WCF YAWAELIMISHA MAAFISA WAAJIRI KUHUSU MISINGI YA KULINDA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI

March 22, 2018

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.

“Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.

Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.
Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
“Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
“Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
“Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.
 
 Mshiriki akisoma machapisho yenye taarifa za WCF
 Dkt. Abdulsalaam (katikati), akifafanua baadhi ya hoja. Wengine, ni Bi. Naanjela Msangi, (Kushoto), na Bw. Faustine George
 Bi. Naanjela Msangi.
 Bw. George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
  Bi. Naanjela Msangi(kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge
 Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo
 Baadhi ya washiriki wakipitia vipeperushi vyenye maelezo kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
 Baadhi ya washiriki wa semina.
 Washiriki wakijiandikisha
 Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa WCF.
 Robert Duguza, Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.


Bi. Tumaini J.Kyando, Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa Kazi kutoka Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio walioandaa semina hiyo, akinakili baadhi ya hoja zilizojitokeza.
Baadhi ya washiriki

Tigo na Samsung wameungana kwaajili ya kutoa Simu mpya ya Samsung S9 na Sumsung S9+ kwa mara ya kwanza kwa wateja wa Tigo

March 22, 2018

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael ( katikati) akizungumza na waadishi wa habari katika hafla ya ushirikiano kati ya  Tigo Tanzania na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.  Wengine kulia Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa Tigo, Davidi Umoh. Hafla ilifanyika Jijini Dar es salaam jana.

       Mkuu wa Idara ya Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, Davidi Umoh              katikati),  Meneja wa Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael wakizindua simu mpya za kisasa aina ya Samsung S9 na Samsung S9+ ambazo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kwa mara ya kwanza.


Simu ya Smartphone yenye GB 3 za internet bure kila mwezi kwa muda wa miezi sita kutoka Tigo.  

Tarehe 22 Machi 2018, Dar es Salaam.  

Wapenzi wa smatphone wanayo sababu nyingine ya kutabasamu baada ya kampuni inayoongoza ya mtindo wa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania kuungana na kampuni ya Samsung Electronics Tanzania kwaajili ya kuwapatia wateja wake nafasi ya kwanza kumiliki simu mpya ya kisasa ya Sumsang S9 na Samsung S9+ zilizojazwa bando la bure la internet ya 3 GB kila mwezi kwa miezi sita kutoka Tigo.  

'Tigo ni kampuni pekee ya simu za mkononi na ya kwanza kuwa na  simu mpya za kisasa za Samsung S9/S9+ nchini. Hakuna mwendeshaji mwingine yeyote wa mtandao wa simu au duka ambalo tayari limeshapokea simu hizi za kisasa za smartphone,' Mkuu wa idara ya Bidhaa na Hudumawa Tigo (Head of Products and Services), Davidi Umoh aliabainisha.  

Umoh aliongeza kuwa 'Tigo imeshika usukani wa mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidigitali . Tuna lenga katika kuendelea kuongeza upatikanaji wa simu za smartphone nchini wakati huo huo tukiwa tunahakikisha kuwa wateja wetu wote wanafurahia huduma bora za kidigitali kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi wa 4G ambao ndio uliosambaa zaidi hapa nchini.


Akielezea kuhusu Ushirikiano uliopo, Meneja wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Suleiman Mohammed  amesema"Tunajisikia fahari sana kushirikiana na Tigo kwaajili ya kuleta fursa za kusisimua na ofa kwa wateja wa Tanzania. Hii ni hatua ya msingi sana katika ukuzaji wa sekta ya simu za mkononi ambayo inaruhusu wateja kupata simu za kisasa katika wakati huo huo ambapo simu hizo zinazinduliwa duniani kote".  

Kuna njia tatu za kununua simu ya smartphone ya Samsung S9/S9+ Kwanza mteja anaweza kutembelea duka lolote la Tigo nchi nzima nakulipia na kujipatia simu mpya ya kisasa aina ya Samsung S9 na S9+. Njia ya pili ya kununua simu hizo nikutembelea Tigo Store katika ukurasa wa mtandao wa manunuzi wa jumia www.jumia.co.tz/tigo-shop. Mwisho wateja wanaweza kupiga menyu mpya ya Tigo *147*00# na kisha kuchagua duka la simu ambako utaweza kuchagua namna ya kulipia ambayo inaruhusu kulipia kidogo kidogo na kuchukua simu yake baadae.  

Simu za smartphone za kisasa za Samsung S9/S9+ zinapatikana katika rangi nyeusi, kijivu na zambarau na zitauzwa reja reja kwa bei ya TZS  2,049,000 kwa Samsung S9 na TZS 2,315,000 kwa Samsung S9+.

Waziri Makamba awasilisha taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Bishara na Mazingira

March 22, 2018
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Innocent Bashungwa akisisitiza jambo kwa watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani) mara baada ya kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais na kujadili utelekezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka fedha 2017/2018 na mapendekezo ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19. Taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kulia ni Katibu wa Kamati Bw. Wilfred Magova.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)Mhe. January Makamba, Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola na  Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia majadiliano ya wajumbe wa kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, hii leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola, Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Phillip wakifuatilia majadiliano ya wajumbe wa kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, hii leo Mjini Dodoma.

Pichani wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Hawa Subira Mwaifunga na Mhe. Omary Ahmed Badwel wakifuatilia majadiliano katika Kamati yao hii leo Mjini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. Kanali (Mst) Masoud Ali Khamis na Mhe. Zainab Mdolwa Amiri wakifuatilia majadiliano kikaoni hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
#Kwa kiasi kikubwa kiwango cha uelewa kwa wananchi na jamii kwa ujumla juu ya masuala ya mazingira kimeongezeka na Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa Umma na suala hili litapewa kipaumbele
#Ofisi ya Makamu wa Rais inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha uwekezaji endelevu na rafiki kwa mazingira.
#Matumizi ya nishati mmbada wa mkaa yanaendea kuhimizwa ikiwa ni pamoja na matumizi ya gesi na matumizi ya majiko banifu na matumizi ya tungamotaka (Bio-Mass).
#Zaidi ya Maafisa Mazingira mia tano (500) wameteuliwa kwa ajili ya kuwa ’wakaguzi wa Mazingira’ambao watafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kifungu namba 182 (2)
#Serikali inaendelea kujenga uwezo wa Taasisi ikiwemo NEMC ili iweze kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa Sheria.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola
#Serikali imeanzisha Mfuko wa Mazingira ambao pamoja na mambo mengine fedha yake itasaidia kampeni kubwa ya upandaji miti hapa nchini
#Taasisi/Vikundi vinavyojihusisha na masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini vinaweza kupewa tuzo ili kutoa chachu kwa vikundi vingine pia
#Kila Wilaya na Halmashauri zinatakiwa kuanzisha Sheria ndogo ndogo kwa ajili ya Hifadhi na usimamizi wa Mazingira katika maeneo yao.
#Serikali imeanza mchakato wa kuandaa orodha ya wachimbaji wadogo wadogo wote hapa nchini ili uandaliwe utaratibu maalumu wa kuwaratibu kwa ujumla wao.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Innocent Bashungwa
#Kampeni za kitaifa za Mazingira zinaonekana na vema juhudi hizi ziendelee kwa kushirikisha wadau wote
#Serikali iangalie upya matumizi ya Mkaa wa kuja na nishati mbadala ili kunusuru ukataji wa miti unaoendelea kwa kasi, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na SIDO katika kutengeneza majiko banifu
#Usimamizi wa Sheria ya Mazingira uzingatiwe ikiwa ni pamoja na kuitaka Migodi mikubwa kufuata taka la kisheria la kurudhisha hali ya mazingira ya awali mara baada ya kukamilika kwa uchimbaji.
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

March 22, 2018
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.
3 4 6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na ujumbe kutoka nchini Israel uliokuwa ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman wa kwanza (kushoto kwake) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wa nne kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florence Turuka wa kwanza kushoto aliyesimama mstari wa nyuma pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wa sita kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florence Turuka wa pili kutoka kushoto pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya Jeshi mara baada ya kumalizika kwa kikao chao na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU