NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTO BITEKO AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF

November 03, 2023

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF, ni miongoni mwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. CPA. Kashimba alipata fursa ya kumpongeza Dkt. Biteko kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 30, 2023 na kula kiapo Septemba 1, 2023. Pia CPA. Kashimba alitumia fursa hiyo kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kumueleza utekelzaji wa majukumu ya Mfuko kama yalivyoainishwa kwenye Sheria namba 2 ya mwaka 2018, iliyoanzisha PSSSF, ambayo ni pamoja na Kuandiskisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kuwekeza na kulipa Mafao. Captions: SALAMU Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, ofisini kwa Naibu Waziri Mkuu kwenye ofisi za Bunge jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. TAARIFA Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko (katikati), akipokea mfuko wenye taarifa mbalimbali kuhusu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, ofisini kwa Naibu Waziri Mkuu kwenye ofisi za Bunge jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe. MAZUNGUMZO Dkt. Bioteko (kulia), akiwa kwenye mazungumzo na ujumbe wa PSSSF ulioongozwa na CPA. Kashimba. Wengine pichani ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe (wapili kushoto) na Afisa Mkuu wa Uhusiano, PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. CODES FOR BLOGS

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, Bungeni jijini Dodoma.

PSSSF, ni miongoni mwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

CPA. Kashimba alipata fursa ya kumpongeza Dkt. Biteko kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo Agosti 30, 2023 na kula kiapo Septemba 1, 2023.

Pia CPA. Kashimba alitumia fursa hiyo kujitambulisha ikiwa ni pamoja na kumueleza utekelzaji wa majukumu ya Mfuko kama yalivyoainishwa kwenye Sheria namba 2 ya mwaka 2018 iliyoanzisha PSSSF, ambayo ni pamoja na Kuandiskisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kuwekeza na kulipa Mafao.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, ofisini kwa Naibu Waziri Mkuu kwenye ofisi za Bunge jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Bideko (katikati), akipokea mfuko wenye taarifa mbalimbali kuhusu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, ofisini kwa Naibu Waziri Mkuu kwenye ofisi za Bunge jijini Dodoma, Novemba 3, 2023. PSSSF iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe.

Dkt. Bioteko (kulia), akiwa kwenye mazungumzo na ujumbe wa PSSSF ulioongozwa na CPA. Kashimba. Wengine pichani ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe (wapili kushoto) na Afisa Mkuu wa Uhusiano, PSSSF, Bw. Abdul Njaidi.


WCF IMETUFUTA MACHOZI-WANUFAIKA

November 03, 2023

 

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

WANUFAIKA wa fidia inayotolewa na WCF, wametoa ya ‘moyoni’ mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kwa kile walichokiita Mfuko huo umewafuta machozi.

Wakitoa ushuhuda Novemba 2, 2023, katika kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Wahariri wa vyombo vya habari, kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya Mfuko huo, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.

Beauty Jackson Letema, ni mnufaika wa WCF, yeye ni mama mjane ambaye alifiwa na mumewe katika ajali wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, lakini pia naishukuru WCF, mume wangu alipofariki aliniacha na watoto watatu na ujauzito, WCF walianza kunihudumia mimi na watoto wangu hao watatu na kisha huyu mwingine, Mimi sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, WCF wanatuhudumia mimi na watoto, tunavaa, tunakula na pia watoto wangu wanasoma bila shaka yoyote, kwakweli wamenifuta machozi.” Alisema

Kutokana na manufaa anayoyapata kutoka WCF, Mnufaika huyo aliwahimiza waajiri kujisajili na mfuko ili wafanyakazi wanapopatwa na madhila wakiwa kazini, basi Mfuko utakuwa mfariji wao.

“Wito wangu kwa waajiri, WCF ni mfuko wenye faida sana, kama mimi mume wangu alivyofariki na mwajiri wake angekuwa hajajisajili WCF, maisha yangekuaje?  Natoa wito kwa waajiri wajiunge na WCF.” Alisisitiza Beauty.

Mnufaika mwingine ni Halima Sheikh, wakati akitekelza jukumu lake kama dereva wa bus la abiria, Super Feo, alikatika mkono baada ya bus alilokuwa akiliendesha kupinduka.

“Baada ya kupoteza mkono na kupata ulemavu wa kudumu, WCF imekuwa ikinilipa fidia kila mwezi, malipo yananisaidia mimi na familia yangu, nimeambiwa nitalipwa maisha yangu yote, hakika nafarijika sana.” Alisema.

“Kwa kifupi naishukuru sana Serikali kwa kuanzisha WCF, Mfuko una manufaa makubwa sana, ninajitegeema asilimia 100, namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa WCF na timu yake, Mfuko umenipatia matibabu vizuri sana hadi kupona,  maisha yangu yanaendelea.” Alisema Mnufaika mwingine, Bw. Hassan Sima Jambau, aliyekuwa mtumishi wa Televisheni ya Taifa, TBC.

Mnufaika wa fidia itolewayo na WCF, Bi. Halima Sheikh, akitoa ushuhuda mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, Novemba 2, 203.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma akifurahia jambo na mmoja wa watoto ambao wanapokea fidia kama wategemezi baada ya kumpoteza baba yao, Jackson Letema.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma akiwasalimia wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF mara baada ya kikao hicho.
Beauty Jackson Letema, mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa habari
Bi. Halima Sheikh
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto), akiteta bjambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Thobia Makoba.
Mwandishi wa habari mwandamizi na Mhariri, Bw. Joe Nakajumo akiwa mwenye hisia wakati akisikilzia ushuhuda wa wanufaika wa fuidia.
Baadhi ya washiriki
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge.

Mkurugenzi Mkuu (WCF), Dkt. John Mduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF.

WIZI WA MISUMARI HOSPITALI YA WILAYA YA PANGANI WAMCHEFUA MWENYEKITI WA CCM TANGA ATOA AGIZO KWA JESHI LA POLISI

November 03, 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhamani  kushoto akikagua nyaraka za manunuzi wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika wilaya hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman kushoto akisisitiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Panganai kulia wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani kulia akionyeshwa maeneo mbalimbali ya Hospitali ya wilaya ya Pangani na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo wakati apofanya ziara ya kushtukiza 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhamani  kushoto akisisitiza jambo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani kushoto akimuonyesha maeneo yanayoendelea na ukarabati katika hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza ya Mwenyekiti huyo

Na Oscar Assenga,PANGANI.

 

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rajab Abdurhamani amekerwa na wizi wa misumari katika Hospitali ya wilaya aya Pangani Mkoani Tanga huku akiliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na watakaowabaini walihusika kwenye tukio hilo hatua kali za kisheria zichukuliwe.

 

Hayo yalibainika wakati wa ziara yake wilayani hapa ya kushtukiza iliyokuwa na lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake hivi karibuni ambapo alisema pamoja na hayo wachukuliwe hatua za kinidhamu na sionewe mtu huku akisisitiza aliyetia mkono wake kuiba vifaa hivyo ashughulikiwe.

 

Akiwa Hospitalini hapo baada ya kukagua ukarabati wa Hospitali hiyo ambao unagharimu milioni 900 ndipo alipoelezwa wizi huo na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah wakati akipopata nafasi ya kuzungumza.

 

Mwenyekiti huyo alisema lazima washughulikiwe kwa kuchukuliwa hatua kali ili iweze fundishwa kwa watu wengine wenye tabia za namna hivyo maanaa zikivumiliwa vitakwamisha juhudi za kimaendeleo ambazo zinafanywa na Serikali.

 

“Kwa maana tutawapa lawama ndugu zetu waliopewa nafasi ya kusimamia miradi ikiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya na katika hili nikutake Mkuu wa wilaya usicheke na mtu na ukiacha hilo ninazo taarifa nyegine nimeweka watu wangu nitakapozithibitisha nitachukua hatua kuna vifaa viliibwa hapa hospitali lakini jana usiku baada ya kusikia ninakuja vimerudishwa watu hawaogopi wala hawana haya hilo halikubaliki”Alisema

 

Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kusimamia mradi huo wa ujenzi wa Hospitali huku akionyesha kuridhika nao kwa kiasi kikubwa kwa sababu thamani ya fedhana kinachoonekana kinaendana.

 

“Niwaombe wananchi wenzangu lazima tumhurumie Rais Wetu Dkt Samia Suluhu kwa maana anahangaika usiku na mchana muda wowote siku zote halali kwa sababu ya kuwasaidia Watanzania kuwaondolea adha zinazowakabili pia mbunge wetu anapambana sana kujenga hoja kwamba hospitali yetu na hapa Hospitalini ameleta Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati hivyo tusiwakatishe tamaa viongozi wetu”Alisema

 

Aidha alisema kwa maana wakati miradi inapotekelezwa zinatumika fedha nyingi ambazo zimeletwa kwenye wilaya yenu katika utekelezaji wa miradi hiyo lazima wananchi wawe waaminifu ili lengo liweze kutimia lakini inapojitokeza watu wanaiba misumari inakwamisha juhudi hizo.

 

Hata hivyo aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika maeneo yao ikiwemo kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu anayejali matatizo ya wananchi anaowaongoza.

 

Mwenyekiti huyo aliwataka wananachi hao kuhakikisha mwaka 2025 hawana Rais mwengine zaidi ya Dkt Samia Suluhu mambo anayoyafanya ni makubwa ya kimaendeleo watapata muda kwenda kuyaelezea.

 

Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alimueleza Mwenyekiti huyo kwamba Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu aliwapelekea million 900 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya wilaya hiyo huku akieleza wakati anapofanya ziara na kamati ya usalama kukagua ujenzi huo ndipo walipobaini uwepo wa wizi huo.

 

Alisema baada ya kulibaini hilo alimuelekeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya hiyo (DMO) aweze kuchukua hatua kutokana na kupotea magunia mawili ya misumari lakini hawakuripoti katika Jeshi la Polisi ili uchunguzi ufanyie na hatua zichukuliwe.

 

“Lakini nilitoe maelekezo kwa DMO achukua hatua ili sheria ichukue mkono wake lakini niliwataka lega ya vifaa vyote vinavyongia na kutoka vya zamani na vipya na hali yake ipoje bahati nzuri DMO aliniandikia taarifa na nilimueleza aende kufungua kesi na kesi tayari imeshafunguliwa kituo cha Polisi na uchunguzi unaendelea na hivi vilipotea wakati wanahamisha vifaa kutoka sehemu waliokuwa wamehifadhi kwenye stoo mpya”Alisema

 

 

Mwisho.