SERIKALI KUONGEZA MABEHEWA YA ABIRIA NA MIZIGO

SERIKALI KUONGEZA MABEHEWA YA ABIRIA NA MIZIGO

October 10, 2016
u1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza  na mkandarasi wa Kampuni ya China Civil pamoja na viongozi wa Serikali mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Ndono-Urambo yenye urefu wa KM 52 kuona hatua iliyofikiwa.
u2
Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), mkoa wa Tabora Qs.Tutu Lusama,   akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi Angelina Kwingwa wakati akikagua ujenzi wake.
u3
Muonekano wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi wake.
u4
Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco kutoka China (kushoto), akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), alipokagua barabara hiyo kuona maendeleo yake.
u5
Mbunge wa Jimbo la Kaliua mkoani Tabora, Mhe. Magdalena Sakaya akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 kuona maendeleo yake.
………
Serikali imesema  itaongeza mabehewa ya abiria na mizigo katika Shirika la Reli la Tanzania (TRL), kwa lengo la kutatua adha ya usafirishaji kwa watumiaji wa reli ya kati  katika mikoa ya  Tabora, Kigoma na Katavi.
Akizungumza katika ziara yake ya kikazi mkoani Tabora, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa uhaba wa mabehewa ya abiria umesababisha wananchi  wa maeneo hayo kutumia njia zisizo rasmi za ununuzi wa tiketi kwa ajili ya usafiri huo.
“Serikali imetambua changamoto kubwa ya usafiri inayowakabili wakazi wa mikoa hii, hivyo ni wakati muafaka kwa TRL kuongeza mabehewa matatu ili kupunguza adha ya usafiri”, amesema Prof. Mbarawa
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa ameupongeza uongozi wa TRL kwa kuokoa matumizi ya zaidi ya Shilingi milioni 100 kwa kukarabati mabehewa ya mizigo 23 kwa kutumia wataalam wazawa wa shirika hilo.
Ameongeza kuwa Shirika hilo limetekeleza dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza matumizi ya fedha na kuzingatia thamani ya fedha na kazi inayofanyika.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya ya kupunguza matumizi ya fedha mnazopata kwenye Shirika, ninaomba muendelee kutumia vyanzo vya ndani ili shirika lifikie hatua ya kujitegemea” amesema Profesa Mbarawa.
Naye, Meneja wa Usafirishaji wa TRL, mkoa wa Tabora Fredrick Masangwa ameiomba Serikali kuendelea na maboresho katika miundombinu ya reli kwa kiwango sawa na jinsi inavyoboresha miundombinu shindani ya barabara ili kuwepo na ushindani sawa katika sekta hizo mbili za usafirishaji.
Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Ndono-Urambo kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 52 na barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi na ukarabati wake.
Profesa Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa miradi hiyo iende sambamba na viwango bora vya ujenzi wa barabara vilivyomo kwenye mikataba iliyosainiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abeli Busalama ameipongeza Serikali kwa juhudi za ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza fursa za kiuchumi katika wilaya yake na wilaya za jirani pamoja na mikoa inayozunguka wilaya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Magdalena Sakaya amemuomba Waziri huyo kufikisha mawasiliano ya simu kwenye wilaya hiyo hususan vijijini ili kuweza kurahisisha mawasiliano kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Waziri Mbarawa amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili katika Mkoa wa Tabora ambapo amekagua miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, reli na mawasiliano.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

KISHINDO CHA TIGO FIESTA CHATIKISA MJI WA MTWARA

October 10, 2016
Roma Mkatoliki  akiwapa mashabiki burudani tosho kwenye tamasha la Tigo fiesta uwanja wa Umoja Nangwanda mkoani Mtwara


Msanii Manfongo akitoa burudani kwenye tamasha la Tigo fiesta lililofanyika uwanja wa Umoja Nangwanda Mtwara jana


Jay Moe akiwaburudisha wakazi wa Mtwara katika tamasha la Tigo Fiesta


Joh MAKINI Akitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta usiku wa jana mjini Mtwara

Weusi wakilivamia katika jukwaa la Tigo Fiesta 


Msanii toka Mtwara aliyepatikana katika shindano la Super Nyota akitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta


MAMA JANETH MAGUFULI AHUDHURIA MSIBA WA SHEMEJIE RAIS MSTAAFU MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE MJINI BAGAMOYO LEO OKTOBA 10, 2016

October 10, 2016

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo  Oktoba 10, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Bw. Mohamed Kikwete  alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo   Oktoba 10, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji akifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
Mawaidha yakitolewa msibani
Bw. Yusuph Kikwete akielekeza waombolezaji sehemu ya kukaa wakati wa msiba huo
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mnbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete alipowasili kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo.
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiongea jambo na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
 Sehemu ya waombolezaji   kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine wakibeba mwili wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
Waombolezaji wakimswalia maiti 
waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa  marehemu Mariam Ramadhani Saburi  kuelekeza makaburini huko Bagamoyo leo

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwafariji watoto wa  shemejie Rais Mstaafu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mariam Ramadhani Saburi,    aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
Sehemu ya waombolezaji msibani
Waombolezaji wakijiandaa kupata chakula cha mchana kabla ya maziko.
Picha na IKULU

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI SEPTEMBA 2016 UMEPUNGUA KWA ASILIMIA 4.5

October 10, 2016
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo, kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Septemba 2016. 
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Hayo yabebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo. 

" Hii inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2016 " alisema Kwesigabo.

Alisema  Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64 
mwezi Septemba 2015.Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa 
mwezi Agosti 2016.

Alisema  kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

"Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8.

Akizungumzia mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

Alisema kupungua kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Kwesigabo akizungumzia mfumuko wa bei kwa bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.34 kutoka asilimia 6.26 mwezi Agosti 2016.

Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.8 mwezi Agosti 2016.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM (10th October 2016).

October 10, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.

Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.

"Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi"  amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.

Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.

"Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada ya kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.

LHRC YAFUNGUA KESI DHIDI YA SERIKALI KUPINGA ADHABU YA KIFO

October 10, 2016
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (katikati), Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia) na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga , wakionesha jarida la kupinga adhabu ya kifo wakati wa uzindi wake Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.
 Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na mauaji.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali  wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.

Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo  kwa sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku  wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.

Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo  Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi  mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Alisema kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na ugaidi.

Dk. Bisimba alisema kituo  kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya kifo na  hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata muuaji auawe.

“Adhabu ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu  kwa wale watu ambao huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk. Bisimba na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza kuzuia watu wengine kutokutenda makosa  kama hayo.

Alisema licha ya adhabu  hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban miaka 22 , taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa kutokana na adhabu hiyo.

Hata hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii juu ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira ya kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria  kwa kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vya muda mrefu  gerezani.



VPL: YOUNG AFRICANS KUTUMIA UWANJA WA UHURU

VPL: YOUNG AFRICANS KUTUMIA UWANJA WA UHURU

October 10, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru jijini.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 6 kipendelea cha kwanza, Young Africans wametambulisha Uwanja wa Uhuru kama uwanja wa nyumbani kwa sasa baada ya kuleta maombi Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) ambako baada ya kuyafanyia tathimini kwa mujibu kanuni hiyo ya sita, kipendelea cha sita, TFF imeiridhia klabu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, kutumia uwanja wa Uhuru.

Hatua hiyo inafuatia na Serikali – mmiliki wa viwanja vya Uhuru na Uwanja Mkuu wa Taifa, kuzuia klabu hiyo pamoja na ya Simba kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa michezo yao ya nyumbani kutokana na vurugu.
Michezo mingine itakayopigwa Jumatano ni kati ya Mbeya City ya Mbeya na Simba ya Dar es Salaam, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Stand United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.

MANISPAA YA ILEMELA YAANZA BOMOA BOMOA KWA WALIOJENGA KWENYE HIFADHI YA MTO MSUKA KILIMAHEWA.

October 10, 2016
Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika. Wananchi wametakiwa kutojenga maeneo yasiyo rasmi.
Na BMG
Zoezi ka ubomoaji likiendelewa ambapo limesimamiwa na mgambo wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Ilemela
Mto huu unapaswa kupanuliwa zaidi na kujengewa kuta maana wakati wa mafuriko huwa unapitisha maji mengi yanayosababisha mafuriko kwa wakazi wa eneo hili la Kilimahewa.
Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubobolewa
Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubobolewa
Na George Binagi-GB Pazzo 
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika.

Mhandisi wa Manispaa hiyo, Jacob Mwakyambiki, amesema zoezi hilo limefanyika baada ya tahadhari kutolewa kwa wakazi wa eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita na kwamba mpango uliopo ni kujenga mtaro mkubwa katika mto huo ili kusaidia maji yake kutosababisha mafuriko wakati wa mvua za masika.

Amesema tayari mkandarasi ameanza kazi hiyo na kwamba ujenzi wa mto huo utakapokamilika, utasaidia maji yake kutiririka moja kwa moja hadi ziwa Victoria badala ya kumwaga maji kwenye makazi ya watu kama ilivyokuwa hapo awali na kusababisha athari za kimafuriko.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wanaoishi katika eneo linalopitiwa na mto Msuka wamesema zoezi hilo limefanyika wakati ambao bado hawajui hatima yao kwani wakati wanajenga makazi yao katika eneo hilo walipata vibali vyote ikiwemo hati miliki za viwanja vyao ambapo wamependekeza kulipwa fidia licha ya Manispaa ya Ilemela kuwatahadharisha kwamba hakuna fidia itakayotolewa kwa waliojenga katika hifadhi ya mto.

Licha ya malalamiko hayo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Ibungilo wanaoishi katika maeneo jirani na mto Msuka wamepongeza zoezi la upanuzi wa mto huo kwani wamekuwa wakipata athari kubwa ikiwemo mali zao kusombwa na maji wakati wa mvua za masika kutokana na makazi ya wananchi yaliyojengwa kwenye karibu na mto huo.

Katika misimu kadhaa ya mvua za masika, athari mbalimbali ikiwemo vifo vya watu na mifugo kutokana na mafuriko ya mto Msuka, zimekuwa zikitokea katika eneo la Kilimahewa kutokana na wananchi kujenga makazi yao hadi kwenye hifadhi ya mto huo hivyo upanuzi na ujenzi wake unaelezwa kuwa mwarobaini wa kadhia hiyo.