoa ya Mara na Mwanza, kiasi cha shilingi Milioni 140 ikiwa ni malipo ya bima baada ya basi la kampuni hiyo kupata ajali ya moto.

Halfa ya kukabidhi hundi ya fedha hizo imefanyika leo kwenye ofisi za kampuni ya Bumaco zilizopo Jijini Mwanza, na kushuhudiwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Meneja wa kampuni ya Bumaco Kanda ya Ziwa, Godlisten Muro amesema kampuni hiyo imekuwa ikilipa madai ya bima kwa wakati, lengo ikiwa ni kuwanusuru wateja wake na majanga mbalimbali yanayowakabiri na hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana kwamba bima hazilipi.

Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa, Sharif Ali Hamad ameipongeza kampuni ya bima Bumaco kwa namna inavyolipa kwa wakati fidia za wateja wake na hivyo kuwasihi wananchi wakiwemo wafanyabiashara kujiunga na mfumo wa bima ili kunufaika na fidia pindi wapatapo majanga.

“Basi la Batco lilipata ajali tarehe 10.06.2017 na leo tarehe 08.09.2017 wanalipwa fidia ya shilingi Milioni 140, ukiangalia tangu kupata ajali hadi kulipwa fidia ni kipindi cha miezi mitatu”. Amesema Hamad na kuongeza kwamba hatua hiyo inaonesha ni jinsi gani kampuni ya Bumaco inavyoshughulikia kwa haraka madai ya wateja wake.

Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Batco, Baya Kusanja Maragi amewasihi wafanyabiashara wenzake kujiunga na kampuni ya bima ya Bumaco kwani imekuwa ikimlipa kwa wakati madai yake ya bima, ambapo pia tarehe 14.02.2015 basi lake lilipata ajali na akalipwa madai yake ndani ya kipindi cha miezi mitatu.
Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa, Sharif Ali Hamad, akionyesha hundi halisi ya malipo kutoka kamouni ya bima ya Bumaco kwa ajili ya kampuni ya mabasi ya Batco ambayo basi lake liliungua moto mwezi wa sita mwaka huu.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Bumaco wakiteta jambo kwenye hafla hiyo ambapo kushoto ni Ayoub Richard na kulia ni Livinus Mberwa.
Attachments area Preview YouTube video KAMPUNI YA BIMA YA BUMACO YAILIPA BATCO MAMILIONI

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA MADINI YA ALMASI NA TANZANITE KUTOKA KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

September 08, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalumu ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Tanzanite kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi na Tanzanite mara baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalumu ya Bunge ya Kuchunguza Madini ya Almasi na Tanzanite Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi Taarifa hiyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa mkono Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kumkabidhi Taarifa hiyo ambayo aliwakabidhi pia viongozi wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum akipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mara baada ya kukabidhiwa Taarifa hiyo ya Uchunguzi.

MKUTANO WA 17 WA BARAZA LA MAWAZIRI UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU UDHIBITI WA BIASHARA FEDHA HARAMU

September 08, 2017
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip I.Mpango mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Dkt. Khalid Salum Mohamed mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wajkati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini South Afrika wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini SWAZILAND wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Zanzibar Nchini Tanzania wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI AGOSTI 2017 UMEPUNGUA HADI KUFIKIA ASILIMIA 5.0

September 08, 2017
 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kupungua kwa mfumuko wa bei. Kulia ni Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja 

SHAKA AZINDUA PROGRAMU YA USHIRIKISHWAJI KWA VIJANA DODOMA

September 08, 2017
                                                 Na Mathias Canal, Dodoma
 
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM)  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  Septemba 7, 2017 Amezindua Programu maalumu kwa Vijana wa CCM katika ushiriki wa shughuli za miradi ya Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii katika ukumbi wa CCM (NEC) Mjini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shaka alisema Wazo hilo limeibuliwa wakati muafaka huku serikali ya CCM awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ikiweka mkazo na vipaumbele kadhaa vinavyomtaka kila mtanzania hususani vijana kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha Mali.

Alisema dhana ya kufanya kazi kwa bidii, malengo na shabaha si ngeni lakini kwa wakati huu inahubiriwa kwa nguvu kulingana na changamoto nyingi zilizopo, fursa, ushirikishwaji kwa kuzingatia mahitaji halisi kutokana na mabadiliko ya dunia Kiuchumi na Kimaendeleo.

Aliwasisitiza Vijana kutambua wajibu wa kukuza shughuli za kazi na maisha zikiongozwa na nguvu ya uzalendo, kujali utaifa na kutambua dhamana iliyopo ya kudumisha amani, Umoja, Mshikamano na Maendeleo.

"Ili kusihi yote hayo hatimaye Vijana waweze kuyafanikisha tunapaswa kuwa na mioyo isiyopwaya au kukosa rutuba ya kutodumisha uzalendo, tunalazimika kwa pamoja kutambua mpango wowote wa kuyafikia maendeleo ya kweli utabaki ni hadithi na ndoto Kama hatutaongozwa na shime ya uzalendo au kutothamini utaifa wetu Kama ambavyo viongozi wanatuhimiza siku Hadi siku" Alisema Shaka

Shaka aliwaeleza Vijana kuwa pamoja na kuwepo juhudi kubwa za mara kwa mara kuchukuliwa na serikali, mashirika hiari ya Kijamii na yasiyokuwa ya kiserikali, kuelimisha juu ya dhana ya ushirikishwaji na ushiriki wa Vijana katika miradi ya Kiuchumi na Kijamii wanapaswa kuwa na utayari, uthubutu, uzalendo, na Utaifa.

Alisema kuwa Vijana wanapaswa kukubali kujadiliana na wenzao juu ya mpango wa maendeleo na hatma ya Taifa na mustakabali wake kwani ndiyo njia pekee ya kukuza uzalendo kwa Taifa.

Alisema mataifa yaliyoendelea yametokana na watu wake kukubali kufanya kazi kwani Ndiko kuliko yakomboa mataifa hayo yaliyoendelea kutoka katika uchumi duni na kuhamia katika uchumi wa Kati na Sasa wakionekana kuwa na uchumi wa maendeleo ya viwanda.

"Mafanikio hayakuja Kama zawadi kwenye kisahani Cha Chai ama kutokea kwa bahati mbaya Kama mtende unavyoota jangwani ni lazima kukubali kwa pamoja kufanya kazi ili kupambana na adui umasikini" 

"Wakati huu ambao serikali imebeba mzigo wa kutoa elimu bure toka msingi Hadi sekondari ni lazima Vijana tuwe na muktadha mmoja wa kujenga mtazamo wa pamoja kwa kujitambua na kukubali kufanya kazi bila kusukumwa" Alisema Shaka
 
Aliongeza kuwa kazi ya Vijana siku zote na kila wakati inapaswa kuwa ni kufikiri, kupambanua, kubuni na kujadiliana ili kumaliza changamoto, vikwazo, fursa na matumizi ya nafasi husika katika Jamii.

Aidha, kupitia kusanyiko hilo aliwaagiza na kuwataka makatibu wote wa Umoja wa Vijana wa CCM wa mikoa na Wilaya nchini kila mmoja kuhakikisha programu hiyo inaanzishwa katika mikoa na Wilaya zake na kusisitiza kuhitajika matokeo makubwa kwani ataandaa utaratibu wa kuthamini programu hiyo kila kipindi Cha robo mwaka.

Sambamba na hayo pia Kaimu  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka alishiriki ujenzi wa shule ya Msingi Mizengo Pinda iliyopo katika Kijiji Cha Chinangali 2 Kata ya Bwigili Wilayani Chamwino.

Pamoja na kushiriki shughuli ya uchimbaji msingi, ufyatuaji tofali na matengenezo ya tungilizi kwa ajili ya upauaji wa majengo ya shule hiyo pia Shaka alichangia mifiko 20 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi walizozianza kwa kujitolea nguvu, muda na rasilimali zao.

MUONEKANO WA JIJI LA TANGA JANA USIKU ENEO LA MATAA RELINI

September 08, 2017
Dalala na Pikipiki zikisubiri kuruhusiwa na mataa ili kuweza kupitia kwenye makutano ya Reli Jijini Tanga jana usiku

MADHARA YA VIPODOZI VYA KEMIKALI YAWATISHA WAKULIMA

September 08, 2017
Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare, Euphrasia Shayo (kulia) akiwasilisha mada yake juu ya madhara ya kemikali za vipodozi na mkorogo kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017
Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo akiuliza swali mara baada ya uwasilishaji.
 
Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.
Sehemu ya washiriki katika semina hiyo.
Sehemu ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 wakifuatilia mada anuai toka kwa wawasilishaji.
MATUMIZI ya vipodozi vyenye kemikali ya sumu yamewatisha wakulima katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Hofu hiyo ilitanda jana baada ya Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare, Euphrasia Shayo kuwasilisha mada yake kwa kundi hilo la wakulima wanaoshiriki tamasha la jinsia kutoka maeneo anuai.
Alisema kemikali za sumu kama zebaki na mericuri zilizomo katika vipodozi na mikorogo isiyo rasmi inayotumiwa hasa na akinamama kujichubua na kubadili nyele zao zina madhara makubwa katika kilimo.
Alisema kemikali hizo mbali na kukaa ardhini kwa muda mrefu zaidi zikiharibu mazao pia vinamadhara makubwa kwenye miili yao, hivyo kuwashauri kuachana navyo mara moja kwa watumiaji.
Alisema kemikali hizo mara baada ya kutumiwa hutelekezwa ardhini na mara mvua zinyeshapo husafirishwa hadi katika vyanzo mbalimbali vya maji hivyo kujikuta vikitumiwa tena na jamii jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na mifugo.
“…Vinamadhara makubwa katika miili yetu, ndio maana sasa hivi magonjwa ya ajabu ajabu ikiwemo kansa vimeendelea kushamiri kwetu, vinginea husababishwa na kemikali hizi zenye sumu. Wapo akinamama wameathiriwa vibaya sana na kemikali hizi zenye sumu,” alisema Bi. Euphrasia Shayo.

Serikali yaombwa kutoa kipaumbele upatikanaji mikopo nafuu ya kilimo

September 08, 2017
Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.
Sehemu ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 wakifuatilia mada anuai toka kwa wawasilishaji.

Mwakilishi wa Forum CC, Jackson Massawe (aliye simama) akiwasilisha mada kwa wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.
 
SERIKALI imeobwa kutoa kipaumbele katika upatikanaji wa mikopo nafuu ya kilimo kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na kupewa haki ya kupata na kumiliki mashamba ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo.

Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Forum CC, Jackson Massawe alipokuwa akiwasilisha mada kwa baadhi ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 linaloendelea katika viwanja vya TGNP Mabibo Dar es Salaam.

KAIRUKI HOSPITALI YAZINDUA KITENDO CHA KUCHUJA DAMU KWA WAGONJWA WENYE MATATIZO YA FIGO

September 08, 2017
SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.

Wito huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.Alisema, kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za  bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.

Makinda, alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.

“Vituo vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale wanaougua magonjwa yenye kulipia  gharama kubwa,”alisema Makinda.

 Aidha alisema ni watu wachache ambao wanauwezo wa kujitibu bila bima ya afya lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo kulingana na gharama kubwa za matibabu katika baadhi ya magonjwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu, alisema nchini Tanzania watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa  na magonjwa yanayosababishwa na matatizo ya figo.

“Kwa hivi sasa ugonjwa huo umeonekana kuathiri  kati ya asilimia 7 hadi 13 ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa  kisukari (Diabetes Mellitus)na shinikizo la damu(Acute Kidney  injury) ,”alisema.

Alisema kwa muda mrefu hospitali yao  imekuwa ikipokea wagonjwa wenye matatizo ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje ya hospitali hivyo kupitia kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.

Alisema kuwa kutakuwa na mashine  10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na hadi kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa mashine hizo ipo ya  kuchuja damu itakayosaidia kuzuia uharibifu wa figo wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.

Dk. Mchomvu, alisema hospitali hiyo inatarajia  kuongeza idadi ya mashine ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi  pamoja na kutoa huduma ya kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHJF), Anne Makinda (katikati), akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
Baadhi ya madaktari waliohudhuria hafla hiyo wakisikiliza hotuba za viongozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki akitoa hotuba yake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda (kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki, Kokushubila Kairuki.