WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA BENKI ZISIZOKIDHI VIGEZO ZIFUTIWE LESENI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA BENKI ZISIZOKIDHI VIGEZO ZIFUTIWE LESENI

December 14, 2017
IMG_7655
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),(kulia), anaeshughulikia masuala ya kibenki Bw. Kened Nyoni na Kaimu Kamishna Msaidizi Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Michael Nyagoga (Kushoto) wakifuatalia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT), uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
IMG_7677
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT), Bw. Mugwagi Stephen akizungumza katika mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mweyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mhe. Hawa Ghasia na Kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
IMG_7704
Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ili aweze kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi kwaniaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
IMG_7740
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihutubia katika mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika mjini Dodoma ili kujadili masuala ya Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania.
IMG_7747
Washiriki wa mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mjini Dodoma.
IMG_7758
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Benard Kibesse (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi –COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), mijini Dodoma.
IMG_7843
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akifurahia jambo na Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia baada ya  kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
IMG_7914
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa Nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
IMG_7983
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mkutano wa wadau  wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
IMG_7991
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………………………………………………..
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania BOT kuzifutia leseni benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibenki nchini.
 Ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT).
 “kwa taarifa niliyonayo hadi sasa baadhi ya benki hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha, hali ambayo haiwezi kuachwa iendelea hata kidogo, kwani haiimarishi sekta ya fedha na haiwasaidii wananchi kuendelea kiuchumi” alisema Waziri Kassim Majaliwa katika hotuba hiyo
 Alisema Benki Kuu ilitoa muda hadi mwishoni mwa Desemba 2017, benki za wananchi ziweze kuongeza mtaji na kwamba muda huo hautaongezwa na wala Serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.
 “Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania haitasita kuifungia benki yoyote na kufuta leseni yake ya biashara pindi itakapobaini inavunja sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja kama tulivyofanya kwa Mbinga Community Bank PLC kuanzia tarehe 12/5/2017” alisema Dkt. Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu.
 Maagizo hayo yamekuja siku moja baada ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango wakati akifungua tawi kuu la Benki ya CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.
 Alisema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha benki za wananchi zinaimarika zikiwemo kuruhusiwa kuanzisha mifumo ya ushirikiano katika Nyanja ya Mfumo wa Mawasiliano na Habari (ICT), Idara za Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit Services), kupunguza wingi wa idara na kuwa na idara tatu (3) tu muhimu, kuruhusiwa kuungana (Federation), ambazo zitapunguza gharama za uendeshaji wa benki za wananchi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma.
 “Napenda kusisitiza kuwa sekta ya benki ni muhimu sana kwa uhai na ukuaji wa  uchumi kama ilivyo damu kwa mwili wa binadamu na kutokana na umuhimu wake huo, sekta hii ni kati ya sekta chache zinazosimamiwa  kwa karibu sana ili kulinda amana za wateja pamoja na kuhakikisha uhimilivu wa mfumo mzima wa sekta ya fedha na mwenendo wa uchumi wa Taifa” aliongeza Dkt. Mpango
 Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT) Bw. Rukwaro Senkoro, alisema hadi kufikia Juni, 2017, Benki za Wananchi nchini zilikuwa na wateja zaidi ya milioni 1.4, wateja wa vikundi zaidi ya 10,000, Matawi 12, Vituo 59, na wanahisa 66,492.
 “Benki hizo zina amana zenye thamani ya shs bilioni 74.2, zimetoa mikopo ya sh. bilioni 56.8, na jumla ya mali zenye thamani ya shs. bilioni 92.3” Alisema Bw. Senkoro
 Hata hivyo, kutokana na Utafiti wa Matumizi ya Huduma za Kifedha uliofanyika mwaka 2017 umebaini kuwa asilimia 28 ya wananchi bado hawapati huduma za kifedha hapa nchini hususan vijijini na kutaja changamoto ya ukosefu wa mitaji ya benki hizo kukwaza sekta hiyo.  
 Dhana kuu ya mkutano huo wa COBAT uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ni “Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania”, ambayo ni dhana mpya.

NAIBU WAZIRI AWESO ATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI TANGA UWASA

December 14, 2017
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na Afisa Rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kuitembelea mamlaka hiyo
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akisalimiana na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo
mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kuitembelea mamlaka hiyo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Phares Aram
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo kwa ajili ya kumpatia taarifa wakati wa ziara yake.

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara hiyo 
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Phares Aram akizungumza wakati wa ziara hiyo
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo
Afisa Rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa),Haika Ndalama akizungumza wakati wa ziara hiyo wa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
 Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia nasaha za Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso katikati akimsikiliza kwa umakini  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akimueleza jambo kwenye ziara hiyo ya Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso  akichimba mtaro katika eneo la Mikanjuni Jijini Tanga wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso  akichimba mtaro katika eneo la Mikanjuni Jijini Tanga wakati alipotembelea mradi wa mfumo wa uboreshaji wa Maji
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akitoa mchanga kwenye mtaro huo mara baada ya kuuchimba na sururu wakati wa ziara yake ya kutembelea mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
aimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga,Phares Aram akichimba mtaro huo katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso








MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KUAGA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI CHINI YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI DRC

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KUAGA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI CHINI YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI DRC

December 14, 2017


PMO_2758
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC
PMO_2836
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wafiwa baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC.
PMO_2782
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC.
PMO_2828
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC, kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ, Upanga jijini Dar es salaam akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli, Desemba 14, 2017.
PMO_2779
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo  baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC.
PMO_2760
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC.
PMO_2784
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC. Katikati ni Rais Mstaafu wa Awamu wa Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC.
PMO_2804
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017  alikomwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo – DRC.
PMO_2788
Askari wa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari 14 wa JWTZ waliouwa wakiwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo –  DRC,`kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ Upanga jijini Dar es salaam  Desemba 14, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari hao.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

SBL yazindua kinywaji kipya cha SMIRNOFF X1 Extra Pure Vodka

December 14, 2017



Meneja Ubunifu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Wankyo Marando akifafanua ubora wa kinywaji kipya   cha Smirnoff X1 Extra Pure Vodka wakati wa  uzinduzi wa kinywaji hicho  mapema jana usiku wa jana.


 Wadau wakionesha chupa yenye kinywaji kipya cha Smirnoff X1 Extra Pure Vodka wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Ukumbi wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.



 Mtaalamu wa kuchanganya vinywaji, Junior Charles akielekeza namna ya kuchanganya kinywaji hicho.
 Mafuriko ya wadau katika uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika Ukumbi wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 Warembo wakiwa na kinywaji hicho kabla ya kwenda kupeleka kwa wadau
 Chupa ya kinywaji hicho ikiwa imeinuliwa juu na wadau.
 Mmoja wa wadau akiangalia chupa yenye kinywaji hicho.
 Uzinduzi ukiendelea.
 Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo
 Muonekano wa kinywaji hicho katika chupa.
 Hapa ni furaha tupu katika hafla hiyo
 Wafanyakazi wa SBL wakigonganisha glasi wakati wa uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakifurahia kichwaji hicho huku wakiburudika kwa muziki.


 Meneja Ubunifu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Wankyo Marando akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha Smirnoff X1 Extra Pure Vodka mapema jana usiku wa jana.



Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza kuingiza kinywaji kipya kinachojulikana kama SMIRNOFF X1 Extra Pure Vodka kwenye soko la Tanzania kwa mara ya kwanza

Kuingia kwa kinywaji hiki kipya, ni mwendelezo wa uwepo wa kinywaji maarufu aina ya SMIRNOFF ambacho wateja SBL wamekuwa wakikifurahia kwa miaka kadhaa hapa nchini.
Kikiwa kimechujwa kwa ustadi wa hali ya juu, SMIRNOFF X1 Extra Pure Vodka inakuja ikiwa na kilevi cha kiwango cha asilimia 43 huku ikiwa na ladha nzuri inayoweza kufurahiwa katika matukio mbali mbali
.
“Kinywaji hiki kipya cha Smirnoff X1 Extra Pure, ni kinywaji murua kwa wanywaji wote wanaokunywa kistarabu hasa wakati huu tunapoelekea kipindi cha sikukuu na mwisho wa mwaka,” alisema Wankyo Marando  ambaye ni Meneja Ubunifu wa SBL wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam.”
“Kutokana na sikukuu za kitaifa, sherehe za nyama choma na muziki, wateja wetu wanaweza kujumuika pamoja kusherehekea matukio kama haya ambayo yanawaleta pamoja huku wakijiburudisha na kinywaji kipya na chenye kuvutia cha Smirnoff X1 Extra Pure,” aliongeza Marando.

Meneja huyo alisema, SMIRNOFF X1 Extra Pure Vodka imefungashwa kwenye chupa zenye ujazo waa mililita 750 na 200 na kuongeza kuwa zitakuwa zikipatika katika maduka ya kuuza vileo kwa bei elekezi ya shilingi 12,000/- kwa chupa yenye ujazo wa mililita 750 na  shilingi 4,000/- kwe chupa yenye ujazo wa mililita 200.

Bei hizi ambazo ni nafuu, zitawawezesha wateja wa SBL kufurahia kinywaji hiki chenye ubora wa hali ya juu na chenye ladha ya kipekee kinachowaleta watu pamoja kwa urahisi.


Kikiwa ni moja kati ya vinywaji aina ya vodka kilichoshinda tuzo nyingi duniani, SMIRNOFF inafahamika kwa ubora wake kote ulimwenguni huku kikitumiwa na wanywaji wastaarabu katika nchi 130 duniani.