UFUNGUZI WA TAMASHA LA BIASHARA LA 3 ZANZIBAR.

UFUNGUZI WA TAMASHA LA BIASHARA LA 3 ZANZIBAR.

January 10, 2017

uyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar sherehe zilizofanyika leo huko katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
uyo-1
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kufungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
uyo-2
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Najma Hussein (katikati) alipotembelea banda la maonesho ya Biashara la Bakhresa Group Companies  mara baada ya kufungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
uyo-3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Injinia Hamis Lusanda (kulia) kutoka Vigor Tp Company Ltd wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali  mara baada ya kufungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar   katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
uyo-4
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Dar es Salaam  Edwin N.Rutageruka wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali  mara baada ya kufungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar   katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
uyo-5
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Ndg.Mohamed Suleiman wa Kiwanda cha Uchapaji cha Serikali  wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali  alipofungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar  leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
uyo-6
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha tiba,ushauri nasaha na Utafiti wa magonjwa Sugu na Ukimwi Dr.John A.Kidua (kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali  alipofungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
uyo-7
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Wajasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza,ambao wanafanya bishara ya mikoba na dawa asilia   wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali  alipofungua  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali,[Picha na Ikulu.] 10/01/2017.
KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS PROF. FAUSTIN KAMUZORA ATEMBELEA NEMC

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS PROF. FAUSTIN KAMUZORA ATEMBELEA NEMC

January 10, 2017

fau
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kutemebelea Ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.  NEMC ni Taasisi iliyopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
fau-1
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  Bw. Bonaventure Baya (Kushoto) mara baada ya kuetembelea Ofisi za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni sehemu ya wajumbe wa Menejimenti katika Ofisi hiyo.
fau-2
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Bonaventure Baya na Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais.
Picha zote na SIGLINDA CHIPUNGAUPI

TUJENGE UTAMADUNI WA KUJIWEKEA MALENGO KILA TUNAPOINGIA MWAKA MPYA

January 10, 2017
 Na Jumia Travel Tanzania
Je, bado unajiuliza ni kwanini mwaka wa 2016 umeisha lakini haujapendezwa na mafanikio uliyoyafikia? Kama ni ndiyo, basi makala haya juu ya kujiwekea malengo itakuwa yenye msaada mkubwa kwako.

Watu wengi bado wanashindwa kuelewa ni kwanini inawawia vigumu kufuatilia hatua za kimaendeleo walizopiga katika maisha yao kutokana na kutojiwekea malengo. Malengo yanatofautiana kulingana na jambo au mambo gani ambayo mtu anatamani kuyatimiza ndani ya kipindi fulani cha muda. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukukumbusha haya mapema, kwani bado mwaka 2017 ni mchanga.


Malengo yanaweza kuwa makubwa au madogo, ya muda mrefu au mfupi kutegemea na mtu atakavyojiwekea. Hivyo ni muhimu kutambua kwamba malengo yako ni ya aina gani kwani itakurahisishia namna ya kuyakamilisha. Kwa mfano, lengo la kujenga nyumba ya kuishi haliwezi kufikiwa kwa mbinu au mikakati sawa na kununua samani za ndani.

Hivyo basi katika kujiwekea malengo haitakiwi kujiwekea vikwazo akilini kwamba hauwezi kulifikia lengo fulani kwa sababu ni kubwa, au hauna uwezo wa kulifanikisha. Weka lengo ambalo unaona utaweza kulifikia na kulifanikisha kulingana na uwezo ulionao ndani ya muda uliopo.

Kwa kawaida, maisha ya binadamu yanaongozwa na malengo, hivyo tunaweza kusema kwamba maisha bila ya malengo hayana maana yoyote. Malengo hayo yanaweza kuwa mtu fulani au kupata kitu fulani, inategemea na matamanio ya mtu.

Kuna watu wanatamani kuwa waandishi wazuri wa habari au vitabu na kuwa mfano wa kuigwa lakini hawaonyeshi jitihada zozote za kufikia lengo hilo. Kwa mfano, ili kuwa mwandishi wa habari kwanza kabisa lazima utakuwa umevutiwa na mwandishi mmojawapo katika tasnia hiyo. Je, unafanya jitihada gani za kumfuatilia mtu huyo alipoanza? Changamoto gani alizopitia mpaka akafanikiwa?



Ni ndoto ya kila mwanafunzi kufaulu vizuri shuleni lakini ni wangapi wanafanya bidii ya kufuatilia masomo na kusoma kwa bidii? Wengi wao wanakosa mbinu za kufikia malengo hayo kutokana na kutojiwekea mikakati thabiti, unakuta hahudhurii au kufuatilia vipindi vya darasani wala kujitengea muda wa ziada kujisomea baada ya ule wa darasani.

Hakuna jambo linalowashinda watu wengi kama kujiwekea malengo ya muda mrefu kama vile kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya kitu fulani. Kwa mfano, kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka watu wengi wanalalamika kuwa fedha hakuna huku mahitaji yakiwa ni mengi. Kipindi hiki asilimia kubwa watu wanahitajika kulipia pango za nyumba, karo za shule, leseni za vyombo vya moto na kadhalika. Lakini hayo yote yatasahaulika baada ya mwezi huu kupita pasipo kujiaandaa yasijekutokea tena kipindi kijacho.

Hiyo ni mifano tu ya malengo mtu anaweza kujiwekea, na namna ya kuyafanikisha kwa sababu hiki ndicho kipindi sahihi. Ingawa ni utaratibu mgumu kwa watu wengi hususani Watanzania, ila una faida kubwa sana kama ukiuanza na kuuzingatia.

MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA

January 10, 2017
Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema hali ya upatikanaji wa dawa kwasasa imeboreshwa kutoka asilimia 54 iliyokuwepo mwaka jana, hadi kufikia asilimia 74 hivi sasa. 

Ameuhakikishia umma uwa upatikanaji wa dawa utaimarika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hadi kufikia asilimia 90.

Amesema kwa sasa kati ya aina za dawa muhimu 135 zinazohitajika kuwepo MSD dawa aina 100 zinapatika kwenye maghala ya MSD

Mkurugenzi wa MSD, Bwanakunu ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, alipokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na idara katika jukumu lake la kutoa nafasi kwa Idara na Taasisi za serikali kuelezea utekelezaji wa majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Bwanakunu ameeleza kuwa, MSD imefanikiwa kurejesha Maghala iliyokuwa imekodi kwa ajili ya kuhifadhia vifaa tiba, hatua ambayo inaokoa sh.Bilioni 4 ambazo zilikuwa zikilipwa kama kodi kila mwaka. 

Ameongeza kuwa, tayari wamekabidhiwa kiwanja eneo la Luguruni, wilayani Ubungo walichopewa na Rais John Magufuli ambacho kitatumika kujenga ofisi za Kanda ya Dar es Salaam.

Kuhusu maduka, ameeleza kuwa wiki ijayo wanatarajia kuzindua  duka la dawa la MSD mkoani Katavi, ambalo litaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka Saba, mengine yakiwa mkoani Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Geita naMbeya. 

Akijibu swali juu ya ukosefu wa vifaa vyakujifungulia wajawazito Mkurugenzi Mkuu amesema vipo vyakutosha,na  zabuni ya manunuzi ya vifungashio kwa ajili ya vifaa hivyo vyakujifungulia iko katika mchakato wa kumpata mshitiri. 

Ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anaangalia namna ya kuwawezesha akina mama wasio kuwa na uwezo wakununua vifaa hivyo ambapo
utaratibu huo atautoa baadae.

Kwa sasa MSD inanunua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, ilikuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unakuwaendelevu na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa hizo, ambazo asilimia 80 zinatoka nje ya nchi.


“MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AWAPA POLE WATU WALIOPOTEZA NDUGU ZAO KWENYE AJALI YA KUZAMA KWA JAHAZI BAHARI YA HINDI”

January 10, 2017

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi  kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika kipindi hiki kigumu.
Ajali ya Jahazi  ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria  12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.
Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi  na kuzama
Akizungumza na MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.
Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.
Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 “Ajali sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.
Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.
Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.
Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.
Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu mengine.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PROF. IBRAHIM GAMBARI MJUMBE MAALUM WA RAIS WA NIGERIA, CHATO MKOANI GEITA.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PROF. IBRAHIM GAMBARI MJUMBE MAALUM WA RAIS WA NIGERIA, CHATO MKOANI GEITA.

January 10, 2017
gm
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliyefika Chato mkoani Geita kwa ajili ya mazungumzo.
gm-1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
gm-2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari uliowasilishwa na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais huyo wa Nigeria, Chato mkoani Geita.
gm-3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
gm-4
Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari  akimshukuru Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
gm-5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
gm-6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU.
………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita. Mazungumzo yao yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.
Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.
Pia, Rais Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa Nigeria.
Profesa Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato, Geita
10 Januari, 2017

Matembezi ya UVCCM kuunga mkono maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar

January 10, 2017


                                                    Na Othman Khamis Ame, OMPR,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Taifa linawategemea Vijana  wakati wowote katika dhana nzima itakayothibitisha kwamba wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yote yanayolikabili Taifa.
Alisema Serikali zote mbili ile na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na iIe ya Mapinduzi ya Zanzibar zinataka kuona  Vijana wake wanakuwa chem chem ya Maendeleo badala ya kuwa dimbwi la matatizo mitaani.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi { UVCCM } kuunga mkono maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Alisema Vijana ambao ndio warithi wa kulinda Mapinduzi ya Zanzibar dhana iliyoanzishwa  na muasisi wa Mapinduzi hayo Mzee Abeid Amani Karume wana wajibu wa  kusimamia vita vya mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya, udhalilishaji wa wanawake na watoto,  uonevu  pamoja na ufisadi.
Balozi Seif alikariri maneno ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume yaliyoeleza maana halisi ya Mapinduzi daima ambayo sio kupindua watu bali ni kuondoa matendo mabaya katika jamii na kusimamia haki na mazuri yote.
Akizungumzia changamoto kubwa zinazowakabili Vijana hasa  ukosefu wa ajira ambalo limekuwa likizikumba nchi mbali mbali Duniani  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imeandaa Mipango imara ya kukabiliana na changamoto hiyo .
Mapema akitoa taarifa ya matembezi hayo Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Ndugu Shaka Hamdu Shaka  alisema Vijana wengi nchini huingia katika majaribu ya kudanganywa  historia ya Zanzibar  na kupelelekea kukejeli Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Nd. Shaka alisema Mapinduzi ya Zanzibar  yametandikwa kwa  zulia la Umoja, Upendo na mshikamano chini ya majemadari waliofanya mapinduzi hayo ambao wanastahiki kuendelea kuenziwa na wananchi na Vijana wa kizazi cha sasa.
Akitoa salamu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anyesimamia Mazingira na Muungano Mh. Januari Yussuf  Makamba alisema Mapinduzi ya Zanzibar ni kielelezo tosha cha kujitambua kwa waafrika wa Visiwa vya Zanzibar.
Mh. Januari alisema Wakombozi wa Mapinduzi ya Visiwa vya Zanzibar wameacha urithi mkubwa kwa vijana wa Kizazi kipya unayostahiki kulindwa na kuendelezwa kwa faida na maslahi ya Wananchi wake.
Alisema njia pekee na sahihi ya kuendelea  kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar  ni kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar kupitia njia ya kuipatia ushindi CCM katika chaguzi zote zinazoendelea kufanyika hapa Nchini.

KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION REWARDS YOUNG SCIENTISTS 2016

January 10, 2017

Diana Sosoka and Nadhra Mresa (All photos: Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog)