RAIS DKT SAMIA SULUHU ATUA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SOEKARNO-HATTA,TANGERANG KWA AJILI YA ZIARA NCHINI INDONESIA

January 23, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang kwa ajili ya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia tarehe 24 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang kwa ajili ya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia tarehe 24 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang kwa ajili ya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia tarehe 24 Januari, 2024.

ASILIMIA 43 YA GESIJOTO INAHITAJI KUPUNGUZWA IFIKAPO MWAKA 2030

January 23, 2024

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema asilimia 43 ya gesijoto inahitaji kupunguzwa ifikapo mwaka 2030 ili kuwezesha joto la dunia kutoongezeka zaidi ya nyuzi joto 1.5.


Amesema hatua hiyo itafanyika kwa kuongeza matumizi ya nishati jadidifu, kuongeza jitihada za kuachana na matumizi ya nishati chafuzi na kuondoa ruzuku kwa matumizi ya makaa ya mawe; kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na ushirikishwaji wa sekta binafsi na asasi za kiraia.

Dkt. Jafo amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 2024.

Aidha, amesema kuwa mikakati ya kupunguza gesijoto, viongozi wa nchi wanachama walijadili jinsi ya kuimarisha jitihada za kupunguza uzalishaji wake hadi kubakia chini ya nyuzi joto 2.

Waziri Jafo amesema pia, majadiliano hayo yalihusu uanzishwaji wa programu ya upunguzaji wa gesijoto na haja ya kuondoa ufadhili na matumizi ya vyanzo vya nishati ya mafuta na makaa ya mawe kutokana na sababu za kuchangia katika uzalishaji wa gesijoto na uchafuzi wa mazingira duniani ambayo hata hivyo, makubaliano hayakufikiwa.

Halikadhalika, nchi wanachama kwa pamoja zimeombwa kutoa fedha kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa mpango kazi wa Kamati ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na kutoa miongozo na mafunzo ili kubaini mahitaji ya nchi zinazoendelea katika kuandaa na kutekeleza mipango ya taifa ya kuhimili changamoto hizo.

Ameongeza kuwa Mkutano wa COP28 umetambua uwepo wa pengo kubwa katika utoaji wa fedha na Dola za Marekani trilioni 5.8 hadi 5.9 zinahitajika kwa mwaka ili kufikia malengo ya upunguzaji wa uzalishaji wa gesi joto ifikapo mwaka 2030.

“Majadiliano katika agenda hii yalijikita katika kuwezesha upatikanaji wa teknolojia zinazohitajika kwa wakati na kwa gharama nafuu kama ilivyobainishwa katika Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi na Makubaliano ya Paris,” amesema huku akiongeza kuwa taasisi za fedha zimeombwa kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia za kuhimili na kupunguza uzalishaji wa gesijoto katika nchi zinazoendelea.

Amesema kuwa ushiriki wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 28 umeiwezesha nchi kuendelea kuimarisha ushirikiano na jumuiya za kimataifa na kikanda pamoja na kuibua fursa zaidi za miradi, uwekezaji na utafiti katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kupitia kwa Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga imeipongeza Serikali kwa maandalizi na kushiriki kwa mkutano huo ambao umeonesha tija.

Amesisitiza kuongeza nguvu katika kuandika maandiko ya kuomba fedha kutoka kwa nchi zilizoendelea ili zizinufaishe nchi zinazoendelea ambazo zimekuwa waathirika wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kikao hicho pia kimepokea taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha taarifa kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifafafanua jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akiongoza kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi akifafanua jambo wakati wa kkikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akifafanua jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a akifafanua jambo ya utendaji wa Mamlaka kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakifuatilia kikao cha kuwasilisha taarifa ya maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 2024.

'MALIZENI MIRADI KWA WAKATI' - RC SENDIGA

January 23, 2024









Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara




Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo Januari 23, 2024 amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelea katika mkoa wake wilayani Babati.




Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.




Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.




Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiteta jambo na Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini.



Pia, Mhe. Queen Sendiga alipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini ulioanza Oktoba 25, 2023.




Mhe. Sendiga amejionea ujenzi huo huku akiwataka wataalamu hao kumaliza kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote vitavyosababisha ukwamishaji wa ujenzi huo.




Ujenzi huo unaogharimu shilingi Mil. 600 ambapo awamu ya kwanza wamepewa zaidi ya mil. 285 kwa ajili ya ukamilishaji wa Boma, msingi mpaka gorofa ya kwanza na sasa ujenzi umefikia asilimia 21.4.




Aidha Jeshi la Zimamoto Walimemshukuru Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwezesha majeshi ya Tanzania katika kukabiliana na majanga mbali mbali huku wakimshukuru Mhe. Sendiga na ofisi yake kwa ujumla kuweza kuwawezesha katika miongozo mbali mbali.


Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati.


Baadae Mhe. Queen Sendiga alifika katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. Mradi ulibuliwa baada ya Serikali kuanzisha mkoa wa Manyara mwaka 2002 na ndipo uhitaji wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa ulipotokea.




Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema utekelezaji unaoendelea ni awamu ya Kwanza ambayo ilianza baada ya Serikali kutoa fedha mnamo mwezi Aprili 2023 jumla ya shilingi milioni mia nane tu (TShs.800,000,000.00) ambazo zilipokelewa Polisi Mkoa Manyara.


Amesema kazi zilizofanyika ni ujenzi wa msingi, nguzo na sakafu za ghorofa zote nne huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa kuta za pamoja na kuezeka na ujenzi wa chumba cha mitambo ya lifti ambapo wanatarajia ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari.


Nae Mhe. Sendiga amewapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kutekeleza mradi kwa vitendo huku akizitaka taasisi nyingine zenye miradi mkoani humo kuiga Jeshi la Polisi.


Aidha Mhe. Sendiga amemtaka mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha ujenzi wa jengo la ofisi ya yake linakamilika kwa wakati maana ujenzi wake umekuwa ukisua sua jambo linaloleta ukakasi kila anapotembelea.

Jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Babati ambapo ujenzi wake umekuwa ukisua sua. (Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara)

BAADA YA MABORESHO KUKAMILIKA, BANDARI YA TANGA YAFUNGUKA NA KUZALIWA UPYA, SHEHENA NA MELI ZAZIDI KUONGEZEKA

January 23, 2024


Na mwandishi wetu, Tanga

Baada ya kukamilika miradi ya maboresho katika bandari ya Tanga, kumepelekea tija kubwa kuonekana katika nyanja tofauti ikiwemo kuongezeka kwa shehena na meli zinazohudumiwa katika bandari hiyo jambo ambalo linachangia ongezeko la mapato.

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 23 Januari, 2024 na Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema, miradi ya maboresho katika bandari hiyo ilitekelezwa kwa awamu mbili na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 429.1.

Kwa upande shehena, Meneja Mrisha ameeleza kuwa, bandari ya Tanga baada ya maboresho hayo sasa itakuwa na uwezo wa kuhudumia hadi tani 3,000,000 kwa mwaka.

Bandari ya Tanga kabla ya maboresho, kwa mwaka ilikuwa na uwezo wa kuhudumia tani 750,000 lakini baada ya maboresho bandari ya Tanga itahudumia hadi tani 3,000,000 kwa mwaka"

Ameendelea kwa kusema kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 (mwezi Julai hadi Desemba) bandari ya Tanga tumeweza kuhudumia tani 572,000 ambapo ni kiwango kikubwa ukilinganisha na kipindi kama hiko kwa mwaka uliopita wa fedha ambapo tuliweza kuhudumia tani 490,000 pekee" alisema Meneja Mrisha na kuongeza kuwa

"Katika mwaka wa fedha 2022/2023, bandari ya Tanga tuliweza kuhudumia tani 987,000 kiwango kikubwa kuliko mwaka wa fedha 2021/2022 tulipoweza kuhudumiwa tani 870, 000. Kwa maboresho yaliyofanyika, tunaweza kusema kwamba bandari ya Tanga imefunguka na kuzaliwa upya"

Kwa upande wa kuhudumia meli, Meneja wa Bandari hiyo amebainisha kuwa, wameweza kuvuka lengo kwa kuhudumia meli nyingi zaidi ikiwa ni mara mbili zaidi katika kipindi cha nusu mwaka huu wa fedha ikilinganishwa na kipindi kama hiko katika mwaka uliopita wa fedha.

"Lengo letu la katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba, 2023 lilikuwa ni kuhudumia meli 110, lakini tumeweza kuhudumia meli 122 tumevuka lengo kwa 11% lakini kipindi kama hiko mwaka 2022/23 tuliweza kuhudumia meli 110 pekee" alisisitiza Mrisha

Baada ya maboresho kukamilika katika bandari ya Tanga, faida lukuki zimeweza kupatikana ikiwemo uharaka katika kuhudumia meli, idadi ya meli kuongezeka, gharama za uendeshaji kupungua, na mapato kuongezeka.

Miongoni mwa maboresho yaliyofanywa katika bandari ya Tanga iliyojengwa katika miaka ya 1890's ni pamoja na kuongeza upana wa mlango bahari, sehemu ya kuingia na kutoka meli (entrance Channel) kwa mita 73, kuongeza kina cha maji kutoka mita 3 hadi mita 13, kuongeza sehemu ya kugeuzia meli (turning base) kutoka mita 3 hadi mita 13, kununua vifaa vya vya bandari ikiwemo mobile harbour crane mbili zenye uwezo wa kubeba tani 100 kila moja, forklift za tani 50 moja, forklift ya tani 16,forklift za tani 5 mbili, terminal tractora mbili, Rubber Tyre Gantry Crane (RTG) moja, spreaders za futi 40 mbili na spreaders za futi 20 mbili.











SERIKALI YAONDOA ZAIDI YA TOZO 374 KUWEZESHA SEKTA BINAFSI KUFANYA KAZI KWA UFANISI

January 23, 2024


KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida,amesema kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) umeweza kupunguza na kuondoa zaidi ya tozo 374 na kurekebisha zaidi ya Sheria na Kanuni 55 zinazowezesha Sekta binasfi kufanya kazi kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa Januari 22, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kida amesema kuwa Tozo zilizoondolewa au kupunguzwa na Sheria na Kanuni zilizorekebishwa zimelenga Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji katika sekta za Uwekezaji, Kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, Utalii, Nishati, Madini, viwanda na Biashara

Aidha, Dkt. Kida amesema kuwa Mradi huo umelenga katika kukuza uchumi, kuongeza ajira na ubunifu kwa vijana na wanawake, kwa kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji pia kuongeza usalama wa mlaji na kuwezesha wajasiriamali wakubwa, wa kati na wadogo kuzingatia ubora wa Bidhaa.

Dkt. Kida amefafanua kuwa, Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), umetoa jumla ya Euro milioni 23 sawa na fedha za kitanzania Bilioni 63.5 ambazo zimeelekezwa kufadhili miradi mitatu ikiwemo Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) ambao awali ilikua ikijulikana kama BLUEPRINT. Vilevile amefafanua kuwa fedha hizi zimelekezwa katika Mradi wa QUALITAN uliojikita kuimarisha maabara za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mradi wa FUNGUO unatekelezwa na UNDP ambao umejielekeza katika kuwawezesha kampuni changa zinazochipukia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Cedric Merel amesema Kamati imejadili kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini na jinsi ya kusaidia kampuni zinazoibukia kukua na kuyafikia masoko.

Naye Mkuu anayesimamia Masuala ya UNIDO Bara la Afrika Bw. Victor Djemba wanaendelea kusisitiza wazalishaji kuzingatia ubora ili kuyafikia masoko makubwa na amehaidi kuendelea kushirikiana na Umoja huo ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akisisitiza jambo wakati akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mahusiano wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Cedric Merel akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Bw.Shigeki Komatsubara akizungumza katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Bw.Shigeki Komatsubara akiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Prof. Mkumbukwa Mtambo akiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Uwekezaji nchini wakiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa uwekezaji na viwanda wakati wa Mkutano wa Kamati Kuu ya Mradi wa "Business Environment Growth Innovation (BEGIN)" uliofanyika Januari 22,2024 jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)