Na Oscar Assenga, Tanga.
TIMU za soka Simba SC na Coastal Union “Wagosi wa
Kaya” leo zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimishana suluhu pacha ya
kutokufungana kwenye mecho wa Ligi kuu Tanzania bara uliokuwa na upinzani
mkubwa.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani
ulikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu zote kuonyesha kandanda nzuri na
kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika ya 5 iliwachukua Coastal Union
kufika langoni mwa Simba lakini shuti la Yayo Lutimba likatoka nje.
Baada ya shambulio hilo,Simba nao walijibu pigo hilo
kwenye dakika ya 9 mpira adhabu uliopigwa na Nassoro Cholo uliwababatiza mabeki
wa Coastal Union ukamfikia tena Cholo lakini shuti lake likapaa nje ya lango.
Dakika 20 Coastal Union tena walipata nafasi nzuri
baada ya Chrispian Odula kuwatoa walinzi kaze na shamte na kutoa krosi kwa Daniel
lyanga aliyogongewa vyema na Yayo Lutimba lakini shuto lake likapaa juu.
Kwenye dakika ya 32 Boban alipata nafasi akiwa na
mlinda mlango wa Simba Abel Dhaira akazembea na kupiga shuti kali na kujikuta
mpira ukitoka nje na kubakia kugongana na mlinda mlango huyo.
Katika dakika ya 37 Simba wanapata pigo baada ya
mlinda mlango wao Abel Dhaira kutolewa nje kutokana na tukio la kugongana na
boban na nafasi yake kuchukuliwa na Abuu Hashim aliyepandishwa kutoka Simba B.
Mlinda mlango huyo aliweza kuwa imara langoni mwa
Simba ikiwemo kuokoa mpira uliotaka kwenda langoni mwao uliopigwa na Haruna
Moshi Boban na hatimaye kuweza kuuokoa.
Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko hakuna timu
iliyoweza kuona lango la mwenzie ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa
timu zote kushambuliana kwa zamu.
Katika dakika ya 78 Zahoro Pazi alipata pasi ya
Messi na kuambaa winga ya ya kulia na kupiga krosi ambayo kado alitokea na
kuiokoa huku akiishia kufanyiwa madhambi na kusababisha kutibiwa kwa dakika
mbili.
Dakika ya 82Uhuru Seleman alishindwa kuungisha kori
ya Haruna Moshi na kujikuta wakizidiwa maarifa na Gilbert Kaze aliweza kucheza
vema na kuuokoa mpira.
Katika mchezo wa leo,Simba iliwakilishwa na Abel
Dhaira,/Abuu Hashim,,Said Masoud,/Christopher Edward,Haruna Shamte,Joseph
Owino,Gilbert Kaze,Jonas Mkude,Ramadhani Singano,Said Ndemla,Hamis Tambwe,Amri
Kiemba/Zahoro Pazi na William Lucian.
Coastal Union waliwakilishwa na Shabani Kado,Mbwana
Hamis,Othuman Tamim,Marcus Raphael,Juma Nyoso,Jerry Santos,Daniel
Lyanga,Christopher Ochela,Yayo Lutimba,Haruna Moshi Bobani,Keneth Masumbuko.