Wakandarasi Wanaovunja Mikataba Wachukuliwe Hatua – Jumaa Aweso

Wakandarasi Wanaovunja Mikataba Wachukuliwe Hatua – Jumaa Aweso

November 08, 2017

8796- Naibu Awesu
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe.Juma Aweso akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa tisa wa Bunge leo Mjini Dodoma.
………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Serikali imewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia hatua wakandarasi wa maji wanaokiuka mikataba walioingia kwa kuchelewa kutekeleza miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini Mendrad Lutengano Kigola juu ya lini Serikali itamaliza kujenga mradi wa Kata ya Mtwango katika Vijiji vya Sawala, Mtwango, Rufana na Kibao. 
 “Viijiji vya Sawala, Mtwango, Rufana na Kibao katika kata ya Mtwango ni miongoni mwa vijiji 12 vilivyopendekezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kupatiwa huduma ya maji kupitia programu ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijjini,” alisema Awezo.
Aliendelea kwa kusema, utekelezaji wa mradi huo ulianza Juni 01, 2015 na ulitakiwa kukamilika Juni 01, 2016 kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.36 ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Sawala pekee ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 50.
“Hadi mwezi Novemba, 2016 mkandarasi alikuwa hajakamilisha kazi na hivyo Halmashauri kuamua kuvunja mkataba na halmashauri ilitangaza upya zabuni kwa ajili ya ukamilishaji wa kazi zilizobaki,” alifafanua Aweso.
Amesema kuwa, mkandarasi mwingine amepatikana na utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Desemba, 2017 kwa muda wa miezi 12 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.81.
Kutokana na ucheleweshaji wa mradi huo, Aweso amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwachukulia hatua wakandarasi wa maji ambao hawatekelezi miradi yao kwa muda uliopangwa ambao kwa kiasi kikubwa unawaathiri wananchi wanaohitaji huduma ya maji kutokana na mradi kutekelezwa kwa muda mrefu.

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BW. DOTO JAMES AWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU DENI LA TAIFA

November 08, 2017
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewatoa hofu watanzania kuhusu ongezeko la Deni la Taifa akisisitiza kuwa Deni hilo ni himilivu.

Bw. James amesema hayo Jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari wakati wa hafla fupi ya kutia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi bilioni 340 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya Mradi wa kuendeleza utalii kwa vivutio vilivyoko katika ukanda wa kusini mwa Tanzania ujulikao kama Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)

Alikuwa akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu na vyombo vya habari vinavyozungumzia Deni la Taifa kwa kutumia neno Deni la Taifa “linapaa”

Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye Mlipaji Mkuu wa Serikali alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu kwa kutumia viwango vya kitaifa na kimataifa kwamba ili nchi iwe katika hatari ya kukua kwa Deni lake la Taifa inabidi lifikie asilimia zaidi ya 50 lakini kwa Tanzania kiwango cha deni hilo ni asilimia 32.

“Deni letu lingekuwa linapaa, hata Benki ya Dunia wasingekubali kutukopesha kwa maana hiyo tukitaka kukopa tutafanya hivyo kwa kuwa tuko chini katika viwango vya ukopaji kwa asilimia zaidi ya 18” alisema Bw. Doto James.

Kwa hiyo nawaomba hili mlichukue muuelimishe umma wa watanzania kwamba deni la Taifa ni stahimilivu, nchi inakopesheka vizuri.

Novemba 7, 2017, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni mjini Dodoma Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maanndalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 alisema kuwa Deni la Taifa limefikia dola za Marekani milioni 26,115.2 mwezi Juni mwaka 2017.

Dkt. Mpango alieleza kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17 ikilinganishwa na dola milioni 22,320.76 katika kipindi kama hicho mwaka 2016.

UYUI WAZIPOKEA KWA MIKONO MIWILI MBEGU BORA ZILIZOFANYIWA UTAFITI KUTOKA COSTECH-OFAB

November 08, 2017
 Wanakikundi cha Upendo kilichopo Kijiji cha Magiri Kata ya Magiri katika Halmshauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakiwa pamoja na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera na Mwanahabari Coleta Makulwa wa RFA (wa pili kushoto), baada ya kukabidhiwa mbegu bora za Viazi lishe aina ya Kabode kwa ajili ya kuzipanda kwenye shamba darasa katika kata hiyo wilayani humo leo.
 Mbegu hizo zikiinuliwa juu baada ya kukabidhiwa.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akimkabidhi mbegu za mihogo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani kwa ajili ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Isikizya wilayani humo. Wengine ni wakulima wa kijiji hicho.
 Wanakikundi cha Mapambano katika Kijiji cha Iberamilundi wakifurahi mbegu bora ya mihogo baada ya kukabidhiwa.
 Wakulima wa Kijiji cha Isikizya wakiwa kwenye uzinduzi wa shamba darasa.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza na wakulima na wakulima wa Kijiji cha Isikizya (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel.



 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Uyui, Hadija Makuwani akizungumza na wakulima kabla ya kuzindua shamba darasa la mbegu ya mihogo katika Kijiji cha Isikizya.
 Wakulima wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkulima, Gervas Fungameza akiuliza swali.
 Mkulima Said Mirambo wa Kijiji cha Isikizya akiuliza swali.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza ubora wa mbegu ya mihogo aina ya mkombozi jinsi ya kuipanda
 Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Hadija Makuwani akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo.
 Diwani wa Kata ya Isikizya akipanda mbegu hiyo.
 Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Uyui, Hamphrey Kilua akizungumza na wanakikundi cha Mapambano kabla ya kuzindua shamba la Viazi lishe katika Kijiji cha Iberamilundi.
 Wanakikundi cha Iberamilundi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi cha Mapambano cha Kijiji cha Iberamilundi namna ya kupanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
 Mwenyekiti wa kikundi hicho, Jumanne Said Mnubi 
akipanda mbegu hiyo.
 Katibu wa Kikundi hicho, Clementina Nyamizi akipanda 
mbegu katika shamba darasa.
Wanakikundi cha Upendo cha Kata ya Magiri wakiwa na mbegu zao mkononi za Viazi lishe

Na Dotto Mwaibale, Uyui Tabora

HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora imezipokea kwa mikono miwili mbegu bora za mahindi aina ya Wema, Viazi lishe na mihogo zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

Mbegu hizo zimetolewa katika vijiji vitano vya wilaya hiyo kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa ambavyo vimetajwa kuwa ni kijiji cha Isikizya kilichopo Kata ya Isikizya ambacho kitakuwa na shamba darasa la zao la mihogo, Ibelamilundi ambacho pia zao lake ni mihogo, Kijiji cha Kigwa ambacho zao lake ni Viazi lishe, Igalula ambacho kitapandwa mahindi na Magiri ambacho kitakuwa na shamba darasa la zao la Viazi lishe.

Akizungumza wakati wa kupokea mbegu hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Hadija Makuwani alisema wao kama wilaya wamezipokea mbegu hizo kwa mikono miwili na watazifanyia kazi ili waweze kupata mazao yenye tija.

"Kwa kweli tunawashukuru sana COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hizi kwani tuna imani zitatuondelea changamoto ya kupata mazao machache kutokana na kutumia mbegu za kienyeji zilizozoeleka kwa wakulima wetu" alisema Makuwani.

Makuwani alisema hata yeye kwa kuwa ni mkulima anaomba apatiwe mbegu hizo ili akazipande kwenye shamba lake ili hapo baadaye nawe aweze kusambaza mbegu hiyo.


Diwani wa Kata ya Isikizya, Ally Mtelela alisema mbegu hizo zitazidisha ari kwa wakulima hao na wataondokana na kilimo kisicho na tija ambacho walikuwa wakitumia mbegu ambazo zilikuwa zikishambuliwa na magonjwa.

Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya mihogo iwapo watalipa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata tani 25 hadi 32 na kwa zao la viazilishe watapata tani 7 hadi 9 kwa hekta moja.

Alisema matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye Viazi lishe wanapata tani moja hadi tatu.

Kibura alisema Viazi lishe hivyo aina ya kabode vina vitamini A ambavyo ni muhimu kwa watoto kwa lishe na rangi yake ni vya njano na vinaisaidia serikali kuacha kutumia matone ya vitamini A badala yake mtu akivila anapata vitamini hiyo moja kwa moja.

Akizungumzia kuhusu mbegu Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.

Mutagwa aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na ziada kuuza.

Mkulima Clementina Nyamizi wa Kijiji cha Iberamilundi ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Mapambano alisema wanaamini mbegu hizo zitawatoa katika umasikini na kuwa watazitunza na kuzilinda na wataachana kabisa na mbegu za kienyeji walizokuwa wakizitumia zamani.


“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”

November 08, 2017

JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo kwa kupata alama D waliopo vyuoni(supplementary).

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus Kadugalize wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa na mpaka sasa hawajapata fedha za kujikimu .

Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu alivyosema kuwa ifikapo ijumaa wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo ambalo linawapa wakati mgumu wanafunzi hao.

Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu ya kuwapa wanafunzi fedha zao za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha kujisajili.

“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba wapo wanafunzi wengi wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza kukamilisha zoezi la kujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu kwa wanafunzi “Alisema.

Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza alisema sasa bodi ya hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata katika upangaji wa awali aliwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13 mwaka huu ambapo rufaa hizo itakuwa ni bure.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi la udahili ambapo ambapo aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na una hatarisha baadhi yao kukosa nafasi ya kusoma.

Alisema vipo vyuo vimefahili wanafunzi zaidi ya idadi wanayotakiwa mfano chuo cha Mwenge na vyenginevyo jambo la ajabu wanapokwenda kuripoti vyuoni wanaambiwa wamekwisha kamilisha idadi walizopangiwa.

“Sasa tunajiuliza kwanini walikubali idadi kubwa ya wanafunzi
wathibitishe kwenye vyuo vyao? kwanini wasiweke ukomo wa idadi kulingana na wanayotakiwa  lakini pia mpaka sasa wapo wanasumbuliwa vyuoni hawajapokelewa na wametoka makwao “Alisema.

“Mfano yupo mwanafunzi ametoka kwao Arusha amekwenda Mwanza kuripoti chuo kalipa na ada kabisa ya chuo sikitaji  na alithibitisha kusoma hapo ajabu amekwenda kuripoti wana mwambia wameshajaza idadi hivyo subiri maamuzi ya TCU kama wataruhusu kuwapokea “Alisema.

Aliongeza kuwa vyuo visipelekee vurugu zisizo na maana yoyote ile endapo wanafunzi hao watakosa nafasi za masomo kwa mwaka huu kwa uzembe wa vyuo kudahili zaidi ya idadi yao kwa hofu ya kukosa wanafunzi .

“Lakini niwaambie sisi kama Tahliso hatutasita kuvichukulia hatua vyuo hivyo kwa kuwalipa fidia ya usumbufu wanafunzi  ambao wamekumbana naowakati wa kufuatilia michakato hiyo “Alisema.
Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa

Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa

November 08, 2017
Kampuni za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz. Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri, mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. “Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015 tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana. Lakini kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs, "Kimsingi hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood (Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood (Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’. Kwa sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na kuongeza. "Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au ‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?” Mashauri alisema kuwa wameanza jitihada za makusudi za kutangaza sinema hizi ikiwa ni pamoja na kuwatangaza wasanii na wazalishaji wa sinema,“Dunia nzima waigizaji wenye majina makubwa ndio wanaovutia walaji au wanunuzi wa filamu, hata kwetu imezoeleka hivyo. Lakini ili muigizaji awe mkubwa lazima kazi yake ionekana, "Kwa msingi huo na kwa ushirikiano wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wadau wetu Clouds Plus, tumeanzisha ‘reality show’ ijulikanayo kama ‘The Producers’ inayoruka Clouds Plus kupitia king’amuzi cha Azam Tv kila siku jumatatu hadi ijumaa saa moja mpaka saa moja na nusu usiku na marudio siku ya jumapili kuanzia saa nne asubuhi ambapo watanzania wataweza kuona namna sinema zinavyotengenezwa na wasanii wanavyofanya kazi zao," alisema Mashauri. Mashauri alisema kupitia kipiendi hicho watu mbalimbali ambao wanandoto za kuwa waigizaji watajua nini wa natakiwa kufanya kwani wataona fursa ziliziopo katika tasnia ya uigizaji na changamoto zinazowapata waandaji na waigizaji. "Tunategemea kufanya kazi na waandaaji kumi kwa mzunguko wa miezi sita sita na kila Producer atatakiwa kuzalisha sinema ndani ya miezi sita na mchakato wa sinema yake utaonyeshwa katika reality show, sinema yake itatangazwa na kupelekwa sokoni," alisema Mashauri. Naye Meneja wa Clouds Plus, Ramadhani Bukini, alisema Clouds Plus imeungana na Bongohoodz katika kufanikisha ukuaji wa soko la filamu nchini kwa kutoa fursa kwa wazalishaji wa sinema kuonyesha kazi zao na kuzipeleka sokoni kupitia matamasha. “Tumeungana na Bongohoodz tukiamini kuwa lazima kuwe na mbinu mbadala za kuuza sinema. Dunia imebadilika sana na huwezi kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, katika dunia ya leo, aina ya kompyuta zinazoongoza kwa kuuza duniani ni za Apple. Watumiaji wa ‘computer’ hizi hawahamasiki kutumia DVDs. Inamaana tunakoelekea hata wenye deki za kuangalia DVDs ni wachache, "Watu wako kwenye simu za mikononi, ndio maana Clouds Plus ikaamua kuungana na Bongohoodz kuja na vyanzo vipya vya mapato kwa tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na matamasha makubwa ya kuonyesha filamu. Kama imewezekana katika muziki tunaamini kabisa inawezekana katika filamu," alisema Bukini. Naye mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Novitech ambayo inashirikiana na Mashauri Studios katika kutayarisha sinema, Mary Mgurusi alisema watanzania wasubirie kwa hamu kazi nzuri za filamu. “Tumeandaa sinema nzuri za kitanzania zenye maudhui tofauti tofauti ambazo tunaamini zinaburudisha na kufundisha. Tayari sinema ya Tatu Chafu imekamilika na tunatarajia kuizindua tarehe 16/12/2017 Mlimani City pamoja na Dar Live Mbagala. Baada ya uzinduzi huo, tunatarajia kuonyesha sinema hii nchi nzima katika mikoa mbalimbali. Zaidi ya Tatu Chafu zipo sinema nyingi katika maandalizi, mfano Tajiri kutoka India, What is Marriage, Rashid Snake Boy Matumla na School Bus," alisema Mgurusi.

MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA

November 08, 2017

Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira (kushoto) Mh. Antony Mavunde (Mbunge), akimkabidhi mshindi wa 14 wa mchezo wa tatu Mzuka Bw. Robert A. Changadiko(45), hundi ya shilingi milioni sitini , Mjini  Dodoma.
Mshindi wa droo ya 14 ya Tatu Mzuka Bw.Robert A. Changadiko (kulia)aliyejishindia donge nono la shilingi milioni sitini wiki hii, akiwa na rafiki yake bwana Bw. Daudi Mwangoto (katikati), ambaye alizawadiwa shilingi milioni moja kutoka katika promosheni ya cheza na washkaji shinda na washkaji ya Tatu Mzuka, kushoto ni Bw.Edwin Kawito ni mshindi wa Tatu Mzuka droo ya kumi (10) aliyejishindia shilingi milioni sitini.
Mshindi wa shilingi milioni sitini kutoka kijiji cha Msembata (Dodoma)Bw.Robert A. Changadiko mwenye umri wa maika 45, ambaye ni fundi minara,akifurahia ushindi wake.
 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde leo amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 60 mshindi wa droo ya Tatumzuka Bwana Robert Changadiko ambaye alijishindia kiasi hicho katika ‘Jackpot’ ya wiki hii katika droo ya kusisimua iliyoonyeshwa siku ya jumapili kupitia vituo vya runinga kote nchini.

Bwana Changadiko ambaye anafanya kazi kama fundi minara mjini Dodoma alielezea furaha yake juu ya ushindi huo ambao hakuutegemea na akaishukuru Tatumzuka kwa kutimiza hitaji lake la pesa wakati alipokuwa akizihitaji zaidi.

"Niliamua kucheza Tatu Mzuka kutokana na matatizo niliyokuwa nayo ya kifedha ambapo nilihitaji fedha za haraka ili kukidhi mahitaji hayo. Kwakweli nina furaha kubwa sana na nashukuru kwamba nilijaribu bahati na ikatimia” alisema.Mavunde alimpongeza mshindi kwa kushinda kiasi hicho na Tatu Mzuka kwa ajili ya kuendelea kutengeneza mamilionea na kubadilisha maisha ya watu.

"Ninakushauri kwamba kabla ya kuanza kutumia pesa yako,tenga muda kufikiri namna utakavyotumia fedha yako ili utimize malengo yako na ili pesa uliyojishindia ilete mabadiliko ya kweli katika maisha yako." Mheshimiwa Mavunde alishauri.Mheshimiwa. Mavunde alihitimisha kwa kusisitiza kwamba hizi pesa ambazo watu wanajishindia kupitia Tatumzuka ni fursa hasa kwa vijana kujitengenezea ajira na kubadilisha maisha ya wale walio karibu yao. 

Afisa wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Patty Mtatiro alielezea kwamba Tatu Mzuka hadi sasa imetengeneza mamilionea 120 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3. Akasema kwamba sio hivyo tu, tarehe 19 Novemba ambapo ni wiki mbili kutoka sasa Tatumzuka kupitia SUPA Mzuka Jackpot itatoa milioni 150 za uhakika kwa mshindi atakayejishindia.

" Kwa sasa unaweza kushinda kwa njia 3 kwa kucheza mara moja tu kwa shilingi 500. Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda hadi Tz 6, 000,000 masaa 24 kwa siku. Kila Tzs500 unayoitumia inakupa nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye Mzuka Jackpot ya kila wiki ambapo unaweza kushinda zaidi ya shilingi Milioni 60. Namna ya tatu ni kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot ambapo dau la uhakika la Milioni 150 litatolewa kwa mshindi. Hakuna dili kali zaidi ya hili "alisema Bibi Mtatiro.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA MAZAO YA CHAKULA WAKATI NA BAADA YA KUVUNA

November 08, 2017


Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal


Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakimlaki Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili kufungua Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.



Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia  Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia  Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.


Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo Novemba 8, 2017.

Na Mathias Canal, Dar es salaam
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Novemba 8, 2017 amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lenye dhima ya kujadili masuala muhimu yanayohusiana na PHM na mchango wake katika uhakika wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda nchini Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisema kuwa anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala muhimu kujadili  masuala muhimu yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya kuvunwa (PHM).
Alisema Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kwa Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.
“Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na unatekelezwa na wadau kwa ufanisi”
“Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango wa kupunguza Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu jitihada za kushughulikia suala hili zianze na kwa sasa suala hili linaanza kueleweka kwa wadau wengi tofauti na uko nyuma ambako msisitizo ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

JOKATE AIFAGILIA TOT

November 08, 2017
Jokate na Khadija Kopa wakati wa mazoezi ya TOT
NA BASHIR NKOROMO
Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo amesema amefurahi na kufarijika sana kuona kundi la Tanzania One Theatre (TOT) likiwa bado lipo imara na kuendelea kutoa nyimbo mpya zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi na ala za muziki.

Amesema, uimara wa TOT unafanya kundi hilo kuendelea kutoa mchango mkubwa  kwa kutoa nyimbo
zenye hamasa kwa wananchi na hasa viongozi katika kuenzi amani, umoja, mashikamano wa kitaifa, uzalendo na uchapakazi na pia kuburudisha.

Jokate amesema hayo, alipotembelea mazoezi ya yimbo za Mkutano Mkuu wa CCM taifa, na za Mikutano Mikuu ya Taifa ya Uchaguzi wa Jumua zote za Chama, yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

"Kwa muda mrefu nyimbo zimekuwa ni sehemu muhimu ya kupeleka ujumbe kwa jamii. Nina furahi kuona kwaya ya TOT inaendelea kuenzi hili kwa kutoa nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi.

Hizi nyimbo walizotunga TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na mikutano ya Uchaguzi Mkuu wa Jumuia za Chama ni nzuri, zinatoa hamasa hasa kwa viongozi wetu wakizisikia nina imani watapata morali ya kuwa bora zaidi katika kazi zao", amesema Jokate.

Nyimbo hizo ambazo ambazo ni kwaya kundi la TOT juzi lilianza kuzirekodi katika Studio maarufu na ya kisasa  ya Highland Studio iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini alisema TOT imezitunga nyimbo hizo kwa ustadi mkubwa ili kuzifanya kuwa za kiwango bora kulingana na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake na pia kuzingatia umuhimu wa mkutano huo mkuu wa CCM taifa na mikutano mikuu ya Uchaguzi Mkuu ya Jumuia hizo za chama.