RAIS KIKWETE KUZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA NSSF KILIMANJARO

February 08, 2015

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini..

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete leo anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro ambapo miongoni mwa shughuli anazotazamiwa kufanya ni pamoja na
kufungua jengo la kitega uchumi la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF).

Mbali na ufunguzi huo Rais Kikwete pia anatarajia kufungua jengo la Upasuaji na kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya wazazi na watoto katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ,mkuu wa mkoa huo Leonidas Gama alisema Rais Kikwete atawasili mkoani humo leo jioni
majira ya saa 11:00 jioni ambapo atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuelekea Ikulu ndogo kwa ajili ya kupokea taarifa ya Mkoa.

Alisema Kesho (February 10) Rais Kikiwete  atafanya shughuli katika Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ikiwemo ufunguzi wa jengo la Upasuaji (Theater) ambalo limekuwa tatizo la muda mrefu katika hosptali hiyo.

“Kwanza kama mnavyo fahamu tumekuwa na tatizo la muda mrefu ya wodi ya upasuaji katika hospitali yetu ya Mawenzi,lakini kwa juhudi zilizofanywa na serikali na ushirikiano wa wadau mbalimbali lile jengo

la Upasuaji limekamilika na liko katika kiwango kizuri kwa hiyo shughuli ya kwanza atakuja kulifungua rasmi jengo la upasuaji.”alisema Gama. 
RAS-Seviline Kahitwa (shoto) RC Gama (Kulia)


Gama alisema pia Serikali tayari  imefanya juhudi za kujenga jengo jipya la Wodi kwa ajili ya Wazazi na Watoto katika hosptali hiyo na kwamba Rais Kikwete ataweka rasmi jiwe la msingi  kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi wa jengo hilo.

Alisema kwa mujibu wa ratiba shughuli ya mwisho anayotazamia kufanya Rais Kikwete ni ufunguzi rasmi wa jengo la kitega Uchumi la NSSF,jengo
ambalo litatumika kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi .

“Ufunguzi rasmi wa jengo hili utabadilisha taswira ya mji wetu,ni jengo la kisasa lenye Hotel,Maofisi mbalimbali,Kumbi za mikutano na maduka mbalimbali makubwa kwa madogo ambayo yatahudumia wananchi wote”alisema Gama.

Gama alitoa wito kwa viongozi na wananchi wote wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa jengo hilo la NSSF majira ya saa 2:00 asubuhi ambapo rais Kikwete pia atapata nafasi ya kuzungumza na wananchi.

“Lengo la Rais Kikwete kuja ni kutuunga mkono sisi wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro katika miradi yetu ya maendeleo hivyo basi tufike mapema katika maeneo hayo ili tumsubiri na tumuone rais na kumshangilia”alisema Gama.
Hili ndio jengo jipya la kisasa la kitega Uchumi la Mfuko wa Hifadhi ya Jami NSSF mkoani Kilimanjaro.

YANGA YAJICHIMBIA KILELENI MWA LIGI KUU YA VODACOM YA SOKA TANZANIA BARA

February 08, 2015

 Beki wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi akimdhibiti beki wa Yanga, Mbuyu Twite.

Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akichuana na beki wa Mtibwa Sugar,  David Luhende wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.

 Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akitoa maelekezo kwa wacherzaji wakei.

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akichuana na kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0. (Picha na Francis Dande)

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akichuana na kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.

Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akimpiga chenga kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed hata hivyo Msuva baada ya kubaki na goli alipiga nje mpira huo.
 Msuva akikosa bao.
 Msuva akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
Kikosi cha Mtibwa Sugar.
Kikosi cha Yanga.
 Benchi la ufundi la Mtibwa Sugar.
 Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiwapanga wachezaji wake.

Airtel yaitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Arusha

February 08, 2015

Meneja Mauzo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha , wakishuhudia (katika) Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma.
Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala (kulia) ,Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha.
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika) akiongea na wandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha wakishuhudia Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mkoani Arusha wakifatilia kwa makini uzinduzi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi uliofanyiaka katika hotel ya Palace Arusha leo ijumaa.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetambulisha promosheni yake ya Airtel yatosha kwa wakazi wa Arusha  na kusisitiza kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku.
Akiongea na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Amesema “tumeona ni vyema kutambulisha  promosheni hii kwa wakazi wa Arusha kwani wao pamoja na watanzania katika mikoa mbalimbali  wananafasi ya kujishindia. Promosheni hii tuliyoizundua rasmi mwanzoni mwa wiki hii inampa nafasi mteja wa Airtel kushiriki na kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST pindi atakaponunua kifurushi chake chochote cha Airtel yatosha”
Matinde aliongeza kwa kusema ”Mteja atakaponunua kifurushi chake cha siku anaingia kwenye promosheni kwa simu hiyo lakini akinununa cha wiki namba yake itaingia kwenye promosheni kwa muda wa siku saba na akinunua cha mwezi namba yake itaingia kwenye droo kila siku kwa siku thelathini.  Lakini mteja atakaponunua kifurushi chake cha Airtel yatosha cha siku zaidi ya mara moja namba yake itaingia kwenye droo ya siku hiyo kwa idadi ya vifurushi vya siku alivyonunua.
Ili kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha Mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kununua vocha ya yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money
Huduma ya Airtel yatosha inampa fulsa mtumiaji wa huduma yetu ya Airtel yatosha kupata vifurushi bora na vya bei nafuu sokoni lakini pia inamuwezesha kushinda Toyota IST aliongeza Matinde
Kwa upande wake Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini Bwana Brighton Majwala alisema, “promosheni hii ni ya pekee na haina gharama yoyote kujiunga, mteja anapata nafasi ya kushinda kutokana na matumizi yake ya kila siku. Wakazi wa Arusha kesho wanapata nafasi ya kuyashuhudia magari haya yakitembea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha na tutawapatia wateja wetu nafasi ya kununua line, kujisajili na kupata huduma zetu nyingi na kuwawezesha kujiunga na vifurushi vya yatosha ili waweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia
Hii ni nafasi ya pekee kwako mkazi wa Arusha kuchangamkia zawadi hii nono kwa kujiunga kwenye vifurushi vya yatosha sasa aliongeza Majwala
Airtel yatosha Zaidi ni promosheni yenye lengo la kuwazawadia wateja wake  nchini nzima ambapo kila siku Airtel itatoa Toyota IST moja kwa mshindi wa siku.
 JAMII YATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA VIJANA WAKATI WA MIPANGILIO YA BAJETI ZAO

JAMII YATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA VIJANA WAKATI WA MIPANGILIO YA BAJETI ZAO

February 08, 2015

2
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha alipoenda kuzindua mradi wa BEYOND 2015 hivi karibuni.
3
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisikiliza maelezo mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru Munasa jijini Arusha juzi.Wa mwisho kushoto ni Mkuwa Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa.
4
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Shirikisho wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.la Ujerumani Bibi. Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bibi. Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya, na Ustawi.
5
Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
7
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akifuarahi mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo watekelezaji wa mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester Mwanjesa aliyeshika kitabu.
8
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiteta jambo na Mkurugenzia wa DSW Tanzania(katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015 Bi. Esther Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha
9
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya Kimasai kutoka kwa Mwanamke mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea maonyesho ya biaadha zao katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.1
Picha ya pamoja
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniella Schadt ametoa wito kwa jamii kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo. Wito huo umetolewa juzi jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa Ujerumani alipokuwa akizindua mradi wa utetezi na ushawishi wa jamii katika kutoa vipaumbele katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo mradi huo unaratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania. Bibi. Daniela alisema kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana kwa kuwa duniani kote vijana ndiyo nguvu kazi katika kuletea maendeleo ya taifa lolote lile. ‘Tunapaswa kuweka mkazo kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye yanaanza kuanzia sasa, tuweke mkazo katika Elimu na Afya kwa vijana wetu ili waeze kutambua fursa na kuzitumia.’’ Alisema Bibi. Daniela. Kwa upande wake Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga amesema kuwa ni wao kama asasi ya kirai wanashirikia na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa sera zinazohusu vijana nchini zinaleta tija Owaga ameongeza kuwa Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa kwa kuwa na Sera na miongozo mbalimbali inayohusu vijana kama vile Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inayotoa fursa kwa kijana kujitambua. Aidha Owaga aliongeza kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao umezinduliwa na Mke wa Rais wa UjerumaniBibi. Daniela Schadt umelenga kuongeza ushawishi na hamasa kwa washirika wa maendeleo ili kutoka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya Elimu , Afya ya Uzazi na Ajira kwa vijana. Akizungumzia mikakati na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa Muhamasishaji na Mawasiliano Bi. Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika mikoa yote nchini ambapo mijadala mbalimbali itakuwa ikifanyika ili kuongeza hamasa ya uashawishi utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana hususan katika nyanja za Elimu, Afya ya uzazi na Ajira. Mradi huu wa BEYOND 2015 ambao ni kifupi cha maneno Building Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post 2015 Development umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya kumalizika kwa muda wa Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.
RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, DAR ES SALAAM

February 08, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, Mama Mzazi wa
Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015
huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam. jky2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakijumuika na
waomboilezaji wengine  katika mazishi ya Marehemu Bibi Bridget
Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi
Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.
jky3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka udongo
kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji
Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko
Kimara King’ongo jijini Dar es salaam. jky4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka shada
kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji
Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko
Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU
Rais Kikwete aongoza mazishi ya Bi.Tajiri Tanga

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Bi.Tajiri Tanga

February 08, 2015

jk1.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Bi.Tajiri Abdallah Kitenge wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga.Marehemu Bi.Tajiri ni mama wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Rashid Othman. jk2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bwana Rashid Othman wakati wa mazishi ya Mama yake Bi.Tajiri Abdallah Kitenge yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga jana(picha na Freddy Maro)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa rai kwa wakulima na wafugaji wote nchini kujikubali ni Watanzania

Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa rai kwa wakulima na wafugaji wote nchini kujikubali ni Watanzania

February 08, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akivunja Bunge. bu2Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Christopher Ole Sendeka, akijibu hoja za wabunge kuhitimisha mjadala.Kamati hiyo iliundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Aridhi, Kilimo, Mifugo,Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.
bu3 
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni Mstaafu John Chiligati, akichangia hoja.
Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, akichangioa taarifa ya kamati teule. bu5 
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Sabrina Sungura aichangia hoja.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman akichangia taarifa. bu7 
Wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya mkutano wa Bunge kuvunjwa. bu8 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.
bu9Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata.
bu10 
Baadhi ya wafugaji waliohudhuria Bungeni wakizaungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
……………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote bila kuvunja sheria.
Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji.
“Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema Pinda
Aliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha.
Hata hivyo Waziri Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko.
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha.
Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili.
“Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.