TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

August 12, 2016
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba  akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.


 Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi  kushoto ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi
TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza  juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki  juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.

CHRISTIAN BELLA ALIVYONOGESHA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA

August 12, 2016

 Mwanamuziki nyota Christian Bella akikonga nyoyo za maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akitumbuiza  maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akiimba mbele ya maelfu ya wananchi wa  jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akipongezwa kwa kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwanamuziki nyota Christian Bella baada ya kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016

MWENYEKITI MPYA WA CCM RAIS DKT MAGUFULI APOKELEWA DAR ES SALAAM KWA NDEREMO NA VIFIJO

August 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).



WIMBO MPYA WA WAPANCRAS WAKIMSHIRIKISHA ABUU MKALI-NITUNZIE SIRI WATOKA RASMI.

August 12, 2016
Kundi la muziki la Wapancras linalojumuisha wasanii ndugu, Mecrass na Payus, la Jijini Mwanza, limeachia wimbo mpya uitwao "Nitunzie Siri", wakimshirikisha Abuu Mkali.

Wimbo umetengenezwa pande za Vibe Nation & Quick Sound ikiwa ni mikono ya Producers, Aniwylee na Day Dream.
Bonyeza HAPA Kusikiliza au bonyeza play hapo chini.
 Na BMG
WAGANDA KUWAAMUA TANZANIA, IVORY COAST, KIKOSI CHATAJWA

WAGANDA KUWAAMUA TANZANIA, IVORY COAST, KIKOSI CHATAJWA

August 12, 2016
Mchezo Mpira wa Miguu wa Ufukweni kati ya Tanzania na Ivory Coast kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa katikati na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.
Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, utarudiwa mwingine huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.

Kocha wa timu hiyo, John Mwansasu, leo Agosti 12, 2016 ametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari Mwansasu amesema kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
Pia Mwansasu amesema wanatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, watarudiana huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kikosi hicho kinaunda  na wachezaji Talib Ame, Ahamada,  Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.
Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
TTCL yahakikisha huduma bora kwa mashirika na taasisi yatakayohamia Dodoma

TTCL yahakikisha huduma bora kwa mashirika na taasisi yatakayohamia Dodoma

August 12, 2016

indexNa Georgia Misama – MAELEZO
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imejipanga kutoa huduma bora kwa mashirika na  taasisi zinazotarajia kuhamia Mjini Dodoma.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano TTCL  Bw. Nicodemus Thom Mushi leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa miaka mitatu wa mageuzi ya kibiashara wa Kampuni hiyo.
Mushi ameeleza kuwa, katika mpango huo TTCL imejipanga vyema kufanikisha azma ya Serikali ya kuhamia mjini Dodoma kwa kutoa huduma bora kwani tayari kampuni hiyo ina rasilimali watu, vifaa na wataalamu wa kutosha katika kutoa huduma za Mawasiliano.
“Nitumie fursa hii kuwaomba taasisi zote za Umma zinazohamia Dodoma na Taasisi zote kwa ujumla kutumia huduma za TTCL ambazo zote zimethibitika kuwa ni huduma bora na za uhakika na zenye gharama nafuu,” amefafanua Mushi.
Aidha, kampuni hiyo imeboresha njia ya kusikiliza wateja ambapo hivi sasa malalamiko ya wateja hushughulikiwa ndani ya masaa matatu toka mteja anapotoa taarifa katika kituo cha huduma kwa mteja.
Akiongelea juu ya maboresho, Mushi amesema kuwa, kampuni hiyo imeleta huduma mpya ya 4G LET ambayo inapelekea intaneti yenye kasi zaidi, vile vile imeboresha miundo mbinu ya mitandao ya simu na data na kuondoa mitambo chakavu.
Sambamba na hayo Mushi amewahakikishia wateja kuwa TTCL ni kampuni pekee ambayo ni suluhisho la huduma bora na ya uhakika wakati wote na mahali popote iwe ni nyumbani, sehemu ya kazi na hata kwenye vyombo vya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
WACOMORO KUWAAMUA SERENGETI BOYS, AFRIKA KUSINI

WACOMORO KUWAAMUA SERENGETI BOYS, AFRIKA KUSINI

August 12, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limemteua Noiret Jim Bacari wa Comoro kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa marudiano utakaozikutanisha timu za taifa za vijana za Serengeti Boys ya Tanzania na Amajimbos ya Afrika Kusini, utakaofanyika Agosti 21, 2016 Kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko Mbagala - nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF iliyofika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapema wiki hii, waamuzi wasaidizi pia wanatoka Comoro. Waamuzi hao ambao ni washika vibendera ni Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir Abdi Hassan.

Jumamosi iliyopita, ikicheza mbele ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kadhalika Naibu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini – Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti kwa kila upande. Afrika Kusini ndio walioanza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Luke Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.
Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa, William Koto kutoka Lesotho.
Itakumbukwa kwamba Afrika Kusini ilianza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
Kubanwa katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika Kusini waliokjuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
Shukrani za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi akishirikiaana nDickson Job.
Shime maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo . Si mabaya kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”
Kwa upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi. Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”

PROFESA BAREGU AONGOZA KONGAMANO LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

August 12, 2016
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mesigwa Baregu (kulia), akizungumza katika kongamano la Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha), ikiwa ni maadhimisho ya siku ya vijana duniani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila.
 Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila akichangia mambo mbalimbali.
 Meza kuu katika kongamano hilo.
 Mkutano ukiendelea.
 Mada zikiendelea kutolewa.
 Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali.
Usikivu ukiwa umetawala katika ukumbi huo.