TAARIFA KWA WATEJA WA BENKI YA NBC KUHUSU MIAMALA KWENYE AKAUNTI ZAO

April 21, 2017
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability

TBL WAZINDUA KAMPENI YA CASTLE LITE UNLOCKS

April 21, 2017


Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya TBL Afrika Mashariki, Thomas Kamphuis akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bia ya Castle Lite 'Castle Lite Unlocks' jijini Dar es Salaam juzi









WATANZANIA KUNUFAIKA NA UMEME WA JUA NA MAJIKO BUNIFU YA SUN KING

April 21, 2017
Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
#BMGHabari
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
George Binagi-GB Pazzo
Wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya Sun King.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.

“Kila Kijiji nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.

Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana, amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira zaidi kwa vijana. Tazama hapa uzinduzi zaidi

JUBILEE NA ZURICH INSURANCE ZAANZISHA BIMA YA AFYA YA GHARAMA NAFUU

April 21, 2017

 Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga (katikati), akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers,  Sudi Simba na Rogation Selengia ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Idara ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance. Kampuni hizo mbili zitashirikiana kuuendesha mpango huo utakaofadisha familia ya watu wanne kwa kulipa sh. 174,000 kwa mwaka. PICHA ZOTE NA RICHARD; MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga  akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga akizungumza na vyombo vya habari kuhusu manufaa ya bima hiyo wakati  akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Uendeshaji wa Idara ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance, Rogation Selengia  akimkabidhi zawadi ya fulana Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers,  Sudi Simba (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fulana  Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu 'Afya Wote'katika hafla iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Kampuni hiyo na Jubilee Insurance  zitashirikiana kuuendesha mpango huo utakaofadisha familia ya watu wanne kwa kulipa sh. 174,000 kwa mwaka.
 Nembo ya mpango huo ambao wanachama wake watanufaika kwa kuhudumia katika hospitali zaidi ya 200 nchini.
 Mkuu wa Idara ya Tiba wa Kampuni ya Jubilee Insurance, Keneth Agunda, akielezea kuwa watakaonufaika katika mpango huo ni baba, mama na watoto wawili na endapo familia itataka kuongeza idadi basi kila atakayeongezwa atatozwa sh. 100,000 kwa mwaka.
 Kaimu Mkurugenzi wa  Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga akifafanua kuwa kwa hivi sasa ni asilimia 25 ya wananchi ndiyo waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hivyo serikali inawakaribisha watu binafsi kuanzisha bima za afya kama kampuni hizo mbili zilivyofanya.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers,  Sudi Simba akiwaelezea wananchi faida mbalimbali watakazopata kupitia bima hiyo ya gharama nafuu.Alitaja huduma zitakazokuwa zinatolewa kuwa ni; magonjwa sugu, huduma za kulazwa, magonjwa ya nje,  kulazwa kwa majeraha ya macho-ajali, meno, uzazi wa kujifungua kawaida na upasuaji na ubani wa mazishi kwa kila mwanachama sh. 500,000.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi huo
 Baadhi ya maofisa wa kampuni hizo
 Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo wa kampeni ya kuhamasisha kujiunga na bima hiyo
Akina mama wakitafakari kuhusu mpango huo wa bima

TBL YAZINDUA KAMPENI YA ‘CASTLE LITE UNLOCKS’ JIJINI DAR ES SALAAM

April 21, 2017
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ijulikanayo, ‘Castle Lite Unlocks’. Kushoto ni Meneja Chapa Msaidizi wa Bia Laini Tanzania, Isaria Kilewo na katikati ni Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.