TUGHE Muhimbili Wapata Viongozi Wapya, Yaongeza Nafasi ya Vijana na Walemavu
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata viongozi wapya wa Chama cha
wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi la
Muhimbili katika uchaguzi uliofanyika leo majira ya alasiri katika
ukumbi wa CPL hospitalini hapo.
Nafasi
zilizogombaniwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Tawi, Katibu wa Tawi,
wajumbe wa Halmashauri ya Tawi, nafasi ya Mwenyekiti Kamati ya wanawake,
Katibu kamati ya wanawake, Mjumbe kamati ya wanawake, Muweka Hazina
kamati ya wanawake, nafasi ya walemavu pamoja na nafasi ya vijana.
Katika
uchaguzi huo Bwana Mziwanda Salum Chimwege ametetea nafasi yake ya
Uenyekiti wa tawi na kuibuka kidedea kwa kupata kura 248, huku nafasi ya
Katibu ikichukuliwa na Bwana Faustine Fidelis Kaitaba ambaye amepata
kura 215.
Walioshinda
nafasi ya halmashauri ya tawi ni Idi Shaweja, Edina
Maneno, Seif Athuman, Rama Sultan, Yusuph Mkando, Adam Alfan,
Josephine Lwambuka, Shaban Zubery, Isaya Mbinga, Charles Kayombo, Aly
Mkali, Musa Mbuhita,Bure Nasoro, Joyce Chirwa, Mecktidis Chonga, Aikael
Kisanga, Hidal Mtoakani pamoja na Dk. Peter Kibacha.
Nafasi
ya Mwenyekiti kamati ya wanawake imechukuliwa na Zainab Mwagala kwa
kupata kura 71 huku Mwajuma Kisengo ameibuka mshindi kwa kupata nafasi
ya Ukatibu kwa kupata kura 75
Muweka
hazina kamati ya wanawake ni Halima Mayumana wakati nafasi ya vijana
imechukuliwa na Husein Jalala Mkangazi ambapo Salama Kasembe ameshinda
nafasi ya walemavu.
Awali akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Tawi la TUGHE –Muhimbili , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- Profesa Lawrence Museru ameupongeza uongozi uliopita wa TUGHE katika tawi hilo kwa kushirikiana vema na Menejimenti pasipo migogoro.
Pamoja
na mambo mengine Profesa Museru amewaeleza wajumbe wa mkutano huo
kwamba kuanzia Julai mwaka huu MNH itaanza kutoa mkono wa heri kwa
wastaafu wake sanjari na kutoa posho kwa watumishi wote wa hospitali
hiyo.
“Posho
hizi zinatolewa si kwamba hospitali ina pesa nyingi lakini tunambua
mchango wa , kwani kila mmoja ametimiza wajibu wake hatua
iliyochangia kuongeza mapato ya hospitali , hivyo nawasihi sana
muendelee kufanya kazi kwa bidii ili suala hili liwe endelevu.”amesema
Profesa Museru.
Pia
ametumia fursa hiyo kuwasisitiza kwamba MNH itaendelea kuchua hatua
kwa wafanyakazi wasiio waaminifu katika utoaji wa huduma .
Viongozi hao wa TUGHE tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili wataongoza kwa muda wa miaka mitano.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali na Afya (TUGHE) wa tawi la hospitali hiyo kabla ya kufanyika
kwa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho leo kwenye ukumbi wa CPL,
Muhimbili.
Katibu wa Tughe Mkoa wa Ilala Jijijini Dar es Salaam, Gaudence Kadiango akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa TUGHE leo.
Wajumbe wa TUGHE wakiimba nyimbo za mshikamano leo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Makwaia Makani akiungana na wajumbe wa TUGHE wakati wakiimba nyimbo za mshikamano.
Mmoja wa wajumbe wa TUGHE, Helmut Ngalawa akipiga kura leo kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.
Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya wajumbe kupiga kura leo kwenye ukumbi wa CPL-Muhimbili.
Wajumbe wakishangilia baada ya viongozi waliowapigia kura kushinda uchaguzi huo leo.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa TUGHE katika Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege (kulia)
na katibu wake, Faustine Kaitaba wakipongezana leo baada ya kuchaguliwa
tena katika nafasi hizo kuongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano.
Mmoja wa wajumbe akimpongeza Mziwanda Chimwege kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa TUGHE katika tawi la Muhimbili.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru, (wa pili
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa tawi la TUGHE
Muhimbili akiwamo mwenyekiti, katibu na wajumbe wa halmashauri ya chama
hicho. Picha na JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mwarobaini wa kukatika kwa umeme Arusha wapatikana, Wateja zaidi ya 89,000 waunganishwa.
Sehemu ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro kama kinavyoonekana pichani.
Meneja
Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Manirabona (wa pili kutoka kulia)
akielezea mafanikio ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV
kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Meneja
wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mkoa wa Arusha Mhandisi Gaspa
Msigwa ( wa pili kutoka kulia) akielezea hali ya upatikanaji wa umeme
mkoani Arusha kutokana na kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA
132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Meneja
Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Manirabona ( katikati) akielezea
namna ya uwekaji wa nyaya za umeme chini ya sakafu kwa lengo la
kuimarisha usalama katika kituo cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani
Kilimanjaro.
Meneja
Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka Shirika la Umeme
Nchini (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Manirabona akielezea jinsi kifaa cha
kuongozea mitambo ya umeme kinavyofanya kazi mbele ya waandishi wa
habari (hawapo pichani).
Sehemu
ya mitambo ya kampuni inayojishughulisha na uzalishaji wa kokoto ya
Ravji Aggregate Limited iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ambayo
ni moja ya wanufaika wa umeme kutoka katika kituo cha KIA 132/33kV.
John
Augustino mkazi wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha akielezea mchango
wa kituo cha KIA 132/33kV katika ukuaji wa uchumi wa wakazi wa mkoa
huo.
Mwarobaini wa kukatika kwa umeme Arusha wapatikana.
Ni baada ya kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA
Wateja zaidi ya 89,000 waunganishwa; TANESCO kukusanya bilioni 9 kwa mwezi
Juni 06, 2016.
Na Greyson Mwase, Arusha
Imeelezwa
kuwa kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA kilichopo karibu
na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kilimanjaro International
Airport) kumepelekea tatizo la kukatika kwa umeme kuisha katika mkoa wa
Arusha na baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro na
kuongeza kipato kwa wakazi wa mkoa huo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mkoa wa
Arusha Mhandisi Gaspa Msigwa, kwenye ziara ya waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini katika miradi ya TEDAP na
mradi wa usafirishaji umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga katika msongo
wa kilovolti 400 (BITP) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).
Lengo
la ziara hiyo lilikuwa ni kuona hatua za utekelezaji, mafanikio na
changamoto za miradi hiyo pamoja na kupata maoni ya wanufaika wa miradi
hiyo.
Akielezea
mradi huo Mhandisi Msigwa alisema ujenzi wa kituo hicho uliogharimu
Dola za Marekani Milioni 7, ulianza mwaka 2011 na kukamilika mapema
Desemba mwaka 2013.
Alisema
kabla ya ujenzi wa kituo hicho, umeme ulikuwa unasafirishwa kutoka
katika kituo cha Kiyungi kilichopo mkoani Kilimanjaro hadi jijini Arusha
umeme ambao ulikuwa hautoshelezi katika matumizi ya majumbani na
katika viwanda vidogo.
Aliongeza kuwa pia kulikuwepo na tatizo la kupotea kwa umeme mwingi kutokana na kusafirishwa katika umbali mrefu.
Alisema
kuwa tangu kukamilika kwa kituo hicho wateja zaidi ya 89,000
waliunganishiwa umeme ambapo mpaka sasa wanapata umeme ambao ni wa
uhakika.
Alisema
kutokana na ongezeko la wateja pamoja na kupatikana kwa umeme wa
uhakika katika mkoa huo, TANESCO imeweza kukusanya shilingi bilioni
tisa kwa mwezi tofauti na kipindi cha awali ambapo makusanyo yalikuwa
yanafikia wastani wa shilingi bilioni nane kwa mwezi.
Aliendelea
kusema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumehamasisha kuongezeka kwa
ujenzi wa nyumba pamoja na kuanzishwa kwa viwanda vidogo katika mkoa
wa Arusha.
Wakati
huo huo Julius Urassa ambaye ni msimamizi wa kampuni inayojihusisha na
uzalishaji wa kokoto ya Ravji Aggregate Limited iliyopo wilayani Arumeru
mkoani Arusha alisema kuwa kabla ya kukamilika kwa kituo hicho hali
ya umeme katika mkoa wa Arusha haikuwa nzuri.
“
Kabla ya kuwepo kwa kituo cha KIA, umeme ulikuwa unakatika mara kwa
mara na kuathiri uzalishaji katika kiwanda chetu; lakini sasa tunapata
umeme wa uhakika,” alisema
Aliogeza
kuwa kutokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika, kampuni yake ina
uwezo wa kuzalisha tani 100 za kokoto kwa siku tofauti na zamani ambapo
walikuwa na uwezo wa kuzalisha kati ya tani 40 hadi 60 za kokoto kwa
siku.
Naye
Meneja wa Kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa matofali kwa njia
ya umeme ya Melck Hardware iliyopo Maji ya Chai nje kidogo ya jiji
la Arusha, Hansi Said alisema kuwa hali ya umeme katika mkoa wa Arusha
imetengemaa hali iliyopelekea uzalishaji kuongezeka katika kampuni
yake.
Alisema
kutokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika, kampuni yake ambayo
hutengeneza matofali kulingana na oda kutoka kwa wateja, imeongeza
uzalishaji kutoka wastani wa tofali 700 hadi 2,000 kwa siku.
Naye
John Augustino mkazi wa Arumeru mkoani Arusha aliongeza kuwa tangu
kuanza kupatikana kwa umeme wa uhakika, hali ya maisha katika familia
yake imeboreka kutokana na kuuza bidhaa zaidi ya maziwa tofauti na
mwanzo katika duka lake.
“Bidhaa
za vinywaji hususan maziwa yalikuwa yanaharibika kutokana na
kukatika kwa umeme, lakini kwa sasa tunapata umeme wa uhakika, hali
inayochangia kuuza bidhaa bora zaidi,”alisisitiza.
USAILI WA KIKOSI KAZI CHA 102.5 LAKE FM MWANZA WAENDELEA KUFANYIKA.
Hiki ni Kikosi Kazi cha baadhi ya Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm, Raha ya Rock City #Radio ya Wananzengo. Radio hiyo ambayo ni inakiki jijini Mwanza hivi sasa licha ya kwamba bado iko kwenye majaribio, inaendelea na usaili wake ili itakapoanza kurusha vipindi vyake rasmi, ianze kwa mwendo kasi zaidi.
Na BMG
MKUU WA MKOA WA MBEYA AKITAKA CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA KUWAANDAA ASKARI WATAKAOSIMAMIA MAGEUZI NDANI YA JESHI LA MAGEREZA
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya amekitaka Chuo cha magereza Kiwira kilichopo wilaya ya
Rungwe KUWAANDAA askari watakasimamia MAGEUZI makubwa ndani ya jeshi la
magereza na magereza yaliopo nchini
Hayo
ameyasema leo katika ziara yake ya kikazi kutembelea Chuo hicho na
kuongea na maofisa, askari na wanafunzi wa Chuo wapatao 1,390 .
Katika
nasaha zake amesema mbali ya majukumu waliobaki ya kuwalinda wafungwa
magerezani ni vema wakaelewa kuwa jeshi hilo sasa lijielekeze ku
jiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha na kusimamia miradi mbalimbali
itakayosaidia magereza kujitosheleza kwa chakula
Aidha
Uwepo wa wafungwa magerezani utengenezaji kuwarekebisha tabia lakini
pia kuwapatia ujuzi wafungwa kupitia kazi katika viwanda v na karakana
za magereza
CHEKI TANZANIA YAZINDUA HUDUMA YA KUTOA MAGARI BANDARINI KWA WANUNUZI WA MAGARI NCHINI
Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo akionyesha jinsi watumiaji wa mtandao wa Cheki.co.tz jinsi wanavyoweza kutumia huduma ya clearing and forwarding.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
mkutano huo wakiendelea na kazi yao ya kuchukua taarifa kwa ajili ya kuupasha
umma kuhusu huduma ya clearing and forwading ambayo inatolewa na cheki.co.tz
Mtandao
wa kuuza magari mtandaoni wa Cheki.co.tz umezindua huduma mpya ya uunganishwaji
wa uigizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji magari bandarini
(clearing and forwarding), huduma ambayo itawarahisishia wananchi ambao
wanaagiza magari nje ya nchi kuwa na uhakika wa usalama wa magari wanayoagiza
mpaka yanakapowafikia.
Akielezea
huduma hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus, alisema
kampuni yake imeanzisha huduma hiyo ili kuwarahisishia Watanzania wanaoanzisha
magari nje ya nchi kutokana na kubaini kuwa wamekuwa wakisumbuka kukamilisha
uagizwaji wa magari na kuyatoa bandarini.
“Tayari
tumewapa wateja wetu chaguo kubwa la magari kutoka kwa wauzaji wa kuaminika
kutoka nje ya huduma hii ya utoaji wa mizigo itarahisisha utoaji wa magari
kutoka bandarini na hivyo wateja kupunguza gharama na muda wa kusubiri,” alisema
Bencus.
Nae
Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo, alisema kuwa kampuni hiyo
haihusiki na uuzaji wa magari ila inachofanya ni kumuunganisha mnunuzi wa gari
na muuzaji ili waweze kufanya biashara kwa haraka na urahisi zaidi.
Ujio
wa huduma hiyo imekuwa mwendelezo wa uboreshwaji wa huduma za ununuzi wa magari
kwa kupitia mtandaoni ambazo zinafanywa na mtandao wa Cheki.co.tz ambao
unafanya kazi na wauzaji wa magari wa kimataifa wa nje ya nchi na wauzaji
wa magari wa hapa nchini.
WAHITIMU WA USCF - TAASISI YA UHASIBU TANZANIA WATAKIWA KUWA WAADILIFU MAKAZINI
Mchungaji wa KKKT akitoa neno wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.
Wahitimu wakifuatilia neno kutoka kwa mchungaji wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.
Katika neno alililolitoa mchungaji huyu aliwaasa wahitimu kuwa na hofu ya Mungu pindi wanapopewa majukumu ya kazi.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (wa tatu toka kushoto) akiserebuka na mchungaji wa KKKT pamoja na wageni waalikwa.
Wahitimu wakijimwaga.
Mchungani akiwaombea wanafunzi wakafanye vyema katika mitihani yao wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita. -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYAPIGWA MSASA NA TGNP
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akifungua semina kwa Wanaharakati pamoja na viongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa waliofika katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Geofrey Adroph)
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akitoa elimu kwa wanaharakati kuhusu utendakazi wao wa kila siku wakati wa semini iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Kibuko, Bw. Valentino Lukoo akitoa ufafanuiz kuhusu maendelea yaliyofikia katika kata yao baada ya kuonekana kwa changamoto nyingi katika kata hiyo
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Igale, Bi Lidya Sankemwa Mwakalinga akizungumzia mipango ya kata yao kuhusu utoaji wa taarifa husika katika kata yao.
Mwanaharakati kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Nsalal Bi. Felister Kais akizungumzia changamoto wanazozipata katika utoaji wa taarifa.
Mwanaharakati kutoka Mabibo, Bw. Furaha Mbakile akichangia mada
Afisa program Utafiti na Uchambuzi kutoka TGNP, Bw. Alphonce Stima akiongea jambo wakati wa utoaji wa Semina kwa Wanaharakati pamoja na viongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa waliofika katika semina hiyo
Wanaharakati pamoja na iongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa wakitazama hotuba ya Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango anasoma na kuwasilisha Hali ya Uchumi
kwa mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo Bungeni
Afisa program Utafiti na Uchambuzi kutoka TGNP, Bw. Alphonce Stima akiongea jambo mara baada ya kumalizika kwa Hotuba ya Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango anasoma ama kuwasilisha Hali ya Uchumi
kwa mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo Bungeni Dodoma
Afisa Programu mwandamizi wa Ushawishi na utetezi kutoka TGNP Mtandao, Bi. Anna Sangai akitoa elimu wanaharakati pamoja na viongozi wa Taarifa na Maarifa katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam leo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akichangia mada
Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akiwaeleza wanaharakati pamoja na viongozi wa Taarifa na Maarifa jinsi ya ufanyakazi wa TGNP Mtandao
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi(kulia) akifuatilia Bunge kupitia njia ya Television katika ofisi ya TGNP Mtandao
Baadhi ya Wafanyakazi wa TGNP Mtandao, Wanaharakati, viongozi wa Taarifa na Maarifa pamoja na wananchi wakifuatilia Bunge kwa njia ya Televisioni ndani ya Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi(kulia) akifuatilia Bunge kupitia njia ya Television katika ofisi ya TGNP Mtandao
Baadhi ya Wafanyakazi wa TGNP Mtandao, Wanaharakati, viongozi wa Taarifa na Maarifa pamoja na wananchi wakifuatilia Bunge kwa njia ya Televisioni ndani ya Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)