MATUKIO MBALIMBALI KUELEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO KUFANYIKA.
Msemaji wa Serikali Bw.Assah Mwambene akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam.
****************************************
Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
SERIKALI
imetoa wito kwa wananchi na vyombo vya habari kushiriki katika shughuli
na matukio mbalimbali ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya
Muungano yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini ambayo kilele
chake kitakuwa tarehe 26,April 2014, siku ya maadhimisho ya sherehe
hizo.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa Serikali na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene amesema kuwa
maadhimisho ya mwaka huu ambayo ni ya kipekee yanaongozwa na kauli mbiu
isemayo Utanzania wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuuimarishe na
Kuudumisha yanaambatana na matukio mbalimbali yanayozihusisha wizara na
taasisi mbalimbali za Muungano.