SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MIFUMO YA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

October 25, 2023

 Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa masuala ya maafa nchini ili kuendelea kuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na maafa nchini.


Akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatembwa amesema kuwa tayari ofisi yake imeendelea kuratibu Mfumo Shirikishi wa kidigitali wa usimamizi wa taarifa za masuala ya maafa, uwepo wa Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, uwepo wa vifaa vya misaada ya kibinadamu vinavyohifadhiwa kwenye maghala, utoaji wa elimu kwa umma pamoja na ujenzi wa kituo cha Usimamizi wa Maafa katika eneo la Nzuguni Dodoma.

Akizungumzia maandalizi katika kuelekea mvua za el nino amesema kuwa, ofisi imeendela kuziwezesha kamati za maafa katika mikoa 14 iliyotabiriwa kupata athari za mvua hizo zilizotabiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini na kuzikumbusha kuendelea kujiimarisha katika maeneo yao ili kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea wakati wa mvua hizo.

“Tumeshaifikia mikoa iliyotajwa kuathiriwa na mvua za el nino kwa kutoa elimu kwa kamati za maafa ngazi ya Mkoa hadi Vijiji lengo ni kuwajengea uelewa zaidi na kukumbusha jamii kuchukua hatua za mapema kabla ya kupata madhara ya uwepo wa mvua hizo,” alisema Mutatembwa.

Aidha akiwasilisha taarifa kuhusu dhana ya menejimenti ya Maafa na Mfuko wa Taifa wa usimamizi wa maafa nchini Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya maafa Bw. Charles Msangi ameeleza kuwa, Ofisi imeendelea kuimarisha mfumo wa mawasilino kupitia kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura ambacho kipo chini ya Ofisi hiyo kinachopokea taarifa za majanga kwa kupiga namba 190 au kuandika ujumbe kwenda namba *190# ok ambapo ofisi inapokea taarifa hizo na kuzifanyia kazi katika maeneo yote nchini.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Japhet Hasunga ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendelea kuratibu masuala ya maafa nchini huku akiwakumbusha kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kwa umma na kuwa na mifumo rahisi ya kuyafikia makundi yote nchini kuanzia ngazi ya Kijiji ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya masuala hayo.

“Endeleeni kutoa elimu kwa umma na kuikumbusha jamii kuchukua hatua hususan katika kipindi hichi kilichotabiriwa kuwepo na mvua za el nino nchini, pia ni wakati sasa wa serikali kuimarisha mawasiliano wakati wa maafa ili kuwa na jamii salama na stahimilivu dhidi ya madhara ya maafa,” alisisitiza Mhe. Hasunga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Anderson Mutatembwa akizungumza kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa wakati wa semina ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyolenga kujenga uelewa kuhusu masuala hayo pamoja na mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe.Japhet Hasunga akiongoza kikao cha kamati hiyo, kilicholenga kujengewa uelewa kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa na mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa nchini chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bungeni Dodoma.





PEXPLA TANZANIA, CHEMBA YA BIASHARA YA CHINA KUWAWEZESHA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA

PEXPLA TANZANIA, CHEMBA YA BIASHARA YA CHINA KUWAWEZESHA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA

October 25, 2023

 Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA - TANZANIA) Jenipha Japheth (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anaye shughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming walipokutana katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Jiji la Hangzhou nchini China Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA - TANZANIA) Jenipha Japheth, akizungumza na ujumbe wa Chemba ya Biashara ya Jinhua ya nchini China (hawamo pichani), wakati wa kikao chao kilicholenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wafanyabiasha wa Tanzania na China, kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Hangzhou China. Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA - TANZANIA) Jenipha Japheth (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anaye shughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming (kushoto), wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Jijini Hangzhou chini China.  Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya PEXPLA - TANZANIA) Jenipha Japheth (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Vijana ya Sayansi na Teknolojia ya Jinhua chini China, Jiang Jingwei.


...............................

Na: Hughes Dugilo, Hangzhou, CHINA

Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi inayojihusisha na kuwawezesha Wafanyabiasha ya Professional Exchange Platform, (PEXPLA - TANZANIA) Bi Jenipha Japheth, amesema kuwa wafanyabiasha wa Tanzania wanaweza kunufaika na uwepo wa mashirikiano ya Kibiashara baina ya taasisi hiyo na Chemba ya Biashara ya Jinhua ya nchini China, kwa kuwafungulia milango ya kuongeza wigo wa masoko yao na kukopeshwa mitaji.

Akizungumza katika kikao maaluum kati ya taasisi hizo mbili, kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Hangzhou nchini China, Jenipha amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina yao yanakwenda kuongeza fursa za kibiashara kwa wafanyabiasha wa Tanzania.

"Kikao hiki ni muendelezo wa taasisi yetu ya PEXPLA katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuwainua wafanyabiasha wa dogo, wakati na wakubwa.

"Pia PEXPLA ina jukumu la kukuza mitaji ya Wafanyabiasha, ambapo kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuanza kuwadhamini wafanyabiasha hao ili waweze kuchukua mzigo kutoka kwa wazalishaji wa China kwa mkopo, na kuziuza na baadae kujisimamia wenyewe katika Biashara zao" amesema Jenipha.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo pia imeweza kutoa udhamini kwa wafanyabiasha zaidi ya 300 kwenda nchini China, kujifunza na kujionea fursa mbalimbali za kibiashara, huku ikiwakutanisha na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali katika mazungumzo ya ana kwa ana.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chemba ya Biashara ya Jinhua nchini China, anayeshughulika na mahusiano ya Biashara na Afrika, Jin Yongming ameishukuru taasisi ya PEXPLA kwa kuonesha nia ya kuongeza wigo kwa wafanyabiasha wa Tanzania, na kuahidi kuendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wafanyabiasha hao ili kufikia malengo yao.:

RAIS SAMIA NA RAIS WA ZAMBIA WAKIWA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI LUSAKA ZAMBIA

October 25, 2023

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Ikulu ya Lusaka nchini Zambia tarehe 25 Oktoba, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake ya Kitaifa Lusaka nchini Zambia mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa nchi hiyo Mhe. Hakainde Hichilema tarehe 25 Oktoba, 2025
Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini humo tarehe 25 Oktoba, 2025

Jiji la Mwanza laanzisha mahusiano na Jiji la Tulsa, Marekani

October 25, 2023

 

Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanzisha mahusiano na Jiji la Tulsa kutoka Jimbo la Oklahoma nchini Marekani yanayotarajiwa kuimarisha fursa za uwekezaji katika sekta za elimu, afya, mazingira, utalii, kilimo na biashara.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine ameyasema hayo Oktoba 25, 2025 wakati wa ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum yenye lengo la kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji jijini Mwanza.

“Dhamira yetu kubwa ni kuimarisha mahusiano na wenzetu wa Tulsa ili kubadilishana wataalamu, ujenzi wa miundombinu pamoja na kuboresha sekta yenye changamoto katika jamii yetu” amesema Sima na kuongeza;

“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea luleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo elimu na afya katika Jiji letu, lakini bado kuna baadhi ya changamoto hivyo mahusiano haya yataongeza nguvu katika kuzitatua” amesema Sima.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum amesema mahusiano hayo yatasaidia kuimarisha fursa za uwekezaji na uchumi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, utalii na kilimo katika majiji yote mawili.

“Tunalenga kuimarisha ustawi wa jamii ya watu wa Jiji la Mwanza kupitia maboresho ya huduma za kiuchumi na kijamii” amesema Bynum.

Mratibu wa Mahusiano ya Miji Dada kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Billy Brown amesema baada ya mahusiano hayo, hatua inayofuata ni kubaini na kutengeneza fursa zenye manufaa kwa jamii ya Jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Awali tulikuwa tukitumia mahusiano haya kuwajengea uwezo watumishi wa Halmashauri, lakini sasa tunaenda mbali zaidi kwa ajili ya kuwa na miradi itakayotekelezwa kwa ajili ya manufaa ya wananchi” amesema Brown.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana amekutana na ujumbe kutoka Tulsa ukiongozwa na Meya Bynum na kumweleza fursa kubwa za uwekezaji zilizopo jijini Mwanza kuwa ni pamoja na utalii, uvuvi wa vizimba na kilimo na kumwahidi ushirikiano katika kuimarisha mahusiano hayo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya majiji hayo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (kushoto) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akimkabidhi ufunguo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) kama ishara ya ukaribisho wa mahusiano baina ya Jiji la Tulsa na Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana (katikati) akizungumza na ujumbe wa Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa Marekani (kulia). Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine akizungumza wakati wa ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum akizungumza wakati wa ziara yake jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tulsa, George Bynum (kulia) akizungumza baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na kulakiwa na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya (katikati). Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kulia) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kulia) akisalimiana na ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kulakiwa na ngoma ya asili ya kabila la wasukuma.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kulakiwa na ngoma ya asili ya kabila la wasukuma.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukisoma bango la ukaribisho katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ulipowasili katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (wa nne kushoto) akiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tula, George Bynum (wa tatu kushoto) kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo kutoka benki ya NMB.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ujumbe kutoka Jiji la Tulsa Marekani ukiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

TAASISI ZA FEDHA ZIMEOMBWA KURAHISISHA HUDUMA ZA KIFEDHA KWA WALEMAVU

October 25, 2023

 





Na Pamela Mollel,Arusha 


Taasisi za Fedha zimeombwa  kurahisisha huduma  za kifedha Kwa watu wenye ulemavu hususan wa macho.


Hayo yamesemwa kwenye  Mkutano wa  wiki ya azaki  unaoendelea  jijinibl Arusha  ambapo wameomba kupatiwa mfumo shirikishi utakaowasaidia kwenye utumiaji wa Teknolojia katika  eneo la kifedha.


Mmoja wa walemavu wa macho  Renatusi  Rupoli   kutoka Iringa amesema   watu wasioona huwa wanatumia  mitandao kwa njia ya sauti ambapo alihoji kwanini kusiwepo na Software  kama hizo  ambazo zinajumlishwa  kwenye Mashine za Kutolea pesa (ATM)  Benki    Ili  kupunguza  usumbufu wakutafuta wasaidizi wakati wa kutumia huduma hizo.


Akizungumza katika Mkutano huo Amali Baziadi kutoka Benki ya Stanbic  amesema changamoto hiyo ameichukua na kwamba wataona namna gani yakulifanyia kazi ili kupata ufumbuzi.


"Ninaimani kuwa siyo tu Stanbic pekee ambao hatuna huduma hii lakini naichukua kama changamoto na tuone namna gani tunaifanyia kazi ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma rafiki kwao"amesema Baziadi.


Aidha wadau hao  wameshauri kuwepo kwa huduma rafiki Kwa wazee na wananchi waishio Vijijini namna ambavyo wanaweza kufungua akaunti za Benki kwa kutumia mitandao badala ya kufuata huduma hizo kwa mawakala wa Benki ambao mara nyingi hupatikana mijini.




Mwishooo.

TUME YA MADINI YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

October 25, 2023



Tume ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini leo Oktoba 25, 2023 inashiriki  katika  Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 


Viongozi wa Tume wanaoshiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Makamishna wa Tume ya Madini, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Eng. Yahya Samamba, Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa.


Mkutano huo unafunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko