DC KOROGWE AWAONYA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUACHA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.

February 09, 2017
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha Azidu Kaonekana wa pili kulia ambao wameshirikiana na A Better World kutoka Canada kufanya ujenzi wa majengo matatu ya maabara kwenye shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayan
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol  kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo  iligharimu kiasi cha sh.milioni 75
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka akifuatilia maendeleo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wilayani korogwe Mkoani Tanga
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Patema Jerome Massawe wakati wakitembelea maabara hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka wa pili kulia akiangalia namna wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wanayofundishwa masomo ya sayansi mara baada ya kukamilika maabara hiyo
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka kulia akiteta jambo na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Patema,Jerome Massawe
 Muonekano wa Majengo ya  maabara hizo


WATUMISHI katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert
  Gabriel wakati akipokea taarifa ya umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.

Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na mdhara
  na watumishi ambao watabainika kuihujumu miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendeleo.

“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa
  wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye tabia kama hiyo waiache mara moja.

Aidha alisema lazima watu wabadilike hasa wale wanaopewa majukumu ya
  kusimamia miradi hiyo kutoka kwa wafadhili na wawe wawazi wakati wa utekelezaji wake ili kujenga heshima kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Baadhi yetu tunatumia fursa hizo vibaya na kujinufaisha kupitia fedha
  za wafadhili kinyume na hitaji husika,kufanya hivyo kunaweza kuwakimbiza wadau hao wa maendeleo na kutia doa kwa Taifa”Alisema Gabriel.

Awali akizungumza katika kikao hicho Afisa Elimu sekondari Halmashauri
  ya Korogwe Vijijini Patricia Mbigili alisema pamoja na jitihada kubwa ambazo wanazifanya kuhakikisha wanakamilisha suala la maabara lakini mpaka sasa zilizokamilika ni 5 kati ya 78 katika shule 26,ambapo kunahitajika maabara 3 kwa kila shule ikiwa ni za chemia,physician na bioligia.

Alisema ili kukabiliana na tatizo la ufaulu wa masomo ya sayansi

katika shule za sekondari maabara na uwepo wa walimu wa masomo hayo unahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuwajengea uwezo wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Mbigili alisema jukumu la kuboresha miundombinu ya shule na makazi ya
  walimu ni la wananchi wote,serkali na taasisi zinazojitolea ili kutimiza azma ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kama ilivyoanza kwa madawati na elimu bure.

Naye kwa upende wake, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Azidu Kaoneka
  alisema umaliziaji wa maabara 3,nyumba 1 ya walimu na kuwawekea kifaa cha kuzalisha umemekupitia jua (mobisol) ambapo kiasi cha shilingi milioni 75 zimetumika.

Azidu alisema taasisi hiyo inaimani kubwa kwa kushirikiana na wananchi
pamoja na serikali wanaweza kujenga mazingira rafiki ya walimu na wanafunzi kwa kuboresha miundombinu ya mashule pamoja na nyumba za walimu kama ilivyofanyika shuleni hapo.

Wizara mambo ya nje yapokea vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video.

February 09, 2017


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima jana amepokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video (Video Conference Facilities) kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP).
Baada ya kupokea msaada huo, Balozi Mlima aliishukuru UNDP kwa msaada huo ambao alieleza kuwa utasaidia shughuli za Wizara katika ofisi mpya ya Wizara mjini Dodoma. Alisema msaada huo ni wa pili kwa Wizara katika muda mfupi ambapo awali UNDP ilitoa ngamizi, printers na cameras.
“Tunamshukuru Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ambaye ndio alianzisha suala hili na kuongea nanyi na kulisimamia bila kuchoka hadi leo vifaa vinapatikana”  “Kwa kweli ni mtu ambaye wakati wote anapenda mambo anayoyasimamia yanatokea” Katibu Mkuu alimwambia Mkurugenzi wa UNDP nchini Tanzania, Bi. Awa Dabo.
Kwa upande wake Bi. Dabo baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa mazungumzo kuhusu maombi ya msaada huo yalianza tokea mwaka 2014 lakini kwa uwezo wa mungu vifaa hivyo leo vimekabidhiwa rasmi Wizarani. Alielezea matumani yake kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa Wizara na pia utaboresha na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali na UNDP.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 09 Februari  2017.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akipokea baadhi ya vifaa vya kuwezesha kufanya Mkutano kwa njia ya video kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo Wizarani Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akiwa katika mzungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja Bi. Awa Dabo mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video  
Kutoka kulia, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kisiga, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi Bw. Manyama M. Mapesi na Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakifuatilia zoezi la makabidhiano

Zoezi la Makabidhiano likiendelea.

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UWT TAWI LA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

February 09, 2017


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT, Tawi la Shirikisho la Wanafunzi vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Anastazia Malamsha, wakati wa mazishi ya kiongozi huyo, yaliyofanyika leo katika eneo la  Shimbo, Rombo Mkuu mkoani Kilimanjaro. Anastazia alifariki dunia Jumapili, Feb 5, 2017,  katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoani huo ambapo pamoja naye viongozi wengiewatatu walifariki pia katika ajali hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoaheshima za mwisho kwa mwili wa Anastazia, kabla ya mazishi hayo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Juma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Anastazia wakati wa mazishi hayo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Anastazia kabla ya mazishi hayo
 Katibu  Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Daniel Zenda akitoa heshima za mwisho wa mwili wa marehemu Anastazia wakati wa mazishi hayo
 Muombolezaji akisadiwa wakati akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya marehemu Anastazia
 Bangolilialondikwa kuomboleza kifo cha anastazia, nyumbani kwao
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Mjumbe wa NEC, Cyril Chami
 Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick Mkuu huyo wa mkoa alipowasili kwenye mazishi hayo
 Kinana na baadhi ya viongozi wa Chama na serikali wakiwa kwenye mazishi hayo. Kulia ni Said Mecky Sadick 
 Waombolezaji wakiandamana kutangulia mbele wakati mwili wa Anastazia ulipokuwa ukipelekwa eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo
 Waombolezaji wakiandamana kutangulia mbele wakati mwili wa Anastazia ulipokuwa ukipelekwa eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo
 Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Anastazia kulipeleka kwenye eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo
 Vijana hao wa UVCCM wakiwa wamelibeba kikakamavu jeneza lenye mwili wa marehemu Anastazia
 Huyu ndiye marehemu Anastazia wakati wa uhai ake
 Waombolezaji wakiwa msibani wakati wa mazishi hayo
 Baba na Mama wa marehemu Anastazia, Innocent Malamsha na Devota Malamsha wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa mazishi hayo
 Baba na Mama wa marehemu Anastazia, Innocent Malamsha na Devota Malamsha wakiwa na nyuso za huzuni mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, wakati wa mazishi hayo
 Baadhi ya wanakwaya ambao ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakiimba nyimbo za maombolezo wakati wa mazishi hayo. Anastazia alikuwa mwanafunzi wa Mwaka wa tatu katika chuo hicho Kikuu cha Ushirika Moshi.
 Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi hayo
 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakiwa kwenye mazishi hayo. Anastazia alikuwa mwanafunzi wa Mwaka wa tatu katika chuo hicho Kikuu cha Ushirika Moshi.
 Wana CCM wakiwa kwenye mazishi hayo
 Wana CCM na wananchi wakiwa kwenye mazishi hayo 
 Waombolezaji
 Badhi ya madereva waliowafikisha viongozi kwenye mazishi hayo
 Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Dk.Gervas Machim, akitoa maneno ya rambirambi kwenye mazishi hayo
 Naibu Mkuu wa Kitivo cha Ushirika na Maendeleo ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Dk. Cyril Komba akitoa maneno ya rambirambi kwenye mazishi hayo
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, William Mbogo akitoa maneno ya rambirambi kwenye mazishi hayo
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, William Mbogo akikabidhi fedha za mchango wa rambirambi kwa Baba na mama wa Marehemu Anastazia, Innocent Malamsha na Devota Malamsha, kwenye mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadik na viongozi wengine wa CCM kwenye mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapa pole baba na mama wa marehemu Anastazia baada ya kutoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa pole baba wa marehemu Anastazia baada ya kutoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi fedha za mchango wa rambirambi kutoka CCM na Jumuia zake, kwa Baba na mama wa Marehemu Anastazia, Innocent Malamsha na Devota Malamsha, baada ya kutoa salam za rambirambi kwenye mazishi hayo
Katibu Mkuu wa CCM, Adrahman Kinana akimshukuru mmoja wa padri aliongoza misa ya kumuombea marehemu Anastazia wakati wa mazishi hayo
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro said Mecky Sadick akitoa heshima za msiho kwa mwili a marehemu Anastazia
 Abubakary Assenga akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Anastazia
 Abubakary Assenga akimpa pole mama wa marehemu Anastazia
 Waombolezaji wakati wakiaga mwili kwa mara ya pili wakati wa mazishi hayo
 Baba wamarehemu Anastazia akiweka udogo kaburini wakati wa maziko
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiweka udogo kaburini wakati wa maziko
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya juu CCM, Daniel Zenda akiweka udongo kaburini wakati wa maziko
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini wakati wa maziko
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akiweka udongo kaburini 
 Mwenyekiti wa CCMmkoa wa Kilimanjaro akiweka udongokaburini
Mwombolezaji ambaye ni mwanafamilia ya marehemu Anastazia akisaidiwa wakati akiweka udogo kaburini.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Anastazia, mwishoni mwa maziko.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO