KINANA AANZA ZIARA MKOA WA TANGA, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA UHAI WA CHAMA WILAYA YA HANDENI

September 23, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mkuu waWilaya ya Handeni, Muhimngo Rweyemamu alipowasili wilayani humo, leo Septemba 23, 2014, kuanza ziara ya siku 11 mkoani Tanga. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga, Hery Shekifu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana kwa furaha na Mbunge wa Handeni,Abdallah Kigoda, alipowasili wilayani humo, leo Septemba 23, 2014, kuanza ziara ya siku 11 mkoani Tanga. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga, Hery Shekifu.(HABARI PICHA KWA HISANI YA BLOG YA CCM)
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani "Majimarefu" wakati wa mapokezi hayo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibvu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi hayo yaliyofanyika katika Kata ya Mkata, Handeni mkoa wa Tanga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimia, wakati Kinana alipozungumza na wananchi wa Kata ya Mkata baada ya mapokezi na kuzinduzi wa mradi wa maji wa kata hiyo leo, Septemba 23, 2014. Kushoto ni Kinana, Shekifu na kulia ni Muhingi Rweyemamu na Dk. Abdallah Kigoda
 Kinana na Shekifu wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano ulioambana na mapokezi hayo katika kata ya Mkata.
Kinana na Kigoda wakifurahia jambo wakati wa kikao cha mapokezi hayo wilayani Mkata mkoa wa Tanga.
 Kinana akizungumza na wananchi wakati wa mkutano ulioambatana na mapokezi nauzinduzi wa mradi wa maji wa Kata ya Mkata leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua mambomba ya mradi wa maji wa kata ya Mkata, leo Septemba 23, 2014. Pamoja naye ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Handeni Dk. Abdallah Kigoda
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, wakishusha bomba, wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Kata ya Mkata.

 Kianana akitia zege kwenye ujenzi wa tanki la mradi wa maji Handeni mkoa wa Tanga
 Dk. Kigoda akisindilia zenge kwenye ujenzi wa tanki hilo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenziwa maabara tatu kwenye shule ys sekondariKwaluguru,wilayani Handeni mkoa wa Tanga.
 Mbunge wa Handeni Abdallah Kigoda akimwaga zege kushiriki ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Kwaluguru, katika jimbo hilo leo, wakati Katibu Mkuu wa CCM Kinana akipokagua ujenzi wa maabara hizo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wazee alipowasili kwenye uzinduzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kwenjugo, Handeni mkoa waTanga leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wananchi kabla ya uzinduzi wa tawi hilo la CCM Kwenjuu, Handeni.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Kwenjugo, Handeni mkoa wa Tanga, leo, Septemba 23, 2014. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU: KUWAWEZESHA VIJANA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KIAFYA BARANI AFRIKA

September 23, 2014

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
Baadhi ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.

TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI WAREMBO MISS TANZANIA BABATI MKOANI MANYARA

September 23, 2014

 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini. Na Father Kidevu Blog
 Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.
 Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo
 Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani…
 Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
 wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
 Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
 Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
 Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.
 MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU AKIWA RUKWA NA DODOMA.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU AKIWA RUKWA NA DODOMA.

September 23, 2014


PG4A7055[1] 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa shule ya Msingi ya Kakuni wilayani Mlele Septemba 22, 2014. Alikuwa njiani akitoka Sumbawanga kuelekea Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Rajab Rutengwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A6322[1] 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua shule ya Sekondari ya Magnificat wilayani Siha Septemba 20, 2014.  Kushoto ni mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A7108[1]
PG4A7110[1]
PG4A7115[1] 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na wazee wa Mpanda  baada ya kuzungumza na mjini Mpanda Septemba 22, 2014. Alikuwa njiani akitoka Sumbawanga kuelekea Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A7199[1] 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni  ya POWERCHINA, Bw. Wang Bin kabla ya mazungumzo yao mjini Dodoma Septemba 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO.

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO.

September 23, 2014

PIX_1.[1] 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX_2.[2] 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX_3.[1] 
Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX_5.[1]
PIX_5.[1] 
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.