MANJI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAWI LA YANGA TANGA

August 02, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga,Yusuph Maji kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tawi la Yanga mkoa wa Tanga lilopo  Chumbageni mtaa wa Mwanzang'ombe jijini Tanga.

Akizungumza na blogg hii,Mwenyekiti wa Tawi hilo,Adam Daudi alisema maandalizi ya ufunguzi huo yamekamilika kwa asilimia kubwa ambapo shamra shamra hizzo zitaanza saa mbili asubuhi.

Daudi alisema tawi hilo linawanachama hai 105 ambapo mpaka kufikia mwezi desemba mwaka huu wanatarajiwa wanachama hao kuongezeka idadi yao na kufikia 1000.

Mwenyekiti huyo alisema tawi hilo linaviongozi mbalimbali wakiwamoDavid Manyilizu ambaye ni katibu wa tawi hilo,katibu msaidizi Ally Mohamed,Mweka Hazina Mohamed Chandima.

Wajumbe katika tawi hilo ni Abdi Kambutu,Kassimiri kifaru,Hassan Mahundi,Omari Hassani na Maalim Bin Nuh

KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN

August 02, 2013
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Rwiza atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.

Matemera atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.
 

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

USAJILI WA WACHEZAJI SASA MWISHO AGOSTI 5

August 02, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.

Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. 


Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.

Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom

MWANAKOMBO KESSY ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA ABUU ABDURAHAM ORPHANAGE CENTRE

August 02, 2013
(Mshiriki wa Miss Utalii mwaka 2013 Mwanakombo Kessy wa pili kushoto akiwa na washiriki wa Miss Utalii dunia hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu,Tanga.
 

MSHIRIKI wa shindano la Utalii aliyeshika nafasi ya tano mwaka 2013,Mwanakombo Kessy jana alitembelea kituo cha watoto yatima Abuu Abduraham Orphanage Centre kilichopo Makorora jijini Tanga na kuwapa msaada ikiwa ni kutimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kukaa nao na kuwafariji katika mwezi mtukufu wa ramadhani.
Kessy ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga alisema kilichomsukuma kwenda kutoa msaada katika kituo hicho ilitokana na nadhiri yake ambayo aliiweka siku za nyuma kuwa siku moja akifanikiwa ni lazima aende kuwasaidia watoto yatima ili kuwafariji na kubadilishana nao mawazo.

MLEZI WA KITUO HICHO ABUBAKARI AKIWA KATIKA PICHA NA ALIYEKUWA MSHIRIKI WA MISS UTALII MWAKA 2013 ALIYESHIKA NAFASI YA TANO MWANAKOMBO KESSSY NA MBUNIFU WA MAVAZI AISHA KISOKI.

WANAFUNZI WANAOLELEWA KWENYE KITUO HICHO WAKIMSIKILIZA MWANAKOMBO KESSY ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NAO KABLA YA KUWAKABIDHI MSAADA HUO

MWANAKOMBO KESSY KATIKATI KULIA KWAKE ALIYEVAA BAIBUI NI MBUNIFU ALIYEMBUNIA MAVAZI KWNYE MASHINDANO HAYO AMBAYE PIA NI MKURUGENZI WA KOKOLIKO DISGNER AISHA KISOKI KULIA KWAKE NI MLENZI WA KITUO HICHO.

MLEZI wa kituo cha Kulelea Watoto Tatima Abuu Abduraham Orphanage Centre kilichopo Makorora jijini Tanga,Abduraham Abubakari akipokea uniti za umeme toka kwa aliyekuwa mshiriki wa Miss Utalii 2013 na kushika nafasi ya tano, Mwanakombo Kessy

MWANAKOMBO KESSY AKIWAGAWIA WATOTO WANAOLELEWA KWENYE KITUO HICHO FEDHA .
Msaada ambao aliutoa kwenye kituo hicho ni maji ya matunda(Juice),fedha taslimu ambazo alimkabidhi kila mtoto,pia aliweza kulipa ankra ya umeme ambayo kituo hicho kilikuwa kikidaiwa  na kuahidi kuwalipia ada za shule kwa wanafunzi .
Katika halfa hiyo,Kessy aliongozana na mjasiliamali na mbunifu wa nguo za asili ya kiafrika nchini ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa  kampuni ya Kokoliko Disgner,Aisha Kisoki.
"Nashukuru nimetimiza nadhiri yangu,nijipangia kwamba nikifanikiwa katika mipango yangu nitatoa chochote kwa yatima,hivi karibu nilipata bahati ya kwenda nchini Yugoslavia,nimerudi na kuamua kuja kuwatembeleeni  nyie wadogo zangu"alisema Mwanakombo
Awali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Mlezi wa Kituo hicho,Abduraham Abubakari chenye jumla ya watoto 65 alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa hakuna kitu kinamchomfanya mwanadamu afanikiwe kama kuwasaidia watoto yatima.

  (Hapa Mwanakombo Kessy akimkabidhi mmoja kati ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho Maji ya Matunda(Juisi) jana.

   "Kituo hiki kwa hakika kinakabiliwa changamoto nyingi sana lakini kubwa ni ada na matumizi ambapo ndani ya mwezi mmoja tunatumia milioni 4 kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali hivyo tunaiomba wananchi wenye uwezo kuhamasika na kuwasaidia watoto hao "alisema Abubakari na kutaja account namba ya kituo kwa atakayeguswa kuwasaidia ni 446280 ya benki ya CRDB.

Mmoja wa watoto yatima wa kituo hicho Hassan Waziri alisema wanakabiliwa na ukosefu wa ada kwenye shule za msingi na Sekondari pamoja na huduma mbalimbali za kijamii na kuomba jamii ijitokeze kuwasaidia.



MWAKIBINGA: MAJIMAJI KAMPUNI ITAKUWA MFANO KUONDOA UBABAISHAJI SOKA LA BONGO

August 02, 2013

(Kikosi Cha timu ya Maji Maji ya Songea kilichokinashiriki Ligi kuu Tanzania bara kabla ya kushuka daraja na kucheza ligi daraja la kwanza)

Na Mwandishi Wetu,Songea.
Aliyepata kuwa Mkurugenzi wa Fedha TFF na Mtaalamu wa masuala ya fedha, hisa na kodi Bwana Silas Mwakibinga amesema kuwa mfumo wa Majimaji Kampuni na kuingizwa kwenye soko la hisa kutakuwa mfano kwa klabu za Tanzania kuona jinsi ambavyo ubabaishaji unaweza kumalizwa kwenye soka.

Bwana Mwakibinga amesisitiza kuwa ili ubabaishaji uishe katika mpira wa Tanzania ni lazima iwepo klabu ya mfano na Majimaji FC inachokifanya kuingia kwenye Kampuni na hisa zake kuuzwa ndio kile ambacho Watanzania wanakitaka.

“Unajua vilabu vyetu vimekuwa na ubabaishaji kutokana na kukosa mfumo unaoeleweka. Lakini Majimaji FC Kampuni na kuingia kwenye soko la hisa kutalazimisha kutoa mapato na matumizi kwa mujibu wa sheria ya soko la hisa kila mwezi jambo ambalo tayari linaondoa ubabaishaji wowote ule.” Alisema Mwakibinga.

Aidha Mwakibinga amewataka wafadhili mbalimbali ambao wanataka kuwekeza kwenye soka kujiandaa kuweka fedha zao Majimaji kwakuwa watapata taarifa zote za uendeshaji wa klabu kwa mujibu wa sheria.

“Sheria itailazimisha Majimaji kutoa mapato na matumizi lakini vilabu vingine vinaingia kwenye migogoro kwa sababu hakuna utaratibu huo kwao na hawalazimishwi na sheria.”

Tayari wadau mbalimbali wamekwishathibitisha kushiriki katika Majimaji Revival Conference, mkutano wa kujadili mfumo na mikakati ya kiuendeshaji ambayo itajengwa kwaajili ya Majimaji FC Kampuni itakayozaliwa tarehe 10 Agosti 2013 katika ukumbi wa Centenary chini ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu.

Pamoja na Silas Mwakibinga mtoa mada mwingine katika Majimaji Revival Conference anatarajiwa kuwa Dkt Damas Ndumbaro, Mwanasheria na wakala wa kimataifa wa FIFA.

Imetolwa na;

Tanzania Mwandi Co Ltd.

Phone: +25522 2120677 or +255756 829071

Fax: +255 22 2122976

Email: ceo@tanzaniamwandi.co.tz,

info@tanzaniamwandi.co.tz

Website: www.tanzaniamwandi.co.tz/events.ht