STARS KUWAFUATA UGANDA ALHAMIS

June 30, 2015
Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo.

Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini Uganda.

“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi, vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

Aidha Mkwasa amesema ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili - Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.

Stars imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya saa 10 jioni.
 Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein Arejesha Fomu leo juni 30, 2015

Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein Arejesha Fomu leo juni 30, 2015

June 30, 2015
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akirejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo-Juni 30, 2015.
[Picha na Ikulu.]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu maalum wakati wa kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu maalum wakati wa kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo akiwa na familia yake waliomsindikiza.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii baada ya kurejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo.
5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoka nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mara aliporejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Viongozi mbali mbali waliomsindikiza nje ya Jengo la Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja   mara aliporejesha Fomu za kuomba ridhaa ya Chama kumchagua kuwa Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia Chama Chake  CCM  katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
 WAZIRI NYALANDU AZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA

WAZIRI NYALANDU AZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA

June 30, 2015
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa wakati alipowasili kwenye klabu ya Yacht ya Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji watanzania kutembelea Mbuga za Taifa iliyozinduliwa leo jijini Mwanza ikiwashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Katika Picha kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
Kampeni hiyo ambayo inaanza kesho Julai 1 itakuwa ni ya miezi 6 mpaka  Desema 31 na kauli mbiu yake inasema   “Tembelea Hifadhi Uzawadiwe”.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi. Devotha Mdachi wakati wa uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akifuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wakati alipowasili kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji Watanzania kutembelea Mbuga za taifa kulia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Bw. Ibrahim Mussa.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa na Johnson Manase Meneja wa Utalii TANAPA.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Baadhi ya maofisa wa TANAPA wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Wahariri wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Mwandishi Jimmy Mengere na Kasilda Mrimira wakiperuzi simu zao wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

U15 YAREJEA DAR

June 30, 2015

Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinarejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mbeya ambapo jana kiliibuk ana ushindi wa ushindi wa mabao 4-1.

U15 ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za vijana chini ya miaka 17 barani Afrika kilikua na ziara ya michezo ya kirafiki miwili jijini Mbeya ambapo katika mchezo wa awali pia kiliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mara baada ya kurejea leo jioni jijini Dar es salaam, kambi ya timu hiyo itavunjwa mpaka watakapokutana tena mwisho wa mwezi ujao kwa ajili ya kuelekea visiwani zanzibar kwa jili ya michezo ya kirafiki.

Lengo la michezo hiyo ya kirafiki ni kutoa nafasi ya kocha Bakari Shime kutambua uwezo wa vijana wake na kuongeza wachezaji wengine katika kikosi hicho kisha kuandaa kikosi bora kitakachoshirki kuwania kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.

FDL KUCHEZWA MAKUNDI MATATU 2015/2016

June 30, 2015

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Mfuko huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao cake kilichofanyika mjini Zanzibar.

Timu ya kwanza katika kila kundi la ligi hiyo itakayoanza Septemba 12 mwaka huu itapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A linaundwa na timu za African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).

TIMU YA WATU 21 YA KAMPUNI YA KUCHIMBA DHAHABU YA ACACIA WASHUKA KUTOKA MLIMA KILIMANJARO,WACHANGISHA MILIONI 800 KWA AJILI YA ELIMU TANZANIA.

June 30, 2015

Timu ya watu 21 ya wafanyakazi ,Ndugu na Marafiki wa Kampuni ya kuchimba dhahabu ya Acacia wakishuka kutoka mlima Kilimanjaro ambako walipanda kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia elimu.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Acacia,Brad Gordon akiwa na Meneja wa Ustawi wa kampuni Asa Mwaipopo wakifurahia mara baada ya kushuka toka kaika kilele cha Uhuru ambako watu 19 kati ya 21 ndio walifanikiwa kufika kileleni.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Necta P Foya akishangilia wakati akishuka toka mlima Kilimanjaro.
Timu ya watu 21 iliyopanda Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Kuchimba Dhabu ya Acacia wakiwa katika Uniform maalumu wakielekea lango la kutokea katika mlima la Mweka huku wakiimba nyimbo mbalimbali .
Mkuu wa wilaya ya Tarime ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika mapokezi ya timu ya watu 21 iliyopanda mlima Kilimanjaro,G;orious Luoga (wa tatu toka kushoto) akiimba na wapandaji hao.
Wapandaji wakiimba mara baada ya kufika katika lango la Mweka,hapa wakiongozwa nyimbo mbalimbali na mmoja wa asakari wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kiliamanjaro.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI ARUSHA

June 30, 2015

Mhe.Jaji  Fransis S.K Mutungu , Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini (kushoto) akizungumza na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati alipomtembelea  Ofisini kwake.
 Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe Godbless Lema akifafanua jambo kwa Mhe. Mutungi alipomtembelea ofisini kwake


Bw. Lewis Y. Mnyambwa ambaye ni Afisa Utumishi Jiji la Arusha, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji akimweleza jambo Mhe. Jaji Mutungi alipotembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha