TGGA YAZINDUA UPANDAJI MITI 600 KILA MKOA TANZANIA

April 27, 2017
 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. PICHA NA JOHN BANDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


John Banda, Dodoma

CHAMA cha Tanzania Girl Guides (TGGA) kimezindua mradi wa upandaji miti kitaifa katika Shule ya Msingi ya Mtumba Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides nchini, Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshaanza upandaji wa miti hiyo katika mikoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza

Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.

Naye Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa, Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Guides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika hilo zinafaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye rutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali   


 Wanachama wa Tanzania Girl Guides wakichimba moja ya mashimo ya kupanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba Manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti katika shule mbalimbali nchini.

 Wanafunzi wanachama wa TGGA
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya kabila la Wagogo wakati wa uzinduzi wa upandaji miti shuleni hapo
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika kitaifa shuleni hapo juzi.

 Mwenyekiti wa TGGA, Marha Qorro akimwagilia mti baada ya kuupanda

 Viongozi na wanachama wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja
 Viongozi wa TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma
 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa TGGA
Wanafunzi wanachama wa TGGA wakiwa na miche ili waendelee na zoezi la kupanda miti shuleni hapo
Sekta binafsi yajipanga kukutana na Rais kwenye Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara- TNBC

Sekta binafsi yajipanga kukutana na Rais kwenye Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara- TNBC

April 27, 2017
WADAU wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu. Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini - TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu, ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. Akiwakaribisha wadau wa Sekta Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi hawakomoani, ndio maana TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili kulifikisha taifa kwenye uchumi wa viwanda. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano wa ndani ulioambatana na chakula cha jioni kilichoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi.[/caption] Dk Mengi pia alisema serikali na sekta binafsi wana malengo yanayofanana ya kutokomeza umaskini na kutengeneza ajira kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kutekelezeka kwa urahisi iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu baina ya serikali na Sekta Binafsi. Katibu Mtendaji wa TNBC Mhandisi Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utakuwa ni fursa nzuri kwa serikali na sekta binafsi kubadilishana mawazo kuhusu wajibu wa kila upande katika kuboresha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini ili kukuza uchumi wa nchi. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akijitambulisha katika mkutano huo. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano ulioambatana na hafla ya chakula cha jioni uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiendelea na mazungumzo na wadau wa Sekta Binafsi kwenye mkutano huo ulioambatana na chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC), Mhandisi Raymond Mbilinyi akifafanua jambo katika mkutano wa ndani ambao ni sehemu ya kujiandaa kukutana na serikali chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) linalotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Mei jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1920" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakati mkutano huo ukiendelea. Mkutano ukiendelea.